Rafed English

Sura Al Fatiha

Sura Al Fatiha

by : Bashir Haiderali Alidina

Naomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa, kuanza kwa Jina la Mola Ambaye ameumba, bila yeye Mwenyewe kuumbwa.

Sifa zote zinamstahiki Allah (S.W.T) Ambaye ameiteremsha Qur'an Tukufu juu ya mja Wake mpenzi mno ili kwamba aweze kuwa mbebaji wa habari njema na muonyaji kwenye ulimwengu. Baraka ziwe juu ya Mtukufu Mtume (S.A.W.) na juu ya kizazi chake kitoharifu ambao walitoharishwa kwa utakaso ulio kamili kabisa.

Naomba mwongozo kutoka kwa mola wa ulimwengu ili kuniwezesha kukamilisha jukumu hili kubwa ambalo ninaliingia kabla ya kuondoka kwenda kwenye awamu nyingine ya maisha yangu. Sijifikirii mwenyewe kuwa na uwezo hata wa kuweza kukwaruza uso wa Kitabu kitukufu mno ya vitabu vyote na nitajiona mwenyewe mwenye bahati kama ningekuwa na uwezo wa kufikisha kitu kidogo mno cha mabadiliko ya milele na maana ya Qur'an Tukufu kwa watu wa kawaida katika namna nyepesi ya kutosha kwa kadiri kwamba iwe rahisi kueleweka. Ili kufanikisha hili nitajaribu na kuepusha nyingi ya hoja za kifundi na kifilosofia ambazo huonekana kwa zaidi katika vitabu vikubwa vya tafsir.

Namuomba Allah (S.W.T.) Aliye juu, kunipa umri mrefu wa kutosha kukamilisha tafsir hii na kukubali jaribio langu hili la unyenyekevu mno kuanza kulipa ajr-e-risaalat.

Kwa mara nyigine tena namuomba Allah (S.W.T.) Yeye aliye juu, kuniongoza na kunisaidia kuweka maelezo yangu kwenye lengo. Hakika Yeye ni Msaidizi na Kiongozi bora.

Mtumishi wa Allah (S.W.T.)

Bashir Haiderali Alidina
Hayo ni kwa sababu
Mwenyezi Mungu ni Mlinzi
wa walio amini na makafiri
hawana Mlinzi – 47:11

Jina

Sura hii inaitwa ‘Ufunguzi Wa Kitabu’, na kuna hadithi nyingi ambazo huonyesha kwamba hili ndilo jina ambalo kwamba kwalo ilijulikana wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.).

Hivyo basi inashangaza kukona Waislamu wengi wakishikilia juu ya dhana kwamba Qur’an Tukufu haikuwa katika hali ya kitabu wakati wa uhai wa Mtukufu mtume (s.a.w.), bali kwamba ilikuwa tu umekusanywa ivyo wakati wa Makhalifa wakati wa mwanzo. Naone nu ukosefu wa mantiki kwa mtu kutaja sura hii kama kuwa ‘Ufunguzi Wa Kitabu’ wakatai kitabu chenyewe kilikuwa hakipo.

Hili hutiliwa nguvu zaidi na hadithi ya mwisho inayokubaliwa na wote ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) kuhusu vitu viwili vizito ambavyo kwavyo kimoja kilikuwa ni Qur’an Tukufu, ambavyo ilitajwa na yeye (s.a.w.) kama ‘kitabu’.

Ni kutokana na sura hii kwamba kawaida njia ya kufikia kwenye kitabu hiki hupatikana, kwa vile huchukuliwa kama mukhtasari mfupi wa kitabu chote.

Qur’an Tukufu ni mwonogozo kwa wacha Mungu, na mtu anavyozidi kuwa Mcha Mungu ndivyo anavyozidi kuongozwa na kitabu hiki. Kitabu hiki kinakawaida ya ‘kufunguka’ kwa ajili ya muongozo kwa wasomaji wake kwa kutegemea kiwango cha uchaji Mungu wao na elimu.

Ama kwa wasomaji wengine anbao sio wacha Mungu, kwa kawaida kitabu hiki hufunga mlango wake, na watapita jiji la elimu kwa kweli bila kuingia ndani yake kwa kupitia mlango wake na kunufaika kutokana nayo.

Hufuatilia kutokana na maneno hayo hapo juu kwamba kitabu hiki kitafunguka zaidi kwa muongozo kwa ‘Imam Al Muttakiin’ kwa vile kwa hakika alikuwa mwenye elimu zaidi na Mcha Mugu zaidi kama ambavyo kwa pamoja marafiki zake na halikadhalika maadui zake isipokuwa Allah (s.w.t.) na wale ambao wamezama ndani kwa imara katika elimu.

Iliteremshiwa Wapi?

Sura hii iliteremshiwa Makka, lakini kuna baadhi ya Wafasir ambao wamechukulia maoni ya kwamba hii ni moja ya Sura ambayo kwa kweli iliteremshwa mara mbili, kwanza ni katika mji wa Makka na mara nyingine tena katika mji wa Madina. Maoni hayo ambayo vile vile yanatolewa na baadhi ya hadithi, yataifanya kuwa ni sura pekee iliyopata kuteremshwa mara mbili, huenda kwanza kama sehemu ya kitabu na tena kama Sura inayojitegemea.

Idadi Ya Aya

Kuna watu wachache walio na maoni ya kwamba Sura hii ina aya sita na kwamba ‘Bismillah’ ni sehemu na fungu la sura hii na kwamba idadi ya aya ni saba. Maoni haya yanategemea juu aya ifuatayo :-

(Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu - 15:87)

Hii huleta swali la iwapo kama sura hii yenyewe ni sehemu ya Qur’an Tukufu au la. Kuna hadithi ya Kitume isemayo kwamba: “Allah (s.w.t.) ameweka juu yangu mimi upendeleo kwa kunipa mimi sura hii, na kuifanya sawa sawa na Qur’an na hii ni moja ya Hazina bora za Arish”.1

Yeye (s.a.w.) binafsi amewaamrisha Waislamu kuiweka sura hii mwanzoni mwa Qur’an Tukufu, na kuifanya kama ufunguzi wa Kitabu. Zaidi ya hayo, Qur’an Tukufu ni Kitabu kamili na sio pungufu katika hali yeyote, kama ilivyoeleza kabla, na hivyo vipi ingeliweza kuwa kamili bila kuwa na ufunguzi wake.

Allah (s.w.t.) Mwenyewe amedai kwamba Yeye (s.w.t.) ameikamilisha dini yetu na ametimiza neema Zake.

Utaalam

Sifa moja ambayo kutofautisha sura hii na nyingine, ni lugha na dhamira yake. Ambapo sura nyingine zimeteremshwa katika maneno ya Allah (s.w.t.), hii iliteremshwa katika hali ambayo kwamba iko katika maneno ya watumishi wa Allah (s.w.t.). Hutupa sisi mafunzo muhimu kutuwezesha sisi kuongea na Allah (s.w.t.). Hutuweka sisi taktika hali wa akili ya sawa sawa kabla ya kwenda kuomba chochote.

Manufaa Yake

Sura hii ni msingi wa Qur’an Tukufa na malipo kwa ajili ya kisomo chake ni saw na yale ya kitabu chote. Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba nguvu za kuponya za sura hii huweza kuponya magonjwa zote isipokuwa kifo. Kwa kweli ziko hadithi ambazo husema kwamba hata kifo kinaweza kuahirishwa kwa msaada wa sura hii.

Mtukufu Mtume (s.a.w.) alisema kwamba: “Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Alisema - ‘Nimegawnya Ufunguzi wa Kitabu hiki kati Yangu na mja mtumishi Wangu; hivyo, nusu yake ni kwa ajili Yangu na nusu nyingine ni kwa ajili ya mtumishi Wangu. Na mja Wangu atapata kile anachokiomba kwayo.

Wakaji mja anaposema:’Kwa Jina la Allah Mwenye kuneemesha na Mwenye Kurehemu’, Allah, ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Husema; ‘Mja Wangu ameanza kwa kulitaja Jina Langu, na ni wajibu juu Yangu Mimi kwamba Yanipasa kukamilisha kazi zake kwa ajili yake na kumbariki katika mambo yake’.

Na wakati akisema:’Shukrani zote zinastahiki Allah, Mola wa ulimwengu wote’. Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Husema; ‘Mja Wangu amenitukuza Mimi, na najua kwamba neema alizonazo zinatoka Kwangu, na kwamba balaa ambazo zimeepushwa kutoka kwake zimeepushwa hivyo kwa Rehemu Yangu; Enyi Malaika Wangu! Nimewateua ninyi kama mashahidi kwamba nitaongeza neema kwa ajili yake za ulimwengu ujao (Akhera) kwa zile za ulimwengu huu, na nitaepusha kutoka kwake misiba ya ulimwengu ujao (akhera) kama nilivyoepusha kutoka kwake misiba ya ulimwengu huu.’

Na wakati akisema: ‘Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu’, Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema :“Mja Wangu anatia ushuhuda kwa ajili Yangu Mimi kwamba Mimi ni Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu; Ninawafanya ninyi mashahidi wangu kwamba hakika kweli kabisa nitazidisha mgao wake katika Rehema Yangu, na kwa hakika kabisa nitaongeza mgao wake katika neema Zangu.’

Na wakati anaposema, ‘Mola kwa siku ya malipo’, Allah Alye Juu Husema; “Ninakufanyeni ninyi mashahidi kwamba, kwa vile amekubali kwamba Mimi ni Mola wa siku ya malipo, kwa hakika kabisa mtafanya hesabu yake kuwa rahisi mno (kwa ajili yake) katika siky ya hesabu, na kwa hakika kabisa nitakubali matendo yake mema, na sitaangalia madhambi yake”.

Na wakati anaposema, ‘Yeye Peke Yake tunamuabudu’, Allah ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema; “Mja wangu anasema kweli, ananiabudu Mimi tu. Kuweni mashahidi wangu kwamba hakika nitampa kwa ajili ya ibada yake zawadi ambayo atakuwa (ni kitu cha) kuonewa wivu kwa wote ambao walimpinga wakati akiniabudu Mimi”.

Na wakati akisema: ‘Na Kwake tunataka msaada’, Allah, Aliye Juu, Husema; “Mja wangu ametaka msaada kutoka kwangu, na kwangu Mimi amechukuwa hifadhi. Kuweni mashahidi wangu kwamba kwa hakika kabisa nitamsaidia katika mambo yake, na nitamsaidia katika shida zake, na nitampa msaada katika misiba yake”.

Na wakati anaposema; ‘Tuongeze katika njia iliyoonyooka . . . ‘, Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema; “Hii (sehemu) ni kwa ajili ya mja Wangu, atapata kile alichokiomba; na nimejibu du’a ya mja Wangu, na nimempa kwa ajili yake kile anachokitumaini; na nimemlinda kwa kile anachokihofia”.2

Kwo wote pamoja imekubaliwa na Waislamu wote kwamba ni wajibu kuisoma sura hii wakati Sala au kwamba vinginevyo Sala hiyo kaitaswihi. Hii peke yake inatosha kwa ajili ya utukufu wake kuhusiana na sura nyingine za Qur’an Tukufu.

Imesimuliwa kutoka kwa Imamu Ja’far Al Sadiq (a.s.) kwamba: “Mara nne Iblisi alilia; kwanza, wakati alipotumwa nje ya mkusanyiko; pili, alipotupwa nje ya bustani na kuletwa chini kwenye ardhi; tatu, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipolekezwa kutangaza utume wake; na nne wakati sura hii ilipoteremshwa.”3

Aya Ya 1

(Kwa Jina la Alah Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu)

Kwa ujumla hukubaliwa kwamba matendo makubwa hufanywa kwa jina la mtu mkubwa, kwa mfano uwekaji wa jiwe la msingi wa nyumba yoyote. Kwa hiyo ilikuwa yastahiki tu kwamba ufunuo wa Kitabu kikubwa mno kabisa ambacho kamwe hakijawahi kuteremshwa, kilipaswa kuanza kwa Jina lisilokuwa lolote lingine kuliko lile la Muumba Mwenyewe, kwa vile ni Yeye to Apatikanaye Atakayebakia kuwepo milele. Hii imeonyeshwa kwa uwazi na ukweli kwamba karibu kila sura ya Kitabu hiki Kitukufu imeanzwa kwa Jina la Allah (s.w.t.), na kuteremshwa kwa sura ya kwanza kwenye moyo wa Mbarikiwa Mtume wetu (s.a.w.), yaani mwanzo wa Kitabu chenyewe ilikuwa kwa Jina la Mungu.

(Soma kwa Jina la Mola Ambaye ameuumba - 96:1)

Siyo tu Muumba aliye tufundisha kufuata njia hii wakati wa kuanza kazi yoyote ile, lakini hali kadhalika hii ilikuwa ni kawaida ya wajumbe wake watukufu. Wakati Nabii Nuhu (a.s.) alipolijenga safina aliwaelekeza abiria kupanda kwa Jina la Allah (s.w.t.)

(Na alisema, Ingieni ndani yake, kwa Jina la Allah . . . 11:41)

Na wakati Nabii Suleyman (a.s.) alipoandika barua kwa malika Bilquis wa Sheba, barua yake ilianza kwa Jina la Allah (s.w.t.) :

(kwa hakika inatoka kwa Suleyman na kwa hakika iko kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu - 27:30)

Katika hadith ya Mtume inayokubalika na wote isemayo: “Kila jmabo muhimu lisiloanzwa kwa Jina la Allah (s.w.t.) litabakia pungufu”, tunaona kwamba kila kazi na kila jambo litakuwa na fungu lake la umilele kwa kiasi kile kile lihusihwavyo kwa Allah (s.w.t.).

Imam Al Sadiq (a.s.) amesema kwamba: “Mara nyingi maisha wetu hutokea kupuuza usomaji wa ‘Bismillah’ wakati wanapofanya tendo, basi Allah (s.w.t.) huwaweka katika aina fulani ya tatizo au janga ili waweze kulitambua hili na vilevile kwamba hata kosa hili liweze kuondelewa kutoka kwenye hesabu yao”.4

Ni lazima izingatiwe hapa kwamba ingawa naendelea kutaja kwamba kila kazi ni lazima ianzwe kwa jina la Allah (s.w.t.), siyo tu mwanzo wake ambao ninaurejelea kwawo. Madhumuni na nia ya hili kuwa kwa ajili ya Allah (s.w.t.) , lazima liwe lipo wakati wote tangu mwanzoni, wakati wa kuendelezwa kwake, na wakati wa kumalizika kwake.

Kwa maneno mengine, wakati mtu anapoanza kwa Jina la Allah (s.w.t.), mtu huyo lazima kuliendeleza jambo hilo kwa ajili yake na kulimaliza kwa jina lake pia.

Allah (s.w.t.) Yeye Mwenyewe ameigawanya khutuba Yake katika vipande mbalimbali, kila kipande kikiwa kinaitwa sura. Inafuatia kutokana na hili kwamba kila sura ni fungu moha katika muundo na katika ukamilifu wa maana na kwanba moha ya kila sura iko tofauti kutokana na nyingine. Kila sura imeteremshwa kwa lengo makhususi katika rai, na kama lengo hilo limepatikana, huwa imefikia mwisho. Kwa hiyo kutokea kwa aya hii ya ‘Bismillah’ takriban katika kila mwanzo wa sura ile. Hata hivyo baadhi ya sura huchukua zaidi ya jambo moja, na hivyo ‘Bismillah’ kwenye mwanzo wa sura hizo yumkini huhusisha, ama dhamira ya jumla ya sura ile au aya zinazofuatilia.

Kwa hiyo aya hii, mwanzoni mwa sura hii maalum, huonyesha vilevile kwenye dhamira ya sura hii. Hutokea kwamba madhumuni yake ni kumtukuza Allah (s.w.t.) na kuahidia utumwa wa mja na kisha kwa Yeye kuomba kwa ajili ya Mwongozo wa Mwenyenzi Mungu. Katika fuo hili, aya hii ingekuwa na maana ‘Kwa Jina la Allah ambaye kwake naahidia untumwa wangu na kutoka kwake natafuta mwongozo’.

Usomaji wa ‘Bismillah’ hutupatia fundisho la kiroho, na huzishurutisha akili zetu katika kufanya kazi yoyote ile. Daima imo akilini mwetu wakati tunapokuwa tunafanya tendo lile ambalo tumelianza kwa Jina la Allah (s.w.t.), na kufanya kama ukumbusho wa siku zote na kizuizi ambacho hutuepusha kutokana na utendaji wa matendo ambayo hayamo ndani ya sharia ya Kiislamu. Kwa mfano, usomaji wake mwanzoni mwa ulaji wa chakula kungetuepusha kutokana na kula chakula ambacho ni haramu au kilichopatikana isivyo halali; usomaji wake mwanzoni mwa kila tendo la kimwili kungetuzuia kutokana na kuktenda dhambi; na matumizi yake ya kila sikku yangetuepusha kutokana na kutenda matendo mema kwa sababu nyingine mbali na zile za kupatia ridhaa ya Allah (s.w.t.).

Nafikiri inafaa kutaja muundo wa neno ‘Bismillah’, imeundwa na herufi kumi na tisa za alfabeti za kiarabu. Profesa mmoja wa Kimisri, alitoa nadharia iliyotegemezwa juu ya namba kumi na tisa (19) na katika hii aligundua kwamba inawezekana kabisa kwamba Qur’an Tukufu yote imetegemezwa juu ya mfuno wa kimahesabu, na kwamba sehemu zake chache zimetengenezwa juu ya namba kumi na tisa (19). Kwa mfano, namba ya Sura za Qur’an Tukufu ni mia moja na kumi na nne (114), ambayo ni kigao cha kumi na tisa, wakati inapohesabiwa kurudi nyuma kutoka sura ya mwisho na ilikuwa na aya kumi na tisa.

Baada ya muda kidogo, nadharia hii ilinyamazishwa polepole, wakati mtu mmoja alipohoji kwamba ikiwa Qur’ani Tukufu yote ilitegemezwa juu ya namba kumi na tisa, basi itabidi tuonyeshe herufi hizo kumi na tisa ni herufi za ‘Bismillah’, kwani zingewezekana kuwa ni herufi za majina ya watu watano watukufu ambao Maisha wanawaamini.

Kwa Kiarabu, jina ‘Muhammad’ lina herufi nne, ‘Ali’ lina herufi tatu, ‘Fatima’ lina herufi tano, ‘Hasan’ lina herufi tatu na ‘Hussein’ lina herufi nne, zikifanya jumla ya herufi kumi na tisa.

Ni baadhi ya maneno haya ya Siri, yametumika kwa ukamilifu kuiunda ‘Bismillah’. Wakati tukiichukua ‘Alif Lam Ra’, ‘Ya Siin’ na ‘Ha Mim’, tunaona kwamba herufi hizi zimetumika pia mara kumi na tisa katika ‘Bismillah’. Mchanganyiko mwingine ungekua ‘Alif Lam Mim’ na ‘Alif Lam Ra’, ambao umetumika mara kumi na tisa. Ni wazi kwamba maneno haya ya Siri huhitaji utafiti mkubwa ndani yake ambao nategemea kufanya baadaye, Allah (s.w.t.) akipenda.

Kwa kadiri uzito wa ‘Bismillah’ uhusikavyo, ingetosha kusimulia kutokana na historia, tukio ambalo lilitokea wakati Firauni wa Misri alipotaka kumpima Nabii Ysufu (a.s.) kwamba kitu gani kingelijafanya mizani iiname mpaka ifikie uwiano. Nabii (a.s.) alimwambia Firauni ampatie yeye (a.s.) karatasi na kalamu ili yeye (a.s.) amwandikie jambo fulani. Hivyo Firauni alimpa Nabii (a.s.) karatasi na kalamu, mdipo alipoandika juu yake ‘Bismillah’ kwa ukamilifu na kumwambia Firauni abadilishe dhahabu zote na vito ya thamani ambavyo vilikuwa juu ya mizani kwa kipande hiki cha karatasi.

Licha ya uamuzi ya dhahiri usio wa kimantiki, katika hili Nabii Yusufu (a.s.) aliona kipande cha karatasi kuwa na uzito zaidi kuliko uzito wote wa vito vyote hivyo vyenye thamani kubwa, Firauni hakutilia shaka hali ya akili ya Nabii (a.s.).

Ingawaje tukio hii lilitokea karne nyingi kabla ya kuteremshwa Qur’ani Tukufu, hutuonyesha dalili za uzito wa Qur’ani Tukufu nzima. Inafaa kukumbuka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika hadithi yake (s.a.w.) ya mwisho aliona Qur’an Tukufu na Kizazi chake kuwa na uzito ulio sawa.Juu ya hili, ni aya ya Qur’an Tukufu isemayo kwamba :

(Ingeteremshwa hii Qur’ani Tukufu juu ya mlima, ungeyeyuka na kukatika vipande vipande - 59:21)

Nguvu ya ujuzi wa ‘Bismillah’ ulionyeshwa na Jinni katika baraza ya Nabii Suleyman (a.s.) wakati Malika Bilquis wa Sheba alipokuwa njiani kwenda kukutana na Nabii Suleyman (a.s.), aliwauliza watumishi wake wa baraza iwapo kuna yoyote miongoni mwao ambaye anaweza kakipata kiti chake cha enzi na kumpatia kabla ya kuwasili wake.

Jinni mmoja alisimama, ambaye kwamba Qur’an Tukufu ilisema kwamba anayo elimu kisasi ya Kitabu, na kudai kwamba anaweza kulifanya hilo katika muda wa kufuma na kufungua jicho :

(Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako - 27:40)

Baadhi wanasema kwamba Jinni huyo alikuwa nayo elimu halisi ya ‘Bismillah’ ambayo ilimwezesha kutekeleza jukumu hili lisilowezekana la kimaumbile.

Hakuna Muislamu awezaye kukanusha tukio hili kwa vile limesimuliwa katika Qur’an Tukufu. Jambo ninalojaribu kuonyesha hapa ni kwamba, kama sehemu ya eilmu ya Kitabu (Qur’an) ina nguvu ya kumwezesha mtu kutekeleza jukakumu kama hilo, Allah (s.w.t.) Peke Yake ndiye ajuaye ni nguvu kiasi gani iliyokuwa chini ya watu ambao walikuwa na elimu ya Kitabu chote.

Be

Imetajwa kwenye hadithi kwamba Imam Ali (a.s.) alisema kwamba: “Yote yale ambayo yamo katika Qur’an Tukufu yaweza kusema kuwa yamo ndani ya ‘Al Fatiha’; yote yale ambayo yamo ndani ya Sura hii yaweza kusema kuwa yamo ndani ya ‘Bismillah’; yote yale ambayo yamo ndani ya ‘Bismillah’ yamo ndani ya ‘Be’ yake; na kwamba mimi ni ile doti chini ya ‘Be’.5

Njia moja ya kuangalia kwenye nukta hii itakuwa kusema kwamba Imam Ali (a.s.) anayo elimu yote ambayo imo ndani ya Qur’an Tukufu, na kwamba yeye alikuwa mfasir sahihi wa Kitabu (Qur’an).

(. . . Na hakuna ajuaye tafsir yake isipokuwa Allah, na wale waliozama katika elimu . . . - 3:7)

Bado hajatokea (na wala hatatokea) yoyote aliyohoji ubora wa elimu yake juu ya jambo lolote kwa kupitia historia yoyote.

(Na wako baadhi miongoni mwao ambao wanataka kukusikiliza wewe, hata wanapoondoka kwako huwauliza wale waliopewa elimu, ‘Amesema nini sasa hivi?’ Hao ndio ambao Allah amewapiga muhuri myoyoni mwao na wakafuata matamanio ya nafsi zao - 47:16)

Nimefahamishiwa kwamba herufi ya Alfabeti ya Ki-Arabu imeundwa kwa idadi maalumu za vidoti na kwamba vidoti vinavyoifanya ‘Be’, idadi yake ni kumi na moja, pamoja na ya kuma na mbili ikiwa chini yake. Hii itaonyesha kwamba Ali (a.s.) ni msingi wa Maimamu wote, na ni kutokana na yeye kwamba Maimamu wengine wanatambuliwa kwaye. Kama tunavyokuona kutoka kwenye herufu ‘Be’, kama tungeiondoa doti chini yake, herufi iliyobakia isingefahimika. Maana yangu hapa sio kuwadogesha Maimamu wengine, ambao walikuwa viigizo vizuri kwa ajili ya wanadamu kuwafuata, bali kueleza tu chuo cha Imamu wa kwanza (a.s.) katika kuhusiana na Maimamu wengine.

Ism Allah

Jina ni alama ambayo kwayo kitu hutambulika. Ingawa inaweza kuwa kweli kusema kwamba kila kitu ni jina la Mwenyezi Mungu, kwani kila kitu kinatokana na kwake, hilo Jina linatorejewa hapa ile Nafsi Tukufu Mwenyewe Allah (s.w.t.). anayo Majina Mazuri mengi, kila moja likishiria sifa Yake maalum, lakini hili Jina ‘Allah’ ni Jina lenye upana wote, kuhusu kwamba linajumulishazile sifa asilia za Majina Yake yote katika jina moja. Haya Majina Muuma, Mkarimu, Mwenye Rehma, Mwenye Kurehemu n.k., ndio yote Majina Mazuri ya Mola, lakini si yenye kujumulisha, ambapo ‘Allah’ ndivyo ilivyo.

(Allah - hakuna aabudiwaye uwa haki isipokuwa Yeye; Yake ndio Majina Mazuri - 20:8)

(Sema: Muombeni kwa jina la Allah au muombeni kwa jina la Mwenye Rehma. Lolote mtakalomwomba kwalo - 17:110)

Kutokana na hayo hapo juu tunaona kwamba tunaweza kumuomba Yeye kwa lolote kati ya Majina Yake Mazuri, lakini kama ilivyotajwa kabla, hili Jina Allah lingeweza kuwa ndio lenye kufaa zaidi kwa sababu rahisi tu kwamba ni Jina lenye kujumulisha sifa zote sa yale Majina Mazuri Yake mengine. Juu ya hili, kilugha, yale Majina mengine yangeweza kuwa na wingi na uke, kwa mfano: Waumbaji, Miumgu, Miumgu wa kike; lakini hili Jina ‘Allah’ halina uke wala wingi.

Al Rahman

Hili limetafsiriwa kama ama Mkarimu au Mwenye Huruma. Lakini kile uwa katika inachoashiria kwacho ni kwamba, yenye kujumuisha yote, Ukarimu au Huruma ya Allah (s.w.t.) inayomhusu kila mtu na kila kitu kwa usawa. Haitofautishi kati ya rafiki au adui, mnyama au mtu. Hii inaweza kusema ya kuwa ni Sifa maalum ya Allah (s.w.t.) ambayo ina matumizi ya kawaida. Kwa maneno mengin, mkana Mungu anaweza kufaidika kwa kiasi kile kile kutoka Uwenye Sifa hii kama ambavyo angenufaika mu’min.

Al Raheem

Hii ni ile Rehema ya Allah (s.w.t.) ambayo imenekwa kwa ajili ya waumini tu juu yaoambao Atawamiminia katika siku ya Hukumu. Hii ni Rehma ya milele ya Allah (s.w.t.).

(Enyi mlioamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi na Mtukuzeni asubuhi na jioni. Yeye ndiye anayekurehemuni na malaika Wake (wanakuombeni) ili kukutoeni katika giza kukupelekeni kwenye nuru Nae ni Mwingi wa Rehma kwa waumini - 33:41-43)

Aya Ya 2

(Shukurani zote ni za Allah, Mola wa walimwengu)

Al Hamdulillahi

Allah (s.w.t.) ni Mzuri katika Majina Yake na Mzuri katika matendo Yake na kila Kizuri huanzia Kwake.

Kila sifa ambayo inasemwa na mtu yeyote kwa ajili ya kitendo chochote iko katika hali halisi katika kuelekezwa kwa Allah (s.w.t.) tu, kwa sabab yeye ni asili ya uzuri wote. Kwa ufupi, ni Zake Yeye sifa za jamii za viumbe na kila aina ya Sifa.

Kwa mfano, kama ningelitaka kusifu ubora wa kiti, basi kwa njia isiyo ya moja kwa moja sifa zangu zitakuwa ni za mtengenezaji wa kiti na sio kiti chenyewe, kwani kiti hakikupata ubora wake wowote kwa chenyewe.

(Huyu ndiye ajuaye mambo ya ghaib na ya dhahiri Mwenye Nguvu, Mwenye Huruma, Ambaye amefanya uzuri wa kila kitu alichokiumba, na alianza uumbaji wa mtu kutokana na mavumbi - 32:6-7)

Kila kitu ni kizuri kwa sababu kimeumbwa na Allah (s.w.t.) na kila kitu kilichoumbwa na Yeye ni kizuri. Ameumba kila kitu kwa Hiari yake Mwenyewe, hakulazimishwa na yeyote au chochote, na kwa hiyo kila kitu ni kazi nzuri Yake Mwenyewe, na hivyo sifa zote kwa lazimazinapaswa ziende Kwake peke Yake. Wakati Yeye (s.w.t.) alipomhutubia Mtukufu Mtume (s.a.w.) Alisema :

(Na sema: Sifa zote njema ni za Allah, Atakuonyesheni alama zake ili kwamba mpate kuzitambua; wala Mola wenu haghafiliki na hayo mnayoyafanya - 27:93)

Na Allah (s.w.t.) alimsemesha Nabii Nuhu (a.s.) wakati Yeye (a.s.) alipokuwa ametendeneza safina :

(Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo ndani ya safina, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu! - 23:28)

(Kilio chao ndani yake kitakuwa: ‘Utukufu ni Wake, E Allah! na salaam yao ndani yake itakuwa amani.’ na mwisho wa kilio chao itakuwa: ‘Sifa zote ni za Allah Mola wa walimwengu wote - 10:10)

Ama kwa viumbe wengine, Allah (s.w.t.) Anasema kwamba wanamtukuza Yeye pamoja na Sifa Zake.

(Mbingu saba zinatangaza utukufu wake na aardhi (vile vile), na wale ambao wako ndani mwao; na hakuna hata kitu kimoja bali humtukuza Yeye kwa Sifa Zake, lakini haelewi utukuzaji wao; hakika Yeye ni Mvumilivu, Mwenye Kusamehe - 17:44)

Na kadiri waja wake watoharifu wanavyohusika, hufanya maneno yao sifa kana kwamba yeye Mwenyewe ameyasema, kwa sababu hawana madhambi na upungufu, kama inavyokubaliwa na wote katika hadithi ya kiutume:

“Mimi si mwenye kuhesabu sifa Zako; Wewe kama ulivyo Wewe Mwenyewe umejitukuza Mwenyewe.”6

Rabbil Alamiina

Neno la Kiarabu ‘Rabb’ limetafsiriwa kama ‘Mola’, lakini maana yake ni pana zaidi mno. Mola ni Yeye Ambaye kwamba, kwake Yeye vitu vyote hutegemea kwake kwa kuwepo kwao. Kwa vile neno ‘Rabb’ hufuatiliwa na neno ‘Alamiina’, hufuatilia kutoka hili kwamba Allah (s.w.t.) ni Mola Ambaye kwamba juu Yake wwalimwengu wote hutegemea kwa ajili ya kuwepo kwao.

Walimwengu katika mjadala hapa yaweza kuoanishwa katika njia nyingi. Ainisho moja lwaeza kuwa vitu visivyoonekana kwa macho; vingine vitakuwa ulimwengu wa jamii ya wanadamu, ulimwengu wa jamii ya wanyama, ulimwengu wa mimea n.k. Kwa ufupi, kila mtu na kila kitu ni chenye kuhesabiwa chini ya kichwa cha maneno ‘walimwengu’.

(Firauni alisema: ‘Na nani huyo mola wa walimwengu?’. (Musa) akasema: ‘Muumba wa Mbingu na ardhi na vilivyo ndani katika alamiina’ - 26:23-24)

Katika maneno mengine, kitu chochote na kila kitu mbali na kuwepo kwa Allah (s.w.t.) kinaweza kuchukuliwa kama kuwemo ndani katika ‘alamiina’.

Hata hivyo ‘walimwengu’ yaweza vile vile kusimama kwa watu tofauti katika vipindi vya nyakati tofauti, kama inavyoweza kuonekana kutoka kwenye aya mbili zifuatazo:

(Na Luti aliposema kuwaambia watu wake: ‘Je! mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieeni yeyote kwa hilo katika ulimwengu!’ - 7:80)

(Na (kumbuka) Malaika waliposema: ‘Ewe Mariamu! Kwa hakika Allah amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote)’ - 3:42)

Lakini wakati tunaangalia aya nyingine, tunaona kwamba ‘walimwengu’ vilevile inaweza kukwa na maana ya manadaamu tu, lakini katika wakati wa vipindi vya nyakati zote.

(Ametukuka Yule Ambaye ameteremsha Furqan kwa mja Wake ili awe muonyaji kwa walimwengu (wote) - 25:1)

Maneno ‘Rabbil Alamiina’ huthibitisha sababu ya maneno yaliyopita ‘Al Hamdulillah’, ndani ya hayo (maneno) hutuambia kwamba ni kwa nini sifa zote ni Zake Yeye Allah (s.w.t.) yaani ni kwa sababu Yeye ni Mola wa Walimwengu.

Aya Ya 3

(Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu)

Nilijadili hili hapo juu wakati ninajadili aya ya kwanza. Hata hvyo kuna tofauti ndogo katika maana kwa ajili ya iliyowekwa katika nafasi yake. Wakati ilipounganishwa kwenye ‘Bismillah’ ilitoa maana ya kwamba yatupasa kuanza kwa Jina la Allah (s.w.t.) Ambaye Kwaye Yeye Sifa zote ni Zake, ni Mwenye Rehema na Mola Mwenye Kurehemu wa walimwengu wote.

Mwenye Kurehemu uumbaji wa walimwengu kwa Rehema Zake, ambazo hutumika kwa sawasawa kwa watu wote na kwa Rehema zake ambazo, kama ilivyoelezwa kabla, zinahifadhiwa kwa ajili ya waumini katika ulimwengu ujao (Akhera).

Aya Ya 4

(Bwana Mwenye Kumiliki Siku Ya Malipo)

Baadhi ya wafasir wamehitalifiana katika kusoma kwao (neno la) ‘Maaliki’ lenye maana ya Bwana na wamelisoma kama ‘Maliki’, lenye maana ya Mfalme. Hata hivyo maana ya kwanza ni sahihi zaidi kwa sababu Mfalme anaweza kuwa na mamlaka juu ya watu wake kwa hakika bila kuwamiliki, ambapo kwamba Bwana sio mtawala tu bali vile vile ni mmiliki. Ufalme ni wa Bwana lakini Mfalme ni mtawala tu juu yake.

‘Bwana’ hapa ina maana pana sana na kubwa mno isichukuliwe kama maana ya kawaida tunayoitana sisi wenyewe.

(Leo Ufalme ni wa nani? Ni wa Allah Mmoja, Mwenye Nguvu (zote) - 40:16)

Swali la kujiuliza hapa ni je, Allah (s.w.t.) sio Bwana wa siku zote na nyakati zote? Basi kwanini kutajwa huku kuwe ni siku ya malipo tu?

Jibu kwa hili ni kwamba ingawa mpaka leo Allah (s.w.t.) ni Bwana, lakini kuna watawala tofauti na wafalme wanaotawala juu yetu vile vile; ambapo katika siku hiyo maghsusi hakuna mamlaka nyingine au sheira itakayotumika isipokuwa mamlaka ya Mungu na Sheria ya Mungu.

Mamlaka kamili itakuwa Yake (s.w.t.) kiasi kwamba hata uombezi utatolewa kwa Amri Yake (s.w.t.). Yatakikana iwekwe akilini kwamba siku hiyo Allah (s.w.t.) hataonekana kwa sababu kiwezekani kwa Yeye kuonekana. Amri ya Mungu siku hiyo itatolewa na watu watuele, mtu ambaye atakuwa na mamlaka ya ujumbe wa kufanya maamuzi ya kufaa.

(Tena nini kitakachokujulisha siku hiyo ya malipo ni siku gani hiyo? Ni siku ambayo nafsi haitamiliki nafsi (nyingine) chochote; na amri siku hiyo itakuwa ya Allah (tu) - 82:18-19)

Aya Ya 5

(Wewe tu ndiye tunaykuabudu, na Wewe tu ndiye tunayekuomba msaada)

Ibada itakuwa ni ibada ya kweli tu pale inapofanywa kwa nia ya kweli na pale mazingatio ya mwenye kuabudu yanapolenga si juu ya mwingine yoyote kuliko Allah (s.w.t.). Matamanio juu ya pepo au hofu ya moto wa jahannamu vinaelekea kuchafua usafi wa nia wakati wa Ibada.

Mwenye kuabudu anaweza kutokuwa na uhusiano na nafsi yake mwenyewe, kwani inaweza kufikia kwenya majivuno na majisifu ambavyo viko kinyume kabisa na unyenyekevu na utumwa.

Kama tulivyoona waziwazi, aya hiyo hapo juu iko katika hali ya wingi, hapo ambapo kabisa inapinga upeke wa mwenye kuabudu, kuondoa kajisifu na kufuta majivuno. Inamfanya mwenye kuabudu kujihisi kwamba hayuko peke yake katika kumuabudu Allah (s.w.t.) ila ye sehemu tu ya kundi la mwenye kuabudu.

Ingawa sentensi hii ina nguvu sawa kwa Sala za pekee, nafasi ya Sala za jamaa daima itakuwa juu. Ujenzi wa sentensi hii katika hali ya msingi inatuhimiza sisi kushiriki kwenye kwenye Sala za jamaa ikiwezekana, kuliko kusali peke yako.

Tonaposoma kwamba tunatumikia Allah (s.w.t.) peke Yake inatufanya sisi tutambue kwamba ni watumwa tu, na kwamba mtumwa hamiliki chochote. Baada ya kumkiri Allah (s.w.t.) kama Mola Pekee, kisha tunaendelea kusema kwamba ni kutoka kwake tu ambako tunaomba msaada.

Huu ndio unyeyekevu kamili unaotakiwa na Allah (s.w.t.).

Hakuna yoyote tunayepaswa kumnyenyekea isipokuwa Yeye, Mola wa Ulimwengu.

(Sema: Hakika Sala zangu na sadaka zangu na uhhai wangu na kifo changu vyote ni kwa ajili ya Allah, Mola wa Ulimwengu wote - 6:162)

Kwa Nini Tuseme ‘Ya Ali Madad?’

Allah (s.w.t.) haji Yeye Mwenyewe kutusaidia, lakini badala yake Yeye (s.w.t.) anawatumia watu wengine kuja ktusaidia, au anafanyiza mazingira ambayokwayo tunasaidika.

Kusema ‘Ya Ali Madad’ hakuwezi kuainishwa kama ushirikiana kwani tunamuomba Ali (a.s.) atusaidie sisi kwa idhini ya Allah (s.w.t.). Kama ambavyo, ingawa sifa zote zinastahiki kwa Allah (s.w.t.), kule kumsifu mtu mwingine yeyote kwa kufanya tendo jema hakuwi na ushiikina ndani yake, halikadhalika kumuomba mtu mwingine mbali na Allah (s.w.t.) hakuwezi kuwa na ushirikina. Kwa hakika, Allah (s.w.t.) Mwenyewe ametangaza ndani ya Qur’an Tukufu kwamba kama temetenda dhambi msamaha ili kwamba tuweze kusamehewa.

(Na hatukumleta Mtume yoyote ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na lau wangalikujia walipojidhukumu nafsi zao na wakaomba msamaha wa M’mungu na Mtume pia akawaombea msamaha, wangemkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu - 4:64)

Kwa nini hawakuambiwa kwenda msikitini wakaombe msamaha moja kwa moja kutoka kwa Allah (s.w.t.) Mwenyewe?

Kwa nini wakambiwa kuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na msamaha wake ukafanywa sharti la awali kwa kusamehewa kwao na Allah (s.w.t.) Mwenyewe? Hii inatufahamisha kwamba kama tumemkosea Mtume yoyote basi msamaha kutoka kwa Mtume yule ni sharti la awali kwa msamaha wetu kutoka kwa Allah (s.w.t.).

Ali (a.s.) ndie mtu pekee aliyedai kwamba yeye (a.s.) atakuwepo kutusaidia sisi hata ndani ya makaburi yetu. Mwingine yeyote angeleta dai kama hili basi tungeweza kufikiria kwaita kwa ajili ya kutusaidia, lakini hakuna sababu ya kumwita mtu kutusaidia ambaye hakuwa tayari kumsaidia hata Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika nyakati za shida. Ni vipi mtu kama huyo atatusaidia?

Aya Ya 6

(Tuongeze katika njia iliyonyooka)

Huu ndio moyo (kiini) cha ‘Al Fatiha’ na kusudio hhasa la matumizi yake. Hii ndio sababukubwa ya kwa nini tumemtukusa Allah (s.w.t.) ya kuukiri miliki Yake juu yetu pale mwanzoni. Tulitaka kitu fulani kutoka kwake, na hilo ndio lilikuwa lengo zima la zoezi hili, uongofu kwenye njia iliyonyooka, au kama wafasiri wengine walivyoiweka, uongofu wa kuweka kwenye njia iliyonyooka.

Hiyo njia iliyonyooka ni kipande kifupi kati ya vituo viwili, na kwa hiyo kunaweza kuwa na njia moja tu iliyonyooka. Katika kituo kimoja yupo Maabudu, na katika hicho kituo kingine yupo Allah (s.w.t.). Inafuata kwamba hiyo njia iliyonyooka tunayoitafuta kaitakuwa na upotovu ndani yake wowote ule. Aya hii kwa hakika lazima itazamwe katika muungano wa pamoja na ile inaofuata ambayo inaelezea ile njia iliyonyooka ambayo tunaiomba, kutoka kwa Allah (s.w.t.). Kwa wakati huu, hata hivyo nitajiwekea mipaka katika kuielezea hiyo njia yenyewe iliyonyooka.

Swali moja linalonijia akilini kila mara ni kwamba, ikiwa tunaomba kuwa katika njia iliyonyooka zaidi ya mara kumi kwa siku kwa muda wote wa maisha yetu, hii ina maana maombi yetu yanapita bila kujibiwa au kwamba tunaomba kitu ambacho tumekwisha kipata? Ukweli ni kwamba tunamuomba Allah (s.w.t.) sutuongoza kwenye njia iliyonyooka kila siku ili kwamba Aweze kutuongoa kwenye kiwango cha juu, kutusogeza sisi daima karibu Yake.

Hivyo ni vipi kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Maimam (a.s.) ambao walikuwa daima kwenye njia iliyonyooka na kwa hiyo hawakuwa na haja ya kuongozwa? Kwa swali hili, natoa ule mfano wa balbu ya taa iliyo washwa na kutoa mwanga. Haichukui muda mrefu kuamua kwamba inafululiza kulishwa na kituo cha umeme. Ule muda ambapo ugavi unakatika, ile balbu itakoma kutoa mwanga. Kadhalika huu ndio msimamo wetu kwamba, tunapaswa kufululiza kupatiwa mwongozo kutoka kwa Allah (s.w.t.) na kwa hiyo inafuata kutoka hapa kwamba tunapaswa kuendelea kumuomba.

Muda ambapo muongozo huu unakatwa tutakuwa tuna thamani sawa na balbu iliokatwa fiuzi itakavyokuwa katika giza. Hii ndio hali ya wasioamini.

Imam Ali (a.s.) amesema: ‘Endeleza juu yetu msaada wako ambao kwao sisi tumekutii katika siku zetu zilizopita, ili kwamba tuendelee kukutii katika siku zetu zijazo pia.7’Ule mfululizo wa kupata muongozo haunabudi udumishwe.

Imam Al Sadiq (a.s.) amesema: ‘Njia iliyonyooka ni Ali (a.s.)’. Kisha aliendelea kueleza: ‘Hiyo njia iliyonyooka ni njia ya kwenye elimu ya Allah (s.w.t.), na kuna njia mbili, moja katika dunia hii na moja katika ile ijayo. Na kwa ile njia katika dunia hii, ni yule Imam ambae utii juu yake ni wajibu; yeyote anyemjua katika dunia hii na akafuata muongozo wake atakuja kupita juu ya ile njia ambayo ndio darafa juu ya Jehannam katika huo ulimwengu ujao; na yoyote yule ambae hamjui yey katika dunia hii, mguu wake utakuja kuteleza juu ya daraja ile na atakuja kuangukia kwenye moto wa Jehannam’.8

Mpaka haoa itatosha kuongeza ile hadithi ya Mtume (s.a.w.): ‘Hakuna mtu atakayeweza kuvuka ile daraja ya akhera bila ya idhini ya maandishi kutoka kwa Ali (a.s.)’.9 Zipo hata hivyo, hadithi nyingi zinazoashiria kwa Mitume na Maimamu kama wao ndio njia iliyonyooka. Sio hivyo tu, kamaingekuwa tuzihesabu kerufi zinazounda ‘Al Siraa Al Mustaqeem’, zizngefikia kumi na nne. Hata kama hatutahesabu ile ‘Al’ iliyoko mwanzoni, itakuwa bado ni kumi na mbilitunayoiangalia. Kama hii haituambii kitu, basi hakuna kitakachotuambia kitu.

Aya Ya 7

(Njia ya wale uliowanemesha, sio ya wale walioghadhibikiwa, wala ya wale waliopotea)

Kwa wepesi wa kkuelewa tunaweza kuigawa aya hii katika sehemu tatu; wale watu ambao juu yao Allah (s.w.t.) Ameshusha neema Zake, watue ambao juu yao Ameshusha ghadhabu Zake, na wale watu ambao wamepotea.

Hili ndio kundi la kwanza la watu kujadiliwa katika aya hii na hawa kwa hakika ndio watu ambao wako katika njia ili iliyonyooka, na njia ambayo kwayo tunaomba tuongozwe.

Kuna aya nyingi katika Qur’an Tukufu zinazoashiria kwa watu ambao juu yao Allah (s.w.t.) ameweka neema Zake, husuan Mtume (s.a.w.).

(Na kwenye kumtii Allah na Mtume, basi wao watakuwa pamoja na wale aliowanemeesha Allah miongoni mwa mitume, wakweli na mashahidi na watu waadilifu; na uzuri ni wa hawa kama marafiki - 4:69)

Katika uwanda wa Ghadir Khum, wakati aya ifuatayo ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume alitangaza kwa Wislamu kwamba inawapasa kumkubali Ali (a.s.) kama Bwana (Mawla) baada yake (s.a.w.). katika hali ile ile kama walivyomkubali yeye mwenyewe.

(... Leo nimekukamilisheni dini yenu, na kukutimizeni neema yangu, na nimekupendekeni Uislamu uwe dini yenu . . . - 5:3)

Nukta ambayo nataka kusisitiza hapa ni kwamba neema zote zilikamilishwa siku ile wakati Ali (a.s.) alipoteuliwa kama Bwana (Mawla) katika maana ile ile kama aliyokuwa nayo Mtukufu Mtume (s.a.w.), na kwa kiyo inakuwa dhahiri kwangu kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Ali (a.s.) walifikiwa ni watu ambao kwao ni njia tulipaswa kuomba kutoka kwa Allah (s.w.t.) hususan wakati tunaangalia kwenye hili katika ,wanga wa hadithi iliyotangulia kutajwa ambayo nimeeleza wakati ninajadili aya iliyopita ya sura hii, kwamba Ali (a.s.) ni njia iliyonyooka. Hii huzidi kutiliwa nguvu zaidi na aya ifuatayo :

(Na tukataka kuwafanyia ihsani wale waliodhoofishwa katika ardhi hiyo na kuwafanya viongozi, na kuwafanya warithi - 28:3)

Hii ndio njia iliyonyooka ambayo kwayo tunaitaja muda wa kusoma sura hii, wakati Allah (s.w.t.) alipokamilisha neema zake na kumfanya yeye (a.s.) kuwa Imamu. na akamfanya yeye kuwa mrithi.

Kundi la watu ambao hustahiki zaidi ghadhabu ya mungu ni lil la watu wasioamini (makafiri).

(. . . Na wamejifanya wenyewe wastahili ghadhabu juu ya ghadhabu, na watakuwa nayo makafiri adhabu ya kudhalilisha - 2:90)

Aya hii, hata hivyo, haionyeshi muda kamili ambao ukosaji imani ulienea katika nyoyo za watu hawa. Ninachomaanisha kusema ni kwamba sio lazima kwa mtu kwamba awe si muumini maisha yake yote kabla hajastahili ghadhabu ya Mungu lakini kwamba ghadhabu ya Mungu inahusika kwa yeyote ambae hana imani katika moyo wake ya aina yoyote, angalau kwa muda ule.

Kwa mfano, kama mtu si muumini kwa miaka arobaini na kisha akawa muumini, basi kwa kiasi cha miaka ile arobaini ya uhai wake alikuwa akistahili ghadhabu ya Mungu.

(Anayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake, isipokuwa yule ambae ameshurutishwa, hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya imani yake, lakini anayekifungulia ukafiri kifua chake, hawa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iko juu yao, na watapata adhabu kubwa - 16:106)

Mfano mmoja wa kufuzu kuingia ndani ya vifua vya waumini utakuwa katika medani ya vita vya kulinda Uislamu. Sio kila muumini alikuwa na shauku ya kifo cha kishahidi na kupata ile fahari ya kujumuika na wale ambao juu yao, Allah (s.w.t.) amewashushia neema, na walikuwapo wengine ambao matumaini yao katika imani yalitingishwa na wengine hata waligeukia kwenye kufuru.

(Enyi muliamini! Mkutanapo na wale waliokufur wakielekea vitani, basi msiwageuzie migongo, na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa amegeuka kwa kumshambulia au amejitoa akaungane na wenzie - basi atakuwa anastahili adhabu ya Mwenyezi Mungu na mahali pake ni Jehannam; na patakuwa ni mahali pabaya pa kushukia - 8:15-16)

Mpangilio huu wa matukio ya baadae ulitumika vizuri sana wakati wa vita vya Uhudi wakati wengi wao wa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) walipokimbia medani ya vita, wakimuachia ajilinde mwenyewe. Ali (a.s.) alikuwa peke yake kabisa, mbali na wachache wengine ambao hawakukimbia. Na alipoulizwa ni kwa nini yeye (a.s.) hakukimbia, yeye (a.s.) alijibu: “Niingie kwenye ukafiri baada ya kuwa nimenyenyekea kwenye Uislamu?”10 Hio inaeleza hali ya imani ya wale waliokimbia.

Katika historia yote tumeona kwamba watawala wa Kislamu wamekuwa wa mbele sana katika kumwaga damu za Waislamu, na kama inavyoweza kuonekana kkutoka kwenye aya inayofuata, ni wenye pia kustahili pia ghadhabu ya Mungu.

(Na mwenye kumua Muumini kwa makusidi, basi malipo yake ni Jehannam, humo atakaa milele, na Mwenyezi Mungu atamghadhibikia na kumlaani na kumuandalia adhabu iumizayo - 4:93)

Aliye maarufu sana miongoni mwe wale ambao waliuliwa na watawala wa Kiislamu, hawakuwa wengine wowote isipokuwa wale Maimamu kumi na moja (a.s.) ambao juu yao Allah (s.w.t.) Ameshusha neema Zake, na njia yao ambayo kila mmoja alipaswa kuwa anaitafuta.

Jambo moja muhimu la kuangalia ni yale matumizi ya neno ‘Ghayr’ linalotenganisha zile aina mbili tofauti za watu. Athari ya neno hili ni kufanya makundi haya mawili ya watu yasiochanganyikana.

Wale ambao Allah (s.w.t.) amewapa Neema hawawi, na hawajawa kamili, ni wale ambao juu yao ghadhabu ya Mungu imekuwa ikitumika. Kwa upande mwingine, wale wanaostahili ghadhabu ya Mungu hawajawa kamwe wale ambao juu yao Allah (s.w.t.) Ameshusha Neema juu yao.

Wale ambao wamepotea, ni watu walipotea wanaochanganyika hapa na pale, wakati huo maisha yao yanatoweka taratibu. Hawana malengo katika maisha, na wako kama majani ya nyasi yanayoyumba kulingana na mueleko wa upepo. Hii ni kwa sababu ya kukosa kwao itikadi au kuwa na imani dhaifu. Kila upotofu, ama kwa maneno au vitendo au hata mawazo, ni ushirikina. Makundi haya ya watu hayahitaji kuwa ni wenye kukufuru maishani, lakini wanaweza kuwa walikuwa waumini kabla na kisha wakaja wakawa waasi.

(Hakika wale waliokufuru, baada ya kuamini kwao, kisha wakazidisha kukufuru, toba yao haitakubaliwa na hawa ndio waliopotea - 3:90)

Kama inavyoweza kuonekana kutoka hapo juu, suala la msamaha kwa mlaaniwa Salma Rushdie halina msingi kwa vyovyote vile itakuwa hali ya kisiasa hapo baadae.

Mfano mmoja kutoka kwenye historia ni wakati wa Nabii Musa (a.s.) wakati mtu mmoja aitwae Bal’am Bin Ba’ur alizoea huko nyuma kuishi huko. Alikuwa ni mtu mkubwa na alikuwa na mawasiliano ya Allah (s.w.t.) ya Allah (s.w.t.) na maombi yake yayakuwa yakienda bila kujibiwa. Lakini wakati Firauni alipomlipa, alikubali kuomba kwa ajili ya kuangamia kwa Mtume Musa (a.s.). Alipotoka juu ya punda wake, aya hi ifuatayo ilishuka ikimtaja yeye kama mbwa. Ni wazi kwamba alikuwa katika wale waliopotea na hatutaki kuwa katika nijia ya watu kama hao, bila kujali ni nini matakwa ya wengi yatakavyokuwa.

(Na wasomee habari za yule tuliempa aya zetu, lakini akajivua nayo mwenyewe, hivyo shetani amemuandama, hivyo yuko katika wale waliopotea. Hivyo mfano wake ni kama mfano wa mbwa . . . - 7:175 & 6)

Hii inaniongoza mimi kuhitimisha kwamba yoyote yule anayetoka kwa nia ya kumuua Mtume wa Allah (s.w.t.) ni wa kufananishwa na mbwa. Nikiandamana na historia, nafikiri kwamba hapa nigetaja baadhi ya mambo ya hadhi ya Abu Talib (a.s.). Inanishikitisha kuona, katika vitabu fulani ambavyo sitaki kuvitaja hapa, kuhusu baba yake Ali (a.s.) kama kafir.

Tunajua kwa uhakika kwamba mtu kafir ni adui wa Allah (s.w.t.) na kwa hiyo ikiwa Muumini hapaswi kufanya urafiki na watu kama hao, hili suala la Mtukufu mtume (s.a.w.) kufanya hivyo halitokezei. Na kwa vile kwaw desturi katika uhai wake wote Mtukufu Mtume (s.a.w.) alimtegemea sana Abu Talib (a.s.) kwa aina zote za msaada, na alimchukulia yeye (a.s.) kama baba yake, kwa hivyo sina hiari ila kuhitimisha kwamba hangeweza kuwa kafir.

(Enyi milioamini! Msiwafanye adui Zangu na adui zenu kuwa marafiki . . . Na anyefanya hivi miongoni mwenu basi hakika amepotea kutoka kwenye njia iniyonyooka - 60:1)

Propaganda ya aina hii ya kuaibisha majina ya watu mbalimbali haikuishia kwenye uhusiano wao na Ali (a.s.), lakini ilikwenda mpaka kufikia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) ambae alichukuliwa kama aliyekuwa akifanya makosa wakati wa sala n.k., si katika vitabu vingine mbali na vile vilivyochukuliwa kama ‘vitabu sahihi sita’ vya hadithi vya wengine wa Waislamu. Hii aya ifuatayo inaangamiza mazoea yote ya kidhalimu ambayo yamejipenyeza katika vitabu vya Waislamu kwa miaka.

(Naapa kwa nyota inapoanguka, kwamba sahibu wenu (Muhammad (s.a.w.) hakosei wala hapotei - 53:1-2)

Hapa ninahitimisha maelezo yangu juu ya sura hii na ninaomba msamaha kutoka kwa Mwenye Enzi Mola wa ulimwengu kama nimeshidnwa katika wajibu wangu.

Al Hajj Bashir Alidina
________________________
1. Tafsir Namoona - Juz 1

2. Tafsir Al Mizan - Juz 1

3. Tafsir Namoona - Juz 1

4. Tafsir Namoona - Juz 1

5. Tafsir Anwa Un Najaf - Juz 2

6. Tafsir Al Mizan - Juz 1

7. Tafsir Al Mizan - Juz 1

8. Tafsir Al Mizan - Juz 1 - Tafsir Al Ayyashi

9. Al Istiyab - Juz 2

10. Kitab Al Irshad

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ