Rafed English

Uadilifu - Amani Na Mtume Muhammad

Uadilifu - Amani Na Mtume Muhammad by : al-islam.org “Nasi hatukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu.” 21 : 107



“Nimeumchunguza yeye (Mohammad). Ni umtu anayevutia ajabu; na kwa maoni yangu, mbali na kuwa mpinga Kristo, ni lazima aitwe mwokozi wa wanadamu.”

“Nina amini kwamba endapo umtu kama huyo angeshika udikteta wa ulimwengu wa kisasa, ange fanikiwa katika kutatua matatizo yake katika namna ambayo ingeuletea ile amani na furaha inayohitajika hasa”

“Kama dini yoyote ingekuwa na fursa ya kutawala uingireza, hasha, bali Ulaya nzima katika kipindi cha miaka 100 ijayo, itakuwa ni Uislamu.”

“Siku zote nimeichukulia dini ya Mohammad katika hadhi ya hali ya juu kwa sababu ya changamoto zake za ajabu. Ndiyo dini pekee ambayo kwangu mimi ninaiona kuwa na uwezo wakuwiana mabadiliko ya kila zama za maisha ambayo inaweza kuvutia katika kila zama.”

George Barnard Shaw katika “The Genuine Islam” Juz. 11 na. 8 (1936)
Kijitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahihi kutoka Kiingereza. Ni tafsiri pana ya khutba iliyotolewa na mmoja wa wanachuoni wetu mashuhuri wa Kiislamu Sayyid Muhammad Rizvi, katika Bunge la Canada, Ottowa tarehe 20 Septemba, 2006 katika lugha ya Kiingereza. Tarjuma yake inatolewa hapa kwa faida ya ndugu zetu wazungamzaji wa Kiswhili wa Afrika ya Mashariki na pengine popote.

Sayyid Muhammad Rizvi kwa ufupi hapa anaelezea kuhusu Mtume Muhammad, uadilifu na amani katika muktadha wake wa Kiislamu. Kwa hakika wasomaji wasio na upendeleo watafaidika kutokana na toleo hili.

Tunawashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia katika utoaji wa tarjuma hii ya Kiswahili ambayo inawasilishwa hapa.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es Salaam , Tanzania
Ninaanza na salamu za Kiislam, “as-salaam alaikum,” ambayo ni slamu ya amani kwa wote, kwa ajili ya dada na kaka zangu katika imani na vilevile kwa ajili ya dada na kaka zangu katika ubinadamu kwa jumla.

Maneno haya ya kiungwana ulioonyeshwa kwa wasiokuwa Waislam kama “dada na kaka katika ubinadamu” sio jambo geni katika akili ya Muislam.

Karne kumi na nne zilizopita wakati Imam Ali bin Abi Talib mkwe na mrithi wa Mtume, alipomteua Malik al- Ashtar kama gavana wa Misri, alimuandikia waraka ambao ulimuonyesha kanuni za msingi za uongozi. Kwa vile Misri lilikuwa ni jimbo lenye imani mchanganyiko la dola ya Kiislam, Imam Ali alimuelekeza gavana wake mpya kama ifuatavyo:

Jaza moyo wako huruma, upendo na upole kwa raia zako. Usiwasimamie kama mnyama mlafi anayeona kwamba inatosha kuwameza, kwani wana namna mbili: ama ni ndugu zako katika imani, au ni kama wewe kimaumbile.1

Hisia hizi za heshima kwa wasiokuwa Waislam yamekuwa ni sehemu muhimu katika Uislam, dini ilipoletwa kwetu na Mtume Muhammad (s.a.w.), Mtume ambaye anafuatwa na moja ya tano ya jumla ya idadi ya wanadamu; na Mtume ambaye ametukuzwa na kupewa cheo cha “Mtu pekee mwenye mvuto mkubwa mno katika historia ya mwanadamu.” Na kwa hiyo ni muhimu sana kumjua yeye na watu wake.

Mazungumzo kati ya staarabu mbali mbali ni haja ya muhimu sana ya wakati wetu huu. Inasikitisha sana kwa hakika, kuona kwamba, japokuwa tunaishi katika zama ambazo ni za njia za haraka na pana sana za mawasiliano, mataifa na jumuiya za kidini bado hazijaweza kuwa na mazungumzo ya maana hasa kati yao, wao kwa wao.

Ni katika msingi huu, kwamba mimi ninaamini kwamba mpangilio wa muda wa programu hii katika Bunge la Canada ni wenye kufaa sana kwa vile ndio kwanza tumepita au kuvuka kwenye tuta la kuzuia kasi la muhimu sana katika barabara ya mazungumzo ya kati ya Imani na Imani tofauti, tuta la kudhibiti kasi ambamo Mtume wa Uislam amekashifiwa kama mtu ambaye hakuleta kitu chochote kile bali mafundisho ya “uovu na ukatili.”2
Miito/Kazi Za Mitume: Uadilifu
Mtume Muhammad alikuwa ni nani? Na ni ipi ilikuwa kazi yake au wito wake?

Kwetu sisi Waislam, mtume Muhammad (s.a.w.) ni wa mwisho katika mfululizo wa mitume 124,000 ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa ajili uongozaji wa jamii ya wanadamu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema ndani ya Qur’ani Tukufu:

“Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili za wazi, na tukakiteremsha kitabu na mizani pamoja nao ili watu wasimame katika uadilifu.” (al-Hadiid; 57:25) Mitume mashuhuri wote wa Mwenyezi Mungu – Adam hadi Nuh, Abraham mpaka kwa Mussa, Isa (Yesu) mpaka kwa Muhammad – walikuja kusimamisha uadilifu katika jamii. Wanadamu wote wanatamani na kuitaka amani katika dunia hii. Lakini amani haiwezi kamwe kupatikana katika ombwe tupu. Yenyewe hiyo imesokotana au imechanganyikana na uadilifu.

Ili kupatikana amani, uadilifu lazima iwe ndio msingi wa mfumo wetu wa kijamii, vinginevyo, hatuwezi kupata amani ya kudumu muda mrefu.

Uadilifu ni nini? Uadilifu maana yake ni kuweka kila jambo mahali pake pa sawasawa; ina maana ya kupima na kuyaangalia mambo katika mpango unafaa na kustahili; ina maana ya kuleta upatanifu. Kama mtu ataanza kuweka mambo katika sehemu au nafasi isiyostahili, basi huyo anatibua utulivu wa kijamii na tena anachafua amani.
Amani Katika Kiwango Cha Binafsi
Amani katika jamii inategemea na amani ndani ya nafsi zetu binafsi. Kwa mujibu wa Mtume Muhammad: tunapaswa kuleana kukuza hisia za uadilifu ndani ya nafsi zetu kwa kuunda utulivu na upatanifu kati ya hisia zetu za hasira na tamaa kwa upande mmoja, na busara na akili zetu kwa upande mwingine; kati ya vipimo vya kimwili na vipimo vya kiroho.

Mtu wa haki, mwadilifu ni yule anayedhibiti hasira zake na ulafi wake kwa nguvu ya tafakari ya akili. Kitendo hiki cha kudhibiti mtu hasira na ulafi wake kwa nguvu ya tafakuri ya akili kimeelezewa na Mtukufu Mtume Muhammad kama “Jihadi kubwa.”

Wakati mmoja, pale jeshi la Waislam liliporudi Madina kutoka kwenye shughuli zake, Mtukufu Mtume aliwasalimia wapiganaji hao kwa kusema: “Karibuni enyi watu ambao mmetoka kufanya Jihadi ndogo, na ambao bado mnangojwa na Jihadi kubwa.”

Wapiganaji hao wakamuuliza, “Ewe Mtme wa Mwenyezi Mungu! Ni ipi hiyo Jihadi kubwa?” Mtume akawajibu, “Ni Jihadi ya kiroho”.

Hiyo Jihadi ya kiroho au ya nafsi sio Jihadi rahisi na nyepesi. Unapaswa kupata udhibiti dhidi ya hisia zenye nguvu sana, na kuishi kulingana na sauti ya hekima na dhamira. Ni wale tu ambao wanaweza kuzishinda nafsi zao ndio wanaoweza hasa kuimarisha amani katika jamii.
Amani Na Uadilifu Katika Kiwango Cha Jamii
Mtume wa Uislam alikuwa mbele kabisa ya nyakati zake katika kukuza na kusimamia amani na haki katika jamii. Inafaa sana kuangalia na kuona jinsi yeye alivyoshughulika na wale wasiokuwa Waislam wachache na pia na maadui wakati wa vita kwa sababu thamani halisi ya jamii inajionyesha wakati inapokuwa chini ya shinikizo.

Kwa jamii ndogo ya wasiokuwa Waislam hapo Madina

Mtume na wafuasi wake walikuwa ni watu wachache walioteswa hapo Makkah. Wakati yale mateso yalipozidi na yakawa hayavumiliki, yeye alihamia Madina, mji ulioko kaskazini ya Arabia, ambao wakazi wake wengi walikuwa wamekwisha kuukubali Uislam. Mara alipokuwa ametulia hapo Madina, alitambua kwamba kulikuwa na jamii ndogo ya Wayahudi katika mji ule ambayo ilikuwa haina mwelekeo wa kuukubali Uislam. Yeye alikutana nao na akawaalika kwenye makubaliano na Waislam ili kwamba kila kundi la kidini hapo Madina liwe linajua haki zake na wajibu wao. Baadhi ya sehemu muhimu za makubaliano hayo zinasomeka kama ifuatavyo:

1. Wayahudi ambao wataingia katika ahadi hii ya maandishi watalindwa kutokana na fedheha na uchokozi wowote; watakuwa na haki sawa kama za watu wetu kwenye misaada na huduma zetu nzuri. Wayahudi wa makabila mbalimbali… na wakaazi wote wengine wa Madina wasiokuwa Waislam, wataunda pamoja na Waislam, umma mmoja mchanganyiko.

2. Watatenda ka mujibu wa dini zao kwa uhuru kabisa kama walivyohuru Waislam.

3. Washirika wa Wayahudi hao watafaidi usalama na uhuru huo huo. Wahalifu watafuatiliwa na kisha wataadhibiwa. Wayahudi wataiunga pamoja na Waislam katika kuilinda Madina dhidi ya maadui wote. Ndani ya Madina kutakuwa ni sehemu takatifu kwa wale wote watakaoukubali Mkataba huu. Wale washirika wa Waislam na wale wa Wayahudi wataheshimiwa kama yale makundi makuu ya Mkataba huu.

Makubaliano haya baina ya ile jamii ya mwanzo ya Waislam na jamii ya Wayahudi hapo Madina yanaonyesha maana ya uadilifu ulioelekezwa picha yake katika tabia ya Mtume katika kushughulika na makundi yawachache. Yanaonyesha dhahiri vile vile kwamba Mtume hakueneza Uislam, hata katika jiji la Madina kwa nguvu, bali kinyume chake yeye alianzisha kuendeleza maisha ya pamoja na wafuasi wa Imani nyingine za kidini, hususan Wayahudi na Wakristo. Kati ya Imani tatu hizi za ki-Abrahamia, ni Uislam pekee ambao umetambua dini ya Kiyahudi na Ukristo katika kiwango cha kitheolojia; Wayahudi na Wakristo wanajulikana katika Uislam kama ‘Watu wa Kitabu’ – Ahlul-Kitab.

Kwa kufuata mfano wa Mtume Muhammad (s.a.w.) watawala wengi katika historia ya Waislam walidumisha uhusiano wa amani na ukunjufu kwa raia wao wasiokuwa Waislam. Kama ingekuwa tulinganishe mwenendo wa watawala wa Kiislam kwa raia zao wachache waliokuwa wakiishi chini ya utawala wao katika kipindi cha karne ya kumi na tisa – na ule mwenendo wa Wazungu na Wamarekani kwa raia zao wa makundi madogo, ninathubutu kusema kwamba sifa ya Waislam itakuwa ni bora zaidi. Profesa Roderic Davison, mwanahistoria maarufu wa dola ya Othumainiya anaandika:

“Kwa kweli inaweza ikajenga hoja kwamba Waturuki wale walikuwa wakandamizaji raia zao wenye afadhali kidogo kuliko walivyokuwa wale wa-Prusiani wa kule Poles, Waingereza wa Ireland, au wa Wamarekani kwa wanegro... Upo ushahidi wa kuonyesha kwamba katika kipindi hiki (yaani mwishoni mwa krne ya 19) ulikuwepo uhamaji wa kutoka Ugiriki huru kwenda kwenye dola ya Othumainiya, kwa vile baadhi ya Wagiriki waliiona ile Serikali ya Othumainiya kuwa ni Bwana mdekezi mwema (kuliko serikali yao wenyewe)”3

Kama ukiichunguza historia ya enzi ya kale huko Ulaya, utaona kwamba mfano pekee wa jamii yenye tamaduni mchanganyiko na imani ya dini mbalimbali, iliyokuwa na amani na utulivu hasa, ilikuwa ni Hispania chini ya utawala wa Kiislam – Hispania ambayo ndani yake Wakristo, Wayahudi na Waislam waliishi kwa amani na utulivu.

Ndugu na Majirani Wasiokuwa Waislam Amri ya kisheria ya Kiislam kuhusu kuwa na upendo na kujali kwa ajili ya jirani inachukua aina zote za majirani:

“Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote, na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali na rafiki wa ubavuni, na msafiri, na waliomilikiwa na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi ajivunaye”. (4:36)

Hata kama wazazi wake Muislam huyo ni waabudu – masanamu, Uislam, dini ya Tauhid, ya Mungu Mmoja – unamuelekeza kuwaheshimu na kuwa mpole kwao. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani Tukufu:

“Na kama (wazazi hao) wakikushurutisha kunishirikisha na yule ambaye hunahabari naye, basi usiwatii, na kaa nao kwa wema hapa duniani…” (31:15)

Kwa Maadui ndani ya Medani ya Vita Qur’ani inawaelekeza Waislam kudumisha haki na uadilifu hata pale wanaposhughulika na maadui zao.

“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtoe ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusiwapelekeeni kutowafanyia uadilifu. Fanyeni uadilifu, huko ndiko kunako mkurubisha na uchamungu, na mcheni Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.” (5:8)

Vita vya kwanza katika historia ya Kiislam ni muhimu sana. Vilitokea mnamo mwaka wa 2 Hijiria, kwa kalenda ya Waislam, kati ya Waislamu na washirikina wa Makkah. Ingawa walizidiwa kwa idadi na maandalizi yao yalikuwa dhaifu, Waislam waliwashinda washirikina hao wa Makkah na wakachukua watu sabini mateka wa kivita.

Kawaida miongoni mwa jamii zote kwa wakati ule ilikuwa ni ama kuwauwa wafungwa wa kivita au kuwafanya watumwa. Lakini Mtume Muhammad aliwaagiza Waislam kuwatendea wafungwa wa kivita hao ubinadamu; hawa walifikishwa salama Madina na wakapewa makazi ya heshima katika nyumba za wale watu waliokuwa wamewachukua kama wafungwa. Qur’ani imeamuru na kuagiza kwamba wafungwa wa kivita wasije wakafanyiwa ubaya wa aina yoyote ile.

Kwa mujibu wa mwandishi wa kimagharibi wa wasifu wa Mtume Muhammad, Sir William Murr: “Kwa kufuata maagizo ya Muhammad, wananchi wa Madina... waliwapokea wale wafungwa na kuwatendea kwa kuzingatia wema kwa makini sana.

Yote haya yalifayika miaka kumi na nne elfu iliyopita, zamani saana kabla ya Mkataba wa Geneva kuja kuwepo.

Katika maficho ya magereza ya siri ambayo yanayoendeshwa na CIA, zile “Kaida na mwongozo wa mateso” zilizoandikwa na jeshi la Marekani ili kuwahoji na kuwadodosa hao wafungwa, na kule kufichuka kwa mateso ndani ya gereza la Abu Ghuraib, ninaweza kusema kwa kujivunia sana kwamba ule mfano na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.) kuhusu wafungwa wa kivita ‘POWS’ ni “mazuri nay a kibinadamu kwa uhakika haswa” hata kwa mujibu, au kulingana na ya viwango vya karne ya 21.
Mabibi na Mabwana, kiini cha mazungumzo ya maana baina ya tamaduni mbali mbali ni kutafuta njia na namna ya kuzileta jumuiya za kidini katika kutenda yale maadili yaliyohubiriwa na Mitume mashuhuri wa Mwenyezi Mungu.

Tunapaswa kukabiliana, kutoa changamoto ya kutaka kujua sababu za wale wenye siasa kali wa pande zote:

Kwa akina Bin Laden wanaoumiza na kutesa na kuua raia wasio na hatia, ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.) alifundisha upendo na huruma hata kwa wanyama na mimea.

Kwa wale wakristo wenye siasa kali wa kusini ya Marekani waliounda hoja ya “vita vya haki” baada tu ya tukio la 9/11 na kuunga mkono vita vya Marekani kwa misingi ya kitheologia na itikadi wakati ambapo Jesus (Yesu) alifundisha upendo na msamaha mwendo mrefu kupita kiasi anachoweza. (3) Unapofika sehemu ya kupumzika, wewe mpandaji, ni lazima kwanza uandae majani kwa ajili ya mnyama wako kabla hujashughulikia haja zako wewe mwenyewe. (4) Wakati wowote unapopita karibu na bwawa la maji au mto, muache mnyama wako akate kiu yake kwanza. (5) Msimpige usoni kwa sababu na wenyewe pia unamtukuza Mwenyezi Mungu.

kwa kusema kwamba “yeyote atakayekupiga kwenye shavu la kulia, basi mgeuzie na lile la kushoto pia”.

Ufumbuzi wa matatizo ya wakati huu sio yenye upungufu wa kidini, bali ufumbuzi au namna ya utatuzi wake ni wa kidini zaidi ili kuweza kuyaleta yale maadili yaliyolinganiwa au kufunzwa na vitendo vilivyotekelezwa kwa kila mmoja. Waislam wajiweke karibu na mfano wa Mtume Muhammad (s.a.w.) na Wakristo wasogee karibu sana na mfano wa Nabii Isa – Yesu (a.s.) – ni hapo tu ndipo tutaweza kuwa na amani ya kudumu katika huu ulimwengu.

Ninamalizia kwa ile dua au maombi yale maarufu tuliyoyafundishwa na Familia ya Mtukufu Mtume: “Ewe Mola! Wewe ndiwe amani, kutoka kwako inaanzia amani na kwako Wewe itarejea amani.”
Heshima Ya La Martine Kwa Mtume
Mwanahistoria wa kifaransa wa karne ya kumi na nane, La Martine, anaandika yafuatayo katika kitabu chake “Histoire de la Turquie (1854) kuhusu Mtume wa Uislam:

“Kamwe mwanadamu hajajiwekea mwenyewe, kwa hiari au bila kukusudia, lengo adhimu sana, kwa lengo hili lilikuwa la nje ya uwezo wa kibinadamu:

Kuangamiza imani za ushirikina ambazo zilikuwa zimeingilia kati baina ya mwanadamu na muumba wake, kumrudisha Mungu kwa mwanadamu na mwanadamu kwa Mungu; kudumisha lile wazo la kimantiki na tukufu la kimungu katikati ya vurugu za miungu ya kidunia na yenye sura mbaya ya uabudu masanamu uliokuwepo wakati huo…..”

“Kama ukuu wa lengo, ufinyu wa nyenzo, na matokeo ya kushangaza ndivyo kigezo halisi cha kipaji cha kibinadamu, ni nani angeweza kuthubutu kumlinganisha mtu yoyote maarufu katika historia ya kisasa na Muhammad?.......”

“Mwanafalsafa, msemaji mwenye fasaha, nabii, mwanasheria, mpiganaji, mtekaji wa mawazo, mdumishaji wa imani zenye mantiki, mtindo usiokuwa na sura mbali mbali (makundi); mwanzilishi wa dola ishirini za kidunia na ufalme mmoja wa kiroho, huyo ni Muhammad. Na kuhusu vipimo vyote ambavyo kwavyo umaarufu wa kibinadamu unaweza kupimwa navyo, tunaweza kuuliza, hivi kuna binadamu yoyote mashuhuri kuliko yeye?”
Lifuatalo Ni Jibu Alilotoa Mtukufu Mtume (S.A.W) Wakati Alipoulizwa Na
Imam Ali (A.S) Kuhusu Ni Nini Iliyokuwa Sunna (Mwenendo) Yake
• Kumbukumbu juu ya Mungu ni Rafiki yangu

• Hekima ndiyo mzizi wa Imani yangu

• Upendo ndio Msingi wangu

• Shauku ndiyo Farasi wangu

• Kumjua Mungu ndio Mtaji wangu

• Uimara ndiyo Hazina yangu

• Huzuni ndiyo Mwenza wangu

• Elimu ndiyo Silaha yangu

• Subira ndiyo Joho langu

• Kinaa ndiyo Ngawira yangu

• Ufukara ndiyo Fahari yangu

• Upendo ndio Sanaa yangu

• Uhakika ndiyo Nguvu yangu

• Ukweli ndiyo Mkombozi wangu

• Utii ndiyo Kitoshelezo changu

• Jitihada ndiyo Tabia yangu
________________________
1. Tazama mkusanyiko wa hotuba, barua na semi za Imam Ali zilizokusanywa na Sayyid Radhi katika Nahju ’l-Balagha, barua ya 53.

2. Hii inarejea kwenye maelezo ya Papa Benedict XVI) kwenye Chuo Kikuu huko Ujerumani ambako alitoa hotuba mnamo 12th Septemba, 2006 juu ya “Imani, Busara na Chuo Kikuu”. Ndani yake alimnukuu Mfalme wa Byzantine, Manuel II Paleologus kama ifuatavyo: “Nionyeshe ni nini hasa alichokileta Muhammad ambacho kilikuwa kipya, na hapo utaona mambo ya uovu na ukatili tu kama vile ile amri au maagizo yake ya kueneza kwa upanga ile Imani aliyoitangaza yeye.

3. Roderic H. Davison, kitabu – Reform in the Ottoman Empire 1856 – 1876 (New jersey: Princeton University Press, 1963) uk 116.

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ