Rafed English

Kupaka Juu Ya Khofu

Kupaka Juu Ya Khofu by : Sheikh Jafar Sub’hani

 

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "Al-Mas’hu ‘Ala ‘l-Khuffayn" Sisi tumekiita: "Kupaka Juu ya Khofu."

Kitabu hiki, "Kupaka Juu ya Khofu" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Jafar Subhany.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake.

Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wame- hitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo.

Kupaka juu ya Khoffu mbili ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu.

Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitila- fu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kus- ababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Harun kwa kukubali juku- mu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam, Tanzania.
Sifa njema ni zake Allah (s.w.t.). Rehema na amani zimwendee Mbora wa viumbe na hitimisho la risala Muhammad (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.). Wao ni kasha la elimu yake, na wahifadhi wa Sunnah yake. Kwa hakika Uislamu ni itikadi na sharia, itikadi ni kumwamini Mungu na siku ya mwisho, na mitume wake.

Na sharia ni hukumu za kiungu ambazo zinadhamini maisha bora ya kibinadamu na kuuhakikishia (ubinaadamu) maisha ya furaha duniani na akhera. Sheria ya Kiislamu imebainika kwa uenezi, na kuweka vitanzuaji vya matatizo yote ambayo humkabili mwanadamu katika fani zote za maisha, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:
الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ{3}
“Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema YangunanimewapendeleeniUislamuuwedini yenu.”(Al-Maidaah - 5:3).
Ila tu kuna mas’ala za kimatawi ambazo kwazo wanachuoni wametofautiana kwa sababu ya kuhitilafiana kwao katika yale yaliyopatikana miongoni mwa athari zilizopatikana kutoka kwa mfikishaji risala, Nabii mwenye hadhi, ni jambo ambalo limesababisha kutofau- tiana kwa neno lao katika hizo mas’ala. Na kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti, basi tumejaribu katika darasa hizi zilizoko katika mlolongo kuziweka juu ya meza ya utafiti, huenda ikawa ndio njia ya kulifanya neno liwe moja na kusogeza hatua karibu katika uwanja huu.
Hivyo basi tofauti katika mas’ala hizo sio tofauti za kiini cha dini na mizizi yake kiasi kwamba ifikie kufanyiana uadui na bughudha, bali hii ni tofauti ya yaliyoelezwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), nalo ni jambo jepesi kwa kulinganisha na mas’ala nyingi zilizo katika muwafaqa kati ya madhehebu za Kiislamu.
Na mwongozi wetu katika njia hii ni kauli yake (s.w.t.):
وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا{103}
Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu; vile mlivyokuwa ninyikwaninyinimaaduinayeakaziunganishanyoyo zenukwaneemazakemkawandugu…….1(Al-Imran - 3:103)
SheikhJafarSub’haniy
ImamSwadiqFoundation,
Qum.
Kupaka Juu Ya Khofu Kwa Hiari Katika Makazi Na Safarini
Imeelezwa kutoka kwa wengi miongoni mwa Swahaba na Taabiina kuwa yajuzu kupaka juu ya khoffu mbili, katika hali ya mtu yu nyumbani na safarini kwa hiari, bila ya dharura inay- olazimisha hivyo, na kuwa mtu mzima mwenye akili timamu (mukallafu) ana hiari kati ya kuiosha miguu miwili, na kupaka juu ya khoffu mbili pamoja na kuafikiana kwao kuwa haijuzu kupaka juu ya miguu miwili mahali pa kuosha katika hali ya hiari na ya dharura.

Ila tu kuna kundi miongoni mwa maswahaba na Maimamu katika Ah’lul-Bayti wote, wamekanusha vikali kujuzu kupaka juu ya khoffu mbili, maneno yao yanakujia kikamilifu na wa mwanzo wao ni:

1-Imamu Ali bin Abiy Taalib (a.s.).
2-Hibrul’ummah Abdullahi bin Abbasi.
3-Ummul’muuminina Ayah.
4-Abdullahi bin Umar, japo ielezwe kutoka kwake kuwa aligeuza kauli hiyo.
5-Imam Malik katika moja ya riwaya mbili, yeye alikanusha kujuzu kupaka juu ya khoffu mbili katika siku zake za mwisho.

Na Al-Raaziy amesema: “Ama kuhusu Malik moja kati ya riwaya mbili kutoka kwake kuwa yeye alikanusha kujuzu kupaka juu ya khoffu mbili, na hapana ubishi kuwa yeye alikuwa katika elimu ya Hadith ni kama jua lichomozalo lau asingetambua udhaifu wa usemi huo asingelisema hilo.

Na riwaya ya pili kutoka kwa Malik ni kuwa yeye hakuruhusu kupaka juu ya khoffu mbili kwa asiyekuwa safarini na aliruhusu kwa msafiri apendavyo bila ya makadirio katika hilo.2

An-Nawawi ameeleza katika (Al-Maj’muui) kutoka kwa Malik riwaya sita, moja ya hizo:

Haijuzu kupaka,
Ya pili: Inajuzu ila ni makuruhu.
Ya tatu: Inajuzu abadan, nayo ni mashuhuri kutoka kwake na yenye uzito kwa wafuasi wake.
Ya nne: Yajuzu kwa wakati.
Ya tano: Yajuzu kwa msafiri si kwa mkazi. Ya sita: Kinyume chake.3

6- Abubakari Muhammad bin Daudi Adhwahiriy, na yeye ni Ibn Daud ambaye madhehebu ya Dhwahiri hunasibishwa kwake yeye.4

Huu ndio msimamo wa Swahaba na Tabiina na Imamu wa Adhwahiriyah katika mas’ala haya, na la muhimu ni kuzidu- rusu dalili, kwa kuwa ijimai haikuthibiti katika mas’ala haya na imetambua kuwepo kwa tofauti kati yao, na kabla hatujaingia kwenye kiini cha maudhui twaona ni vyema tuionyeshe nukta muhimu hapa.

Kwa kweli kutofautiana katika rai huwa kunafaa tu endapo itakuwa natija ya ijitihadi katika kuzifahamu dalili, kama tofau- ti za wanaoswali katika kuosha miguu miwili na kuipaka, kwa ajili ya tofauti ya ku-atifia (arjulakum) katika kauli yake (s.w.t.) "Na pakeni vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili." -walipotofautiana - kwamba je imeati- fiwa (kuunganishwa) juu ya (sehemu ya vichwa vyenu) hivyo itakuwa hapana budi ipakwe au juu ya (nyuso zenu na mikono yenu) iliyotajwa katika jumla iliyotangulia hivyo itakuwa hapana budi ioshwe!

Kwa ajili hiyo Waislamu wamekuwa makundi mawili tofauti katika hukmu ya miguu.

Na aina hii ya tofauti hufanyiwa taswira endapo tu katika mas’ala kutakuwa na dalili kutoka kwenye Qur’ani na Sunnah iwezayo kufanyiwa ij’tihadi na yafuatia, na yaweza kuwa mahali pa kutofautiana katika kushindana, ama ikiwa hakuna dalili yoyote ya tamko, mbali na kuona tendo la Nabii kuwa yeye alikuwa anapaka juu ya khoffu, tofauti ni ya ajabu sana katika mfano kama huo, kwa sababu yeye (s.a.w.w.) alikuwa anatawadha mbele ya watu, usiku na mchana na watu walikuwa wanashindania kutabaruku na mabaki ya maji ya wudhu wake, pamoja na hivyo maswahaba baada ya kutoweka kwake walikuwa aina mbili, kuna ambao wanathibitisha kupaka juu ya khoffu moja kwa moja, na ambaye anakanusha moja kwa moja, na kuna anayepambanua kati ya asiyekuwa safarini na msafiri, hali ikiwa kundi linalokanusha ni watu waliokuwa wako pamoja naye maisha yao yote akiwa nyumbani na safarini kama Ali na Aisha na walikuwa wanahesabika mfano wa vazi lake!

Kadiri iwavyo dalili ndio ya kufuatwa, kwako sasa darasa la dalili za wanaokanusha. Kwa kweli wametoa hoja kwa Qur’ani na Sunnah na kuafikiana kwa Maimamu katika Ahlul’bayti.
1. Kutolea Hoja Kitabu Kitukufu
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: "Na pakeni vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili."

Kwa hiyo dhwaahiri ya Aya ni faradhi, yaani wajibu kuihu- sisha upakaji miguu yenyewe, na kupaka juu ya khoffu mbili sio kupaka juu ya miguu, na katika Sura Al-Maida iko Aya ya wudhu, nayo ni Sura iliyoteremka kwa Nabii (s.a.w.) mwisho kama alivyobainisha Ummul’muuminina Aisha.

Al’Hakimu ameeleza kutoka kwa Jubayr bin Naufayr, amese- ma: “Nilihiji na nikaingia kwa Aisha (r.a.) na aliniambia: ‘Ewe Jubayr, wasoma Al-Maida?’ Nikasema: Ndio. Akasema: ‘Kwa hakika yenyewe ni Sura ya mwisho iliyoshuka, mukikutacho humo miongoni mwa halali basi kihalalisheni na mukikutacho miongoni mwa haramu kiharamisheni.”

Kisha al’Hakimu alisema: “Hii ni hadithi sahih kwa sharti ya masheikh wawili na wala hawakuiweka (ndani ya Sahih zao).

Na pia imenakiliwa kutoka kwa Abdullah bin Amri, kuwa Sura ya mwisho iliyoteremka, ni Sura ya Al-Maida, na alisema: “Hii ni Hadithi sahihi kwa sharti ya masheikh wawili na wala hawakuiweka, na Dhahabiy amekiri na kuiona kuwa ni sahihi.5

Kwa mujibu huo hatuwezi kuacha zilizo katika Sura hii mion- goni mwa hukumu ila kwa dalili thabiti ambayo yajuzu kwayo kukinasikhi kitabu, ikisemwa yajuzu kufanya hivyo katika hali ya ukazi au safari kwa hiari japo kwa muda mfupi.

Raziy amesema: “Wafasiri wameafikiana kwa kauli moja kuwa Sura hii (Al-Maidah) haina kilichonasikhiwa kabisa ila kauli yake Taala: (Enyi mlioamini msipuuze alama za heshi- ma za Mwenyezi Mungu..) kwa kuwa baadhi yao wamesema Aya hii imefutwa (imenasikhiwa). Na ikiwa hivyo kauli ya wajibu wa kuosha miguu miwili imenasikhiwa.

Kisha habari ya kupaka juu ya khoffu mbili kwa kukadiria kuwa ilikuwa imetangulia kabla ya kuteremka Aya, ilikuwa ni hadithi iliyosimuliwa na mtu mmoja (khabarul’wahid) imenasikhiwa na Qur’an, na lau ingekuwa kinyume chake ingekuwa kwamba hadithi ya mtu mmoja (khabarul’wahidi) ndio iliyonasikhi Qur’an.6 Wala Qur’an hainasikhiwi na khabarul’wahidu na iweje sahihi.
2. Kutoa Hoja Kwa Kutumia Sunnah (Al’ih’tijaju Bi Sunnah).
Al’Bayhaqiy ameeleza kutoka kwa ibun Umar amesema: Nabii (s.a.w.w.) alitawadha mara moja moja halafu akasema: Huu ni wudhu wa ambaye Swala haikubaliwi kwake ila kwa huu. Halafu alitawadaha mara mbili mbili na akasema: “Huu ni wudhu wa ambaye huongezewa ujira mara mbili.” Halafu alitawadha mara tatu tatu na alisema: “Huu ni wudhu wangu na wudhu wa mitume kabla yangu.7”

Wala hapana shaka kuwa Nabii (s.a.w.w) alifanya kitendo (wudhu) kwenye miguu yenyewe wala sio juu ya Khoffu, kwa sababu lau angefanya wudhu juu ya Khoffu mbili isingejuzu isipokuwa kwa wudhu huo na hilo halikupatikana kwa maafikiano. Kutokana mwanga huo mwenye kutawadha na kupaka juu ya Khoffu mbili Swala yake haitokubaliwa kulingana na ufafanuzi wa Mtume.
3. Maafikiano Ya Maimam Wa Ahlul-Bayt (A.S.).
Maimamu katika Ahlul’bayt (a.s.) wameafikiana kuwa yazuili- ka. Na riwaya kutoka kwao zimesaidiana. Tunazitaja miongoni mwazo hizi zifuatazo:

1. Sheikh Tusi ameeleza ndani ya kitabu Atah’dhiibu kwa sanadi iliyo sahihi kutoka kwa Zurara bin A’ayan, kutoka kwa Abiy Jaafar (a.s.), alisema: “Nilimuuliza, je kuna taqiyya katika kupaka juu ya Khoffu mbili?” Akasema: “Katika vitatu simfanyii taqiyya yeyote: Kunywa mvinyo, kupaka juu ya Khoffu mbili na mut‘a ya Hijja.8

2. Sheikh Tusi ameeleza kwa sanadi yake kutoka kwa Abu al- Ward amesema: “Nilimuuliza Abu Jaafar (a.s.): Kwa hakika Abu Dhabyanu amenihadithia kuwa alimuona Ali (a.s.) alimwaga maji kisha alipaka juu ya Khoffu mbili, akasema: Kadhaba Abu Dhabyani, ama balaghaka Qaulu Ali (a.s.), fiikum sabaqal’kitabu al’Khoffayni (Amesema uwongo Abu Dhabyani haijakufikia kauli ya Ali (a.s.), kwamba katika nyinyi kitabu kimetangulia Khoffu mbili)

Nikasema: Je ni ruhusa kati- ka Khoffu mbili? Akasema: la illa min aduwin taqiihi, au thaljin takhafu ala rijlayka (Hapana isipokuwa kwa adui wam- chelea, au kwa theluji wauhofia mguu wako).9

3. Sheikh Tusi ameeleza kutoka kwa Zurara, kutoka kwa Abu Jafar al’Baqir (a.s.) alisema: “Nilimsikia akisema: Umar bin al’Khattabi Swahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kati yao akiwemo Ali (a.s.), akasema: “Mnasema nini kuhusu kupaka juu ya khoffu mbili?” Alisimama Mughiira bin Shu’uba akasema: “Nilimuona Mtume wa Mungu (s.a.w.) akizipaka Khoffu mbili. Ali (a.s.) alisema: “Kabla ya al-Maidah au baada yake?” Akasema: “Sijui." Ali (a.s.) akasema: Sabaqal’kitabu al Khuffayni innama unzilatil’Maidatu qabla an’yuqbadhwa bishahrayni au thalatha. (Khoffu mbili zimetanguliwa na kitabu, iliteremshwa al-Maidah kabla hajafishwa kwa miezi miwili au mitatu.)10

4. Suduqu ameeleza kwa sanadi yake kutoka kwa Thabiti Thamaliy, kutoka kwa Habbabatu al-Walibiyah katika Hadith kutoka kwa Amirul’mu’uminina (a.s.) Alisema: “Nilimsikia akisema: “Kwa kweli sisi ni Ahlul-Bayt hatupaki juu ya Khoffu mbili, basi mwenye kuwa miongoni mwa Shia wetu aongoke na sisi na afanye Sunna zetu.11

Na mahali pengine alisema: “Wala haikuwa inajulikana kuwa Mtume anazo Khoffu isipokuwa Khoffu ambazo alimzawadia Najaashiy na zilikuwa sehemu ya juu ya nyayo iko wazi, hivyo basi Nabii (s.a.w.w.) alipaka juu ya miguu yake miwili akiwa na Khoffu zake, kwa ajili hiyo watu (kwa dhana) wakasema amepaka juu ya Khoffu zake.

5. Ameeleza Suduqu kwa sanadi yake kutoka kwa Al-Aamashi, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad (a.s.) Alisema: “Hizi ni sharia za kidini kwa anayetaka kushikamana nazo, na Mungu akitaka humuongoza: Kutimiliza wudhu kama Mungu alivyoamrisha kitabuni mwake chenye kutamka, kuosha uso na dhiraa mbili mpaka kwenye viwiko, na kupaka kichwa na miguu miwili mpaka kwenye ka’abu mbili mara moja moja na inajuzu mara mbili, na wudhu haubatiliki ila kwa mkojo na kutokwa na upepo, kulala na haja kubwa, na janaba. Na mwenye kupaka juu ya Khoffu mbili atakuwa amemkhalifu Mungu na Mtume wake na Kitabu chake, na wudhu wake hau- totimia, na Swala yake haitoshelezi ... 12

6. (Riwaya) Zilizosaidiana kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa yeye alikuwa anatoa hoja kwa wanaojuzisha, kuwa Kitabu kimeutangulia upakaji juu ya Khoffu mbili.13
Zinazounga Mkono Kauli Ya Kuziwia
Kuna sababu zinazoikazia kauli inayokataza, nasi twazitaja ili kufuata:

7. Yaliyoelezwa kutoka kwa ibun Abbasi (r.a.) alisema: “Waulizeni hao waonaopaka je, Mtume wa Mungu (s.a.w.) ali- paka baada ya kuteremka Al-Maidah? Wallahi Mtume wa Mungu (s.a.w.) hakupaka baada ya kuteremka Al-Maidah, na mimi nipake juu ya mgongo wa mbuzi, katika swala yapendeza mno kwangu kuliko nipake juu ya khoffu mbili.14

8. Na ambayo yameelezwa kutoka kwa Aya kuwa yeye alisema: Kwa hakika nitapendezewa mno miguu yangu zikatwe kuliko kupaka juu ya khoffu mbili.15

Naam imenakiliwa kutoka si kwa mmoja kuwa Ali (a.s.) na Aisha waligeuka mbali na kauli ya kukataza na kusema kuwa inajuzu.

Isipokuwa kauli yao ya kukataza imethibiti kwa watu wote na kugeuka kwao kinyume na waliyosema ni ‘khabarun wahidun isiyofaa kutegemewa mahali hapa. Na kuwa Imamu Ali na (mama) Aisha walikuwa (mara nyingi) pamoja na Nabii (s.a.w.) usiku na mchana wake, itakuwaje isemwe: Ilifichikana kwao jinsi ya wudhu wa Nabii kwa hiyo wakatoa fatwa ya kuzuwia na ukweli ulipowabainikia, wakarudi kinyume na kauli yao?!

9. Kwa kweli kuichukuwa kauli ya kujuzu endapo ingekuwa imekuja nyuma na ushukaji wa Al-Maidah hivyo (kauli) hiyo ingekuwa yainasikhi Qur’an tukufu, na Qur’an hainasikhiwi na khabarul’wahidu, na Wana-usuli wote wameafikiana ila aliye- jitenga kulingana na tuliyokwishasema, basi si muhali Hadith kuwa yapingana na Qur’an tukufu, na imekwisha elezwa kuwa (habari) kutoka kwake (s.a.w.) kuwa alisema: idha ruwia lakum an’niy hadiithun fa a’aridhuhu ala kitabi llahi, fa in wafaqahu faq’baluuhu wa illa fa rudduhu (Mkielezwa hadith kutoka kwangu ipimeni na kitabu cha Mungu, ikiafikiana nacho ikubalini, kama sivyo ikataeni.”16

10. Wameafikiana wanavyuoni wa kisunni kuwa kupaka juu ya ngozi ya mwili haifai badala ya kuosha. Kwa hiyo kauli isemayo kuwa kupaka juu ya Khoffu mbili yatosheleza badala ya kuosha miguu miwili ni jambo la kustaajabisha, lakinzana na akili wazi wazi.

11. Tofauti kubwa kati ya wanavyuoni ni kati ya kujuzu na kutojuzu, (hii tofauti) yasababisha kuanguka kwa riwaya zina- zojuzisha na kutojuzisha, hapo itakuwa hakuna kimbilio ila kurejea kwenye maana ya dhahiri ya Kitabu cha Mungu.

12. Kwa hakika kupaka juu ya Khoffu mbili katika hali ya hiari badala ya kuosha au kupaka lau kungekuwa jambo limethibiti kisheria, maswahaba wote wangelijua na usingetokea mzozo kati yao na lingefikia kiwango cha tawatur, kinyume chake tunaona mzozo kati yao ulishika kasi.

Hayo yote yanajulisha kutojuzu, na lau kwa mfano tu tuseme imethibiti kupaka juu ya Khoffu mbili kutoka kwa Nabii (s.a.w.) yawezekana kuoanisha kati yake na Aya tukufu kwa Sura mbili zifuatazo:

Kuwa Nabii (s.a.w.) alipaka juu ya Khoffu mbili katika muda makh’susi kabla ya kuteremka Aya ya wudhu ndani ya Suratil’Maidah, na Kitabu kimenasikh yaliyokuja katika athari kutoka kwa Nabii (s.a.w.). Kwa hiyo yawezekana kuoanisha kati ya kujuzu kupaka juu ya Khoffu mbili na kulazimika kui- husisha miguu miwili moja kwa moja, Na ambayo yameelezwa kutoka kwa Ali (a.s.) yanasaidiana kuwa sabaqal’kitabu al’khuffayni, yanaishiria hilo.

Na kwamba kupaka juu ya khoffu mbili ilikuwa ni ruhusa kutoka kwa Nabii (s.a.w.) kwa kipindi fulani, ila tu kwamba Kitabu kimenasikhi ruhusa hii.

Nabii alipaka juu ya Khoffu aliyopewa zawadi na Najashi, na zilikuwa sehemu zake za juu ya nyayo zina uwazi haiziwii kuipaka ngozi, hivyo basi Nabii (s.a.w.) alipaka juu ya miguu yake ikiwa na Khoffu zake mbili, hapo watu wakasema: Kuwa yeye (s.a.w.) alipaka juu ya Khoffu zake bila ya kung’amua kuwa yeye (s.a.w.) hakupaka juu ya Khoffu zenyewe bali juu ya miguu yake iliyo na Khoffu.

Kulingana na tulilosema miongoni mwa sababu mbili yawezekana kuoanisha kati ya yaliyonakiliwa kutoka kwa Nabii (s.a.w.) kuwa yeye alipaka juu ya Khoffu mbili, na Kitabu kinafahamisha ulazima wa kujihusisha na miguu yenyewe ndivyo ilivyo kwa Maimamu katika Ahlul’bayt (a.s.) na kundi katika maswahaba na kiongozi wao akiwa Ali bin Abii Talib (a.s.) ambaye Nabii (s.a.w.) alimtambulisha kwa kauli yake:

“Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali, hawatengani mpaka watarejea kwangu kwenye Bwawa la Kauthar.”

Na ni yule ambaye Imam Raziy amesema kumhusu katika mas’ala ya kuidhihirisha Bismillahi - kwa kuwa Imam Ali alikuwa anaona lazima kuidhihirisha Bismillahi katika Swala za jaharia-:

Na mwenye kumchukua Ali kuwa ndio Imamu wake kwa ajili ya dini yake, basi atakuwa kwa hakika ameshikamana na kishiko thabiti katika dini yake na nafsi yake.
Dalili Za Wasemao Yajuzu Kupaka
Kwa hakika umetambua dalili za wasemao kuwa yazuilika, kwa hiyo njoo pamoja na mimi tuzifanyie darasa dalili za wase- mao kuwa yajuzu, nazo ni idadi kadhaa ya riwaya:
Ya Kwanza Riwaya Ya Jarir Bin Abdillah Al-Bujaliy
Wasemao kuwa yajuzu wametoa hoja kwa riwaya ya Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Jarir bin Abdillah al’Bujaliy na imeelezwa kutoka kwa Ibrahim al’ Ad’ham kuwa alisema:

“Sijasikia Hadith nzuri zaidi ihusuyo kupaka juu ya miguu kuliko Hadith ya Jarir.”17

Kwa hiyo Muh’sin ametoa kwa al’Aamashi, kutoka kwa Hammamu alisema: “Jarir alikwenda haja ndogo halafu alitawadha na alipaka juu ya Khoffu zake. Ikaulizwa: “Wafanya hivi?” Akasema: “Ndio, nilimuona Mtume wa Mungu (s.a.w.) alijisaidia haja ndogo halafu alitawadha na ali- paka juu ya Khoffu zake.”

Al’Aamash akasema: “Ibrahim alisema: “Hadithi hiyo ilikuwa inawastaajabisha, kwa sababu Uislamu wa Jarir ulikuwa baada ya kushuka Al-Maidah.”

Na Nawawi aliieleza sababu ya kustaajabishwa kwao na usemi wake: “Kwa hakika Mungu Mtukufu amesema katika Suratil- Maidah: (Basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili.) Lau ungekuwa Uislamu wa Jarir uliu- tangulia uteremkaji wa Al-Maidah ingechukuliwa Hadithi yake kuwa imenasikhiwa na Aya ya Al-Maidah, na ulivyokuwa Uislamu wake umekuja nyuma, tumejua kuwa Hadithi yake yatendewa kazi, nayo yabainisha kuwa mradi wa Aya ya al- Maidah sio mtu mwenye Khoffu, na Sunnah inaifanya Aya kuwa makh’susi, na Mungu ndiye ajuaye.18
Izingatiwe:
Kwanza: Kitabu hakinasikhiwi na khabarul’wahidu. Kwa kuwa Kitabu Kitukufu kina nafasi ya hali ya juu hakikurubiwi na kitu isipokuwa na Sunnah iliyofikia daraja ya tawatur au habari iliyozungukwa na muktadha zinazofaidisha elimu sio khabarul’wahidu sembuse hadithi ambayo anastaajabishwa nayo mwelezaji wake na matendo ya Jarir, lau kama kingekuwa kitu kilichoenea kati ya Waislamu asingestaajabishwa nayo.

Pili: Kwa hakika kuitolea dalili (Khabarul’wahidu) ni tawi la kuwa Uislamu wa Jarir baada ya kuteremka Al-Maida na hilo halikuthibiti, bali lililothibiti ni kinyume chake kwa kuwa alisilimu kabla yake.

Ibun Hajar al-Asqalaniy alisema: “Amekata shauri Ibin Abdil’Bar kuwa Jarir alisilimu kabla ya kufariki Nabii (s.a.w.) kwa siku arobaini, na hilo ni kosa.”

Na katika Swahihaini kutoka kwake kuwa Nabiy (s.a.w.) alisema: “Watu walinyamaza katika Hijjatul-Wadai, na Al-Waqidiy alikata shauri kuwa alikwenda kwa Nabii mwezi wa Ramadhan mwaka wa kumi, na ya kwamba kutumwa kwake Dhul’Khalswat kulikuwa baada ya hivyo, na kuwa yeye alitekeleza pamoja na Nabii Hijja ya kuaga mwaka wake ule – mpaka alisema: “Kwa hakika Sha’abiy alielezea kutoka kwa Jarir kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) alituambia: “Kwa hakika ndugu yenu An-Najashiy amekufa. Tabrani ameitoa, na hii yajulisha kuwa kusilimu kwa Jarir kulikuwa kabla ya mwaka wa kumi, kwa kuwa An-Najashiy alikufa kabla ya hapo. 19

Nasema: An-Najaashiy alikufa zama Mtume yu hai mwezi wa Rajabu mwaka wa tisa wa Hijiria. Adh-Dhahabiyu alisema: “Nabii aliwaambia watu kuwa: Kwa hakika ndugu yenu amek- ufa katika ardhi ya Uhabeshi. Alitoka nao mpaka jangwani na kuwapanga safu, halafu aliwasalisha. Hivyo baadhi ya wanavyuoni walinakili kuwa hilo lilikuwa katika mwezi wa Rajabu mwaka wa tisa wa Hijiria 20

Na imenakiliwa katika Al’mausua ya Kiarabu ya dunia nzima kuwa alikufa katika mwaka wa tisa wa Hijiria sawa na 630 A.D.21

Kutokana na mwanga huu haiwi sahihi kutolea hoja habari ya Jarir, kwa kuwa yawezekana kabisa kuwa tendo la Nabii lilikuwa kabla ya kuteremka kwa Al-Maidah kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo Suratul’Maidah ilinasikh kama alivyosema Ali (a.s.): sabaqal’kitabu al’khofayni.

Lau tuchukulie kuwa Uislamu wake ulikuwa baada ya Suratul’Maidah kwa hiyo itakuwa ni Khabarul’wahidi, Kitabu hakiwezi kunasikhiwa nayo, kwa kuwa Kitabu kina daraja kubwa hailingani na kitu chochote.
Riwaya Ya Al-Mughira Bin Shu'ba
Muslimu ametoa (habari) kwa sanadi yake kutoka kwa Al- Aswadu bin Hilal, kutoka kwa Mughira bin Shu’bah alisema: “Usiku mmoja mimi nikiwa na Mtume wa Mungu (s.a.w.) punde aliteremka na alikidhi haja halafu alikuja nilimmiminia maji kutoka kwenye chombo nilichokuwa nacho, basi alitawadha na alipaka juu ya Khoffu zake Na amezitoa (habari hizi) kwa njia zingine na zote zinaishia kwa Mughira bin Shu’bah.22
Ichunguzwe Riwaya:
Kwanza: Kwa kweli Mughira bin Shu’bah Hadith zake hazichukuliwi kuwa ni hoja kwa sababu ya maovu yake ya hapo kabla ya Uislamu wake na baada ya Uislamu wake japokuwa yeye ana Hadithi kumi na mbili katika Swahihayni. Na latosha tutakalokusomea kutoka ovu lake la kutisha dhidi ya watu wake.

1. Wanahistoria wameeleza: Alisafiri Mughira kwenda kwa al’Muqauqis akiwa na watu kutoka Bani Malik, naye (Al'Muqauqis) aliwazawadia alichowazawadia, walipotoka kwake wakawa Bani Malik wananunua zawadi kwa ajili ya ahali zao, walitoka wakiwa wamebeba pombe.

Mughira anasema: “Tulikuwa tukinywa pombe nikaazimia kuwaua, basi nilijifanya mgonjwa na nikakifunga kichwa changu, na waliweka vinywaji vyao, nikasema:

“Kichwa changu kinauma lakini nitawahudumieni kuwapa kinywaji hawakukataa, nikawa ninawakithirishia, na ninawatolea gilasi zote, hivyo wakawa wanakunywa wala hawajitambui, mpaka walilala wakiwa wamelewa. Nikachupa na nikawauwa wote na nikachukuwa vyote walivyokuwa navyo.

Nikaenda kwa Nabii (s.a.w.) nilimkuta ameketi msikitini pamwe na Swahaba zake, na mimi nikiwa na nguo za njano, nilimtolea salamu. Abubakari akasema: “Mmekuja kutoka Misri?” Nikasema: “Ndiyo.” Akasema: “Wamefanya nini Bani Malik?” Nikasema: “Nimewaua, na nimechukuwa vitu vyao na nimekuja navyo kwa Mtume wa Mungu ili achukuwe Khumsi.” Nabii (s.a.w.) akasema: "Uislamu wako tunaukubali, wala sichukui kitu kutoka mali zao, kwa sababu hii ni khiyana wala hapana kheri katika khiyana." Basi yakanichukua yaliyo karibu na yaliyo mbali. Nikasema: Niliwaua pale tu mimi niko katika dini ya kaumu yangu, halafu nilisilimu hivi punde.

Akasema: "Uislamu unakata yaliyokuwa kabla yake." Na alikuwa amewaua kumi na watatu.23

Hili ni ovu lake linalochukiza katika zama za jahiliya na lafichua ubaya wake wa ndani kwa sababu amewaua watu kumi na watatu katika jamaa zake kwa tamaa ya mali zao. Na Uislamu japo uwe wayakataa yaliyokuwa kabla yake kwa upande wa hukumu ya taklifu, ila tu haubadilishi ubaya wa sera ya mtu aliyokomaa nayo ila kwa kukaa kwenye mlango wa toba na kushikamana na matendo mema na kudumu nayo.

Huu ndio ukurasa mweusi wa maisha yake kabla ya Uislamu, ama baada yake hayakutofautiana sana, na mambo matatu yafuatayo ni ushahidi:

2. Ametoa (khabari) Dhahabiy kutoka kwa Abdillah bin Dhwalim amesema: Mughira alikuwa ndani ya hotuba yake anamkebehi Ali, na aliwaweka makhatibu ili wamkebehi, na alimtajia Said bin Zaid Hadithi kuwahusu watu kumi walioshuhudiwa Jannah.24

3. Kwa hakika Mu'awiyah aliwaweka watu miongoni mwa Swahaba na watu miongoni mwa Taabiina kuelezea habari mbaya kumuhusu Ali (a.s.) zinazosababisha kumponda na (watu) kujiepusha naye, na kwa kazi hiyo aliweka malipo ili kuvutia (kwenye kazi hiyo) na walitengeneza (habari) ambazo zililimridhisha, basi miongoni mwao alikuwa Mughira bin Shu’bah.25

4. Ahmad ametoa katika Musnad yake kutoka kwa Qutbata bin Malik alisema: “Mughira bin Shu'ba alimkebehi Ali, hapo Zaid bin Arqam alisema: Kwa hakika nilijua kuwa Mtume wa Mungu alikuwa anakataza kuwatukana waliokufa, basi kwa nini wamtukana Ali na amekwisha kufa!26

5. Pia ametoa Hadithi za kumkebehi kwake Amirul’Mu’uminin (a.s.) ndani ya Musnad yake katika hotuba yake na ukinzani wa Said bin Zaid dhidi yake.27

6. Ibnul’Jauziy amesema: “Makhatibu walikuja kwa Mughira bin Shu'bah huko Kufa, Swa’aswa’atu bin Suhani alisimama na akaongea, hapo Mughira alisema: “Muombeni na msimamisheni kwenye Mistwabah - yaani benchi - amlaani Ali.” Akasema: “Mungu amlaani mwenye kumlaani Mungu na kumlaani Ali bin Abi Talib.” Walimpa habari ya hilo, akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu mumfunge mikono," akatoka akasema: Kwa kweli huyu anakataa isipokuwa Ali bin Abi Talibi basi mumlaani ili Mwenyezi Mungu amlaani. Mughira akasema: Mtoeni ili Mwenyezi Mungu aitoe nafsi yake.28

Kwa kweli hali yake ya nyuma inaeleza kuwa alikuwa mtu wa ujanja akitumia vibaya ujanja wake ili kufikia malengo yake kwa thamani yoyote ile japo vitaishia kwa hesabu ya Uislamu.

7. Adh Dhahabiy ameeleza kuwa Mu'awiyah alimwita Amri bin al’Aas huko Kufa, na alisema: “Nisaidiye hii Kuufa.” Alijibu: “Vipi Misri?” Akasema: “Muweke mwanao Abdullah bin Amr.” Alijibu: “Basi ni neema, na wao wakiwa katika hali hii Mughira bin Shu'bah alikuja – naye alikuwa Mu'tazila huko Ta'ifu - Mu'awiyah alimnog’oneza, Mughira akisema: “Unamfanya Amr kuwa amiri huko Kuufa na mwanawe huko Misri na wewe unakuwa kama aliyekaa kati kati ya ndevu za simba.” Akajibu: “Waonaje?” Akasema: “Mimi nitaku- tosheleza kuihusu Kuufa.” Akasema: “Basi fanya hivyo.”

Muawiyah alipofikiwa na asubuhi alimwambia Amri: “Kwa kweli mimi nimeona kadha.” Amr alifahamu, na alisema: “Je nisikujulishe Amiri wa Kuufa?” Akasema: “Ndivyo, nijulishe.” akasema: “Ni al’Mughirah, taka msaada wa rai yake na nguvu zake dhidi ya vitimbi, na kwa kuhusu mali mvuwe madaraka, kabla yako walikuwa Umar na Uthmani walifanya hivyo.” Alisema: “Ni neema uliyoona.” Mughira aliingia kwake na alisema: “Mimi nilikuamuru askari na ardhi, halafu nilikumbuka Sunnah ya Umar na Uthmani kabla yangu.” Akasema: “Nimekubali hasa.29

Na Sunna ya Umar na Uthmani zinatosha kuwa dalili kwa kiwango gani mtu alikuwa anafurahia uaminifu na uchamungu katika haki za Waislamu na mali zao!

8. Na ambayo ni ushahidi wa mambo yake ya kuangamiza huyu bwana, na kuwa yeye hakubadilika ni kama vile alivyokuwa zama za Jahilia, ni kuwa yeye alituhumiwa kuzini hali akiwa Amiri wa mji wa Kuufa wakati wa ukhalifa wa Umar bin al’Khattabi na walitoa ushahidi dhidi yake mashahi- di wanne, miongoni mwao:

Abu Bakrah, Naafiu, na Shublu walitoa ushahidi kuwa wal- imuona anaingiza na kutoa na yuaingiza uingizaji wa kijiti cha wanja kwenye kichupa cha wanja. Na shahidi wa nne ambaye ni: Ziyad bin Abiihi alipojaribu (kutoa ushahidi) Khalifa ali- fanya jaribio la kumuepushia mbali na Haddi (shar’i), kwa kigezo cha Shub’ha, alimsemesha kwa kauli yake: “Kwa haki- ka mimi namuona mtu ambaye Mungu hamfedheheshi Muhajiru kupitia ulimi wake.

“Khalifa akamwambia: “Je ulimuona akiingiza kama kijiti cha wanja kwenye kidau cha wanja?” Akasema: “La, lakini mimi niliona kikao kibaya na nilisikia pumzi zilizopanda na nilimuona amemuambata kwa tumbo lake…"30 Kwa hayo alimuepushilia mbali Hadu Shar’ii kwa shub’ha.* Hii ndio nafasi ya huyu bwana kati ya Waislamu, je yawezekana ikubaliwe Hadithi ya mtu kama huyu kulihusu suala la kiibada ifanywayo na Waislamu usiku na mchana wao?!

Pili: Tufanye mfano kuwa yeye ni mtu ambaye Hadithi zake zaweza kuwa hoja, na kwamba Uislamu umekata yaliyokuwa kabla yake, lakini wapi imethibiti kuwa kitendo cha Nabii (s.a.w.) kilikuwa baada ya kuteremka al-Maidah? Kwa kuwa yawezekana kilikuwa kabla yake kwa muda mrefu. Na huyu mtu alisilimu kabla ya sulhu ya Hudaibia ambayo ilikuwa kati- ka mwaka wa sita, na hilo linapata nguvu kwa aliyoyaeleza Ad- Dhahabiy kutoka kwa Abu Idrisa amesema: “Mughira bin Shu'bah alikuja Damaskasi - mji mkuu wa ya Syria - nika- muuliza, akasema: “Nilimtawadhisha Mtume wa Mungu (s.a.w.) katika shambulio la Tabuk; alipaka juu ya Khoffu zake.31
Somo La Riwaya Zingine
Wameeleza si mmoja miongoni mwa wana Hadithi kitendo cha Nabii akiwa safarini au safarini na nyumbani kuwa yeye alipa- ka juu ya Khoffu, na agh’labu ni kunakili kitendo cha Nabii bila ya kutajwa tamko lake. Na kuwa yeye aliamrisha kupaka juu ya Khoffu haikuainishwa hali ya tendo. Na Abubakari al- Bayhaqi amekusanya riwaya zote katika Assunanu, hivyo twataja kiasi kikubwa alichoelezea:

1- Kutoka kwa Saad bin Abii Waqas, kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) alipaka juu ya Khoffu.

2- Kutoka kwa Hudhaifah amesema: “Mtume wa Mungu alik- wenda kwenye jaa la kaumu ya watu akajisaidia haja ndogo wima, halafu aliomba maji. Nilimpelekea maji, alitawadha na kupaka Khoffu zake.

Na alisema: “Bukhari ameieleza ndani ya Sahih kutoka kwa Adam bin Abii Abbasi, na Muslimu ameieleza kwa njia nyingine kutoka kwa al’Aamashi.”

Yatosha riwaya hii kuwa dhaifu kwa kuwa yeye amemnasi- bishia Nabii (s.a.w.) na lisilolingana na daraja yake na nafasi yake, kitu (cha kujisaidia wima kwenye jaa) ambacho hakifanywi ila na watu duni. Vipi anasibishiwe Nabii (s.a.w.) kuwa eti alijisaidia haja ndogo wima hali ikiwa yaliyoelezwa kutoka kwa Ibn Mas’udi kuwa alisema: “Ni katika yanayochukiza uwe wakojoa nawe uko wima.” Na Saad bin Ibrahim alikuwa haupitishi ushahidi wa mwenye kukojoa wima.

Amesema (bibi) Aisha: “Mwenye kukuhadithieni kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) alikwenda haja ndogo wima musimsadiki, alikuwa hajisaidii ila amechuchumaa.”

Halafu Ibnu Qudama alipoinakili (Hadithi hii) alijaribu kuifanya iwe sahihi kwa kauli yake: “Huenda Nabii alifanya hivyo ili kubainisha kuwa inajuzu, na wala hakufanya ila mara moja tu, na yawezekana kuwa ilikuwa mahali ambapo hawezi kuchuchumaa.32 (maelezo hayo ni dhana ya Ibnu Qudama)

Na maelezo ya sababu ya kwanza hayakubaliki, kwa kuwa Mtume alikuwa anaweza kubainisha kuwa inajuzu (kujisaidia wima) kwa maneno yake wala si lazima iwe kwa kitendo ambacho chahesabika kuwa ni miongoni mwa sifa za watu duni wasiojali hukumu za kisheria.

Ibnu Majah ametoa (habari) kwenye Sunanu yake kutoka kwa Umar amesema: “Mtume wa Mungu aliniona najisaidia wima. Akasema: “Ewe Umar, usijisadie wima."33

Kuongezea kuwa dhwahiri ya Hadithi ni kuwa Nabii (s.a.w.) hakujitahirisha haja ndogo kwa hiyo hapana budi isemwe kuna la kufuta na kukadiria katika jumla hii ya Hadith - na endapo ufanywe mfano kuwa Hadith ni sahihi kwa hiyo inakuwa, kinanakiliwa kitendo cha Nabii (s.a.w.) bila ya kuchunga hali zake kwa hiyo (Hadithi kama hii) haiwi hoja ya kukabiliana na Qur’ani tukufu.

Huenda ilikuwa kabla ya kushuka kwa Aya ya wudhu, kwa hali hiyo inadhihiri hali ya riwaya ya Sa'ad bin Abi Waqas kuwa haikuainisha eneo la tendo na kuwa je hivyo ilikuwa kabla ya kuteremka kwa al-Maidah au baada yake?

3- Kutoka kwa Jafar bin Umayyah bin Dwamriy, kutoka kwa baba yake: "Nilimuona Mtume wa Mungu (s.a.w.) amepaka juu ya kilemba chake na Khoffu zake."

Maneno katika Hadithi hii ni yale yale katika Hadithi mbili zilizotangulia. Kutoka kwa Ka’abu bin Ajrata alisema: “Bilal alinihadithia (Hadithi) kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kuwa alitawadha na ali- paka juu ya Khoffu mbili na Khimaru.”

Kutoka kwa Sulayman bin Buraydah kutoka kwa baba yake, alisema: “Nilimuona Mtume wa Mungu (s.a.w.) alitawadha mara moja moja na alipaka juu ya Khoffu mbili, na aliswali Swala zote kwa wudhu mmoja. Umar alisema: "Umefanya kitu hukuwa wakifanya. Akasema: Nimefanya makusudi ewe Umar."

Nasema: Mtume wa Mungu (s.a.w.) alifanya tendo lake hili siku ya al-Fat’hu kabla ya kuteremka Suratul’Maidah kwa ushahidi wa riwaya ya Buraydah alisema: “Aliswali Mtume wa Mungu (s.a.w.) siku ya al-Fat’hu swala tano kwa wudhu mmoja na alipaka juu ya Khoffu zake. Umar akamwambia: “Kwa hakika mimi nimekuona umefanya kitu hujapata kuki- fanya,” akasema: “Makusudi nimefanya.”

4- Miqdamu bin Shariihi ameeleza alisema: Nilimuuliza Aya kuhusu kupaka juu ya Khoffu. Akasema: “Nenda kwa Ali kwani yeye ni mjuzi mno wa hilo kuliko mimi.” Nilikwenda kwa Ali nikamuuliza kuhusu kupaka, akasema: “Mtume alikuwa anatuamrisha apake mkazi mchana na usiku na msafiri siku tatu.”

Haisihi kutolea hoja hadiithi hii na iliyo mfano wa hii ikiwa haijathibitisha eneo la tendo na je kitendo cha Nabii kilikuwa baada ya kushuka Suratul’Maidah!34
Maulizo Kuhusu Mas’ala Ya Kupaka Juu Ya Khoffu
Halafu kuna maswali kuhusiana na mas’ala hii tunayatupa kwenye utafiti na darasa, huenda faqihi mwenye kutoa fatwa ya kujuzu kupaka juu ya Khoffu mbili katika zama zetu hizi atakuwa na majibu: Hapana shaka kuwa wudhu japo uwe ni ibada na (pia) sharti ya kusihi swala lakini wudhu wakati huo huo ni kujitahirisha kwa mtawadhaji.

Mungu anasema mwisho wa Aya ya wudhu:
لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {6}
“…..bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juuyenuilimpatekushukuru."
(Al-Maidaah - 5:6).
Ikiwa wudhu ni kama ghuslu na tayammum ni sababu ya tohara, basi kujiambatanisha na miguu miwili ni tawi sio Khoffu mbili, viatu wala si soksi, kwa kuwa kupaka juu ya vitu hivyo hakuleti tohara ikiwa mikono haitoathiriwa na uchafu ulio kwenye Khoffu, viatu au soksi.

Kwa hiyo kuijuzisha katika ukazi na safari, ni chaguo la wakati au si la wakati ni kinyume na usafi ambao Uislamu umeagiza katika mafunzo yake kadhaa.

Kwa kweli kupaka juu ya Khoffu ni mas’ala ya matawi ya kifiq’hi ambamo maswahaba na Taabiina wametofautiana humo, na ilikuwa mashuhuri kutoka kwa Ali, Ibnu Abbasi, Aya, na Maimamu katika Ahlul-bayt wote, na wengine wanalizuia hilo. Na alikuwa imamu na mwanafunzi wake Hibrul’ummah wanatoa dalili kuwa Aya ya wudhu imenasikhi (hukumu) hii, pamoja na hayo tofauti katika haya hakuvuki nje ya tofauti za hukumu za matawi.

Tofauti nyingi zilioje katika hukumu za matawi (far’iyah).

Pamoja na hayo tunaona Shihabud-diin Ahmad bin Muhammad al-Qastalaniy ndani ya sherehe yake ya Sahih Bukhari ananakili kutoka kwa al’Karkhiy kuwa alisema: “Nahofia ukafiri kwa asiyeona (jaizi) kupaka juu ya Khoffu mbili, na wala kupaka hakujanasikhiwa na Hadithi ya Mughira katika vita vya Tabuk navyo ni vita vyake vya mwisho (s.a.w.) na Al-Maidah iliteremka kabla yake katika vita vya Al’Marysi’i, naskhi ya kupaka iko wapi 35

Katika maneno yake haujifichi udhaifu.

Kwanza: Alilosema haliepukani na kukithirisha katika kauli. Hivi kuna ulazimiano gani kati ya kutojuzu kupaka juu ya Khoffu mbili na kutoka nje ya uwigo wa Kiislamu, na wala katika mas’ala ila ni Khabarul’waahidu kama habari ya Mughira haifidishi elimu wala (wazo la) mkato.

Na aendaye kinyume na kauli hiyo kumtuhumu ukafiri ni uovu uangamizao, Mtume wa Mungu (s.a.w.) amenena: (Idha kafara rajulun akhahu faqad baa’a biha ahaduhuma) (Mtu akimkufurisha nduguye atakuwa amerudi nao (ukafiri) mmoja wao).36

Pili: Ni kwamba al-Maidah iliteremka kabla ya kutoweka kwake (s.a.w.) kwa miezi mitatu au chini yake. Ama vita vya al-Marysi,i vilikuwa katika mwezi wa Shabani mwaka wa sita wa Hijiria, na kuna kauli yasema kabla yake, ndiyo humo iliteremka Aya ya tayamumu nayo ni ile kauli yake(s.w.t.):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا {43}
(Enyi mlioamini! Msikaribie swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema, wala hali mna janaba, isipokuwa kama mmo safarini, mpaka muoge. Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake, na msipate maji, basi tayamammuni kwa mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu.HakikaMwenyeziMunguniMsamehevunaMwenye maghfira."(An-Nisaa -4:43)
Na ushahidi wa kuwa mzozo kati ya swahaba na Taabiina katika mas’ala ya kupaka juu ya Khoffu mbili ulikuwa umeshika kasi kati ya unyayo na muundi kwa kuwa baadhi ya ambao walikuwa wanaeleza riwaya ya kupaka juu ya Khoffu mbili kutoka kwa Nabii (s.a.w.) wanafanya kinyume chake.

Al-Bayhaqi ametoa riwaya kwa Abdur-Rahman bin Abii Bakar kutoka kwa baba yake kuwa Mtume wa Mungu aliulizwa kuhusu kupaka juu ya Khoffu mbili, akasema: “Kwa msafiri siku tatu na usiku zake, na kwa mkazi siku moja na usiku, na baba yangu (Abu Bakri) alikuwa anavua Khoffu zake na anaosha miguu yake. (As-Sunanul’kubraa): 1/276.

Na madamu mwisho wa Hadithi hii kuna udhaifu wa anayoy- aeleza kutoka kwa Nabii (s.a.w.) kwa kuwa tendo lake lilikuwa kinyume na Riwaya yake, wengi miongoni mwa muhadithina wamejaribu kuisahihisha.37

Kwa kweli dhahir ya riwaya nyingi ambazo Al-Bayhaqi amezinakili katika Sunan yake yaonyesha kuwa yajuzu kupaka juu ya Khoffu mbili katika hali zote mbili safarini na katika ukazi. Na amefanya mlango kwa anuani hii: (Babu mas’hu Nnabii(s.a.w.) alal’Khoffayni fii safari wal’hadhwar).

Na umekwishaitambua riwaya ya Hudhayfa na Usamah kuwa Nabii (s.a.w.) alipaka juu ya Khoffu naye yuko Madina. Na maana yake ni kuwa yajuzu mukalafu achaguwe umri wake wote kupaka juu ya Khoffu mbili, na kuosha miguu miwili ni makh’susu kwa asiyevaa Khoffu mbili. Na roho ya kifiq’hi hairidhiki na kitu hiki wala sera ya mfanya sheria wala hekima ya wudhu.

Endapo utakuwa na shaka na hilo, hizo kwako fatwa za wanafaqihi kwa kusudi hili:

Kundi kubwa la wanafaqihi wa ki-Hanafiy na Shafi’iy na Hambaliy wanaona kuuwekea kikomo muda wa kupaka juu ya Khoffu siku moja na usiku katika hali ya ukazi na siku tatu kwa msafiri, lakini wana-Malikiyah wanajuzisha kupaka juu ya Khoffu katika hali ya ukazi na safari bila ya muda wenye kikomo, kwa hiyo hazivui ila kwa jambo linalowajibisha kuoga, na ni Sunna (nad’bu) kwa mukalafu kuzivua kila wiki mara moja siku ya Ijumaa japo awe hataki kuoga kwa ajili yake, na kuzivua mara moja kila wiki mfano wa siku ile aliyoivaa, na endapo atakuwa amezivua kwa sababu au kwa jambo lingine ni wajibu kuosha miguu miwili.

Na wametolea dalili riwaya ya Ibun Abi Ammaarah, amesema: “Nilisema, ewe Mtume wa Mungu, je nipake juu ya Khoffu mbili? Akasema: “Naam.” Nikasema, siku moja? Akasema: “Na siku mbili.” Nikasema: Na tatu? Akasema: “Naam na upendavyo.”38

Kwa kweli jambo la ajabu hasa (na la kushangaza) ni kuwa wanavyuoni hawakujuzisha kupaka kwa maji ya wudhu juu ya miguu yenyewe si katika hali ya ukazi wala safarini, pamoja na hivyo wamejuzisha kupaka juu ya Khoffu japokuwa Khoffu hazina uhusiano wowote na (wudhu) wa mwenye kutawadha bali zenyewe ni (aina) ya chombo tu cha kuvaa miguuni?!

Halafu kuna ambao wanafanya taswira kuwa hekima ya kujuzu kupaka juu ya Khoffu mbili ni kuwarahisishia na kuwafanyia wepesi mukalafiina (wabeba majukumu) ambao kuvua viatu na kuosha miguu kunawawia mashaka wakati wa majira ya baridi kali, na safarini na wayabebayo katika matu- mizi ili kuendelea na safari.39

Hekima iliyonenwa – endapo ingesihi - ingekuwa wajibu kupa- ka kuwe makh’susi wakati au maeneo ya dhiki na dharura tu. Je hii wapi na wapi na fatwa inayoruhusu bila ya kikomo?

Nadhani kushikilia kubakia na hukumu ya kupaka juu ya Khoffu mbili kulifanyika kwa ajili ya kumkinza Imamu Alii (a.s.) kwa kuwa yeye na watoto wake walikuwa wanadhihirisha kuzuia kupaka juu ya Khoffu. Na wanaojuzisha wameipa mas’ala hii zaidi kuliko yanavyostahiki.

Abubakari bin al’Mundhir amesema: “Tumeeleza kutoka kwa Hasan al-Baswariy, walinihadithia Swahaba wa Mtume (s.a.w.) sabini kuwa yeye (s.a.w.) alikuwa anapaka juu ya Khoffu. Alisema: “Hakuna tofauti katika suala la kupaka juu ya Khoffu… Inajuzu, jamaa kadhaa katika salafu (waliotangulia) wamesema kama hivyo.40

Kama ambavyo Al-Bayhaqi ameyataja karibu majina ishirini ya maswahaba waliojuzisha kupaka juu ya Khoffu miongoni mwao: Umar bin al’Khattaabu, Sa'ad ibn Abiy Waqas, Abdullah bin Mas’udi, Hudhayfa bin al’Yamani, Abu Ayyubu al’Answariy, Abu Musa al’Ash’ariy, Ummar bin Yaasir, Jaabir bin Abdillahi, Amr bin Al’Aas, Anas bin Malik, Saha bin Saad, Abiy Mas’udi al Answariy, Mughiyrah bin Shu'bah, al’Barrau bin Aazibi, Abiy Said al’Khidriy, Jabir bin Samrah, Abu Amamah al Baahiliy, Abdullahi bin al’Harithi bin Juzur na Abu Zaidi al’Answariy.41

Na la ajabu ni kuwa wao wamemuunga Ali (a.s.) na Ibn Abbasi pamoja na hao jamaa ili kuzidisha kuaminika kwa kujuzu (kupaka).
Matawi Ya Mas’ala
Halafu kwa kweli waliosema kuwa kupaka juu ya Khoffu ni jaizi wametofautiana sana mas’ala inaporejea kwenye matawi, kwa hiyo wametofautiana katika maudhui zifuatazo:

Mpaka wa mahali: wametofautiana humo jamaa miongoni mwao wamesema: Ambalo ni wajibu kuhusu suala hili ni kupaka sehemu ya juu mno ya Khoffu na ya kuwa kupaka kwenye tumbo - nakusudia: sehemu ya chini ya Khoffu - mustahabu. Na Maliki ni mmoja wa walioona rai hii, na Shaafi’iy; na miongoni mwao kuna ambao waliojuzisha kupaka nje yake na ndani yake, na hiyo ni madhehebu ya Ibun Naafi’i katika watu wa Malik.

Na miongoni mwao kuna waliojuzisha kupaka nje tu wala hawakufanya mustahabu kupaka ndani, nayo ni madhehebu ya Abu Hanifa, Daudi, Sufyani na jamaa.

Na Ash’habu amekuwa wa pekee, amesema: “Kwa kweli wajibu ni kupaka ndani au juu, yoyote katika mbili hizo apake. Na sababu ya kutofautiana kwao ni kupingana kwa athari zilizokuja katika suala hili na kushabihisha kupaka na kuosha.

Aina ya mahali pa kupaka kwakuwa wasemao hilo wameafikiana kujuzu kupaka juu ya Khoffu mbili na wametofautiana katika kupaka juu ya soksi, kundi limejuzisha na kundi limezuia. Na miongoni mwa waliozuwia hilo: (kupaka juu ya soksi) Malik, Shafiy, na Abu Hanifa. Na miongoni mwa waliojuzisha hilo: Abu Yusuf na Muhammad swahiba wawili wa Abu Hanifa, na Sufiani Thauriy.

Na sababu ya kutofautiana kwao ni katika kusihi athari zilizokuja kutoka kwake (s.a.w.) kuwa alipaka juu ya soksi na viatu. Na pia kutofautiana kwao ni: Kuwa je, yawezekana kuifanyia qiasi Khoffu kingine, au yenyewe ni ibada haifanyiwi qiasi wala haitoki mahali pake?

Hali ya Khoffu, kwa hakika wao wameafikiana kujuzu kupa- ka juu ya Khoffu iliyo nzima na wametofautiana katika iliy- ochanika. Malik na swahiba zake wamesema: “Atapaka juu yake kama mpasuko ni kidogo, na Abu Hanifa amehadharisha kiasi kile kinachochukiza dhahiri yake chini ya vidole vitatu. Na kaumu ya watu wamesema: yafaa kupaka juu ya Khoffu zilizochanika maadam bado zaitwa Khoffu japokuwa mpasuko wake uchukize.

Na miongoni mwa hao walioeleza hivyo kutoka kwake ni al-Thauriy, ama Shafi'i amezuia ikiwa sehemu ya Khoffu mpasuko unaonyesha unyayo, japo kidogo katika mojawapo ya kauli mbili kutoka kwake. Halafu alitaja sababu ya kutofautiana kwao.
Wakati
Kwa hakika wanavyuoni wametofautiana katika wakati. Rai ya Malik, hilo halina wakati ulio na mipaka na kuwa mwenye kuvaa Khoffu atapaka juu yake maadam hajazivua au hajapat- wa na janaba. Na madhehebu ya Abu Hanifa na Shaafiy ni kuwa hilo lina wakati ulioainishwa. Na sababu ya kutofautiana kwao ni tofauti ya athari kuhusu hilo.
Sharti
Sharti za kupaka Khoffu mbili ni: Miguu iwe tohara, tohara ya wudhu na hicho ni kitu muwafaka isipokuwa tofauti zisizo za kawaida. Na imeelezwa kutoka kwa ibnil’Qaasimi kutoka kwa Malik, Ibni Libaba ameitaja katika al’Muntakhabu wengi

wameielezea kwa sababu ya kuthibiti katika Hadithi ya Mughira na wengine, anapotaka kuvua Khoffu akasema (a.s.): “Ziache kwa kuwa mimi nimeingiza (miguu) ikiwa tohara, na mpinzani ameichukulia tohara hii kuwa ni tohara kwa maana yake ya lugha.
Vitanguzi
Tofauti katika vitanguzi vya tohara hii, wao wamewafikiana kuwa ni vitanguzi vile vile vya wudhu, na wametofautiana kuwa je, kuzivua Khoffu kunaitangua tohara hii au hapana? Kaumu imesema: Kwa kweli akizivua na akaosha nyayo zake mbili tohara yake itakuwa imebaki, na kama hakuziosha na akaswali atailipa Swala baada ya kuziosha nyayo zake. Na miongoni mwa waliosema hayo ni Malik na Swahiba zake, Shafiy na Abu Hanifa - mpaka akasema na kaumu wamesema: Tohara yake imebaki mpaka afanye hadathi inayotangua wudhu akiwa hana wajibu wa kuoga. Na miongoni mwa waliosema kauli hii ni Daudi na Ibnu Abiy Layla.

Na amesema Al-Hasan bin Hay: “Akivua Khoffu yake tohara yake itakuwa imebatilika.”42

Na tofauti hizi katika matawi msingi wake ni kauli isemayo yajuzu kupaka kwa hiari, na mzizi ukiwa batili maneno kati- ka matawi ni maneno yasiyo na maana na yasiyo na faida japo wazidishe usemi wasemao kuwa yajuzu.
________________________
1. Aal'Imrani:103

2. Atafsiyrul'kabeeru lirraziy:11\163.

3. Al'maj'mu'u:1\500.

4. Al'maj'mu'u:1\500.

5. Mustadrak al’Hakim: uk. 311.

6. Tafsiyru Raziy: Jalada 11, uk. 163.

7. Assunanul’Kubra:1\80, mlango wa fadhailu tikraru fil’wudhuu. Ibun Majah ameeleza katika Sunanu yake:1/419. na angalia Ah’kamul’Qur’an ya Al’Jaswas:3/351.

8. At-Tah’dhiibu: Juz. 1, uk. 362, Hadithi 1093.

9. At-Tah’dhiibu: Juz. 1, uk. 361 Hadithi 1092

10. At-Tah’dhiibu: /371, Hadithi 1091

11. Al’Faqiihu: Juz. 4, uk. 298.

12. Al’Wasailu: Juz. 1, uk. 279, Hadiithi 18 mlango15 miongoni mwa milango ya wudhu.

13. Sunanul’Bayhaqiy: Juz. 1, uk. 272. Umdatul’Qaariy: Juz. 3, uk. 97. Naylu’Autari: Juz. 1, uk. 223.

14. Al’Mabsutu li Sarkhasiy: Juz. 1, uk. 98; Tafsyir-Raaziy: 11/163, na katika tamko la Raaziy ni: Nipake juu ya ngozi ya punda.

15. A l-Mab’sutu: Juz. 1, uk. 98.

16. at-Tafsir Kabirul-ar-Raziy: Juz.11, Uk. 163.

17. Sharh Sahih Muslim ya Nawawi, Jalada la 3, uk. 164 – 165 Hadithi ya 72.

18. Sharh Sahih Muslim ya Nawawi, Jalada la 3, uk. 164 – 165 Hadithi ya 72.

19. Al’Isaba: Juz.1, uk. 234, na Tarjuma ya Jarir, Na. 1136.

20. Sayru I’ilamu An-Nublaai:1/443. Na. 86.

21. Al’Mausuatul’Arabiyatu al’Alamiyah: 25/220.

22. Sherehe ya Sahih Muslim ya Nawawiy: 3/171, HadithNa.76, na angalia Na. 75 na77 na 78 na 80.

23. Sayru Aalamu Annubalaau: 3/25, tarjuma ya 8.

24. Sayru Aalamu an-Nubala’u: 3/31, tarjuma ya 7.

25. Sherehe ya Nah’jul’balaghah ya Ibin Abil’Hadid: 1/358.

26. Musnad Ahmad: 4/369.

27. Al’Musnad:/188.

28. Kitabul’adh’kiyau cha Ibin al’Jauziy: 142 chapa ya Darul’fikri.

29. Sayru Aalamu Nublau: 3/30, tarjuma ya 7.

30. Sayru Aalami an-Nablai; 3/28, tarjuma ya 8. Al-Aghani: 14/146. Tarikh Tabari: 4/207. Al-Kamilu: 2/228, na rejea nyinginezo nyingi.

* Shub’ha: Ni utata, au hali isiyokuwa wazi.

31. Sayru Aalamu An-Nubalau: 3/22.

32. Al’Mugh’niy: 1/156.

33. Sunan ibn Majah: 1/112, Hadith Na. 309.

34. Ili kufahamu habari za ma’athura hizi angalia Sunanul’Kubra ya al’Bayhaqi: 1/277-270.

35. Rejea Irshadu Saariy: 1/278.

36. Swahihu Muslim: Juz. 1, uk. 56, Kitabul’imani babu man qala liakhihi yaa kaafiru.

37. Ash-Shar’hu al’Swaghiiru: 1/152,153,158; Jawahirul’Iklili: 1/24, na vile vile angalia Al’mausuah Al’fiq’hiyah Al’Kawniyah, Juz.37, (mas’hu).

38. Kitabul’Majmuui Sharhul-Madh’habu lin Nawawiy: 1/505.

39. al’Mausuatul’fiq’hiyah: 38/266.

40. al’Maj’mu’u: 1/501.

41. Sunanu Al-Bayhaqi: 1/272.

42. dayatul’Mujtahid: 1/18- 23.
Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation:
1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na sita

2. Uharamisho wa Riba

3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza

4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili

5. Hekaya za Bahlul

6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8. Hijab vazi Bora

9. Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu

11. Mbingu imenikirimu

12. Abdallah Ibn Saba

13. Khadijatul Kubra

14. Utumwa

15. Umakini katika Sala

16. Misingi ya Maarifa

17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia

18. Bilal wa Afrika

19. Abudharr

20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

21. Salman Farsi

22. Ammar Yasir

23. Qur'an na Hadithi

24. Elimu ya Nafsi

25. Yajue Madhehebu ya Shia

26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu

27. Al-Wahda

28. Ponyo kutoka katika Qur'an.

29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii

30. Mashukio ya Akhera

31. Al Amali

32. Dua kwa mujibu wa Ahlul Bayt

33. Udhuu kwa mtazamo wa Qur’an na Sunna.

34. Haki za wanawake katika Uislamu

35. Mwenyezi Mungu na sifa zake

36. Amateka

37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)

38. Adhana.

39 Upendo katika Ukristo na Uislamu

40. Nyuma yaho naje kuyoboka

41. Amavu n’amavuko by’ubushiya

42. Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

43. Kukusanya sala mbili

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ