Rafed English

Maadili Ya Islam

Maadili Ya Islam by : Amiraly M.H. Datoo

 

Katika Qur'rani Tukufu, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:

"Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo safi" (26:89)

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

Imenakiliwa kutoka kwa Imamu Sadique (a.s) kuwa: "Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile ila Allhah (s.w.t) tu"

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allhah tu.

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Mtumfu (s.a.w.w.) ambamo twaambiwa: "Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba yake, mama yake, watoto wake mali yake na hata kuliko maisha yake."

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah (s.w.t.) na wale wapendwao kwa ajili ya Allah (Mtume na Ahali yake)
Sharti lingine la moyo au Nafsi ni 'kutubu' na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Mwenyezi Mungu.

"... Na anayemuogopa ( Mwenyezi Mungu Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa m oyo ulioelekea ( kwa Mwenyezi Mungu)." (50:33)

Kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah (s.w.t) kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah (s.w.t.) imo ndani yake thabiti. Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Mwenyezi Mungu yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah na wala haitorudi kamwe kwa Allah.
Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur'rani inatuambia:

"... Anayemuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake"(64:11)

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah (subahana wa Tala), yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yale yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.
Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni "kuridhika. Qur'an:

" Sikiliza: Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. "(13:28)

Na vile vile mwishoni mwa sura al-Fajr twaabiwa (89:28)

"Ewe nafsi yenye kutua"!

"Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika ..."

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah (swt) tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti.

Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza mghalimu na kumpotosha yeye.

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume mtukufu (s.a.w.w.) na ma - Imamu (a.s.), waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.
Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, (The virtuosly cautious self) nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na roho) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu:-

"... Anayezihishimu alama za (dini ya) Mwenyezi Mungu, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo. "(22:32)

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha "Taqwa" kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allhah (s.w.t.) na yele yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, sheriah, waumini wake Makka Ka'aba Tukufu n.k. kwa ufupi. Chochote kile kinachohusika na Mungu huwa kina kuwa na umuhimu na ta 'adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya 'taqwa'.
Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu (uvumilivu), yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah (swt)

Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Surah al Hajj:

"... waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao"(22:54)

Kwa sababu nyoyo hizi hujiimamisha chini mbele ya Mungu na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allhah s.w.t hawavunji kamwe maamrisho ya Mwenyezi Mungu na wala hazisaliti au kuzipinga.
Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au roho iliyo mtakatifu (the pure self). Katika Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akisemea nafsi, anatuambia:

"Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)" (91:9 & 10)

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwakuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele. (The person who self-become purified is assured of salvation and bliss!)
Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur'ani Tukufu inatuelezea:

"Naapa kwa siku ya Kiama. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)". (75:1-2).

Ni dhahiri kuwa iwapo Mwenyezi Mungu akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.
Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Mungu. Twaambiwa kaika Qur'ani:

" Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake" (91:8)

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- 'Nafsi halisi si' ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah (swt) yatafikia kikomo chake.

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.
Iwapo roho au nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur'ani inazungumzia kulipa kwa amana:

"Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia dhambini."(2:283)

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.
Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah (swt). Anaelezea Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu

"Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao..." (18:28)
Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho ya kungwa, inatuambia:

"Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwasababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu."

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allhah (swt) hadi kudharau na kutokubali ujumbe wake na maamrisho ya Allah ambayo Mwenyezi Mungu ambazo amewekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo moyo wake unaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho Matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athali yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimiza kwa nafsi na kushindwa kwake.
Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Qur'ani inatuambia kuwa:

"Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka. (22:46)

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah (swt) na hazimwoni Mwenyezi Mungu. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah (swt) na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.
"Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi." (2:10)

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Mwenyezi Mungu) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na akhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno.

Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa avutiwa navyo kama kambwa ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi ilikwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika sala na kutii Sheria Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa huo moyo wake umeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kisita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur'rani Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga waa moyo, i.e.., wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.
Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.

Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakubwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Mwenyezi Mungu. I.e njia iliyo nyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu

Katika Qur'ani, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Mwenyezi Mungu anatuambia:

"Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi........" (3:7)

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih au allegorical) wa aya za Qur'ani ili kuitumia Qur'ani kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.
Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili.

"... Na tukazifanye nyoyo zao kuwa ngumu" (5:13)

"... Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu" (57:16)

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!
Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu iipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya dini ya Islam kama vile kushuka kuwapo kwa Allah (swt), akhera, Unabuwa na vile vile Uimamu (a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.

"Nyoyo zao zina shaka; kwahivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao." (9:45)

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza hadi aya za Quarani na hadithi Tufuku za Mtume (s.a.w.w.) na ma -Imam (a.s.) na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).
'Kutu' ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha moyo ambavyo ni sehemu ya umuhimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza rudishwa iwepo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Mwenyezi Mungu.

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Mwenyezi Mungu kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Mwenyezi Mungu, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia nuru iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia (reflect ) kutoka na kwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa matilaba yake. Qurani ikiwa inatumbusha kuwa:

"Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma." (83:14)

Katika 'aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadithi Tukufu kuwa: "Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Kiama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka 'naomba msamaha wa Mwenyezi Mungu' chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa Hivyo inambidi kila Mwislam mmoja wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Mwenyezi Mungu azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.
Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matnedo ya madhambi bila kiasi. Katika Qurani, kuhusu kisa cha Mtume Yussuf, Nafsi inasemwa:

"Nami sijitasi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu ." (12:53)

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Nabii Yussuf. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Yussuf alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile zidi ya Yussuf. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Yussuf au ni wote vyovyote vile, Qur'an inatuambia kuwa

"Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. (12:53)

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma'asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, iliramdi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na matilaba yake; na ile nafsi elimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

Hatimaye: Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa 'Nafsi halisi na 'Nafsi ridhika' n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya "kupigwa mihuri" au 'zilizopofuka' na 'zenye maradhi' zikiwa ni kama mifano.

Hali hii inadhihiridha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ