Rafed English

Visa Vya Kweli

Visa Vya Kweli by : Sayyid Ali Akbar Sadaaqat

 

Dhana ya maadili imekuepo toka alipoumbwa mwadamu. Siku za zamani, kulikuwa na tofauti ya wazi kati ya maadili “mema” na maadili “mabaya” ingawa si mara zote watu walikuwa wakifuata maadili mema. Katika zama za sasa, tofauti kati ya maadili mema na mabaya imefifia na kwa kiasi kikubwa maadili yametibuliwa. Na matokeo yake, kuna hatari kwamba ufisadi utakuwa wa nguvu kuliko maadili duniani kote.

Hakuna kisingizio kwa Mwislaamu kunasa katika hali hii mbaya na ya hatari. Kuna mwongozo uliowazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia Qur’ani tukufu na Mitume na Ma’sumin. Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mwenyewe alisema, “Nimetumwa kama Mtume kwa lengo la kuyakamil- isha maadili.” Moja ya njia bora kabisa za kuyaelewa maadili ni kwa kusoma mifano halisi kutoka katika maisha ya Mitume na Ma’sumin, amani iwe juu yao wote.

Vitabu vichache vimeshaandikwa juu ya hadithi za maadili kutoka katika ulimwengu wa kiislamu, kimojawapo kikiwa “Pearls of Wisdom” (Lulu za Hikma), kilichochapishwa na Islamic Education Board of World Federation, machi mwaka 1993. Kwa kuzingatia umuhimu wa mada ya Akhlaq, Bodi ya elimu ya kiislamu ya World Federation inachapisha “Visa vya kweli kwa ajili ya kutafakari katika sehemu tano. Chanzo cha chapisho hili ni kitabu “Yaksad Mawzu wa 500 Dastani” cha Sayydi Ali Akber Sadaaqat. Tarjuma ya kutoka kifarsi kwenda Kiingereza ilifanywa na Sheikh Shahnawaz Mahdavi. Bodi ya Elimu ya Kiislamu World Federation ingependa kuwashukuru Sayyid Ali Akbar Sadaaqat na Sheikh Shahnawaz Mahdavi kwa jitihada zao na inawaombea kwa Mwenyezi Mungu awalipe vya kutosha.

(Tunaomba) Mwenyezi Mungu aikubali kazi hii kama jitihada nyingine ya Bodi ya elimu ya Kiislamu ya World Federation ya kueneza Uislamu.
Bodi ya Elimu ya Kiislamu
The World Federation of Muslimu Communities
Sha’aban 1424
Oktoba 2003.
Kuna njia nyingi kwa ajili ya mwanadamu kupata mwongozo na kuibuka kutoka kwenye giza na kuelekea kwenye nuru. Kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu na ukamilifu wa maadili yake, Mwenyezi Mungu ameumba uthibitisho, ushahidi na dalili1, katika idadi kubwa kiasi kwamba ziko nje ya uwezo wa kuhesabiwa na kukokotolewa. Kwa ajili ya mwongozo wa mwanadamu alituma mitume na dalili zilizo wazi,2 vitabu, miujiza na ishara ili pengine watu wanaweza kuitambua njia iliyonyooka na kupata ustawi na mafanikio.

Katika kipindi chote cha utume wake, Mtukufu Mtume (saw), katika suala la utakatifu wa kiroho na ukamilifu wa maadili, alikuwa ni kiigizo katika kauli na matendo, na hata alisema: “Nimetumwa (kama Mtume) kwa (kusudio la) kuyakamilisha maadili.3”

Tatizo la mwanadamu lipo katika kutozingatia kwake amali njema, kuten- da kwake maovu, kupupia matamanio na utii kwa shetani. Baadhi ya watu wamejiachia (katika kufanya maovu) kiasi kwamba wanaendesha maisha yao kama wanyama. Kwa lengo la utakatifu na kuyaponya madili ya wanadamu, kupunguza kasi na kudhibiti hulka ya asili, Mtukufu Mtume alifanya kila aliloliweza na alitaja yote yaliyopaswa juu ya jambo hili.

Kupata fanaka katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao (Akhera) kunawezekana tu chini ya uangalizi wa mwalimu na wakati huo huo si kila mtu anaweza kubainisha nukta mbili za mwisho (yaani maadili bora kabisa na duni kabisa) ili kuonyesha kwa vitendo njia ya kati na iliyo sawa. Yule mwenye Hikma isiyo na kikomo aliwaleta mitume wote na hususani Mtukufu Mtume (saw) kama “mwalimu na mkufunzi” wa maadili, ili kwa kufuata nyayo zake, watu wajitenge na maovu na wapate heshima ya duni- ani na Akhera.

Katika Qur’ani, kuna sura iitwayo Al-Qasas (masimulizi), ambayo yenyewe tu ni ushahidi kuwa mwanadamu anahitaji hadithi na masimulizi.

Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za mitume wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengele, hususani maadili.

Suratul Yusuf yote imetumika kusimulia kisa cha Yusuf, Yaqub, Zulekha na nduguze. Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu anasema:

“Tunakusimulia (Ewe Mtume) masimulizi bora kabisa kwa (kupitia) yale tuliyokufunulia katika Qur’ani hii. (Suratul Yusuf; 12:13)

Ambapo katika aya ya mwisho sura hii, anasema katika historia yao

“kwa hakika kuna mazingatio kwa watu wenye akili.” (Suratul Yusuf 12: 111).

Kwa hakika moja ya ustadi mkubwa kabisa wa Qur’ani ni hadithi hii ya Yusuf (as) iliyotajwa kuwa ni “simulizi bora kabisa” na mwisho (Qur’ani) inase- ma: “katika hadithi hizi kuna mazingatio kwa wale wanaotaka kuadilika na kufuata njia ya watu watimilifu.

Juu ya hili Amirul Muuminina (as) katika Nahjul Balaghah, anamuambia mwanawe Imam Hasan (as): “Ingawa sijafikia umri ule uliofikiwa na wa kabla yangu, nimezitazama tabia zao na nimetafakari matukio ya maisha yao.

Nilitembea katika maanguko yao mpaka nikawa miongoni mwao. Kwa kweli, kwa wema wa mambo yao niliyo (bahatika) kujua, ni kama nimeishi nao mwanzo hadi mwisho.

Hivyo nimeweza kubaini kilicho kichafu na kisafi na chenye manufa na chenye madhara.

Nimekuchagulia bora kabisa ya mambo hayo na nimekukusanyia nukta nzuri huku nikiyaacha yale yasiyo kuwa na manufaa.”

Miaka kadhaa huko nyuma, nilikuwa nimeandika kitabu juu ya maadili (kwa ajili ya kutibu maovu), kwa jina la Ihyaul Qubul. Tokea wakati huo, nilikuwa nikitafakari juu ya kuandika kitabu, juu ya hadithi za maadili. Hivyo ilitokea kwamba, kwa bahati ya Mungu, fursa ilinijia pamoja na hamasa ya kufanya kazi hii. Licha ya ukosefu wa vitabu muhimu, nili- tosheka na vile vilivyokuwepo na nikaanza kuandika kitabu hiki, nikiandi- ka hadithi nne mpaka tano kwa kila mada.

Kwa kweli sijakutana na kitabu chochote kilichoandikwa kwa mtindo huu. Vitabu kama Namunah-e-Maarif Islam na Pand-e-Taarikh vimekuwepo kwa takribani miaka 30 na nimevitumia pia (katika kuandaa mkusanyiko huu) lakini katika vitabu hivyo aya za Qur’ani, Hadithi, mashairi na ulin- ganishi, vyote vimekusanywa pamoja, ambapo mimi nimetosheka kwa kutaja hadithi tu huku nikiepuka kutoa maelezo yanayohusiana na aya za Qur’ani, hadithi, mashairi na ulinganishaji, (vitu ambavyo) visingeongeza tu ukubwa wa kitabu, bali pia vingeleta ugumu wa kueleweka kwa waso- maji wengi. Mkusanyiko huu ni kwa ajili ya umma kwa ujumla, watoto na wakubwa pia, ambao wana elimu ya msingi ya kusoma na kuandika. Kwa kadri nilivyoweza nimejitahidi kukwepa masuala ya kisayansi na vipen- gele vile vinavyohusiana na hadith ambavyo kueleweka kwake kungehita- ji uangalifu mkubwa na kulazimisha kwa jumla kwa ajili ya umma.

Ingawa baadhi ya visa vinawezekana visiwe na vipengele vyovyote vya uhalisi na uhakika, nilichokizingatia ni kunasihi na “kuchukua somo” la kipengele kilichomo humo, ambacho ninataraji wasomaji watukufu watafahamu na kuelewa.

Kadiri suala la kuhusisha kisa na mada mahususi linavyohusika, sisemi kwamba visa vinavyodokeza kwenye mada moja tu au ile mahususi ambayo imetajwa hapa; bali ni visa ambavyo vinaweza kuhusishwa na mada nyingine pia, kwa nyongeza kwenye mada ambayo chini yake imeta- jwa hapa.

Wakati kikisimulia maandishi au nikifanya tarjuma, sikujibana katika maana halisi, bali kwa utambuzi mzuri zaidi, nimeishia kwenye ufafanuzi wa maneno, kudokeza na maelezo yenye maana pia.

Ili kuepuka kuingiliana kwa mada na kurefusha mjadala, nimeepuka kule- ta mada zinazohusiana na zile ambazo tayari zimeshawasilishwa. Kwa mfano, Ithaar (tabia ya kufikiria wengine kuliko nafsi yako mwenyewe) imewasilishwa kama moja ya mada, lakini Infaaq (kutoa katika njia ya Allah) imeachwa.

Ili kuzuia msomaji asipatwe na uchovu na uchoshi, na kwa ajili ya sababu mbali mbali, nimeacha kuwasilisha visa vya kukinaisha, kama vile za wanafalsafa na washairi, lakini nimejitahidi kufanya mkusanyiko uwe tofauti tofauti. Kwa njia hii nataraji wasomaji watafurahia zaidi masimulizi haya.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba uaminifu lazima uzingatiwe, nimetaja kila simulizi iliyowasilishwa hapa, kutoka kwenye kitabu, juzuu gani, na ukurasa gani imechukuliwa. Ni kwa ajili ya kupata mtiririko mzuri zaidi wa kazi kwamba nimejitahidi kusahihisha, kunakshi au kubadilisha baadhi ya maneno au sentensi za maandishi ya asili.

Inatarajiwa kutoka kwa wasomaji kwamba, baada ya kuvipitia visa na simulizi hizi, watatafakari na kuchukua mazingatio ili waweze kujijengea nguvu za kwenda katika ukamilifu wa madili, na Allah swt. akipenda wale waliojaaliwa maadili yenye kusifika wawasimulie wengine, kwa ajili ya kuzirekebisha roho dhaifu zaidi.

Na dua yetu ya mwisho (ni) Sifa zote njema zinamstahiki Allah swt, Mola wa walimwengu.

Said Ali Akbar Sadaaqat
Mordad, 1378 (July 1999)
________________________
1. Qur’ani Tukufu, Sura Ibrahim – 14: 5

2. Ibid, Suratul Hadiid 57:25

3. Safinah al-Bihar, Juz 1,uk 411
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Anecdotes. Sisi tumekiita, Visa vya Kweli. Kitabu hiki kime- andikwa na Sayyid Ali Akbar Sadaaqat.

Kitabu cha Visa vya Kweli kimekusanya simulizi za visa vya kweli vilivyosimuliwa katika Qur’aniTukufu, hadithi na riwaya na vyanzo vingine sahihi. Kwa kweli, visa hivi hufundisha maadili mema kwa wanadamu, hivyo, kitabu hiki tunaweza kukiita kuwa ni cha maadili kwa kuwa visa vilivyoelezewa humu ni vya kimaadili.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili. Kitabu hiki kitawafaa sana vijana walioko mashuleni na vyuoni, halikadhalika watu wa wazima.

Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kwa lugha ya Kiswahili kwa malengo yaleyale ya kuwahudumia wasomaji wetu wazungumzao Kiswahili ili wapate kuongeza elimu yao ya dini na ya kijamii kwa ujumla.

Tunawashukuru ndugu zetu, Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 1970
Dar-es-Salaam,
Tanzania.
Allah Mwenye hikma Anasema:

“Na hakika wewe una tabia tukufu.” (Suratul Qalam: 4)

Mtukufu Mtume (saw) alisema: “Nimetumwa (kama mtume) ili kuja kukamilisha maadili.”

(Jaame Al Saadaat, Juz, 1. Uk. 23)

Maelezo mafupi:

Kwa mwanadamu, maadili huleta heri na fahari katika ulimwengu huu na wepesi huko Akhera. Kunyanyua hadhi ya mtu katika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu na humsaidia katika ukamilifu wa dini yake, Mitume wote, mawalii na wateule wa Mwenyezi Mungu walikuwa na maadili ya kupigiwa mfano, na kila mu’umini anapaswa kujipamba kwa maadili hayo, ili mizani ya amali iwe nzito zaidi Siku ya Hukumu.

Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Hatima ya muda wetu ni moja, kwa yule mwenye maadili mazuri. Maadili mabaya humfanya mtu ataabike kwa kubanwa mbavu kaburini na (adhabu ya) moto wa jahannam (huko akhera) na ukosefu wa marafiki katika ulimwengu huu.”

Mtu hapaswi kupimwa kwa mujibu wa maarifa yake, utajiri au cheo, bali kwa mujibu wa tabia zenye kusifika, zinazomfanya akubalike mbele ya macho ya Allah na kwa kuwa mtukufu na msifiwa mbele ya macho ya watu. (Taz: Tadhkirah al-Haqaaiq, uk. 57)
1. Mtukufu Mtume (Saw) Na Nua’imaan
Nua’imaan Ibn Amr Ansaari alikuwa ni mmoja wa masahaba wa mwanzo wa Mtukufu Mtume (saw) na alikuwa na maumbile ya uchangamfu na ukarimu.

Imesimuliwa kuwa siku moja Bedui mmoja aliwasili Madina na akampunzisha ngamia wake nyuma ya Msikiti (kisha) akaingia ndani ili awe kwenye hadhira ya Mtukufu Mtume (saw)

Baadhi ya masahaba wa Mtume walimshawishi Nua’imaan kwa kusema “Ikiwa utamuua ngamia huyu, tutagawana nyama yake miongoni mwetu, na Mtukufu Mtume (saw) atalipa bei yake kwa mmiliki.”

Kwa kufuata ushauri wao Nua’imaan alimuua mnyama yule. Mmiliki alipotoka nje ya msikiti na kukuta ngamia wake amekufa alikasirika sana na akaamua kulileta jambo hili mbele ya Mtukufu Mtume (saw). Nua’imaan wakati huo alikuwa amekwishakimbia.

Mtukufu Mtume (saw) alitoka nje ya msikiti, akamuona ngamia aliyekufa na kuuliza “Ni nani anayewajibika kwa kitendo hiki? Wale waliokuwepo walimtuhumu Nua’imaan, hivyo Mtukufu Mtume (saw) akamtuma mtu kwenda kumleta Nua’imaan mbele yake. Habari zilivuma kuwa Nua’imaan alikuwa amejificha katika nyumba ya Dhubaa’h Bint Zubeir1 ambayo ilikuwa karibu na msikiti. Alikuwa ameingia kwenye shimo kisha akajifunika na majani mabichi. Mtukufu Mtume (saw) alielezwa juu ya maficho ya Nua’imaan na yeye na masahaba zake wakaelekea kwenye nyumba ya Dhubaa’h walipofika hapo, mjumbe aliomuonyesha Mtume (saw) maficho ya Nua’imaan ambaye Mtume (saw) alimuamuru (mjumbe) alifungue shimo. Baada ya kufanyika hilo, Nua’imaan aliibuka huku mashavu na kipaji chake cha uso vikiwa vimefunikwa na majani mabichi.

Alipomuona, Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza “Ewe Nua’imaan! Ni nini hiki ulichokifanya?

Aljibu, “Ewe Mtume wa Allah (Naapa) kwa Allah! hao watu waliokuleta kwenye maficho yangu, ndio hao hao walionishawishi nimuue ngamia!”

Mtukufu Mtume (saw) alitabasamu na kufuta majani kutoka kwenye mashavu na kipaji cha uso cha Nua’imaan kwa mikono yake mitakatifu. Kisha akalipa gharama ya ngamia kwa yule Bedui kwa niaba ya Nua’imaan.2
2. Khuzaima Na Mfalme Wa Urumi
Khuzaima Abrashi mfalme wa Arabuni, kamwe hakufanya kazi yoyote kubwa bila kwanza kutaka ushauri kutoka kwa mfalme wa Rumi ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu. Wakati fulani, alikuwa na nia ya kupata maoni ya Mfalme (wa Urumi) juu ya heri ya wanawe, alimtumia barua kupitia mjumbe wake, katika barua aliandika:

“Nahisi ninapaswa kutenga utajiri mkubwa kwa kila mwanangu wa kiume na wa kike ili wasije wakataabika baada yangu. Ni nini maoni yako juu ya jambo hili?”

Mfalme wa Urumi Akajibu: “Utajiri ni kishawishi, hauna uaminifu na haudumu! Kitu bora kwa watoto wako itakuwa ni kuwapamba kwa maadili mema na tabia zenye kusifika, ambazo zitawapeleka kwenye uongozi wa kudumu katika ulimwengu huu na msamaha (wa dhambi) huko Akhera.3
3. Mwendo Wa Imam Sajjad (As)
Wakati fulani, ndugu wa Imam Sajjad (as) alimuendea Imam (as) na akaan- za kumkashifu na kumtukana. Imam (as) hakutamka neno lolote kumjibu lakini, baada ya yule mtu kuondoka kwenye mkusanyiko ule, aliwageukia watu waliokuwepo na kusema:

“Mmesikia aliyosema mtu huyu, sasa ninataka muambatane na mimi mkasikie kile nitakachosema kujibu kashfa na matusi yake”

Masahaba wakakubali, “kwa hakika tutaambatana nawe, kwa kusema kweli tulitaraji kuwa ungemjibu wakati ule ule”

Imam (as) aliondoka kuelekea kwenye nyumba ya mtu huyo na alisikika akisoma aya ya Qur’ani ifuatayo:

وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ {134}

“Na ambao wanazuia hasira (zao) na wanasamehe (makosa ya) watu; kwani Allah anawapenda wale wafanyao wema (kwa wengine) (Quran 3: 134)

Msimuliaji anasema: “Tuliposikia kisomo cha aya hii, tulijua kwamba Imam (as) alikusudia kuonyesha wema kwa mtu ambaye punde tu alikuwa amemtukana”

Alipofika kwenye nyumba ya mtu huyo, Imam (as) alimuita na akamjulisha kuwasili kwake. Alipomuona Imam, yule mtu akajua kuwa amekuja kujibu kashfa zake.

Lakini, mara tu Imam (as) alipomuona yule mtu, alisema, “Ewe ndugu (yangu)! Ulikuja kwangu na kusema vitu vya kutisha na visivyopendeza.

Ikiwa uliyoyasema juu yangu ni ya kweli, (basi) ninaomba msamaha kwa Allah, lakini ikwa sio, basi ninamuomba Allah ‘Azza wa Jallah akusame- he.” Yule mtu alishtushwa kusikia maneno haya na akatubu. Alimbusu Imam (as) baina ya macho na akaomba msamaha, akisema:

“Matusi yangu na kashfa hayakuwa na msingi na hayawezi yakahusishwa na tabia yako. Kwa kweli matusi yale yananistahili mimi zaidi kuliko wewe.”4
4. Ali (As) Na Mfanyabiashara Asiye Na Heshima
Imam Ali (as) wakati wa ukhalifa wake, mara nyingi alikuwa akitembelea masoko na kuwashauri na kuwaongoza wafanya biashara. Siku moja, alipokuwa akipita katika soko la tende, alimuona msichana mdogo akilia, Imam aliuliza sababu ya machozi yake ambapo (msichana) alieleza:

“Bwana wangu alinipa dirham moja (kwa ajili) kununulia tende. Nilizinunua (tende) kwa mfanya biashara huyu, lakini niliporudi nyum- bani, bwana wangu alizikataa. Sasa ninataka kuzirudisha lakini mfanya biashara anakataa kuzichua.”

Imam Ali (as) Ali alimgeukia mfanya biashara na kumuambia, “Mtoto huyu ni mtumwa na hana mamlaka yake mwenyewe. Chukua tende na umrudishie fedha yake.”

Mfanya biashara alisogea mbele na huku wafanya biashara na watazamaji wengine wakimtazama, alimpiga Imam kifuani katika jitihada za kum- sukuma atoke mbele ya duka lake. Watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, walikimbia na kumuambia huyo mwanaume:

“Unafikiri unafanya nini? Huyu ni Ali Ibn Abi Talib (as)!”

Uso wa mfanya biashara ulipauka alipokuwa amesimama akaduwaa. Mara moja alichukua tende kutoka kwa msichana na akamkabidhi fedha. Kisha akamgeukia Imam (as) akaomba, “Ewe Amirul Muuminuun! Niwie radhi na nisamehe.”

Imam (as) alijibu,” Nitakuwa radhi na wewe tu pale utakapobadili tabia yako na kuwa njema na ukajali maadili na heshima.”5
5. Maliki Ashtar
Wakati fulani, Maalik Ashtar alikwa akipita katika soko la Kufah akionekana masikini sana. Alikuwa amevaa nguo nzito (iliyotengenezwa kwa kitambaa cha turbai) na alikuwa ameweka turbai kichwani kwake badala ya kilemba. Mmoja wa wafanya biashara alikuwa amekaa dukani mwake macho yake yalipoangukia kwa Maalik. Alimtizama kwa twezo na kwa dharau akamtupia kipande cha udongo.

Maalik alimpuuzia na aliendelea na safari yake. Hata hivyo mtu aliyem- tambua Maalik na aliyekuwa ameshuhudia tukio hilo, alimkanya mfanya biashara:

“Aibu juu yako! Unamjua uliyemdhalilisha punde tu?”

“Hapana.” Alijibu mfanya biashara

“Alikuwa ni Maalik Ashtaar, sahaba wa Ali (as).”

Baridi iliingia mwilini mwa mfanyabiashara alipowaza juu ya uovu alio- ufanya. Mara moja aliondoka na kumfuata Maalik ili akaombe msamaha.

Alibaini kwamba Maalik alikuwa ameingia msikitini ambako alikuwa akisali na akamua kumsubiri. Maalik alipomaliza kusali tu yule mfanya biashara alimuangukia miguuni na kuanza kuibusu, Maalik alimnyanyua na kumuuliza alichokuwa akifanya.

“Ninaomba msamaha kwa dhambi niliyofanaya,” alijibu mfanya biashara. Maalik akaeleza, “Hakuna dhambi juu yako. (Naapa) kwa Allah, nilikuja msikitini makhsusi kwa ajili ya kukuombea msamaha.”6
________________________
1. Alikuwa ni binamu wa Mtukufu Mtume (saw) na mke wa Miqdad Ibn al-Aswad

2. Lataaif al-Tawaaif, uk. 26

3. Namunah-e-Ma’arif, Juz. 1, uk. 64, Jawaame al-Hikayaat, uk. 270

4. Muntahal Aa’maal, Juz. 2, uk. 4

5. Daastaan-ha Wa pand –ha, Juz. 1, uk. 46; Bihar al-Anwar, Juz. 9, uk. .519

6. Muntahl Aa’maal, Juz. 1, uk. 212; Majumua’h Warraam - Ibn Abi Farraas
Allah Mwenye Hikma, amesema:

“Kwa hakika Allah yupo pamoja na wanaojilinda na maovu na wanaofanya wema (kwa wengine).”1

Maelezao mafupi:

Allah humpenda mtu mwenye sifa ya ukarimu, kama ambavyo tu Allah ameonyesha upole kwetu, ni muhimu kwetu kuonyesha ukarimu zaidi kwa wengine. Hata kama mtu ametukosea, tunapaswa kujibu kwa upole na tusilipe uovu kwa uovu, kwani hili litaongeza mafuta kwenye moto na kuzidisha chuki na uadui.

Mwenendo wa wajumbe wa Allah (na Maimam) ulikuwa kwamba wak- isalimiwa, wanaitikia kwa salamu iliyo bora zaidi na kwa ukamilifu zaidi na wakifanyiwa wema, walikuwa wakiulipa, (tena) kwa kuzidisha (walivyofanyiwa wao).

Wale wanaofanya wema na kuonyesha ukarimu kwa wengine, huvuta mioyo ya watu, na wakati huohuo matendo yao yanamuumiza shetani.

Lazima ikumbukwe kwamba wale wanaofanya wema huwa hawamdhalilishi (wanayemfanyia wema) au kuharibu amali zao kwa kuweka aina yoyote ya masharti (kwa huyo waliyemfanyia wema).

Myahudi masikini alipata kukutana na muabudu moto tajiri wakiwa safari- ni. Muabudu moto aliyekuwa anamiliki ngamia na masurufu ya kutosha kwa ajili ya safari, alimuuliza, “Ni nini imani na Itikadi yako?”

Myahudi alijibu, “Ninaamini kwamba ulimwengu huu una aliyeuumba na ninamuabudu yeye na ninaomba hifadhi kwake. Ninaonyesha wema kwa yeyote anayeikiri imani yangu, lakini ninamwaga damu ya yeyote anayeto- fautiana na mimi. Ni nini itikadi yako?”

Muabudu moto alijibu, “Nina wapenda viumbe wote, simdhuru yeyote na ninaonyesha ukarimu na wema kwa marafiki na maadui pia. Mtu yeyote akinikosea, nina jibu kwa wema kwa sababu najua kuwa ulimwengu huu una muumba.”

Aliposikia hivi, Myahudi alisema, “Usidanganye sana. Mimi ni binadamu kama wewe, lakini wakati wewe unasafiri juu ya ngamia na una masurufu ya safari, hunipi chakula chako wala huniruhusu nikae kwenye ngamia wako.”

Muabudu moto aliteremka kutoka kwenye ngamia wake na akatandika kitambaa chini, akaweka chakula chake mbele ya mwenzake, myahudi alikula mkate na kisha akakaa kwenye ngamia ili kuondoa uchovu. Walikuwa wamesafari umbali fulani pamoja. Ghafla myahudi alipompiga ngamia kwa bakora alimlazimisha kukimbia. Yule Mwabudu moto alimwita:

“Ewe mtu! Nilionyesha upole kwako lakini sasa, unalipa ukarimu wangu kwa kuniacha peke yangu jangwani!”

Lakini haikujalisha chochote alichosema, nasaha zake hazikuwa na faida. “Nilikutajia kwamba nina muangamiza yeyote anaye tofautiana na mimi katika imani na itikadi,” Myahudi alimkemea huku akikimbia.

Muabudu moto alitizama juu mbinguni na kuomba: “Ewe Mola wangu! Nimemtendea mtu huyu vyema, lakini amenilipa uovu. Nitendee uadilifu.” Alipokuwa akisema haya, aliendelea na safari yake. Alikuwa amesafiri umbali mfupi tu, ghafla macho yake yalipoangukia kwenye ngamia wake, aliyekuwa amesimama peke yake baada ya kumbwaga myahudi chini. Myahudi, aliyekuwa ameumizwa vibaya, alikuwa akilalama kwa mau- mivu.

Alikuwa na furaha sana, muabudu moto alichukua ngamia wake, akapanda mgongoni mwake na alipokuwa anataka kuondoka Myahudi alilalamika: “Ewe mtu rahimu! Umevuna matunda ya wema wako na nimeshuhudia matokeo ya uovu wangu; sasa kwa kuzingatia imani zako, usiondoke katika njia ya wema; kuwa mpole kwangu na usinitelekeze katika jangwa hili.”

Muabudu moto alijiwa na huruma na akamruhusu kukaa kwenye ngamia na akampeleka mjini.2
1. Wema Wa Imam Husein (As) Kwa Mpanda Ngamia
Imam Sadiq (as) alisema: “Mwanaume mmoja alikuwa akimvuta mwanamke alipokuwa (mwanamke) amejishughulisha katika kutufu Kaaba. Mwanamke huyu alikuwa akinyanyua mikono yake mwanaume yule alipoweka mkono wake juu ya mkono wake (mwanamke) wakati huo Allah aligundisha mkono wake katika mkono wa mwanamke.

Watu walimiminika (kwenda) kushuhudia tukio hili la ajabu kwa wingi mkubwa kiasi kwamba utembeaji ulikwama. Mtu mmoja alitumwa kwa Amiri wa Makka kumjulisha juu ya tukio hili. Alikusanya wanazuoni wote na kwa ujumla wakajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hili. Watu wengi pia wa kawaida walikusanyika wakitaka kujua hukumu itakayotolewa kwa uhalifu huu. Wote wakiwa wamesimama (huku) wametatizika, hatimaye Amiri alisema: “Je kuna mtu yeyote hapa kutoka katika familia ya Mtukufu Mtume (saw)?”

Wale waliokuwepo wakasema, “Ndio! Husein Ibn Ali (as) yupo hapa” Usiku ule Amiri aliamuru Imam (as) akaletwe mbele yake. Alitaka kujua hukumu ya tukio hili kutoka kwa Imam (as)

Kwanza, Imam (as) aligeukia Ka’aba na kunyoosha mikono yake alisima- ma katika hali hii kwa muda kisha akaomba dua.

Kisha alimfuata mwanaume yule akautenganisha mkono wake kutoka katika mkono wa yule mwanamke kwa nguvu ya Uimam wake. Yule Amiri alimuuliza Imam (as): “Ewe Husein (as) nimuadhibu?” “Hapana,” alijubu Imam (as).

Mtunzi anasema huu ulikuwa ni wema ambao Imam (as) aliuonyesha kwa mpanda ngamia lakini ni mtu huyu huyu aliyelipa kitendo hiki cha wema kwa kukata mikono ya Imam ili akwapue mkanda wake, katika giza la usiku wa 11 Muharram 61H.A.3
2. Abu Ayyub Ansaari
Abu Ayyub Ansaar alikuwa ni mmoja wa masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (saw). Mtukufu Mtume (saw) alipohama Makka kwenda Madina, makabila yote ya Madina yalimuomba akae lakini alisema:

“Sehemu nitakayokaa inategemea sehemu atakayokaa ngamia wangu.” Msafara ulipofika sehemu karibu na nyumba ya Maalik Ibn Najjar, ambayo baadaye ilikuja kuwa mlango wa msikiti wa Mtume, ngamia alikaa chini kupumzika. Lakini muda mfupi baadaye alisimama tena na akaanza kutembea, kisha akarudi sehemu ile ile aliyokuwa amekaa awali.

Watu wakaanza kumuendea Mtukufu Mtume (saw) na kumuomba akawe mgeni wao. Alipoona hivi, Abu Ayyub alinyanyua mfuko uwekwao kwenye siti ya ngamia wa Mtukufu Mtume (saw) kutoka kwenye mgongo wa ngamia na akaupeleka nyumbani kwake.

Mtukufu Mtume (saw) alipobaini kuwa mfuko wake haupo, aliuza “Nini kimetokea juu ya mfuko wangu?” Wale waliokuwepo walimjulisha kwam- ba Abu Ayyub alikuwa ameupeleka nyumbani kwake.

Mtukufu Mtume (saw) akasema: “Mara nyingi mtu anatakiwa aambatane na mzigo wake” kisha akaelekea kwenye nyumba ya Abu Ayyub na akakaa hapo hadi nyumba katika eneo la msikiti zilipokuwa zimejengwa.

Awali, Mtukufu Mtume (saw), alikuwa akiishi katika chumba cha chini wakati Abu Ayyub aliishi juu ghorofani lakini baadaye aliomba: “Ewe Mjumbe wa Allah! Sio sawa kwamba wewe ukae chini, wakati sisi tunaishi ghorofani juu: itafaa zaidi ikiwa utahamia juu.”

Mtukufu Mtume (saw) alikubali na akaomba vitu vyake vihamishiwe juu. Abu Ayyub alikuwa pamoja na Mtukufu Mtume (saw) na alishiriki katika vita kama Badr na Uhud, akipigana dhidi ya maadui wa Uislam akionye- sha ushujaa na ukakamavu wa kusifika.

Usiku akiwa anarudi nyumbani baada ya vita vya Khaibar, Abu Ayyub alikesha usiku kucha akilinda hema la Mtukufu Mtume (saw). Asubuhi ilipopambazuka, Mtukufu Mtume (saw) aliuliza: “Ni nani yupo nje huko?”

“Ni mimi, Abu Ayyub”, lilitoka jibu.

Mtukufu Mtume (saw) alisema mara mbili, “Allah akurehemu!”

Hivyo, Abu Ayyub kwa kupitia wema wake kwa Mtume, kwa fedha zake na roho yake, alinufaika na dua hii ya Mtukufu Mtume (saw).4
3. Malipo Ya Mashairi
Siku moja ya Nawruz, Mansur Dawaaniqi, Khalifa kutoka ukoo wa Bani Abbasi aliyechukua ukhalifa baada ya kaka yake Abu al-Abbas Saffaah, alimuamuru Imam Musa Kadhim (as) kuhudhuria katika Eid ya Nawruz, ilifanywa hivi ili watu waje na kumsalimia na kumpa zawadi ambazo ali- paswa kuzikubali.

Imam (as) alimuambia Mansur, “Nawruz ni Eid ya kimila ya Wairan haku- na kilichotajwa juu yake katika Uislam”

Juu ya hili Mansur alijibu “kitendo hiki kina hamasa za kisiasa na inakusudiwa kuwafurahisha askari wangu. Ninakuweka chini ya Mola mkuu kuwa ukubali ombi langu na uhudhurie katika mkusanyiko huo.” Imam (as) alikubali na akawasili katika hadhara ya Majenerari wa jeshi, Mamwinyi na watu wa kawaida walipita mbele yake wakamsalimia na kumpa zawadi zao.

Wakati huo huo Mansur alikuwa amemuamuru mmoja wa watumwa wake akae karibu na Imam akitunza kumbukumbu ya fedha na zawadi zina- zowasilishwa kwake.

Mtu wa mwisho kuja kumuona Imam (as) alikuwa ni mzee aliyemuambia: “Ewe mtoto wa Mjumbe wa Allah! Mimi ni mtu masikini na sina fedha za kukununulia zawadi, lakini zawadi yangu kwa leo ni aya tatu za shairi la maombolezo, ambazo babu yangu amezitunga kwa ajili ya babu yako, Husein Ibn Ali (as).” Baada ya kusema hayo akasoma aya hizo.

Imam (as) alishukuru kwa kusema; “Nimeikubali zawadi yako” kisha akamsomea dua mtu huyo. Kisha akamgeukua mtumwa na kumuagiza “Nenda kwa Mansur mjulishe juu ya zawadi hizi na muulize zifanyweje.” Mtumwa alifanya kama alivyoagizwa na aliporudi, alimuambia Imam (as): “Khalifa amesema: “Nimekupa wewe (Imam Musa Kadhim) kama zawadi, zitumie utakavyo.”

Imam (as) alimuambia yule mzee: “Chukua utajiri huu na zawadi hizi, kwani ninakupatia vyote hivi kama zawadi.”5
4. Yusuf (As) Na Nduguze
Miaka kadhaa baada ya tukio la nduguze Yusuf (as) kumchukuwa kwa udanganyifu nje ya mji. Kumpiga na kumtupa kisimani na hivyo kumlaz- imisha baba yao kulia mfulululizo na kusonononeka kwa hasara yake, wale ndugu walisikia kuwa Yusuf amekuwa Mfalme wa Misir. Wao na baba yao walienda kuonana naye.

Sentensi ya kwanza kabisa ambayo Yusuf aliitamka alipowaona, ilikuwa:

“Na kwa hakika alikuwa mwema kwangu aliponitoa gerezani…”6

Inavyooneka ni kwa sababu ya tabia njema kwamba Yusuf aliepuka kutaja matatizo aliyoyapata; kwanza kutupwa kisimani, kisha kufanywa kwake mtumwa na kisha matukio yasiyofurahisha, aliyokumbana nayo kutokana na matendo ya nduguze. Hakutaka kufufua kumbukumbu hizo chungu, ambazo zingewasababishia fedheha na mfadhaiko.

Kisha aliongeza, “Ni shetani aliyewashawishi ndugu zangu kunifanyia yale matendo yasiyofaa, kunitupa kisimani na kunitenganisha na baba yangu; hata hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu alinifanyia wema kwani aliyafanya matendo hayo kuwa ni njia ya kuipatia familia yetu utukufu na heshima!”

Kuyahusisha matendo ya kidhalimu na nduguze na shetani na kumuona yeye (shetani) kama mhusika mkuu wa uhalifu wa nduguze, ulikuwa ni mfano mwingine wa ukarimu na moyo wa kusamehe wa Yusuf. Hivyo ali- wakinga dhidi ya mfadhaiko na akawaacha na fursa ya kuomba msamaha kwa matendo yao.

Alisema:

لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ ۖ {92}

“Hakutakuwa lawama dhidi yenu (kuanzia) siku hii (Quran 12:92)

Kaeni kwa amani juu yangu, kwani nimewasamehe na nimeyasahau yote yaliyotokea, na kwa niaba ya Mwenyezi Mungu pia, ninaweza kuwapeni habari njema na tafuteni kutoka kwake ili Allah awasamehe na Yeye ni Mwenye rehema kuliko wenye rehema wote.7 ?

نَّهُ مَنْ يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ
“Kwa hakika yule ajichungaye (dhidi ya maovu) na akawa na subira (hulipwa) kwani kwa hakika Allah huwa hapotezi ujira wa wafanyao wema.” (Qur’an 12:90)

Neno la mtunzi: Somo ambalo Hadhrat Yusuf (as) alimfundisha kila mmoja ni lile la kuonyesha wema na ukarimu kama majibu ya tabia mbaya, na tunataraji sisi pia tunaweza kufanya hivyo kwa ndugu zetu katika Iman, Inshaallah!
________________________
1. Qur’ani Tukufu Suratu’l-Nahl 16:128

2. Jawaame al–Hikayaat, uk. 24, Namunah- e ma’arif, Juz. 1, uk. 29

3. Raahinama –e- Sa’adat, Juz. 1 uk, 36; Shajarah-e-Tuba, uk 422

4. Payghambar Wa yaraan, Juz. 1, uk. 20-27; Bihaar al –Answaar, Juz. 6, uk. 554

5. Muntahal Aamal, Juz, 2 uk.187

6. Qur’ani Tukufu Suratul Yusuf 12:100

7. Qur’ani Suratul Yusuf 12:92
Allah Mwenye hikma, amesema:

فَاعْبُدِ اللَّهَ مُخْلِصًا لَهُ الدِّينَ {2}

“Hivyo muabuduni Allah (peke yake) mkiwa waaminifu Kwake kati- ka dini.” (Quran 39:2)

Imam Ali (as) alisema: “Fanya matendo yako kwa unyofu, kwani (ukifanya hivyo) hata kidogo kitakutosha.1

Maelezo mafupi:

Unyofu ni ufunguo wa kukubaliwa amali zote. Mtu ambaye amali zake zimekubaliwa na Allah hata ziwe ndogo kiasi gani, ni mtu mnyofu na mtu ambaye amali zake zimekataliwa na Allah, licha ya wingi wake, sio miongoni mwa watu wanyofu.

Mtu mnyofu hujitahidi kuitakasa roho yake kutokana na maovu na hujibadilisha kufanya amali njema na kudumisha (unyofu wa) nia ili Allah azikubali amali zake.

Kiwango cha nia, maarifa na matendo yanahusiana na utakaso wa kiroho na usafi (wake), na kama mtu mnyofu angezingatia kikamilifu nafsi yake ya ndani, angeitambua dhana halisi ya upweke wa Allah. Kiwango cha chini kabisa cha unyofu ni wakati mtu anapofanya jitihadi kwa kadiri ya uwezo wake wote, akiwa hatarajii malipo kwa matendo yake wala hayapi umuhimu wowote.2
1. Watu Watatu Katika Pango
Mtukufu Mtume (saw) amesimulia:

“Watu watatu kutoka katika kabila la Bani Israil walikusanyika na wakaan- za safari, walipokuwa njiani, mawingu yalikusanyika na mvua kubwa ikaanza kunyesha na hivyo wakatafuta hifadhi katika pango lililokuwa karibu.

Ghafla jiwe kubwa lilibilingika na kuziba lango la pango, (na hivyo) kuwakwamisha watatu hao ndani na kuubadili mchana kuwa usiku kwa giza. Walikuwa hawana jingine la kufanya isipokuwa kumgeukia Allah kwa msaada.

“Tutumie matendo yetu ya unyofu kama njia ya kupata nusra kutokana na tatizo hili,” alishauri mmoja wao. Wengine wote walikubaliana na ushauri huo. Mmoja wao alisema “Ewe Mola! Unajua kuwa nina binamu yangu anayevutia sana kabisa na kwamba nilivutiwa naye na kumpenda sana, siku moja nilipomkuta akiwa peke yake, nilimchukua na nilitaka kukidhi matamanio yangu ya kimwili, aliposema: ‘Ewe binamu yangu! Muogope Allah na usiuharibu ubikra wangu.’

Niliposikia hivi nilivyunjilia mbali matamanio yangu ya kimwili na nikaamua kutofanya kitendo kiovu. Ewe Mola! Ikiwa kitendo changu hicho kilitokana na unyofu wa kweli na kwa nia ya kupata radhi Zako tu, tunusuru kutokana na huzuni na adhabu. Ghafla waliona kwamba lile jiwe limesogea kidogo, likiruhusu mwanga hafifu kuingia ndani ya pango.

Mtu wa pili alisema: “Ewe Mola! Unajua kwamba nilikuwa na baba na mama, walikuwa wazee sana kiasi kwamba miili yao ilikuwa imepinda kutokana na umri uliopindukia, na kwamba nilikuwa nikiwahudumia kila mara. Usiku mmoja nikiwa nimewaletea chakula, nilibaini kwamba wote walikuwa wamelala. Nilikesha usiku kucha karibu yao, na chakula mkononi, bila kuwaamsha nikihofia kuwasumbua. Ewe Mola! Ikiwa kiten- do changu hiki kilikuwa ni kwa ajili ya kupata radhi na furaha Yako, tufun- gulie njia na tupe wokovu.” Alipomaliza kauli yake, kundi lile lilibaini kuwa jiwe lile lilikuwa limesogea pembeni zaidi.

Mtu watatu aliomba: “Ewe Mjuzi wa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri! Unajua mwenyewe kwamba nilikuwa na mfanyakazi aliyekuwa akinifanyia kazi. Mkataba wake ulipokuwa umefikia mwisho, nilimkabidhi ujira wake, lakini hakuridhika na alitaka zaidi na katika hali ya kutoridhi- ka na kutofurahi, aliondoka. Nilitumia ujira wake kununulia mbuzi, na nil- imhudumia tofauti, na punde nikawa na kundi la mbuzi. Baada ya kipindi fulani, yule mfanyakazi alinijia akitaka ujira wake na nikamuonyesha kundi la mbuzi.

Awali alifikiri ninamdhihaki, lakini baadae alipotambua umakini wangu alichukua kundi lote (la mbuzi) na kuondoka.3 Ewe Mola! Ikiwa kitendo hiki kilisukumwa na unyofu na kilikuwa kwa ajili ya kutaka radhi Zako, tuokoe katika mkwamo huu”

Kufikia hapo jiwe lote liliondoka katika lango la pango na wote watatu wakatoka, wakiwa na furaha na msisimko, na wakaendelea na safari yao.4
2. Ali (As) Katika Kifua Cha Amr
Amr Ibn Abd Wuud alikuwa ni mpiganaji ambaye, katika vita alikuwa ni sawa na askari 1000. Katika vita vya Ahzaab, aliwapa changamoto askari wa Kiislamu kupigana naye, lakini hakuna hata aliyekuwa na ujasiri wa kusimama mbele yake hadi Imam Ali (as) alipokwenda mbele ya Mtukufu Mtume (saw) na kuomba ruhusa ya kupigana naye.

Mtukufu Mtume alimuambia Ali (as): “Tambua kuwa huyu ni Amr Ibn Abd Wuud!” Imam Ali (as) kwa unyenyekevu alisema “(Na) mimi ni Ali Ibn Abi Talib,” na kisha akaenda katika uwanja wa vita na kusimama mbele ya Amr.

Baada ya mapambano makali, Imam (as) hatimaye alimuangusha chini na akakaa juu ya kifua chake. Walipoona hivi, jeshi zima la Waislamu lilimuomba Mtukufu Mtume (saw): “Ewe Mjumbe wa Allah, muamuru Ali (as) amuue Amr mara moja!”

“Muacheni kwani anayajua matendo yake vizuri zaidi kuliko mwingine yeyote,” alijibu Mtukufu Mtume (saw).

Ali (as) alipokuwa amekikata kichwa cha Amr, alikileta kwa Mtukufu Mtume (saw) ambaye alimuuliza “Ewe Ali! Ni nini kilichokufanya usite kabla ya kumuua Amr?

Akasema, “Ewe Mjumbe wa Allah! Nilipokuwa nimemwangusha chini, alinikashifu matokeo yake nikapatwa na hasira. Nilihofia kuwa kama ningemuua katika hali ile ya hasira, ingekuwa (nimemuua) kwa ajili ya kijifariji na kuiridhisha roho yangu. Hivyo niliondoka juu yake mpaka hasira yangu ilipokwisha na nikarudi kukitenganisha kichwa chake kutoka katika mwili kwa ajili ya furaha ya Allah na kwa ajili ya kumtii Yeye.”

Ilikuwa ni kwa sababu ya unyofu na pigo lenye thamani kwa upande wa Imam Ali (as) kwamba Mtukufu Mtume (saw) alisema: “Dhoruba la upan- ga wa Ali katika siku ya vita vya Khandaaq ni bora kuliko ibada ya wanadamu wote na majini.”5
3. Shetani Na Mchamungu
Katika kabila la Bani Israil, alipata kuishi mchamungu mmoja. Siku moja watu walimjulisha kuwa katika sehemu fulani, kulikuwa na mti uliokuwa ukiabudiwa na watu wa kabila hilo. Aliposikia hivi, aliruka kwa hasira, akachukuwa shoka yake na kuondoka kwenda kuukata mti ule.

Ibilisi, akatokea mbele yake kwa sura ya mtu mzee, alimuuliza, “Unakwenda wapi?” alijibu “Nina kusudia kukata mti ambao unaabudiwa ili badala yake watu wamuabudu Allah.”

“Jizuie mpaka utakaposikia nitakayoyasema.” Ibilisi alisema kumuambia yule Mchamungu. Yule Mchamungu akamuambia aendelee kusema. Ibilisi aliendelea: “Allah ana mitume, wake kama ingekuwa ni muhimu kuuan- gusha mti angekuwa amewatuma kuja kufanya kazi hiyo.” Lakini, Mchamungu hakukubaliana na Ibilisi na akaendelea na safari yake.

“Kwa vyovyote vile sitakuruhusu” ibilisi alisema kwa hasira na akaanza kupigana mieleka na mtu yule, katika mpambano huo mchamungu alimb- waga ibilisi chini. “Subiri nina kitu cha kukuambia” alisihi ibilisi “Sikiliza! Wewe ni mtu masikini kama ungekuwa na mali ambayo kwayo ungetoa zaka kwa waumini wengine ingekuwa bora zaidi kuliko kukata mti. Ukijizuia kukata mti, nitaweka dinari mbili chini ya mto wako kila siku.”

Mchamungu akasema huku akiwaza: “Ikiwa unasema ukweli, nitatoa dinari moja kama sadaka na nitaitumia dinari nyingine.

Hili ni bora kuliko kukata mti katika hali yoyote, sijatumwa kufanya kazi hii wala mimi sio Mtume mpaka nijitwishe mzigo wa huzuni na mashaka yasiyo ya lazima.” Hivyo alikubaliana na ombi la ibilisi na akamuacha.

Kwa siku mbili, alipokea dinari mbili na akazitumia, lakini katika siku ya tatu, hapakuwa na dalili ya fedha. Akiwa ameudhika na kusononeka, akachukua shoka yake akatoka kwenda kukata ule mti.

Njiani alikabiliana na shetani, aliyemuuliza: “Unaelekea wapi?

“Ninakwenda kukata ule mti.”

“Kwa vyovyote huwezi kwenda kufanya hivyo” alisema shetani.

Kwa mara nyingine tena walianza kupambana lakini mara hii ibilisi alimzi- di nguvu na akamwangusha chini, (kisha) akamuamuru, “rudi nyuma sivyo nitatenganisha kichwa na kiwiliwili chako.” Mchamungu alisema, “Niache na nitarudi, lakini niambie ilikuwaje nikaweza kushinda katika tukio la awali?”

Ibilisi alijibu: “Katika tukio lile umetoka kwa ajili ya Allah na ulikuwa na ikhlasi katika nia yako na matokeo yake Allah akanidhoofisha kwa ajili yako, lakini safari hii ulikasirika kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe na dinari zako na hivyo nikaweza kukuzidi nguvu.”6
4. Siri Ya Mtumwa Muaminifu
Sa’eed Ibn Musayyab anasimulia: “Mwaka mmoja, kulikuwa na njaa kali na hivyo watu walikusanyika pamoja ili kuomba dua kwa ajili ya mvua. Nilitazama hivi na macho yangu yakamuangukia mtumwa mweusi aliyekuwa amejitenga na umati wa watu na akaibukia kwenye kilele cha kilima kidogo. Nilikwenda katika uelekeo alipokuwa na nilipomkaribia, nilibaini kwamba midomo yake ilikuwa ikijongea (akisoma) dua. Alipomaliza tu dua yake, wingu lilikusanyika angani. Alipoona wingu, mtumwa alimsifu Allah na akaondoka. Mara tu mvua ikatupiga sana mpaka tukafikiri kuwa tunaweza kuangamia. Nilimkimbilia mtumwa yule nikaona kwamba ameingia katika nyumba ya Imam Sajjad (as). Niliwasili mbele ya Imam (as) na nikasema:

“Ewe bwana wangu! Katika nyumba yako kuna mtumwa mweusi; tafad- hali niuzie” Akasema, “Ewe Sa’eed! Kwa nini badala yake nisikupe kama zawadi?” Na akamuamuru mkuu wa watumwa kuwaleta watumwa wote mbele yake. Walipokuwa wamekusanyika, nilibaini kuwa mtumwa mweusi hakuwa miongoni mwao. Nikasema, “Ninayemtaka hayupo hapa.” Imam (as) akasema hakuna mtumwa aliyebaki isipokuwa mmoja. Kisha akaamuru akaletwe, mtumwa huyo alipoletwa mbele yangu niliona kuwa ndiye mtu mwenyewe niliyekuwa nikimtafuta na hivyo nikasema: “Huyu ndiye ninayemhitaji!”

“Ewe mtumwa! Kuanzia sasa, Sa’eed ni bwana wako na nenda naye” aliagiza Imam (as). Mtumwa akanigeukia na kusema, “Ni nini kilichokusukuma unitenganishe na bwana wangu?” Nikajibu, “Niliposhuhudia dua yako ya mvua ikijibiwa nilitamani kukumiliki.” Aliposikia hivi, mtumwa alinyoosha mikono yake kwa ajili ya dua na akigeuzia uso wake angani akiom- ba: “Ewe Mola wangu! Hii ilikuwa ni siri baina yangu na wewe. Sasa kwa vile umeivujisha, nipatie kifo na unichukue kwako.”

Imam (as) na wote waliokuwepo walibubujikwa na machozi kutokana na hali ya mtumwa, huku nikitokwa na machozi nilitoka nje ya nyumba. Nilipofika nyumbani kwangu tu, mjumbe wa Imam (as) alifika na kusema, “Njoo kama unataka kushiriki katika mazishi ya sahibu yako.” Nilirudi nyumbani kwa Imam (as) pamoja na yule mjumbe na kukuta mtumwa ameshafariki.7
5. Ombi La Nabii Musa (As)
Nabii Musa alipata kumuomba Allah:

“Ewe Mola! Ni utashi wangu kumuona kiumbe wako aliyejitakasa kwa ajili ya ibada Yako na ambaye hajachafuliwa katika utii wake Kwako” Aliambiwa: “Ewe Musa! Nenda katika fukwe za bahari fulani ili nikuonyeshe unachotaka kukiona”

Nabii Musa alikwenda mpaka akafika karibu na bahari. Alipotazama pem- beni, aliona kuwa tawi la mti lililokuwa limeinamia juu ya maji, alikuwa amekaa ndege, akiwa amezama katika kumdhikiri Allah. Musa alipo- muuliza ndege (habari zake), ndege alisema: “Tangu Allah aliponiumba, nimekuwa katika tawi hili, nikimuabudu Yeye na dhikiri. Kwa kila dhikiri yangu moja hutokea dhikiri 1000 nyingine, na furaha ninayoipata kutokana na dhikiri ya Allah hunipatia virutubisho.”

“Je unatamani kitu chochote katika ulimwengu huu?”Aliuliza Musa (as). “Ndio. Ninatamani sana kuonja tone moja la maji kutoka kwenye bahari hii.” alijibu ndege Musa (as) akasema kwa mshangao “Lakini hakuna umbali mkubwa kati ya mdomo wako na maji! Kwa nini hutumbukizi mdomo wako ndani (ya maji) na kunywa?” Ndege akajibu, “kutokana na hofu kwamba isije ikawa raha inayotokana na maji ikanifanya nisahau raha ya kumdhukuru Mola wangu.” Aliposikia hivi, Nabii Musa (as) alishika kichwa chake kwa mshangao mkubwa.8
________________________
1. Jaame’ al Saadaat Juz. 2, uk. 404

2. Tadhkirah al Haqaaiq, uk 73

3. Katika kitabu Mahaasim imetajwa kwamba ujira wake ulikuwa ni nusu dirham lakini alipokuja kuchukua, alipewa mara 18,000 zaidi!

4. Naamunah-e-ma’arif , Juz.1, uk. 53; Farajun Ba’d al shiddah, uk 23; mahaasin e- Barqi, Juz. 2, uk 253

5. Pand –e- Tarikh, Juz 5, uk. 199; Anwaar al- Nu’maaniyah; Ainal –Hayaah.

6. Namunah-e-maarif, Juz. 1, uk. 54; Ihyaa al- uluum Juz. 4, uk.380; Riyadh al- Hikaaya, uk.140

7. Muntahal Aamal, Juz. 2, uk. 38; Ithbaat al- Wasiyyah (cha Maasudi)

8. Khazinah al- Jawaahir, uk. 318
Allah mwenye Hikma Anasema:

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَنْ تَابَ مَعَكَ {112}

“Kisha simama imara (Ewe Mtume wetu Muhammad) katika njia iliy- onyooka kama ulivyoamrishwa (na Mola wako) pamoja na wale waliomgeukia Allah pamoja nawe. (Quran 11:112)

Imam Sadiq (as) anasema:

“Muumini yeyote anayepatwa na balaa na kisha akafanya subira, atalipwa thawabu sawa na mashahidi 1000.”1

Maelezo mafupi:

Kuvumilia na kustahamili kunaweza kupunguza ukali wa mabalaa na mis- iba. Mtu mwenye imani huwa haonyeshi ukosefu wa subira anapo patwa na mitihani, ili imani yake isiathirike. Imesemwa: “Muumini ni imara zaidi kuliko mlima. Hii ni kwa sababu (yeye) ni imara mbele ya maadui na kuonyesha ukakamavu wakati wa mabalaa kiasi kwamba huzuni huwa haipati nafasi katika moyo wa muumini mkamilifu.

Maisha, pamoja na matatizo yake mengi, hayataleta tatizo kwa wale wenye mioyo migumu. Ni wale tu ambao hawana unyofu katika ustahamilivu wao ndio huvunjika moyo wanapopatwa na msiba hata mdogo kabisa. Na iju- likane kama dini ya Allah imetufikia leo hii, ni kwa sababu ya ustahamilivu wa Mtukufu Mtume (saw) na subira ya Imam Ali (as).
1. Familia Ya Yasir
Katika kipindi cha kwanza cha Uislamu, familia ndogo ya watu wanne na iliyokuwa inakandamizwa ilisilimu. Kila mmoja wao alionyesha kiwango cha juu cha ustahamilivu katika kukabiliana na mateso ya kikatili ya washirikini. Watu hawa wanne walikuwa ni Yasir, mkewe Sumaiyah na waoto wao wawili Ammar na Abdullah.

Yasir alisimama imara katika dini yake akisumbuliwa na kashfa za maadui, hadi hatimaye alipokufa. Mkewe Sumaiyah licha ya umri mkubwa, kwa ukakamavu alistahamili mateso ya maadui hadi hatimaye Abu Jahl alipom- patia jeraha lake la mwisho.

Hivyo Sumaiyah alikufa shahidi kutokana na kipigo katika Tumbo Lake.

Abu Jahl, mbali na kumtesa Sumaiyah mwili wake, pia alikuwa akimtesa kisaikolojia wakati (Sumaiyah) alipokuwa mzee na dhaifu. Alikuwa akimuudhi kwa kusema: “Umefuata dini ya Muhammad sio kwa ajili ya Mungu bali kwa sababu umempenda Muhammad na umetekwa na sura yake nzuri.”

Mtoto wa Yasir, Abdullah pia alipewa mateso makubwa lakini yeye pia alibakia imara. Mtoto mwingine Ammar, alikuwa akipelekwa katika jang- wa linalounguza, akivuliwa nguo na kuvishwa koti la chuma la moto kati- ka mwili wake uliounguza nusu na kulazimishwa kulala katika mchanga wa moto, na chembe chembe zake zilikuwa kama vipande vya chuma kuto- ka katika tanuri la mhunzi. Mataokeo yake vyuma vya koti la chuma vilikuwa vikipenya kwenye mwili wa Ammar na walikuwa wakimuambia “mkane Muhammad (saw) na uwaabudu Lat na Uzza,” lakini Ammar kamwe hakusalimu amri kutokana na mateso yao.

Chuma kilichoungua kiliacha alama katika mwili wake kiasi kwamba Mtukufu Mtume (saw) alipomuona Ammar alikuwa anaonekana kufanana na mtu mwenye ukoma.

Alama kama za ugonjwa huo zilionekana usoni, mikononi na katika mwili wa Ammar (na) zilifanya aonekane kama mkoma.

Mtukufu Mtume (saw) alikuwa akisema hivi juu ya familia ya Yasir: “Enyi familia Yasir! Kuweni na subira na bakieni imara, kwani bila shaka peponi ndio makazi yenu”2
2. Wewe Sio Duni Kuliko Mchwa
Amir Taimur Gurgaan, alikuwa ni mtu imara na asiyeyumba katika kila tatizo, kiasi kwamba alikuwa haogopeshwi na tatizo lolote. Alipoulizwa sababu ya sifa hii, alisema: Wakati fulani nikiwa nimewakimbia maadui zangu na nikitafuta hifadhi katika gofu, nilikuwa nikitafakari juu ya hatma yangu ghafla macho yangu yalipomuangukia mchwa mdogo na dhaifu akiwa amebeba nafaka kubwa kuliko (hata) yeye mwenyewe, akijitahidi kupanda kwenye kilele cha ukuta.

“Nilipotizama kwa makini na kuhesabu kwa usahihi, nilibaini kwamba nafaka ilianguka kutoka kwenye kucha zake mara 67 kabla ya mchwa yule hatimaye kufanikiwa kufika na nafaka ile kwenye kilele cha ukuta. Kuona jitihada hizi za mchwa kulinitia nguvu kubwa ambayo kamwe sitaisahau.” Nilisema “Ewe Taimur! Kwa namna yoyote wewe sio dhaifu kuliko mchwa. Inuka na rudi kazini. Niliinuka nikakusanya nguvu zangu hadi hatimaye nikaja kupata ujasiri nilionao.”3
3. Hadhrat Nuh (As)
Hadhrata Nuh (as) aliishi maisha marefu na magumu ambayo yalitokana na kutumia muda mwingi miongoni mwa waabudu masanamu wagumu, akijaribu kuwaondolea imani zao za uongo. Hata hivyo licha ya hilo alistahamili na kuonyesha uimara bila kujali mateso na matatizo yao.

Wakati fulani watu walikuwa wakimpiga kiasi cha kupoteza fahamu kwa siku tatu nzima huku damu zikiendelea kutoka kwenye masikio yake. walikuwa wakimkamata na kumtupa ndani ya nyumba, lakini akirudiwa na fahamu alikuwa akiomba dua:

“Ewe Mola! Waongoze watu wangu kwani hawaelewi!”

Kwa takribani miaka 950 alikuwa akiwaita watu kwa Allah, lakini watu ndio kwanza walikuwa wanazidisha uasi wao na ukaidi. Walikuwa waki- waleta watoto wao kwa Nuh (as) wakiwaonyesha na kusema:

“Enyi watoto! Ikiwa mtatokea kuishi baada yetu, kuweni waangalifu kutomfuata mtu yeyote kichaa!” Kisha walikuwa wakimuambia, “Ewe Nuh! usipoacha hutuba zako, utapigwa mawe mpaka ufe. Hawa watu wanaokufuata, ni duni na dhalili, ambao wamesikia mazungumzo yako na kuukubali wito wako bila kutafakari na kuchunguza.”

Nuh (as) alipokuwa anaongea nao, walikuwa wakitia vidole vyao masikioni na kuvuta nguo zao kichwani ili wasisikie maneno yake wala kumuona uso wake. Mambo yalifikia hali isiyovumilika kiasi kwamba Nuh (as) alikosa cha kufanya isipokuwa kuomba msaada wa Allah na hivyo aliomba dua: “Ewe Allah! Nimezidiwa nguvu, nisaidie na niepushe nao.” 4
4. Sakkaki
Siraj al-Deen Sakkaki alikuwa ni mwanachuoni wa Kiislamu na mwenyeji wa Kharazm. Sakkaki alikuwa ni mhunzi kitaaluma. Wakati fulani, akiwa ametengeneza boksi dogo na laini la chuma kwa jitihada kubwa na matatizo, aliamua kulipeleka kwa mfalme wa wakati huo.

Mfalme na mawaziri waliipenda kazi ile lakini wakati amesimama akisubiri ujira wake, mwanachuoni aliingia katika jumba la kifalme, ambapo kila mmoja alimheshimu na kukaa mbele yake kwa kumtukuza na heshima. Sakkaki alivutiwa sana na akuliza ni nani alikuwa. Alijulshwa kuwa alikuwa ni mmoja wa wanachuoni wa zama hizo.

Sakkaki alisononeshwa na asili ya taaluma yake na (hivyo) akaamua kutafuta elimu. Alikuwa na umri wa miaka 30 alipokwenda shuleni na kuelezea haja yake ya kupata elimu. Mwalimu wa shule alimuambia: “Katika umri wako, ninatia shaka ikiwa unaweza kupata maendeleo yoyote, nenda zako na usipoteze wakati wako bila sababu.”

Lakini baada ya kusisitiza sana, Sakkaki alipata ruhusa na kutafuta elimu. Kumbukumbu yake ilikuwa dhaifu sana, wakati fulani, mwalimu wake alimuambia ahifadhi hukumu ifuatayo ya kidini: “ngozi ya mbwa hutaharika kwa kusindikwa;” lakini siku inayofuata alipotakiwa kuisoma mbele ya mwalimu wake, alisema: “Mbwa alisema: Ngozi ya mwalimu hutaharika kwa kusindikwa.” Waliposikia hivi wanafunzi na mwalimu waliangua kicheko na kumkejeli.

Miaka kumi ya jitihada haikutoa matokeo yoyote kwa Sakkaki, ambaye alihuzunika na kukata tamaa. Alikwenda milimani lakini alipokuwa kitem- bea huko, alifika sehemu ambapo matone ya maji yalikuwa yakidondokea kwenye jiwe kutokea juu. Udondokaji mfululizo wa maji ulikuwa umechimba shimo kwenye jiwe. Sakkaki alilichunguza jiwe kwa muda kisha akajisemea:

“Kwa hakika moyo wako sio mgumu kama mwamba huu. ukistahamili, hatimaye utafanikiwa. Alipokuwa ameazimia juu ya hili, alirudi shuleni kwake na kuanzia katika umri wa miaka 40, alianza kusoma kwa bidii kubwa zaidi, nguvu na subira.

Sakkaki hatimaye alifikia hatua ambayo katika fani ya sarufi ya Kiarabu na fasihi, wanazuoni wa zama zake walikuwa wakimtizama kwa heshima kubwa. Aliandika kitabu Miftaah al- U’luum, ambacho kina matawi kumi na mbili ya fasihi ya kiarabu na kinaonekana kuwa ni moja ya kazi kubwa na nzuri kabisa katika somo hili.5
________________________
1. Jaamae’ al –Saadaat, Juz.3, uk. 404

2. Hikaayaat -ha- e- Shanidan, Juz.5, uk. 25, Tafsir al-Manaar, Juz. 2, uk . 376

3. Namunah –e- Maarif, Juz,1 uk. 174; Akhlaq –e- Ijtmaae uk, 41

4. Taarikh –e- Anbiyaa, uk. 48-52

5. Dastaan-ha-e-Maa, Juz.3, uk45
Mwenyezi Mungu Mwenye hekma, amesema: “Na ikiwa pande mbili za waumini zitakuwa katika ugomvi, rejesheni amani baina ya pande mbili hizo.” (Suratul Hujurat; 49: 9)

Imam Sadiq (a.s) anasema:

“Kupatanisha baina ya watu wawili (wanaozozana) ni bora zaidi kwangu kuliko kutoa dinari mbili katika sadaka.”1

Maelezo Mafupi:

Moja ya matendo ya wajibu yanyotuwajibikia ni kuzikagua na kuzireke- bisha roho zetu. Mpaka mtu atakapojirekebisha yeye mwenyewe ndipo atakapoweza kuleta marekebisho kwa wengine. Kujaribu au kufanikiwa kuleta usuluhishi baina ya ndugu katika imani, ndugu, au majirani, ni jambo linalopendwa sana na Mwenyezi Mungu.

Kwa lengo la kuimarisha umoja na maelewano badala ya utengano na mifarakano ni muhimu kufanya kila jitihada kuleta suluhu. Kwa kweli katika baadhi ya kesi, huruhusiwa (hata) kutumia uongo mweupe. Wakati mwingine hufikia hata kuwa wajibu ili chuki ife na faraka iishe.
1. Utaratibu Wa Kusuluhisha
Wakati fulani, enzi za Imam Sadiq (a.s), Abu Hanifa, mtawala wa Hajjaaj, alikuwa na ugomvi na mkwe juu ya urithi. Mufadhal Ibn U’mar Kufi, mmoja wa masahaba wa karibu wa Imam Sadiq (a.s) alipita kwenye ugomvi huo. Aliposikia mabishano hayo alisimama na kusema kuwaambia hao wanaume wawili: “Twendeni nyumbani kwangu.” Walifanya kama alivyoomba. Walipofika nyumbani aliingia ndani na muda mfupi baadaye alitoka na mfuko wenye dirhamu mia nne alizowapatia (hao) watu wawili na akawasuluhisha. Kisha akaeleza: “Hizi sio fedha zangu bali ni za Imam Sadiq (a.s). Alinielekeza: “Wakati wowote utakapoona shia wetu wawili wakizozana juu ya fedha, wapatie fedha hizi na wasuluhishe.”
2. Uchukue Tahadhari Katika Usuluhishi
Abdat Malik amesema: Ulizuka mzozo baina ya Imam Baqir (a.s) na baad- hi ya watoto wa Imam Hasan (a.s). Nilimwendea Imam na nikamuomba niingilie katika jambo hilo ili niwasuluhishe, lakini Imam (a.s) alishauri: “Usiseme neno katika mzozo huu kwani tatizo letu ni kama lile la mzee kutoka katika Bani Israel, aliyekuwa na mabinti wawili. Mmoja wao ali- olewa na mkulima wakati mwingine aliolewa na mfanyakazi. Wakati fulani aliamua kuwatembelea. Kwanza alimtembelea binti yake aliyekuwa mke wa mkulima na alipofika katika nyumba yake, aliuliza juu ya afya yake, binti alisema: “Baba mpendwa, mume wangu amelima eneo kubwa la ardhi na kama mvua ingenyesha tungekuwa ni matajiri wakubwa katika Bani Israil yote.” Kisha alipokwenda kwenye nyumba ya binti mwingine, ambaye mume wake alikuwa ni mfanyakazi, aliuliza juu ya afya yake. Binti alisema “Baba mpendwa, mume wangu amefinyanga vyungu kwa kiasi kikubwa na kama Mwenyezi Mungu angezuia mvua mpaka vyungu vikauke, tungekuwa matajiri kuliko Bani Israil wote.” Alipoondoka kuto- ka kwenye nyumba ya binti yake wa pili, aliomba: “Ewe Mungu! Fanya kama unavyoona inafaa, kwani katika hali hii, siwezi kumuombea yeyote kati yao.”

Kisha Imam akamniambia, “Wewe pia huwezi kuingilia katika jambo hili. Kuwa mwanagalifu, usije ukaonyesha utovu wa nidhamu kati- ka upande mmojawapo. Jukumu lako kwetu, kwa ababu ya uhusiano wetu na Mtukufu Mtume, ni kututendea tofauti na kwa heshima.” 2
3. Malipo Ya Usuluhishi
Fudhail ibn A’yyadh amesema: Mtu mwenye sononeko la moyo alichukua kamba ambayo mke wake alikuwa ameisokota kwenda kuiuza sokoni ili kujinusuru yeye mwenyewe na familia yake kutokana na njaa. Baada ya kuiuza kwa dirhamu moja, alikusudia kununua mkate alipokutana na watu wawili wakigombana na kurushiana makonde kwa sababu ya dirhamu moja. Mtu (yule) alisogea mbele akawapa dirhamu moja na kusuluhisha baina yao. Kwa mara nyingine tena, akiwa hana kitu mkononi, alikwenda nyumbani na kusimulia tukio zima kwa mkewe. Mkewe alifurahi kwa mwenendo wake. Alitafuta ndani ya nyumba, akapata gauni kuukuu ambayo alimkabidhi mumewe, ili aiuze na kupata chakula.

Yule mtu alilipeleka gauni sokoni lakini hapakuwa na mtu aliyekuwa tayari kulinunua. Alipotazama pembeni alimuona mtu mwenye samaki mikononi mwake. Alimwendea yule mtu na kusema, “Tubadilishane bidhaa. Nipe samaki wako nitakupa gauni langu.” Muuza samaki alikubali na yule mtu alirudi nyumbani na samaki. Mke wake alikuwa akijishughulisha na usafishaji wa samaki, wakati ghafla kitu cha thamani kilipotoka tumboni mwa samaki. Alimkadhi mumewe kitu hicho ili akakiuze sokoni. Mumewe alikiuza kwa bei nzuri sana na alirudi nyumbani lakini kabla hajaingia ndani mtu fukara alikuja kwenye mlango na kusema, “Nipeni kutokana na hivyo alivyokupeni Mwenyezi Mungu.” Mara tu mtu yule aliposikia wito ule, alileta fedha zote na akamtaka maskini achukue fedha anazotaka. Muombaji alichukua fedha kiasi na akaanza kuondoka. Lakini alikuwa ametembea hatua chache tu wakati aliporudi na kusema: “Mimi sio masiki- ni. Nimetumwa na Mwenyezi Mungu na ninapaswa kukujulisha kuwa fedha ulizopata ni ujira wako kwa kuwasuluhisha watu wawili waliokuwa wakigombana.” 3
4. Mirza Jawad Agha Maliki
Juu ya mwanazuoni Mirza Jawad Adha Maliki (aliyekufa mwaka 1343A.H.), imerekodiwa kwamba katika hatua za awali za kutafuta utaka- so wa kiroho na baada ya kuwa amesoma chini ya mwalimu wake, mwanazuoni mkubwa Mulla Hasainquli Hamadani (aliyekufa mwaka 1311A.H.), kwa miaka miwili, alilalamika kwa mwalimu wake? “Katika kutafuta kwangu utakaso wa kiroho, bado sijaweza kupata kitu chochote”. “Jina lako ni nani?” aliuliza mwalimu. Akajibu “Wewe hunitambui mimi? Mimi ni Jawad Maliki Tabrizi.”

Hasainquli Hamadani aliuliza, “Je una uhusiano na familia fulani na fulani ya Maliki?” Mirza Jawad alikubali na kisha akaanza kuzungumza kwa kuwakosoa. “Wakati wowote utakapofika wa wewe kuwawekea viatu vyao mbele yao ili wavae, (ambacho unakiona ni kitendo duni na dhalili), mimi binafsi nitakuja kukuongoza,” alishauri Husainquli Hamadani.

Siku iliyofuata Mirza Jawad alipokwenda darasani alikaa nyuma ya wana- funzi wote na pole pole alianza kuzoea na kuwa na tabia ya kirafiki na wanafunzi wa familia ya Maliki wanaoishi Najaf. Iliendelea hivi mpaka ikafikia hatua ambapo alikuwa hata akiwawekea viatu mbele yao ili wavae. Ndugu wanaoishi Tibrizi walipolijua hili, chuki na faraka iliyokuwepo miongoni mwa wanafamilia hao, na amani ikaanzishwa miongoni mwao.

Baadaye Mirza Jawad alimwendea mwalimu wake, ambaye alimwambia, “Hakuna maelekezo mapya kwa ajili yako (Baada ya kuwasuluhisha wana ndugu wa familia ya Maliki). Endelea kufuata utaratibu huu wa sheria na nufaika kutokana nayo.

Neno la Mwandishi: Kwa bahati, kitabu Miftaah al-Falaah cha marhum Sheikh Bahaai ni kitabu bora kabisa cha kufuata.

Polepole Mirza aliendelea katika utafuaji wake. Alikuja katika Hauza ya Qum ambapo alianza kuwafundisha na kuwaongoza wanafunzi katika fani ya utakaso wa kiroho. Idadi kubwa ya watu, watu wa kawaida na wasomi walinufaika kutokana naye na mafundisho yake.
5. Ushauri Wa Waziri Wa Ma’mun
Wakati fulani, Ma’mun Khalifa wa ukoo wa Abbas alichukizwa na Ali Ibn Jahm Saami mshairi wa baraza, na akiwa katika shinikizo la hasira aliwaa- muru watumishi wake: “Muueni na mnyang’anyeni mali zake zote.”

Waziri wa Ma’mun, Ahmad Ibn Abi Dawood, katika njia ya kusuluhisha alimwendea na kuomba, “Ikiwa utamuua, mali zake tutamnyang’anya nani?” “Kutoka kwa warithi wake” alijibu Ma’mun. Ahmad akasema, “Katika hali hiyo, khalifa hatokuwa amemnyang’anya mali zake (Ali) bali zile za warithi wake, kwani baada ya kifo chake, atakoma kuwa mmiliki wa mali zake. Na kuchukua mali ya mtu kwa sababu ya kumwadhibu mwingine ni kitendo cha dhulma, ambacho hakifai kwa wadhifa wa khalifa.”

Ma’mun akasema, “Vizuri, kama mambo yako hivi, basi mfunge gerezani, pokonya mali zake na kisha muue.”

Ahmad aliondoka, akamuweka Ali Ibn Jahm gerezani na akamshikilia akiwa hai mpaka hasira ya Ma’mun ilipokwisha. Ma’mun alimsamehe Ali Ibn Jahm na akamsifu waziri kwa mwenendo wake

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ