Rafed English

Kuanzia Ndoa Hadi Kuwa Wazazi

Kuanzia Ndoa Hadi Kuwa Wazazi by : Abbas na Shaheen Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho From Marriage to Parenthood. Sisi tumekiita, Kuanzia Ndoa Hadi Kuwa Wazazi.


Kitabu hiki kinazungumzia masuala yote yanayohusu wanandoa: kuanzia kufunga kwao ndoa - waishi vipi, mpaka watakapopata watoto - wawalee vipi - kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Kama ambavyo inafahamika kwamba Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha, basi kwa hakika haukuacha hata kitu kimoja kinachohusu maisha ya mwanadamu, pamoja na kumhudumia kiroho. Ndoa ni taasisi ambayo iliasisiwa na Allah ‘Azza wa Jallah Mwenyewe pale alipowaunganisha baba yetu Adam na mama yetu Hawa kuishi pamoja kama mume na mke.

Kwa hiyo, Uislamu kama dini na mfumo wa maisha, umeweka kanuni, sheria na hukumu za kufuatwa ndani ya taasisi hii tukufu (ya ndoa). Waandishi wa kitabu hiki wamefanya juhudi kubwa ya kukusanya mafundisho yote muhimu yenye kuhusu taasisi hii kutoka katika vyanzo vikubwa na chimbuko la sheria na mafundisho ya Uislamu, ambavyo ni Qur’ani na Sunna

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam, Tanzania

Ni pale tu tunapofikiri na kutafakari juu ya mwongozo na hadithi zilizosimuliwa na Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.) tunapoweza kutambua zile hazina walizoacha kwa ajili yetu sisi. Johari hizi za hekima zinaangaza njia kuelekea Mbinguni kwa kutupatia ushauri na maarifa katika kila hatua kwenye maisha yetu.

Kwa bahati mbaya, nyingi ya johari hizi zinapatikana kwa Kiarabu na Kifursi tu, na kuwaacha wasomaji wa Kiingereza (na lugha nyingine) kijisehemu tu cha kile kinachopatikana, hivyo kuwalazimisha kutegemea moja kwa moja juu ya taarifa za kilimwengu ili kuziba pengo hili.

Mbili ya johari hizi ni mafundisho ya kiislam ya mahusiano ya kijinsia baina ya mwanaume na mwanamke, na upatikanaji wa mtoto halali wa ‘kiungu.’

Taarifa hizi kwa hiyo, zimetafsiriwa kutoka kwenye vitabu mbalimbali vya Kifursi na kukusanywa katika kitabu hiki cha mwongozo. Ni matumaini yetu kwamba hiki kitawapatia wasomaji wa Kiingereza mwon- gozo wa Kiislam utakaounganishwa na kutumika sambamba na taarifa nyingine zote zinazopatikana, kumuwezesha mtu sio tu kupata manufaa yake katika dunia hii, bali kumsogeza mtu karibu na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na Pepo.

Taarifa za ndani ya kitabu hiki cha mwongozo zimeegemea kwenye vyanzo sahihi na vya asili vya mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.). Mahali ilipowezekana, hadithi kutoka kwa watu hawa watukufu zimejumuishwa ili kuupa umuhimu ule msingi imara wa Kiislam unaounga mkono yale mapendekezo yaliyotolewa, na vilevile kumtia moyo msomaji katika kuwa mzoefu na maneno ya viongozi wetu katika Uislam. Kwa nyongeza, uingizwaji wa hadithi hizi unatia msisitizo umuhimu unaowekwa na Uislam katika kila kipengele cha maisha, kamwe bila kutuacha sisi tukikosa mwongozo katika hatua yoyote ile.

Katika hatua hii ni muhimu sana kueleza kwamba inawezekana kuwa hao Ahlul-Bayt (a.s.) wamezisimulia hadithi hizi katika muda mahususi, mahali au hali, ambayo taarifa kwa bahati mbaya hazijatufikia sisi. Tumejaribu kiasi cha uwezo wetu kuwaletea hadithi kama zilivyosimuliwa katika vyanzo, ili kwamba ziweze kuwa na manufaa na mafanikio.

Kitabu hiki kinaanza na mjadala kuhusu ule usiku wa harusi, pamoja na amali ambazo zimependekezwa kwa ajili ya usiku huu, kuwawezesha Bwana na Bibi harusi kuanza hatua hii mpya ya maisha yao katika njia nzuri zaidi iwezekanavyo. Kisha hii inafuatiwa na mahusiano ya kijinsia na umuhimu wake katika Uislam, na vilevile mapendekezo kwa ajili ya matendo hayo na nyakati ambazo muungano wa kijisia haswa unaoshauri- wa au usiporuhusiwa.

Mlango juu ya kanuni za kifiqhi zinazotoa taarifa muhimu katika namna rahisi unafuata. Kanuni zote za kifiqhi ni kwa mujibu wa Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Hasan as-Sistaniy. Muqallidin (wafuasi) wa mujtahid wengine wanashauriwa kurejea kwenye risala zao wenyewe juu ya milango hii.

Kuhusu mahusiano ya kijinsia, upangaji wa familia na kipindi cha kushika mimba, mapendekezo ya kiislam yamepewa umuhimu sana kuhusiana na vyakula, matendo na nyakati zake, ili kuandaa mazingira kwa ajili ya kutengeneza mtoto wa halali na mzuri, insha’allah.

Mara tu unapopatikana ujauzito, wote mama na baba wanahitaji kutambua majukumu wa wajibu wao, ili kuwawezesha kuyatimiza haya katika namna nzuri iwezekanavyo. Kwa mara nyingine tena, mapendekezo kwa ajili ya vyakula, matendo na madua vimeainishwa, ili kuanza kumrutubisha na kumlea mtoto huyo kuanzia kwenye hatua hizi za mapema akiwa ndani ya tumbo la mama yake.

Vitendo vinavyopendekezwa kwa ajili ya kujifungua kuliko salama na kwepesi na kwa ajili ya kile kipindi cha mara tu baada ya kujifungua hapo tena vinajadiliwa, kuendelea hadi wakati wa kunyonyesha, ambako kunajulikana kama moja ya haki za mtoto. Hili, halafu linafuatiwa na kanuni muhimu za ziada ya kifiqhi juu ya mama, zikishughulika hasa na suala la nifaas (ile damu anayoona mama baada ya kujifungua).

Mwisho lakini sio kwa umuhimu wake, kitabu hiki kinamalizia na mlango juu ya malezi ya watoto, pamoja na nukta arobaini juu ya namna ya kutendeana na mtoto wako, kudukiza au kuingiza kidogo kidogo mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s.) ndani yao na vidokezo na ushauri wa kuhifadhi Qur’ani kwa wazazi na watoto.

Sehemu hii taarifa muhimu na za kuvutia ambazo kama zitashikwa kikamilifu, zinaweza kutumika ili kupata matokeo chanya na yenye manufaa kwa mtoto.

Ni muhimu kutaja nukta fulani fulani ambazo zinaweza zikazuka katika akili ya msomaji pale anapopitia kile kiwango kikubwa cha taarifa kilichokuwepo. Kwanza, mapendekezo fulani yanaweza kuonekana kuwa maalum sana na mafinyu, kama yale ya nyakati ambazo mtu anapaswa na pale ambapo hapaswi kushika mamba, hata hivyo, ni lazima ikumbukwe kwamba Uislam sio dini ngumu, na mapendekezo haya hayapo ili kuweka vizuizi visivyo na lazima juu yetu. Bali kwa usahihi zaidi, mapendekezo haya yanawekwa pale kwa faida yetu, na Muumba ambaye anatujua vizuri sana kuliko tunavyojijua sisi wenyewe.

Juhudi ndogo kutoka upande wetu sisi zitakuwa zichukue matokeo ya muda mrefu ambayo tunaweza hata pia tusiyatambue. Kwa kweli ni muhimu kuona kwamba mengi ya mapendekezo yamebaki hivyo, ni mapendekezo tu. Tunayotakiwa kufanya sisi ni kuyaendea haya kwa nia sahihi, kuhakikisha kwamba vitendo vya wajibu vinafanyika na kujaribu kwa uwezo wetu wote na hayo mengine, na insha’allah Yeye atakuongoza katika njia iliyobakia.

Pili, wanawake wa Kiislam hususan hasa wanao wajibu wa nyongeza wakati wa ujauzito na baada, kwamba wasifanye yale mambo ya kiafya tu na ushauri unaopaswa kushikwa, bali na mambo ya kiroho pia. Hili zaidi hasa ni gumu kama mimba yenyewe ni ya matatizo. Kwa mara nyingine tena, mtu ni lazima azingatie akilini kwamba manufaa yanazidi gharama zenyewe.

Kwa nyongeza, sio lazima kwamba kila tendo moja lililopendekezwa laz- ima litekelezwe; bali mama mwenyewe lazima aone ni kipi kinachofaa zaidi kwake na kutekeleza kile anachoweza kukifanya kwa ubora wa uwezo wake wote na kuyaacha mengine mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye ni Mjuzi wa yote. Hili hasa linafungamana vizuri kwa kuchukulia kwamba mapendekezo yenyewe yatakuwa na matokeo yanayotakiwa tu kama yakitendwa kwa moyo uliotulia na wenye amani, kuliko wenye wasiwasi na mfadhaiko.

Kweli, katika vipengele vyote vya maisha, Uislam umetoa umuhimu kwenye ‘njia ya kati’ na kukataza mambo ya kuzidi kiasi. Kadhalika, ni jambo la busara kukumbuka kwamba mapendekezo yaliyomo katika kitabu hiki, kila moja lina wakati wake na mahali pake, na hayapaswi kuingiliwa kwa nguvu kupita kiasi, wala kupuuzwa moja kwa moja.

Kwa mfano, moja ya mapendekezo kwa ajili ya mtoto mzuri ni kwamba baba anapaswa kula komamanga; hata hivyo, hii haina maana kwamba baba huyo afanye komamanga kuwa ndio tunda lake peke yake, na hata kulibadilisha kwa ajili ya milo yake mikuu kwani jambo hilo lina madhara na ni hatari. Ni pale tu ambapo njia ya wastani au ya kati na kati itakapofuatwa ambapo manufaa ya kina ya kiroho ya mapendekezo haya yanapokuja kufanya kazi na kuathiri maisha yetu.

Kwa kumalizia, kwa ajili ya mtazamo mpana kwenye maeneo haya, tungependa kupendekeza kwamba kitabu hiki kisomwe kwa kushirikiana sambamba na dua zilizomo kwenye kitabu ‘A mother’s Prayer’* (Dua za Mama) kilichotungwa na Saleem Bhimji na Arifa Hudda.

Tungependa kuwashukuru wale wote ambao wamechangia kwenye kitabu hiki kwa njia moja au nyingine, na kukisaidia wakati wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu awalipe kwa ajili ya kila kitu..

Mwisho, tunaomba msamaha kwenu endapo kuna mapungufu yoyote au makosa ndani ya kitabu hiki; tafadhali tujulisheni na insha’allah, sisi tutajaribu kukiboresha kwa ajili ya wasomaji wa baadae. Maoni au ushauri mwingine wowote unakaribishwa pia. Wakati unapotumia kitabu hiki, tafadhali kumbuka familia zetu katika du’a zako, na pia Marehemu wote kwa kusoma Suratul-Fatihah.

Tunaomba kwa unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atukubalie juhudi zetu hizi, na kama atatukubalia, basi tunaziwasilisha kwa Hadharat Ma’sumah (a.s.) ambao katika ujirani wao tumeikamilisha kazi hii, na Mtukufu Imam wetu wa zama, Imam Mahdi (a.s.).

“Sifa zote njema ni Zake Allah (s.w.t.). Mola wa walimwengu wote.”

*Kitabu hiki kinaweza kununuliwa kutoka Islamic Humanitarian Service kwenye Mtandao kupitia www.al-haqq.com [14]. Ili kuwasiliana na mwandishi unaweza kutuma baruapepe kwa anuani tph@tph.ca [15].

Abbas na Shaheen Merali
1 Julai, 2005
Qum Shariif.

A’mali Za Usiku Wa Harusi

Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Milango ya Peponi kwa ajili ya rehema itafunguliwa katika hali nne: Wakati inaponyesha mvua; wakati mtoto anapoangalia kwa huruma usoni kwa mzazi wake; pale mlango wa Ka’ba unapokuwa wazi, na wakati wa (kutokea) harusi.”1

Kama inavyoonyeshwa na hadithi hiyo hapo juu, dhana ya harusi katika Uislam ni tukufu mno na yenye kuthaminiwa, kiasi kwamba milango ya rehema ya Mwenyezi Mungu inafunguliwa katika tukio hili.

Naam, hili halishangazi pale mtu anapochukulia kwamba ndoa inahifadhi sehemu kubwa ya imani ya mtu na kuilinda na uovu wa Shetani, kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakuna kijana yeyote atakayefunga ndoa katika ujana wake, isipokuwa kwamba shetani wake anapiga makelele akisema: ‘Ole wake, ole wake, amezikinga sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutokana na mimi;’ kwa hiyo mwanadamu lazima awe na taqwa (mwenye kumcha Mungu) kwa Mwenyezi Mungu ili kulinda sehemu moja ya tatu ya imani yake iliyobakia.2

Ni muhimu kwa hiyo, kwamba wawili hao, pale wanapoingia kwenye hatua hii, wachukue hadhari ya hali ya juu kulinda usafi wa muungano huu mtukufu na wala wasiutie doa tangu mwanzoni mwake kwa kuruhusu lile tukio la sherehe ya harusi kuwa ni chanzo cha madhambi na israaf.

Hususan ule usiku wa harusi ndio usiku wa kwanza ambao mwanaume na mwanamke wanakuja pamoja kama mume na mke, na imekokotezwa sana kwamba wanaunda muungano huo kwa nia ya kupata ukaribu na radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanya zile A’amali zilizopendekezwa kwa ajili ya usiku huo.

Wakati huu ni muhimu kuangalia ni hali gani yule ‘Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu,’ Hadhrat Fatimah (a.s.) aliyokuwa nayo ule usiku wa harusi yake, na ni vipi alianza maisha yake na mume wake, Imam Ali (a.s.): Katika ule usiku wa harusi Imam Ali (a.s.) alimuona Hadhrat Fatimah (a.s.) alikuwa amefadhaika na akitokwa na machozi, na akamuuliza kwa nini alikuwa kwenye hali ile.

Yeye alijibu akasema: “Nilifikiria kuhusu hali yangu na vitendo na nikakumbuka mwisho wa uhai na kaburi langu; kwamba leo nimeondoka nyumbani kwa baba yangu kuja nyumbani kwako, na siku nyingine nitaondoka hapa kwenda kaburini na Siku ya Kiyama.

Kwa hiyo, namuapia Mungu juu yako; njoo tusimame kwa ajili ya swala ili kwamba tuweze kumuabudu Mwenyezi Mungu pamoja katika usiku huu.”3

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu4

1. Jaribu kuwa katika Udhuu kwa kiasi kirefu kinachowezekana cha usiku huo, na hususan wakati wa A’amal zifuatazo hapa chini.

2. Anza kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu halafu useme “Allahu Akbar,” ikifuatiwa na Swala ya Mtume – Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad).

3. Swali rakaa mbili, kwa nia ya ‘Mustahab Qurbatan ilallah’ – kujisogeza karibu na Allah (s.w.t.). (Swala inayopendekezwa kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu) ikufuatiwa na Swala ya Mtume.

4. Soma Dua ifuatayo, ikifuatiwa na Swala ya Mtume. Kwanza bwana harusi aanze kuisoma, baada yake ambapo bibi harusi atapaswa kusema: Ilahi Amin (Mwenyezi Mungu aitakabalie Dua hii).

“Allahumma rzuqniy ilfahaa wa wudhahaa wa ridhwaahaa wa radhwiniy bihaa thumma j’ma’u bayinanaa bi-ahsani j’timaa’in wa asarri itilaafin fainnaka tuhibbul-halaala wa takrahul-haraam.”

“Ewe Allah! Nijaalie na upendo wake, mapenzi na kunikubali kwake mimi; na nifanye mimi niridhike naye, na tuweke pamoja katika namna bora ya muungano na katika muafaka kamilifu, hakika Wewe unapenda mambo ya halali na unachukia yale ya haram.”5

5. Hata kama wawili hao hawadhamirii ushika mimba katika usiku huo wa harusi, inapendekezwa kwamba Dua zifuatazo zisomwe kwa ajili ya watoto wazuri (wakati wowote itakapotunga mimba):

a. Bwana harusi anapaswa aweke kiganja cha mkono wake wa kulia kwenye paji la uso la bibi harusi kwa kuelekea Qibla na asome:

“Allahumma bi-amaanatika akhadhtuhaa wa bikalimaatika stahlaltuhaa fain qadhwayta liy minhaa waladaan faaj’alhu mubaarakaan taqiyyan min shiy’ati aali Muhammad wa laa taj’al lil-shaytwaani fiyhi shirkaan wa laa naswiybaan.

“Ewe Allah! Nimemchukua (binti) huyu kama amana Yako na nimemfanya halali juu yangu mwenyewe kwa maneno Yako. Kwa hiyo, kama umenikadiria mtoto kutokana naye, basi mfanye mbarikiwa na mchamungu kutoka miongoni mwa wafusi wa familia ya Muhammad; na usimfanye Shetani kuwa na sehemu yoyote ndani yake.”6

b. Dua ifuatayo pia inapaswa kusomwa:

“Allahumma bi-kalimaatika stahlaltuhaa wa bi-amaanatika akhadhtuhaa. Allahumma-j’alhaa waluwdaan waduwdaan laa tafraku taakulu mimmaa raaha wa laa tas-alu ‘ammaa saraha.”

“Ewe Allah! Nimemfanya awe halali juu yangu kwa maneno Yako, na nimemchukua katika amana Yako. Ewe Allah! Mjaalie awe mwenye kuzaa na mwenye upendo.”7

6. Bwana harusi aioshe miguu ya bibi harusi na anyunyize maji hayo katika pembe zote nne za chumba na nyumba. Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa aina 70,000 za umasikini, aina 70,000 za neema zitaingia ndani ya nyumba hiyo na neema 70,000 zitakuja juu ya bibi na bwana harusi. Bibi harusi atakuwa salama kutokana na wendawazimu, vidonda vya tumbo na ukoma.8

Mambo Kadhaa Kuhusu ‘Aqd Na Ndoa

Mambo Kadhaa Kuhusu ‘Aqd Na Ndoa 9

1. Mtu anapaswa kujiepusha na kufanya Aqd au ndoa wakati wa Qamar dar Akrab – pale mwezi unapopita kwenye eneo la ng’e (scorpio).
Kanuni hii haiungwi mkono na Shi’a wote – Mtarjuma.
2. Mtu sharti ajiepushe kutokana na kufanya Aqd au ndoa nje chini ya mwanga wa jua.
3. Inapendekezwa kwamba Aqd na ndoa zifanywe wakati wa usiku.

Dokezo: Ni muhimu kukumbuka kwamba lengo kuu la ndoa ni kumuun- ganisha mwanaume na mwanamke. Mara nyingi sana harusi zinazofanyi- ka leo hii huwa ni ndefu sana na zenye kuchosha kwa bibi na bwana harusi; wanafika chumbani kwao usiku sana wakiwa hawana nguvu za kufaa kwa ajili ya A’amali zilizopendekezwa kwa ajili ya usiku huu mtukufu, wala nyingine zaidi. Kwa hiyo, inapendekezwa kwamba taratibu za usiku huu zinawekwa rahisi na kwa kiwango kidogo kabisa. Kama sherehe nyingine zinahitajika, basi zipaswe kufanyika katika usiku uliotangulia au unaofuata ule wa harusi.

Baadhi Ya Mambo Kwa Ajili Ya Bibi Na Bwana Harusi

1. Sio lazima kwamba kujamiiana kwa kutimiza ndoa kufanyike katika ule usiku wa harusi; bali unaweza kuchukua siku chache au hata majuma machache.

2. Uchovu, wasiwasi na fadhaa vinaweza kufanya hilo liwe gumu zaidi; hivyo ni muhimu kwamba mume na mke wachukue muda wa kutosha kuweza kuwa wametulizana na kuzoeana na kwenda kwa mwendo wao wenyewe.

3. Mafuta ya kulainishia yanaweza yakahitajika kwa siku zile chache za mwanzo au majuma ili kufanya kule kujamiiana kuwa rahisi zaidi na kwenye starehe zaidi.10

4. Kumaliza mapema au kusikotarajiwa kunaweza kuwa ni tatizo kwa mara chache za mwanzoni; hata hivyo, hili linapaswa kutatuliwa baada ya kupita muda na kupatikana uzoefu.

5. Kizinda (cha bikra) kinaweza kivuje au kisivuje damu. Unyegereshano, upole na kuingiliana tena mara tu baada ya hapo kunaweza kupunguza maumivu ya uchanikaji wa hicho kizinda.

6. Baada ya kujamiiana (wakati wowote itakapokuwa), bibi harusi asije akatumia maziwa, siki, giligilani, tuhafa chungu au tikitimaji kwa kiasi cha juma moja, kwani vinasababisha tumbo la uzazi kukauka na kuwa la baridi na gumba. Kula siki wakati huu vilevile kunatokezea kwa mwanamke kutokuwa msafi (tohara) kutokana na damu ya hedhi, giligilani (na tikitimaji) kunasababisha matatizo ya wakati wa uchungu na tuhafa linasababisha kusimamisha ukawaida wa hedhi, na yote haya yanaishia kwenye kuleta maradhi.11

7. Watu wanaweza wakatoa maoni fulani juu ya siku chache zinazofuatia. Ni muhimu sana kufanya hilo lisikuathiri wewe, na usivutike kwenye mazungumzo yao.

8. Usizungumze kuhusu mambo yako ya ndani kwa watu wa nje, chunga heshima kwa mwenza wako na kwenye uhusiano wenu.

Harusi Ya Imam Ali (A.S.) Na Hadhrat Fatimah (A.S.)

‘Aqd (Mkataba Wa Ndoa)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipenda hotuba ya ndoa isomwe msikitini na mbele ya mahudhurio ya watu. Imam Ali (a.s.) alikwenda pale msikitini kwa furaha sana, na Bwana Mtume (s.a.w.w.) vilevile akaingia msikitini mle. Muhajirina na Ansari wakakusanyika kuwazunguka. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akenda juu ya mimbari na baada ya kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:

“Enyi watu! Jueni kwamba Jibril amenishukia mimi na kuniletea ujumbe kutoka kwa Allah (s.w.t.). kwamba sherehe za ndoa ya Ali (a.s.) zimefanyika mbele ya Malaika huko ‘Bait al-Ma’mur.’

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamuru kwamba mimi nifanye sherehe hizi hapa duniani na niwafanye nyote nyie kuwa mashahidi.” Kufikia hapa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasoma hotuba ya ndoa (‘Aqd).

Halafu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Imam Ali: “Simama na utoe hotuba.” Imam Ali (a.s.) aliianza hotuba yake na akaonyesha kufurahi na kuridhika kwake kwa ndoa yake na Hadhrat Fatimah (a.s.).

Watu wakamuombea yeye na wakasema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu aibariki ndoa hii, na aweke mapenzi na usuhuba ndani ya nyoyo zenu.”12

Harusi Yenyewe

Sherehe za harusi zilifanyika mnamo mwezi mosi Dhul Hijjah, mwaka wa pili Hijiria13 (au tarehe 6 ya Dhul Hijjah, 2 A.H.)14 mwezi mmoja baada ya hotuba ya ndoa.

Muda kati ya hotuba ya ndoa na sherehe za harusi, Imam Ali (a.s.) alikuwa ana haya ya kuongea kuhusu mke wake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Siku moja, kaka yake, Aqiil, alimuuliza: “Kwa nini humleti mke wako nyumbani ili tuweze kukupongeza kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa kwako?” Jambo hili lilimfikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alimwita Imam Ali (a.s.) na kumuuliza: “Je, uko tayari kwa kufunga ndoa (kuoa)?”

Imam Ali (a.s.) alitoa jibu la kukubali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Insha’allah, leo usiku au kesho usiku, mimi nitafanya maandalizi kwa ajili ya harusi.” Wakati huo, yeye Mtume (s.a.w.w.) akawaambia wake zake wamvalishe Hadhrat Fatimah (a.s.) na kumtia manukato na kuweka mazulia kwenye chumba chake ili kujiandaa kwa ajili ya sherehe za harusi.15

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Imam Ali (a.s.): “Hapawezi kuwa na harusi bila ya wageni.” Mmoja wa viongozi wa Ansari aliyeitwa Sa’ad akasema: “Mimi nakuzawadia kondoo mmoja,” na kikundi cha Ansari nao vilevile wakaleta kiasi16 cha nafaka,17 na maji ya maziwa yaliyoganda, mafuta na tende pia vililetwa kutoka masokoni. Nyama hiyo ilipikwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na usafi wake alichukua jukumu la kupika kwa ajili ya harusi hiyo, na kwa mikono yake iliyobarikiwa, akavichanganya (viungo) na akaanza kutengeneza aina ya chakula cha kiarabu kinachoitwa Habis au Hais.18

Hata hivyo, ingawa chakula kilitayarishwa, mwaliko ulikuwa wa jumla. Idadi kubwa ya watu ilishiriki na kwa baraka za mikono ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kila mmoja alikula na akashiba kutokana na chakula hicho, na kulikuwa na kingine kamwe kilichobakia kwa ajili ya masikini na wenye shida; sinia la chakula vile vile liliwekwa kwa ajili ya bibi na bwana harusi.19

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia wake zake waandae sherehe kwa ajili ya Hadhrat Fatimah (a.s.). Baada ya chakula, wanawake hao walijiku- sanya karibu na Hadhrat Fatimah (a.s.) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamsaidia kupanda juu ya farasi wake Mtume mwenyewe.

Salman al- Farsi alizikamata hatamu za farasi huyo na kwa sherehe hiyo maalum, wanaume majasiri kama vile Hamza na idadi kadhaa ya wana familia na maharimu wa Hadhrat Fatimah (a.s.) wakajikusanya karibu ya farasi huyo wakiwa na panga zilizochomolewa. Wanawake wengi walisubiri nyuma ya bibi harusi na wakasoma Takbira.

Farasi akaanza kutembea, na wale wanawake wakaanza kusoma Takbira na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu Kwa wakati ule, mmoja baada ya mwingine, walisoma qaswidah nzuri na, tamu ambazo zilikuwa zimetung- wa kwa utukufu na shangwe, wakampeleka bibi harusi nyumbani kwa bwana harusi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile alilikuta kundi hilo na akaingia chumbani kwa maharusi.

Aliitisha karai la maji, na wakati lilipo- letwa, yeye akanyunyiza kiasi juu ya kifua cha Hadhrat Fatimah (a.s.) na akamwambia atawadhe na kuosha kinywa chake kwa yale maji yaliyobakia. Alinyunyiza kiasi juu ya Imam Ali (a.s.) pia na akamwambia atawadhe na kuosha kinywa chake.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akachukua mkono wa Hadhrat Fatimah (a.s.) na akauweka kwenye mkono wa Imam Ali (a.s.) na akasema: “Oh, Ali! Ubarikiwe wewe; Allah (s.w.t.). amemuweka juu yako binti ya Mtume wa Allah, ambaye ndiye mbora wa wanawake (wa ulimwengu).”

Kisha akaongea na Hadhrat Fatimah (a.s.) na akasema: “Oh, Fatimah! Ali ni kutoka kwa wabora wa waume.”20

Kisha akawaombea Dua juu yao: “Ewe Allah, wafanye wazoeane (wakaribiane) na kila mmoja wao! Ee Allah, wabariki hawa! Na weka neema kwa ajili yao katika maisha yao.”

Wakati alipokaribia kuondoka, yeye akasema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu amekufanyeni ninyi na kizazi chenu kuwa tohara. Mimi ni rafiki wa marafiki zenu, na ni adui wa maadui zenu. Sasa nakupeni mkono wa kwaheri na kukukabidhini kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu”21

Asubuhi iliyofuata, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kumuona binti yake. Baada ya kuwatembelea huku, yeye hakwenda tena nyumbani kwao kwa muda wa siku tatu, bali akaenda katika siku ya nne.22

Matakwa Ya Hadhrat Khadija (A.S.)

Katika ule usiku wa harusi ya Hadhrat Fatimah (a.s.), Asma bint Umais (au Umm Salama) ambaye alikuwa miongoni mwa wanawake hao, aliomba ruhusa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama angeweza kukaa karibu na Hadhrat Fatimah ili aweze kutekeleza mahitaji yoyote atakay- oweza kuwa nayo. Alimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Wakati wa kifo cha Hadhrat Khadija ulipofika hapo Makkah, mimi nilikuwa karibu naye na niliona kwamba Khadija alikuwa analia.

Nilimuuliza: “Wewe ni ‘Bibi wa wanawake dunia zote’ na mke wa Mtume (s.a.w.w.) na licha ya yote hayo bado unalia ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupa habari njema za peponi?”

Hadhrat Khadija alijibu: “Silii kwa sababu ya kifo; bali mimi ninalia kwa ajili ya Fatimah ambaye ni msichana mdogo, na wanawake katika usiku wa harusi wanahitaji mwanamke kutokana na ndugu zao na wale wa karibu (maharimu) watakaoweza kuwaambia wao siri zao zilizofichika, na nina- hofia kwamba usiku huo, kipenzi changu Fatimah hatakuwa na mmojawapo.”

Kisha nilimwambia Khadija kwamba: ‘Ninaapa kwa Mola wangu kwamba kama nitabakia kuwa hai mpaka siku hiyo, usiku huo mimi nitakaa ndani ya nyumba hiyo mahali pako (badala yako).’ Sasa ningeomba ruhusa kutoka kwako kwamba unisamehe ili niweze kutimiza ahadi yangu.’”

Baada ya kuyasikia haya, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza kulia na aka- nipa ruhusa kubakia na akaniombea Dua. 23

Suti Ya Harusi Yenyewe

Katika ule usiku wa harusi ya Imam Ali (a.s.) na Hadhrat Fatimah (a.s.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa binti yake suti (vazi) ya harusi ya kuvaa usiku ule. Wakati Hadhrat Fatimah (a.s.) alipokuwa amekwenda kule kwenye nyumba ya harusi na pale alipokuwa ameketi kwenye mkeka wa kuswalia ili kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu mara akatokea mtu mwenye shida kwenye mlango wa nyumba ya Hadhrat Fatimah (a.s.) na kwa sauti kubwa akasema: “Kutoka kwenye mlango wa nyumba ya utume, mimi ninaomba suti ya zamani, chakavu.”

Kwa wakati ule, Hadhrat Fatimah (a.s.) alikuwa na suti mbili, moja iliyochakaa na nyingine bado mpya. Yeye alitaka kutoa ile suti ya zamani kulingana na maombi ya yule mtu mwenye haja wakati ghafla alipokum- buka aya inayosema: “Humtapata uchamungu mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda mno…..”24 Hadhrat Fatimah (a.s.) ambaye alijua kwamba anaipenda ile suti mpya zaidi, alifanya kulingana na aya hii na akatoa ile suti mpya kumpa yule mtu mwenye haja.

Siku iliyofuata, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoiona ile suti ya zamani mwilini mwa Hadhrat Fatimah (a.s.), yeye alimuuliza: “Kwa nini hukuvaa ile suti mpya?” Hadhrat Fatimah akajibu: “Niliitoa kumpa mtu mwenye haja.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kama ungevaa ile suti mpya kwa ajili ya mumeo ingekuwa vizuri na yenye kufaa sana.” Hadhrat Fatimah (a.s.) ali- jibu akasema: “Hili nimejifunza kutoka kwako.

Wakati mama yangu Khadija alipokuja kuwa mke wako, alitoa utajiri wake wote kwenye mkono mtupu uliokuwa kwenye njia yako, ilikuwa haina kitu, hadi ikafikia mahali wakati alipokuja mtu mwenye shida kwenye mlango wa nyumba yako na kuomba nguo. Kukawa hamna nguo ndani ya nyumba yako hivyo ukavua shati lako na ukampatia yeye, na ndipo ikashuka aya hii: “Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue kabisa, usije ukakaa hali ya kulaumiwa (na) kufilisika ukajuta.”25

Akiwa amezidiwa na mshangao kwa upendo na uaminifu wa binti yake Zahraa (a.s.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalimdondoka machozi kutoka machoni mwake, na kama ishara ya upendo, yeye alimshikilia Hadhrat Fatimah (a.s.) kifuani kwake (s.a.w.w.).26
________________________
1. A Bundle of flowers, Uk. 149

2. Muntakhab Mizan al-Hikmah, Jz.. 1, Uk.457

3. Kitab al-Irshad, Jz. 1, Uk. 270

4. Halliyatul-Muttaqin, uk. 116-117

5. Al-Kafi, Jz. 3, uk. 481

6. Al-Kafi, Jz. 5, uk. 500

7. Al-Kafi, Jz. 5, Uk. 501

8. Wasail ash-Shi’a, Jz. 20, Uk. 249, hadithi ya 25555

9. Halliyatul-Muttaqin, uk. 108-109 (nukta ya 1-3)

10. Pasukh be Masa’il-e Jinsii wa Zanashuii, Uk.235

11. Wasa’il ash-Shi’a, Juz. 20, Uk. 250 hadithi ya 25556

12. Bihar al-Anwar, Juz. 43, Uk.. 120 na 129

13. Bihar al-Anwar, Juz. 43, Uk.. 92

14. Baadhi wamesimulia kwamba ule wakati baina ya ndoa na harusi kuwa ni mwaka mmoja)

15. Bihar al-Anwar, Juz. 43, Uk. 130-131

16. Takriban ratili 8

17. Bihar al-Anwar, Juz. 43, Uk 137

18. Bihar al-Anwar, Juz. 43, Uk 106 na 114

19. Manaqib ibn Shahr Ashub, Juz.3, Uk. 354

20. Izdawaaj Maktab Insaan Saazi, Juz. 2, Uk. 300

21. Manaqib ibn Shahr Ashuub, Juz. 3, Uk. 3554-355

22. Manaqib ibn Shahr Ashuub, Juz. 3, Uk. 356

23. Sar Guzashthaaye Hadhrat Ali (a.s.) wa Fatimah (a.s.), Uk.30

24. Surat al-Imran; 3:92

25. Surat al-Isra; 17:29

26. Sar Guzashthaaye Hazrat Ali wa Fatimah (a.s.), uk. 31

Kujamiiana na mahusiano ya kijinsia, pamoja na mwenza halali yanatawaliwa na maumbile asilia, na wakati huo huo ni sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.). Yametajwa pia kwamba ndio jambo la kuburudisha zaidi maishani. Kikundi cha marafiki na Shi’a wa Imam as-Sadiq (a.s.) wanasimulia kwamba, Imam alituuliza sisi: “Ni nini kinachoburudisha zaidi?” Sisi tukasema: “Kuna vitu vingi vinavyoburudisha.” Imam akasema: “Kile kinachoburudisha zaidi hasa ni kufanya mapenzi na wake zenu.”1

Imesimuliwa vilevile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Ama katika dunia hii au katika akhera, mtu hajawahi, na wala hatawahi, kupata starehe yenye burudani zaidi kuliko mahusiano ya kijinsia na wanawake, na hakika haya ndio maelezo ya maneno ya Allah (s.w.t.). ndani ya Qur’an, katika Surat Aali Imran, aya ya 14 Yeye ambapo anasema: “Watu wamepambiwa kupenda matamanio pamoja na wanawake na watoto…..”

Halafu yeye akasema: “Hakika, watu wa Peponi hawapendelei sana katika starehe za Pepo zaidi kuliko Nikah;2 si chakula wala vinywaji ambavyo vina buru- dani kama hiyo kwao.”3

Na kuhusu hali nyingine zote za maisha yetu, Uislam unatoa kutupatia sisi taarifa zote muhimu kwa ajili ya maisha ya kijinsia ya mwanaume na mwanamke. Sababu ya hili ni rahisi; Uislam unatambua hulka ya kimaumbile ya mwanadamu, na umeamuru mahusiano ya kijinsia kwa ajili ya starehe na sio kwa ajili ya kuzaa tu. Matamanio ya ngono hayawezi, na hayapaswi kuzuiwa, bali hasa kurekebishwa kwa ajili ya hali njema ya mtu katika ulimwengu huu na akhera. Endapo kanuni na sheria hizi zitazingatiwa kwa makini na kutekelezwa kwa lengo la burudani na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujitenga mbali na maovu ya Shetani, kunahesabiwa kuwa miongoni mwa wema mkubwa kabisa.

Umuhimu Wa Mahusiano Ya Kijinsia

Kuna hadithi nyingi sana zinazobeba ule umuhimu wa uhusiano wa kijin- sia. Una kituo cha ibada na sadaka, na umeitwa kuwa ni Sunnah ya Mtume (s.a.w.w.).

Imam as-Sadiq (a.s.) anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizungumza na mmoja wa masahaba zake katika siku moja ya Ijumaa na akamuuliza: “Je, umefunga leo?” Yule sahaba akajibu. “Hapana.” Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza tena: “Je, umetoa chochote leo kama sadaka?” Akajibu, “Hapana.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Basi nenda kwa mke wako na hiyo ndio sadaka hasa kwake yeye.”4 Katika hadithi nyingine, Imam as-Sadiq (a.s.) anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mtu mmoja: “Wewe umefunga leo?” Akajibu akasema, “Hapana.”

Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza: “Je, umekwenda kutembelea mgonjwa yoyote?” Akajibu, “Hapana.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza: “Je, umekwenda kusindikiza jeneza?” Akajibu, “Hapana.” Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza: “Je, umetoa chakula kwa mtu masikini?” Akatoa majibu ya kinyume tena. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Nenda kwa mke wako, na kumwendea mke wako ni sadaka (Mwendee ili upate malipo kwa ajili ya matendo yote hayo).”5

Muhammad bin Khalad anasimulia kutoka kwa Imam ar-Ridhaa (a.s.): “Mambo matatu ni kutoka kwenye sunnah za manabii watukufu na mitume wa Allah (s.w.t.)., na haya ni kutumia manukato, kukata nywele na kijiingiza sana kwenye mahusiano ya ndoa na wake zao.”6

Kukaa mbali na mahusiano ya kindoa ya mtu na mke wake ni matokeo ya minong’ono ya Shetani, na kuna matokeo ya kinyume mengi sana kama vile mabishano na chuki baina ya mume na mke wake.

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): Mabibi watatu walikwen- da kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kulalamika. Mmoja wao akasema: “Mume wangu huwa hali nyama.” Yule mwingine akasema: “Mume wangu hanusi manukato na wala hatumii manukato.” Na yule wa tatu akasema: “Mume wangu mimi hasogei karibu na wanawake (yaani, hajishughulishi na kujamiiana).”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akiwa hana furaha, katika namna ambayo kwamba joho lake lililobarikiwa lilivyokuwa likiburuzika ardhini, aliondoka na kwenda msikitini na akiwa juu ya mimbari, alimtukuza Mwenyezi Mungu na kisha akasema: “Ni nini kimetokea, kwamba kikundi cha wafuasi wangu hawali nyama, au hawatumii manukato, au hawawaendei wake zao? Ambapo mimi ninakula nyama, ninatumia manukato, na pia ninamwendea mke wangu. Hii ndio sunnah yangu, na mtu yoyote anayekwenda kinyume na sunnah hii huyo hatokani na mimi.”7

Imam as-Sadiq (a.s.) vilevile amesimulia: Mke wa Uthman bin Ma’dhun alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kila siku Uthman anafunga na wakati wa usiku anajishughulisha katika Swala.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaokota makubazi yake na kwa hasira akaenda kwa Uthman (kiasi kwamba hakun- goja kuvaa makubazi yake) na akamkuta katika hali ya Swala.

Kwa vile Uthman alimuona Mtume (s.a.w.w.) aliiacha Swala yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamhutubia akasema: “Allah hakunituma mimi kuwa sufii (anayejitenga peke yake), ninaapa Wallahi, kwamba hilo limenichochea mimi kwenye dini hii safi, yenye imani halisi na rahisi, mimi ninafunga, ninaswali na ninakwenda kwa mke wangu, na yeyote anayependa desturi yangu, ni lazima ashikamane na sunnah yangu na mwenendo wangu, na Nikah8 ni sunnah yangu.9

Umuhimu Wa Kumridhisha Mke Wako

Kumridhisha mke wake mtu ni jambo muhimu sana katika Uislam, kama lilivyoonyeshwa na hadithi ifuatayo hapo chini; kwa kweli, kukosa kuridhika kwa kipindi cha muda mrefu kunaweza kusababisha kukosa ashiki na chuki ya mke kwa mumewe.

Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s.): Wakati yeyote kati yenu anapotaka kulala na mke wake, basi asimharakishe kwani wanawake wanayo mahitaji pia.10 Ni muhimu kwa mume kutambua kwamba hamu ya kujamiiana ya mwanamke inachukua muda mrefu kujionyesha yenyewe, lakini mara inapokuwa imevutika, inakuwa na nguvu sana, ambapo kwa mwanaume ni rahisi, anapata ashiki haraka sana na vilevile anaweza kuridhishwa haraka sana. Mwisho, inatia moyo kuona kwamba umuhimu uliowekwa na Uislam juu ya kuridhika kwa wote, mwanaume na mwanamke ni kiashirio cha wazi cha uadilifu na wema wa Mwenyezi Muntu (s.w.t.), kwa kweli, imerudia kukaririwa ndani ya Qur’ani kwamba mwanaume na mwanamke waliumbwa kutokana na nafsi moja,11 na huu ni mfano mmoja tu wa hili.

Vitendo Vilivyopendekezwa

Hakuna kanuni maalum kwa ajili ya kujamiiana; chochote ambacho kinawaridhisha wawili hao ni sawa, kadhalika, chochote ambacho hakiwaridhishi wawili hao ni lazima kiepukwe; kikwazo pekee kwenye kanuni hii ni kile ambacho Shari’ah inakikataza kwa uwazi kabisa. Hata hivyo, kuna vitendo kadhaa vilivyopendekezwa ambavyo, kama vikifuatwa, vitatarajiwa kuongozea kwenye hali ya kuridhisha zaidi.

Kabla Ya Kujamiiana

1. Piga mswaki meno yako na tafuna kitu chenye harufu nzuri ili kuondoa harufu mbaya yoyote mdomoni. Kadhalika, jaribu kutokula vyakula vyenye harufu isiyopendeza kabla ya kukutana pia, kama vile kitunguu na kitunguu saumu.

2. Hakikisha unanukia vizuri – harufu safi zaidi ni ile ya mara tu baada ya kuoga au kujisafisha kwa haraka, na harufu mbaya zaidi ni ile ya jasho! Hususan wanawake wanahisia kali sana juu ya harufu.

Matumizi ya manukato, mafuta mazuri na vitu kama hivyo vinapendekezwa sana, ingawa ni muhimu sana kutambua kwamba kutumia vitu vya asili ni bora sana, ambavyo havina mchanganyiko na kemikali ambazo zinaweza kusababisha madhara mwilini.

Hasa, wanja (kuhl) umependekezwa sana juu ya wanawake. Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.): “Kupaka wanja kuyazunguka macho kunakipa kinywa harufu nzuri, na kunazifanya kope za macho kuwa na nguvu na kunaongeza nguvu na mvuto wa kujamiiana.12

Imesimuliwa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (s.a.): Kupaka wanja nyakati za jioni kuna manufaa kwenye macho na nyakati za mchana ni katika sunnah.13

Jalizo: Ingawa hadithi zinapendekeza matumizi ya wanja (kuhl), haziruhusu matumizi
yake katika maeneo ambayo yanaweza kuonekana kwa wanaume na yakaweza kuwa chanzo
cha mvuto na ushawishi.

Unyegereshano (Kutiana Ashiki)

Umuhimu Wa Unyegereshano

Kama ilivyosisitiziwa mapema, mume kumridhisha mke wake ni muhimu sana, na kujiingiza kwenye kujamiiana haraka na kwa pupa sio njia sahihi. Kuna wastani wa tofauti ya dakika nane kati ya muda ambao mume na mke wanafikia kileleni; mwanaume kwa kawaida anachukua dakika mbili kufikia kileleni na mwanamke anachukua dakika kumi kufikia kileleni. Kwa hiyo, ili kumridhisha kikamilifu mke wake, mwanaume lazima ampapase na kumchezea kimapenzi na kujishughulisha katika kunyegereshana (kutiana ashki) ili wote wafikie kileleni kwa pamoja kwa wakati mmoja.Uislam unatilia mkazo sana umuhimu wa unyegereshano, kama unavyoashiriwa katika hadithi zifuatazo hapa chini:

Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Usijishughulishe katika kujamiiana na mkeo kama kuku; bali kwanza kabisa jishughulisha katika kutiana ashiki kwa unyegereshano pamoja na mke wako na kuchezeana naye halafu ufanye mapenzi naye.”14

Imesimuliwa pia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Starehe na michezo yote haina maana isipokuwa kwa mitatu tu: Upanda farasi, kurusha mishale na unyegereshano na mke wako, na hii mitatu ni sahihi.”15

Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s.): “Yeyote anayetaka kuwa karibu na mke wake lazima asiwe na papara, kwa sababu wanawake kabla ya kuji- ingiza kwenye tendo la kufanya mapenzi lazima wajiingize kwenye unyegereshano ili kwamba wawe tayari kwa ajili ya kufanyiwa mapenzi.16

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Malaika wa Mwenyezi Mungu na wale ambao ni mashahidi juu ya matendo yote ya wanadamu wanawaangalia katika kila hali isipokuwa wakati wa mashindano ya kupanda farasi na ule wakati ambapo mwanaume anajiingiza katika kujishughulisha na unyegereshano na mke wake kabla hawajajihusisha katika kujamiiana.” 17

Taratibu Za Kunyegereshana

Kuna vikwazo vichache sana kwenye taratibu zinazotumika katika unyegereshano; kupigana mabusu, kukumbatiana na kadhalika yote haya yanaruhusiwa. Hapa chini ni baadhi ya mbinu zinazofaa kwenye taratibu maalum:

A) Upapasaji Kwenye Matiti

Imesimuliwa kutoka kwa Imam ar-Ridhaa (a.s): “Usijiingize kwenye kujamiiana isipokuwa kwanza ujishughulishe katika unyegereshano, na ucheze naye mkeo sana na kumpapasa matiti yake, na kama ukifanya hivi atazidiwa na ashiki (na kusisimka kwa upeo kamilifu) na maji yake yat jikusanya. Hii ni ili ule utoaji wa majimaji uchomoze kutoka kwenye mati- ti na hisia zinakuwa dhahiri usoni mwake na kwenye macho yake na kwamba anakuhitaji kwa namna ileile kama wewe unavyomhitaji yeye.” 18

B) Mapenzi Ya Mdomo (Maongezi)

Imam al-Kadhim (a.s.) aliulizwa: “Kuna tatizo kama mtu atabusu sehemu za siri za mke wake?” Imam alijibu akasema: “Hakuna tatizo.”19

DOKEZO: Ingawa kupiga punyeto (kujisisimua mwenyewe uchi wako mpaka ukatoa manii) kunakatazwa, katika suala la watu waliooana hakuna tatizo kama mke anasisimua tupu ya mume wake mpaka kutokwa na manii, au mume anasisimua tupu ya mke wake hadi anafikia kilele cha raha ya kujamiiana. Hili linaruhusiwa kwa sababu haliingii kwenye (kujisisimua mwenyewe;) ni kujisisimua kwa njia ya mwenza halali

C) Mengineyo

Iliulizwa kwa Imam as-Sadiq (a.s.) “Endapo mtu atamvua nguo mke wake (na kumuacha uchi) na halafu akawa anamwangalia, je kuna tatizo lolote katika hilo?” Yeye akajibu akasema: “Hapo hakuna tatizo, hivi kuna stare- he bora kuliko hiyo ambayo inaweza kupatikana?” Likaulizwa swali jingine tena: “Kuna tatizo lolote iwapo mume atachezea sehemu za siri za mke wake?”

Imam akajibu: “Hakuna tatizo, kwa sharti kwamba hatumii kitu chochote mbali na viungo vya mwili wake (asitumie kitu cha nje cha ziada).”

Halafu tena Imam akaulizwa: “Kuna tatizo lolote kufanya ngono ndani ya maji?” Imam akajibu: “Hakuna tatizo.” 20

Dokezo: Hadithi hiyo hapo juu inasisitizia makatazo ya kutumia vitu vya nje.

Baada Ya Kujamiiana

1. Ni mustahabu kwamba josho la janaba ‘Ghusl al-Janaabat’ linafanywa mara tu baada ya tendo la ndoa, na linapochukuliwa mapema zaidi ndio bora. Vilevile, kama mtu angependa kufanya ngono zaidi ya mara moja katika usiku mmoja, ni bora kwamba kila mara waoge josho la janaba. Hata hivyo, kama hilo litakuwa haliwezekani kutendeka, inapendekezwa kwamba mtu atawadhe kabla ya kila tendo.21

2. Mara tu baada ya kumaliza tendo la ngono, mume hana budi kuoga josho na wakati huohuo ale sehemu ya nta ya nyuki (inayosifika kwa kuponya aina zote za majeraha, hususan mipasuko na mivunjiko) iliyochanganywa na asali na maji au iliyochanganywa na asali safi, halisi, kwani hii itafidia yale majimaji yaliyopotea.22

3. Kama nguvu za kiume za mtu zikiisha haraka baada tu ya kujamiiana, hana budi kujipasha mwili moto na kisha kulala.23

4. Mume na mke hawana budi kutumia mataulo tofauti katika kujisafisha wenyewe. Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba kama litatumika taulo moja tu, hii itasababisha uadui na utengano baina ya wawili hao.24

Vitendo Visivyopendekezwa

Vitendo Vinavyoleta Karaha (Makruuh)

1. Liwati!

Kuna baadhi ya Wanavyuoni wanaosema kuwa Liwati inaruhusiwa kwa ridhaa ya mke, lakini ni kauli zisizo na nguvu, na pia ni kitendo kinachochukiwa sana!

Zayd ibn Thabit anasimulia kwamba mtu mmoja alimuuliza Imam Ali (a.s.): “Je, unaweza kumsogelea mkeo nyuma kwake?” Imam Ali (a.s.) akajibu akasema: “Likatae, lichukie hilo liwe kinyaa kwako! Mwenyezi Mungu anakushusha kwa njia hii (ya kumwingilia mwanamke). Hukuyasikia maneno ya Mola Wako kwamba imesimuliwa kutoka kwa Lut ambaye alisema kuwaambia kaumu yake:

وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُمْ بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِنَ الْعَالَمِينَ {80}

“Kulikoni! Mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa (ufasiki) huo katika walimwengu? (Al-A’araf; 7:80). 25

Kuna baadhi ya watu wanaolihalalisha tendo hili kwa kutumia aya ya Qur’ani Tukufu ifuatayo:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ {223}

“Wanawake ni mashamba yenu, basi yaendeeni mashamba yenu kwa namna muitakayo …”
(Al-Baqarah; 2:223).

Hata hivyo, Imam as-Sadiq (a.s.), katika tafsiri yake juu ya aya hiyo ya Qur’ani hapo juu anasimulia kwamba: “Madhumuni ya aya hii ni kwamba kujamiiana hakuna budi kufanyika kutokea mbele, kwani sababu ambayo kwamba mwanamke katika aya hii amefananishwa na shamba linalotoa mavuno (kutokea juu ya udongo) ambao ni kama tu kule mbele kwa mke kwa sababu huku ndiko ambako kwamba mtoto hutokea kupatikana na kuja ulimwenguni humu.”26 Abuu Basiir anasimulia kwamba yeye alimuuliza Imam kwamba ni nini hukmu ya mtu anayemwendea mke wake nyuma. Imam alilichukulia tendo hili kutokubalika na akasema: “Kaa mbali na nyuma kwa mkeo, na maana ya aya hii tukufu ya Surat al-Baqarah hapo juu sio kwamba unaweza kumwingilia mkeo kutokea popote unapotaka, bali haswa ni kwamba huna budi kufanya ngono, na kwa hiyo maana ya aya hiyo ni kumkurubia mkeo kwa wakati wowote uupendao kufanya hivyo.”27

2. Kuwa Na Qur’ani Au Majina Ya Allah (S.W.T.) Mwilini Mwako

Imesimuliwa kutoka kwa Ali, mtoto wa Imam as-Sadiq (a.s.): Nilimuuliza ndugu yangu Imam Kadhiim (a.s.): “Je, mtu anaweza kujamiiana na akaenda bafuni wakati akiwa na pete mkononi mwake yenye jina la Allah au aya ya Qur’ani iliyoandikwa juu yake?” Imam alijibu akasema: “Hapana – hilo ni makuruhu.”28

3. Kufanya Mapenzi (Ngono) Kwa Kusimama Wima

Inasimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Mume na mke wasije wakajamiiana kama punda wawili waliong’ang’aniana pamoja, kwa sababu kama ikiwa namna hiyo, malaika wa rehma watakaa mbali nao na neema ya Mwenyezi Mungu itaondolewa kutoka kwao.29

4. Kujamiiana Wazi (Bila Kujifunika Nguo)

Imesimuliwa kwamba Muhammad ibn al-Ais alimuuliza Imam as-Sadiq (a.s.): “Je, inaruhusiwa kumwendea mke wangu nikiwa uchi kabisa (yaani kujamiiana bila kujifunika)?” Imam alijibu akasema: “Hapana, usifanye jambo kama hilo…..”30

5. Kushughulika Na Ngono Chini Ya Anga

Imesimuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.): “Allah anazichukia tabia 24 kwa ajili yenu, enyi watu, na amekukatazeni kutokana nazo; moja ya tabia hizi ni kujamiiana chini ya anga.”31

6. Kushughulika Na Kujamiiana Panapokuwa Na Watu Wengine (Na Wanaweza Kuwasikia Na/Au Kuwaona) Ndani Ya Nyumba

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.): “Ni makuruhu kwamba mtu ashughulike katika kujamiiana na mke wake kama, pamoja na kuwepo kwao, kuna mtu mwingine pia ndani ya nyumba hiyo.32

Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Twaeni tabia tatu kutoka kwa kunguru; kujamiiana kwa siri, kwenda kutafuta riziki mwan- zoni mwa asubuhi, na akili na hadhari dhidi ya hatari zinazoweza kujitokeza.” 33

7. Kujishughulisha Na Kujamiiana Mbele Ya Mtoto Mdogo

Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s.): “Mtume amekataza kwamba mtu amwendee mke wake (kwa ajili ya kujamiiana) na mtoto katika susu lake anaweza kuwaona. 34

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.): “Epukana na kujamiiana katika sehemu ambayo panaweza kuwa na mtoto anayeweza kuwaoneni.35

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Jiepushe na kwenda kulala (kwa ajili ya kujamiiana) na mke wako wakati ambapo mtoto anaweza kuwaoneni, kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua sana hasa kwamba kitendo hiki ni Makruhu na cha kuaibisha sana.”36

8. Kushughulika Na Kujamiiana Ndani Ya Jahazi, Ufukweni 63Au Barabarani

Imesimuliwa katika hadithi kwamba kujamiiana ndani ya jahazi au barabarani kunaishia kwenye laana ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ya Malaika kuwa juu yako mtu.37

Imesimuliwa katika hadithi nyingine kutoka kwa as-Sakuni kwamb Imam Ali (a.s.) aliwapita wanyama wawili waliokuwa wakijamiiana mahali njia ya watu wengi. Imam aligeuka mbali nao.

Ikaulizwa: “Ewe Amirul-Mu’minin, kwa nini uligeukia pembeni mbali nao?” Imam (a.s.) akajibu akisema: “Sio sahihi kwamba mkaribiane katika njia ya watu kama wanyama hawa; kitendo kama hicho kimekatazwa na kifanyike mahali ambapo si mwanaume au mwanamke awezaye kuona.” 38

9. Kuelekea, Au Mtu Kukipa Mgongo Qiblah

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekataza watu kujamiiana wakati wakiwa wameelekea Qiblah, au mtu mgongo wake kuelekea Qiblah, na amesema kwamba endapo kitendo kama hicho kikifanyika, kinaleta matokeo ya laana ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika na wanadamu wote kuwa juu yako mwenye kufanya hivyo.39

Dokezo: Ikiwa pale unapokaa wima kutoka kwenye hali ya kulala, uso wako unaelekea Qiblah, hii inafahamika kama kuelekea Qiblah, na kinyume chake (yaani na mgongo pia).

10. Kukataa Kujamiiana (Kwa Sababu Mbalimbali)

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwaambia wanawake: “Msirefushe Swala zenu kiasi kwamba ikawa ni kisingizio cha kutokwenda kulala (kwa ajili ya kujamiiana) na waume zenu.”40

Nyakati Zinazopendekezwa

Nyakati Za Wajibu

1. Ikiwa Kuna Hofu Ya Haramu (Iliyokatazwa)

Endapo mtu anahofia kwamba anaweza kushindwa na tamaa zake za kingono na minong’ono ya Shetani na akaweza kujiingiza katika vitendo vya haramu, ni wajibu kwamba wajichunge na wajilinde nalo hili.41

Kama mtu yuko peke yake, ni lazima afunge ndoa na hivyo kujiweka mbali na vitendo vyovyote vinavyowezekana kuwa vya haramu (vilivyokatazwa).

Imesimuliwa kutoka kwa Ayatullah Khomeini (r.a.) “Ni faradhi kwa mtu ambaye, kwa sababu ya kutokuwa na mke ataangukia kwenye haram, afunge ndoa.” 42

2. Mara Moja Kwa Kila Miezi Minne

Mtu ni lazima apate kujamiiana na mkewe kijana angalau mara moja katika miezi minne. Hii ni moja ya haki za ndoa za mke na wajibu huo unabaki kufanya kazi isipokuwa ima kama una madhara kwa mume, unahusika na kutumia jitihada za ziada zisizo za kawaida, au mke kusamehe haki yake au masharti ya awali kama hayo yalikuwa yamewekwa na mume wakati wa kufunga ndoa. Haina tofauti kama mume yuko mbali safarini ama yupo nyumbani.

Safwan ibn Yahya alimuuliza Imam ar-Ridhaa (a.s.): “Mtu anaye mke kijana na akawa hajamkaribia kwa kiasi cha miezi, au hata mwaka. Sio kwa sababu anataka kumtaabisha yeye (kwa kukaa mbali naye), bali hasa ni janga fulani limewashukia. Je, hili linahesabiwa kama ni kosa?”

Imam akajibu akasema: “Endapo atamwacha kwa kiasi cha miezi minne, hilo linahesabiwa kama ni dhambi.”43

Nyakati Zinazopendekezwa (Mustahab)

Kujamiiana, kama kutafanywa katika namna inayoruhusiwa, basi wakati wote kunakuwa ni mustahabu. Hata hivyo, kuna nyakati ambazo kunapendekezwa zaidi.

1. Wakati mke anapokuhitaji kutoka kwa mumewe.
2. Wakati mume anapokuwa amevutiwa na mwanamke mwingine.44

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) “Mtu yoyote atakayeona mwanamke na akavutiwa naye ni lazima aende kwa mke wake na aka- jamiiane naye, kwa sababu kile ambacho yule mwanamke mwingine ana- cho, na mke wako pia anacho, na mtu asimwachie nafasi Shetani katika moyo wake.

Na endapo mtu hana mke, ni lazima aswali Swala ya rakaa mbili, amtukuze sana Allah (s.w.t.). na kumswalia Mtume – kumtakia rehma yeye na kizazi chake na amuombe Mwenyezi Mungu amjaalie kumpa mke muumini na mchamungu, na kwamba Yeye Allah (s.w.t.). amfanye asiwe mwenye kuhitaji yaliyoharamishwa.45

Nyakati Zisizopendekezwa

Nyakati Haram – Zinazokatazwa

1. Wakati wa heidhi (siku za mwezi za mwanamke):

Allah (s.w.t.). anaeleza ndani ya Suratul-Baqarah, aya ya 222 kama ifuatavyo:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ {222}

“Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie: Huo ni uchafu, basi jitengeni na wanawake (wakiwa) katika hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watakapotoharika …..” (Al-Baqarah; 2:222).

Endapo mtu anayejamiiana na mke wake akagundua kwamba kipindi chake cha hedhi kimeanza, basi na ajiondoe na kujitenga naye mara moja.

Ndani wa kipindi cha hedhi, vitendo vingine, mbali na kujamiiana vinaruhusiwa kufanyika kama inavyoonyeshwa na hadithi ifuatayo hapa chini:

Mu’awiyah ibn Umar anasimulia kwamba, yeye alimuuliza Imam as-Sadiq (a.s.): “Ni nini kinachoruhusiwa kwa mwanaume wakati mwanamke anapokuwa kwenye hali ya hedhi?” Imam akajibu akasema: “Mbali na sehemu zake za siri (yaani, mwili wote uliobakia isipokuwa sehemu zake za siri tu). 46

Imran ibn Qanzali anasimulia kwamba yeye alimuuliza Imam as-Sadiq (a.s.): “Ni vipi mwanaume anavyoweza kufaidika kutoka kwa mwanamke ambaye yuko kwenye hali yake ya hedhi?” Imam akajibu akasema: “Yale mapaja mawili (ya mwanamke huyo).” 47

Hata hivyo, ingawa mwili wote uliobakia, wa mwanamke (ukiachilia mbali sehemu zake za siri) unaruhusiwa kwa mume, lile eneo tokea kitovuni hadi magotini ni makuruhu (haipendekezwi kufikiwa);48 kwa hiyo inashauriwa sana kwamba mume azikwepe sehemu hizi vile vile.

Ni muhimu kutambua kwamba haipendekezwi kujishughulisha na ngono baada ya kwisha kwa hedhi. Hata hivyo, kama ni lazima, mwanamke anapaswa kuoga kwanza.49

Mwenyezi Mungu analieleza hili katika muen- delezo wa aya hiyo hapo juu: “Na wanapokuwa tohara, basi waingilieni kama alivyokuamuruni Mwenyezi Mungu.” (Al-Baqarah; 2:222).

2. Wakati wa Nifaas 50

3. Wakati wa kufunga katika mwezi wa Ramadhani.51

4. Wakati katika hali ya Ihraam na kabla ya kuswali swala ya Tawafun Nisaa.52

5. Pale ambapo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa amma mwanaume au mwanamke. Kujamiiana kunaruhusiwa endapo hakuwezi kuleta madhara makubwa.53

Nyakati Makuruhu

1. Katika Hali Ya Ihtilaam

Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ni Makruh kwamba mwanaume ambaye amekuwa Muhtalim (yaani, aliyekuwa katika hali ya janaba akiwa usingizini – kwenye ndoto) amwendee mkewe (ili kujamiiana naye) akiwa katika hali hii, isipokuwa pale atakapooga kwa ajili ya ihtilaam yake.”54

2. Wakati Wa Safari, Na Kukiwa Na Uwezekano Wa Kukosekana Maji

Imesimuliwa kutoka kwa Is’haaq ibn Ammaar: “Nilimuuliza Imam as- Sadiq (a.s.): “Mwanamume amefuatana na mke wake wakati wa safari, lakini hakupata maji yoyote kwa ajili ya kufanyia Josho. Je, anaweza kulala (kujamiiana) na mke wake?” Imam akajibu: “Hilo silipendi kama akifanya hivyo nalo ni makruh, isipokuwa kama akiwahofia kwamba kama hatakiendea kilicho halali yake, ataangukia kwenye kilichoharamishwa.”55

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Kadhim (a.s.): “Silipendi lile jambo la kwamba mtu anapokuwa safarini, ambaye hana maji halafu anajishughul- isha katika kujamiiana, isipokuwa kama anahofia madhara.” 56

(Katika hali kama hizi, kwa mujibu wa kanuni za Fiqhi, mtu anaweza kutayamman badala ya josho ili kuweza kuswali).

3. Usiku Wa Kupatwa Kwa Mwezi Na Mchana Wa Kupatwa Kwa Jua

Usiku mmoja, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa karibu na mmoja wa wake zake na jioni ili kukatokea kupatwa kwa mwezi, na hakuna lolote lililotokea baina yao. Mke wa Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kwa nini huna furaha na mimi usiku wote wa leo?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “

Ni nini unachokisema, jioni hii ilikuwa ni usiku wa kupatwa kwa mwezi na mimi ninajua kuwa ni Makruh kwamba nipate starehe usiku huu, kwa sababu Mwenyezi Mungu anakikaripia kikundi cha watu wasiojali na wasio makini kwenye Hujja na ishara Zake, na amewaelezea katika namna ifuatayo:

وَإِنْ يَرَوْا كِسْفًا مِنَ السَّمَاءِ سَاقِطًا يَقُولُوا سَحَابٌ مَرْكُومٌ {44}

“Na kama wakiona kipande cha mbingu kikianguka husema: ni mawingu yanayobebana.”
(At-Tuur: 52:44) 57

 

4. Baina Ya Subh As-Sadiq (Adhana Ya Alfajir) Na Kuchomoza Kwa Jua Na Kati Ya Kuzama Jua Na Kutoweka Kwa Wekundu Wa Mbingu

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Kupata kuwa na janaba wakati wa wekundu wa jua linapochomoza na wekundu wa jua linapozama ni Makruh.”58

5. Wakati Wa Tetemeko La Ardhi (Na Matukio Mengine Yanayolazimu Kuswali Salat Al-Ayaat)

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.) kwamba: “Mtu ambaye haachi raha na starehe katika wakati wa Ishara za Mwenyezi Mungu zinapodhihiri, anatokana na wale watu ambao wamezichukulia ishara zake Mwenyezi Mungu kuwa ni kama mzaha.”59

Mwili Wenye Afya Njema

Mwili wenye afya njema hurusu kuwa na maisha ya uhusiano timamu wa kijinsia. Vitendo kadhaa vimependekezwa katika Uislam, na kama maelekezo haya yatafanyiwa kazi, yatasababisha kuwa na mwili safi na wenye afya njema.

Mambo Yanayopendekezwa:

Mambo Yanayopendekezwa: 60

1. Kusafiri

2. Kufunga swaumu

3. Kula zabibu kavu 21 kwenye tumbo tupu lenye njaa

4. Kunywa maji ya mvua. 61

5. Kuswali Swala ya usiku Salaat al-Layl.

6. Kuosha mikono kabla na baada ya kula.

7. Kujisaidia pale inapohitajika haja ya choo.

8. Kuosha miguu (nyayo) kwa maji baridi baada ya kuoga.

9. Kuulinda mwili kutokana na baridi ya majira ya kupukutika kwa majani ya miti bali sio kuukinga na baridi ya wakati wa majira ya kuchipua (yaani kuvaa nguo nzito wakati wa kupukutika na nyepesi wakati wa majira ya kuchipua).

10. Kupata kiwango cha kutosha cha mapumziko.

11. Kula binzari nyembamba (aniseed) na tende.

12. Kutafuna vyema chakula chako.

13. Kula chakula pale tu unapojisikia njaa na kuepuka kula wakati umeshiba.

14. Kula chakula kiwango cha kiasi na hivyo kunywa kiasi cha kadiri

Matumizi Ya Mafuta Ya Kuchulia

Matumizi Ya Mafuta Ya Kuchulia62

Hususan mafuta ya kuchulia ni yenye manufaa sana kwa mwili wenye afya njema na vilevile ashiki ya kujamiiana, kiasi kwamba Maimam (a.s.) wamesimulia hadithi juu ya jambo hili:

Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba: “Kuupaka mwili na mafuta ya kuchulia kunalainisha ngozi, kunaboresha hali, kunafanya mtiririko wa maji na vimiminika ndani ya mwili kuwa rahisi, kunaondoa zahama, makunyanzi, afya mbaya na ugumu wa kipato na kunaleta nuru kwenye uso.”63

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.) kwamba: “Kuupaka mwili mafuta ya kuchulia wakati wa jioni ni chanzo cha mzunguko katika mishipa ya damu na (hili) huipa nguvu tena hali ya ngozi na kung’arisha uso.”

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Angalau mara moja kwa mwezi, au mara moja, mbili kwa wiki, pakaza mafuta kwenye mwili wako. Hata hivyo, kama wanawake wakiweza, ni lazima wajaribu kutumia mafuta kwenye miili yao kila siku.

Aina Za Mafuta Zifuatazo Zimependekezwa

1. Mafuta Ya Urujuani

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Mafuta ya urujuani ni mafuta ya nguvu: yasugue katika mwili wako ili yaweze kuondoa mau- mivu ya kichwa na macho.”

Mtu mmoja alianguka chini kutoka kwenye ngamia wake, na wakati maji yalipoanza kutoka kwenye pua yake, Imam as-Sadiq (a.s.) akamwambia: “Mwagia mafuta ya urujuani juu yake.” Yule mtu alipofanya hivyo, alitibika na akapona vizuri kabisa. Baada ya hapo Imam akasimulia: “Mafuta ya urujuani wakati wa kipupwe ni ya vuguvugu na wakati wa kiangazi ni yanakuwa poa kidogo64 kama watu wangeelewa yale maufaa ya mafuta haya, wangekunywa kiasi chake kikubwa; mafuta haya yanaondoa maumivu na kutibia na kuponya pua.”

2. Mafuta Ya Willow (Catkin)

Mtu mmoja alikuja kwa Imam as-Sadiq (a.s.) na kulalamika juu ya mikono na miguu iliyoatuka na kuwa na mikwaruzo. Imam akamwambia: “Chukua pamba, iloweke kwenye mafuta ya mti wa willow na uiweke hapo katikati (ya muatuko/mpasuko).” Yule mtu alipofanya kitendo hicho, yale maumivu yakatoweka.

3. Mafuta Ya Yungiyungi

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Mafuta ya yungiyungi yana tiba kwa magonjwa 70, na ni bora kama itakuwa yungiyungi nyeupe, ambayo inajulikana pia kama Jasmini ya Kiarabu.”

4. Mafuta Ya Zeituni

Kama mafuta ya zeituni yatachanganywa na asali na yakanywewa badala ya maji kwa muda wa siku tatu, yanaongeza nguvu ya kijinsia (za kujamiiana). Kama mafuta ya zeituni yatapakwa kwenye nywele, yanazuia zisikatike au kuota mvi nyeupe. Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Kula mafuta ya zeituni kunaongeza shahawa na nguvu ya uwezo wa kujamiiana.”65

Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Hasa kula mafuta ya zeituni kwa sababu dawa hii inatibia nyongo, inaondoa kikohozi, inaimarisha neva, inaponya maumivu, inafanya akhlaq kuwa nzuri, inafanya kinywa kunukia vizuri na inamuondolea mtu huzuni.”66

Imesimuliwa pia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kula mafuta ya zeituni na yasugue mwilini, kwani yanatokana na mti uliobarikiwa.”67

Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Mtu yoy- ote anayekunywa mafuta ya zeituni na kuyasugua mwilini mwake, Shetani hatamsogelea karibu yake kwa asubuhi arobaini.”

5. Mafuta Mengineyo

Mume na mke ambao wanataka kuongeza kiwango chao cha mshughuliko wa kujamiiana, lakini wakawa hawajui ni nini wanalazimika kukifanya, kadhalika watu ambao wangependa kufikia starehe zaidi ya kujamiiana, wanapaswa kutumia mafuta ya kuchulia kama vile zeituni ya Kiarabu, mafuta ya nazi, mafuta ya urujuani na mafuta ya zeituni.68

Mambo Yasababishayo Madhara Mwilini Kuhusiana Na Kujamiiana

1. Kujamiiana mwanzoni mwa usiku, iwe wakati wa kiangazi ama wa kipupwe, kunasababisha madhara kwenye mwili kwa sababu wakati huo tumbo na mishipa ya damu kwa kawaida inakuwa imejaa. Kujamiiana kunaweza kusababisha chango (msokoto wa tumbo bila kuharisha), kupooza (kwa uso), jongo (gout), mawe na kutiririka kwa mkojo, henia na udhaifu wa macho.69

Kwa hiyo, kushughulika katika kujamiiana mwishoni mwa usiku kunapendekezwa zaidi kwa ajili ya kudumisha mwili wenye afya njema, kwani kuna mwelekeo wa dhahiri kwamba wakati huo mtu hatakuwa na tumbo lililojaa.

2. Kadhalika, kujamiiana wakati wowote ule ukiwa na tumbo lililojaa ni kwenye madhara. Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Mambo matatu huharibu mwili wa mtu, nayo haya ni pamoja na: kwenda kuoga ukiwa na tumbo lililojaa shibe, kujihusisha na ngono pamoja na mkeo ukiwa na tumbo lililojaa, na kujihusisha na kujamiiana na wanawake wazee, waliodhaifika na wenye umri mkubwa.”70

3. Kuzuia kumwaga manii kwa kurudia mara kwa mara kunaweza kus- ababisha matatizo kwa wanamume, na vile vile hata kwa wanawake.71

Kuimarisha Na Kudhoofisha Tamaa Ya Ngono

Vitu Vinayoongeza Tamaa Ya Ngono:

Vitu Vinayoongeza Tamaa Ya Ngono:72

1. Karoti
2. Vitunguu
3. Nyama
4. Mayai
5. Tikiti maji
6. Komamanga freshi
7. Maziwa halisi
8. Zabibu tamu

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ