Rafed English

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia by : Sayyid Sadiq al-Husaini al-Shirazi

 

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni mkusanyo wa tarjuma ya vitabu viwili vya Kiarabu. Cha kwanza ni, al-Imam al-Mahdiyyu fii Riwayati Ahli's-Sunnah, kilichoandikwa na Sayyid Abdul Rahim al-Musawi. Sisi tumekiita, Imam Mahdi katika Riwaya za Sunni. Na cha pili ni: al- Mahdawiyyah 'Inda Ahli 'l-Bait kilichoandikwa na Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani . Sisi tumekiita: Umahdia katika Ahlul Bait. Tumevikusanya pamoja kwa vile tumeona maudhui yao yanafanana.

Vitabu hivi ni matokea ya utafiti wa kielimu pamoja na hoja zenye nguvu na utumiaji sahihi wa akili uliofanywa na wanachuoni wandishi wa vitabu hivi.

Kwa Waislamu, imani ya kuja kwa Mahdi (Muhudi) karibu ya mwisho wa dunia ni imani ambayo ina asili katika dini. Waislamu wote bila kujali tofauti za madhehebu zao wanakubaliana juu ya imani hii kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) alisema: “Hata iwe imebakia siku moja tu kwa dunia hii kufikia mwisho wake Allah atairefusha siku hiyo ili kumwezesha Imam huyo kutawala na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu wakati ambapo ulikuwa umejaa ufisadi na dhulma.”

Kitu cha kuvutia ni kwamba imani hii haiko kwa Waislamu tu bali hata katika dini nyingine wana imani kama hii kwamba atatokea mtu wakati wa mwisho ambaye ataondoa dhulma na ufisadi na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu.

Mkusanyo wa vitabu hivi ni wenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuvichapisha vitabu hivi kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kuvitarjumi vitabu hivi. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam, Tanzania.
Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbal- imbali za taaluma za kiislamu.

Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait.

Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehe- bu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiisilamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote.

Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu.

Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama.

Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa.

Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungum- zo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo sala- ma.

Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafu- ta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungum- zo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zina- zotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishau- ri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinabore- ka kwa kasi ya pekee.

Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanavyuoni watukufu, hivyo tunatoa shuku- rani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi.

Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichoki- weza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait
Kitengo cha utamaduni
Utangulizi
Imani ya ulazima wa kudhihiri suluhisho la ulimwengu huu na kusi- mamisha dola yake ni imani isiyohusu watu wa dini tu, bali inayajumuisha hata makundi ya kitheolojia na kifilosofia yasiyokuwa ya kidini. Kwa mfano kundi la wapagani wajulikanao kwa jina la Al-Jadliyyah ambalo limefasiri historia kwa kigezo cha kutokuwepo uwiano kinaamini kuwa ipo siku iliyoahidiwa mpishano huo utatoweka na nafasi yake kuchukuliwa na uwiano na amani.1

Kama pia tunavyowakuta baadhi ya wanafikra wasiokuwa wanadini waki- amini ulazima huu, kwa mfano mwanafikra mashuhuri wa kiingereza Bertrand Russell anasema: “Hakika ulimwengu unalingojea suluhisho litakaloukusanya chini ya bendera moja na tamko moja.”2

Na kauli yenye maana hii hii ameisema mfizikia maarufu Albert Einstein kwa kusema: “Hakika haiko mbali siku ambayo ulimwengu wote utatawaliwa na amani na usafi na watu kuwa katika hali ya kupendana na undugu.”3

Ama mwanafikra wa kiayalandi Bernard Shaw yeye katamka wazi mno na kwa undani kuliko uwazi na undani wa hawa wiwili, katika kutoa wasifu wa suluhisho na kuelezea ulazima wa umri wake kuwa mrefu kabla ya kudhihiri kwake amesema: “Hakika yeye ni mwanadamu hai mwenye mwili wenye afya bora na nguvu ya kiakili isiyokuwa ya kawaida. Ni mwanadamu wa hali ya juu kiasi kwamba mwanadamu huyu wa chini anamfikia baada ya juhudi za muda mrefu. Na hakika umri wake utarefu- ka mpaka avuke miaka mia tatu, na anaweza kunufaika na yale aliyoyaku- sanya ndani ya muda wote wa uhai wake mrefu.”4

Ama upande wa dini za kimungu zenyewe zimeashiria ulazima wa kudhi- hiri suluhisho la ulimwengu, na atakayefuatilia utabiri wa kimungu ndani ya vitabu vya biblia atavikuta vinaelekeza kwa huyu Mahdi ambaye ndiye anaaminiwa na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), kama ulivyothibitisha hilo uchambuzi mbalimbali unaohusu maelezo ya nukuu hizo za utabiri.5

Al-Qadhi As-Sabatwiy amezungumzia moja ya utabiri unaopatikana ndani ya kitabu cha Yoshua kutoka ndani ya Agano la kale ndani ya biblia unaoli- husu suluhisho la ulimwengu, akasema: “Maelezo haya yanamzungumzia Mahdi (a.s.).” Akaendelea mpaka akasema: “Shia Imamiyya wamesema: Yeye ndiye Muhammad bin Hasan Al-Askari ambaye alizaliwa mwaka mia mbili na hamsini na tano na mjakazi wa Hasani Al-Askari aitwaye Nargis huko Samrau zama za mtawala Al-Muutamid, kisha akaenda ghaibu muda wa mwaka mmoja6, kisha akadhihiri na kisha akaenda tena ghaibu na hiyo ndio ghaibu kubwa, na baada ya hapo harejei ila pindi Mwenyezi Mungu atakapotaka.

Na kwa kuwa kauli yao iko karibu mno na kile kinachozungumziwa na maelezo haya, na kwa kuwa lengo langu ni kuutetea umma wa Muhammad (s.a.w.w.) bila kujali upendeleo wa kimadhehebu ndio maana nimek- wambia kuwa lile wanalodai Shia Imamiyya ndilo lenye kuoana na maele- zo haya (ya agano la kale).”7

Pia Allamah Muhammad Ridha Fakhrul-Islam ambaye mwanzo alikuwa mkiristo kisha akawa mwislamu na kujiunga na madhehebu ya Ahlul-Bayti naye amefikia kwenye natija hii ambayo aliifikia As-Sabatwiy. Na ame- andika kitabu cha maarifa “Anisul-Aalam” akiwajibu mayahudi na wakris- to, na katika uchambuzi wake amezungumzia utabiri mbalimbali, na mwisho akahitimisha kuwa unaoana na Mahdi bin Hasan Al-Askari (a.s.).8

Hivyo anayechunguza kwa makini ndani ya maelezo hayo ya utabiri anakuta yanatoa wasifu wa suluhisho la ulimwengu usiyooana na mwingine asiyekuwa Mahdi mwenye kungojewa kwa mujibu wa imani ya kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.). Hivyo asiyekubali imani hii hawezi kupata mfano halisi unaozungumziwa na utabiri huo, kama tunavyolishuhudia hilo kwenye kauli za wafafanuzi wa Injili wanapozungumzia msitari wa kwanza mpaka wa kumi na saba wa kitabu cha ufunuo wa Yohana sura ya kumi na mbili, wao wametamka wazi kuwa mtu anayezungumziwa na utabiri huu uliyomo ndani ya mistari hii bado hajazaliwa, na hivyo tafsiri yake ya uwazi na maana yake dhahiri imeachwa mpaka mbele na muda usiojulikana ambao ndani yake atadhihiri.”9

Na kuna baadhi ya wanavyuoni wa kisunni wanaamini uchunguzi huo na natija hiyo, kwa mfano ustadhi Said Ayyub ameongoka kwa kusema kuwa mfano halisi unaozungumziwa na misitari iliyotangulia ya kitabu cha ufun- uo wa Yohana ni ule mfano halisi unaoaminiwa na kambi ya Ahlul-Bayt, akasema: “Imeandikwa ndani ya vitabu vya manabii kuwa Mahdi katika matendo yake hamna dosari.” Kisha maelezo haya akayaongezea kwa kusema: “Nakiri hakika mimi nimeyakuta hivyo hivyo ndani ya vitabu vya watu wa kitabu, hakika watu wa kitabu wamefuatilia habari za Mahdi kama walivyofatilia habari za babu yake (s.a.w.w.), na hivyo habari za kitabu cha ufunuo wa Yohana zikaelekeza kwa mwanamke ambaye ndani ya mgongo wake kutatoka wanaume kumi na wawili.” Kisha akaashiria mwanamke mwingine, yaani ambaye atazaa mwanaume wa mwisho ambaye yeye ni kutoka kwenye mgongo wa babu yake. Kitabu kimesema: “Hakika mwanamke huyu atazingirwa na hatari, na alama ya hatari ni kwa jina la “At-Tanin” (joka kubwa). Na ikasema: “At-Tanin alisimama mbele ya mwanamke mwenye kujiandaa kujifungua ili ammeze mtoto pindi tu atakapojifungua.”10

Maana yake ni kuwa utawala ulikuwa unataka kumuua kijana huyu, lakini baada ya mtoto kuzaliwa; Barkel anasema ndani ya ufafanuzi wake kuwa: “Pindi hatari ilipomshambulia, Mwenyezi Mungu alimnyakua mwanawe na kumuhifadhi.” Na maelezo “Mwenyezi Mungu alimnyakua mwanawe.”11 Maana yake ni: “Hakika Mwenyezi Mungu alimpeleka ghaibu mtoto huyu.” Kama ilivyo ndani ya kauli ya Barkel: “Kitabu kime- sema kuwa: “Hakika ghaibu ya kijana itakuwa siku elfu moja na mia mbili na sitini.12” Nao ndio muda wake na alama yake kwa watu wa kitabu.”

Kisha Barkel akasema kuhusu kizazi cha mwanamke wa kwanza kwa ujumla: “Hakika At-Tanin atafanya vita kali pamoja na kizazi cha mwanamke, kama alivyosema ndani ya kitabu: “At-Tanin akamkasirikia mwanamke na akaenda kuweka vita pamoja na kizazi chake kingine, ambao wanahifadhi usia wa Mwenyezi Mungu.”13

Baada ya maelezo hayo yaliyotangulia, ustadh Abu Said Ayyub akasema: “Huu ndio wasifu wa Mahdi na ndio ule ule wasifu wake kwa Shia Imamiyya wafuasi wa Maimamu kumi na wawili.14

Na akaipa nguvu kauli yake kwa maelezo aliyoyaweka pambizoni yaki- husu uonaji wa wasifu wa Mahdi na Mahdi wa nyumba ya Mtukufu Mtume.15

Hivyo uchunguzi mwingi umesisitiza kuwa utabiri unamwashiria Mahdi Al-Muntadhir mwenyewe anayeaminiwa na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.). Hebu sasa tuelekee kwenye riwaya za kambi ya Sunni ambazo zime- toka zikimzungumzia Imamu na kitambulisho chake, ili tuone je, zenyewe zimevuka kutoka kwenye anuani mpaka zikafika kuzungumzia utu wake baada ya riwaya za kudhihiri kwake kuwa nyingi mno, au ziliishia kwenye anuani tu?

Jibu ni: Inajulikana wazi kuwa anayeamini kudhihiri na ana yakini kabisa kuwa atatokea lakini hajapambanukiwa ni nani Mahdi aliyeahidiwa zama za mwisho, hatohesabiwa kuwa anamwamini Mahdi kama utakavyo Uislamu, kwa sababu anamwamini Mahdi kama anuani tu, lakini hamwamini mlengwa mwenyewe, ilihali kitendo cha kutofautisha kati ya kumwamini Imam mlengwa na kuamini kudhihiri kwake kinaharibu imani ya Mahdi, ni mfano wa imani ya mtu anayeamini wajibu wa Swala lakini yeye hajui nguzo zake.

Hivyo ili tufikie kumjua Imam Mahdi mwenyewe aliyelengwa na aliye hal- isi kwa kupitia riwaya za kisunni tutalazimika kuugawa uchambuzi katika mambo mbalimbali:
________________________
1. Buhuth Hawlal-Mahd cha As-Sayyid As-Shahid Muhammad Baqir As-Sadri: 87.

2. Al-Mahdi Al-Maw’uud wadaf ’ush-Shubhati An’hu cha As-Sayyid Abdur-Ridha As-Shuhrustaniy: 6.

3. Al-Mahdi Al-Maw’uud wadaf ’ush-Shubhati An’hu cha As-Sayyid Abdur-Ridha As-Shuhrustaniy: 6.

4. Bernadisho: Abbas Mahmuud Al-Uqad: 124 – 125.

5. Rejea kitabu Basharati Ahadayni cha Shaikh As-Sadiqiy, kimetafsiriwa kwa kiarabu kwa jina la “Al-Basharatu Wal-Muqaranatu”.

6. Kilichothibiti ni kuwa ghaibu ya Imam Mahdi baada ya kifo cha baba yake ilien- delea mpaka mwaka wa 69 A.H.

7. Al-Barahin As-Sabtwiyyah: Imenukuliwa kutoka kwenye kitabu Kashful-Astar cha Al-Mirza An-Nuriyyu: 84.

8. Basharati Ahadayni cha Muhammad As-Sadiqiy: 232.

9. Basharati Ahadayni cha Muhammad As-Sadiqiy: 232.

10. Ufunuo wa Yohana 12: 3.

11. Ufunuo wa Yohana 12: 5.

12. Muda wake umepatikana ndani ya kiebrania kwa kusema: “Atakwenda ghaibu dhidi ya At-Tanin zama moja, zama mbili na nusu zama.” Rejea Basharati Al-Ahadayn: 263.

13. Ufunuo wa Yohana 12: 13.

14. Al-Masih Ad-Dajjal: Said Ayyub 379 – 380 imenukuliwa kutoka kwenye Al- Mahdi Al-Muntadhar Fil-Fikri Al-Islamiy: Imetolewa na Markazi Ar-Risalah: 13 – 14.

15. Rejea Al-Imam Al-Mahdi Dhimnu Silsilatu Aalamul-Hidayah cha Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt: 9 – 24.
Kuna matamko mengi ya kukiri kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshazaliwa ambayo Sunni wameyasajili kwa kalamu zao. Na baadhi wamefanya kazi ya kuchunguza kukiri huku katika uchambuzi hasa unaojitegemea, hivyo uchunguzi huu ulikuwa unafuatana zama kwa zama kiasi kwamba haishindikani mwenye kukiri sasa kuhusu kuzaliwa kwa Mahdi kukutana na aliyekiri zama zilizotangulia, na hilo ni kuanzia zama za ghaibu fupi ya Imam Mahdi (a.s.) (260 – 329 A.H.) Na mpaka zama zetu hizi.

Sisi tutafupisha kwa kuwataja baadhi yao, ama atakayetaka kwa urefu na upana ni juu yake kurejea uchunguzi uliotangulia kuhusu kukiri huko,1 na hao baadhi ni:

1. Ibnul-Athir Al-Jazariy Izud-Din aliyefariki mwaka 360 A.H. Amesema ndani ya kitabu chake Al-Kamil fit-Tarikh kwenye mlango wa matukio ya mwaka 260 A.H. kuwa: “Ndani ya mwaka huo alifariki Abu Muhammad Al-Alawi Al-Askari, naye ni mmoja wa Maimamu kumi na wawili wa madhahebu ya Imamiyya, na yeye ndiye mzazi wa Muhammad ambaye wanamwamini kuwa ndiye anayengojewa.”2

2. Ibnu Khallakan aliyefariki mwaka 681 A.H. Amesema ndani ya kitabu Wafayatul-Aayan: “Abu Qasim Muhammad bin Hasan Al-Askari bin Ali Al-Hadiy bin Muhammad Al-Jawwad aliyetajwa kabla ni Imam wa kumi na mbili kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyya maarufu kwa sifa ya Hujah….mazazi yake yalikuwa siku ya Ijumaa nusu ya Shabani mwaka mia mbili hamsini na tano.” Kisha akanukuu kutoka kwa mwanahistoria Ar-Rahalah Ibnul-Azraqu Al-Fariqiy aliyefariki mwaka 577 A.H. kuwa amesema ndani ya kitabu Tarikh Mayyafariqina kuwa: “Hakika Hujjah aliyetajwa amezaliwa Mfunguo sita mwaka mia mbili hamsini na nane, na imesemekana kuwa ni mwezi nane Shabani mwaka hamsini na sita, na ndio kauli sahihi mno.”3

Nasema: Kauli sahihi kuhusu siku ya kuzaliwa kwake (a.s.) ni ile aliyoise- ma mwanzo Ibnu Khallakan, nayo ni siku ya ijumaa nusu ya mwezi wa Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano, kauli hiyo wameafikiana Shia wote. Wametoa riwaya nyingi sahihi kuhusu hilo huku wanavyuoni wao waliotangulia wakithibitisha hilo, hakika Sheikh Al-Kulayni aliyeishi zama za ghaibu ndogo ameitoa tarehe hii kwa ukamilifu, kutoa kulikosal- imika na akaitanguliza kabla ya riwaya zinazoikhalifu tarehe hiyo. Amesema kwenye mlango unaohusu kuzaliwa kwake (a.s.): “Amezaliwa (a.s.) nusu ya Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano.”4

As-Saduq aliyefariki mwaka 381 A.H. Amepokea kutoka kwa Sheikh wake Muhammad bin Muhammad bin Iswam Al-Kulayniy kutoka kwa Muhammad bin Yaqub Al-Kulayniy kutoka kwa Ali bin Muhammad bin Bandari amesema: “Imam wa zama hizi (a.s.) alizaliwa nusu ya Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano.”5 Na Al-Kulayniy hajanasibisha kauli yake kwa Ali bin Muhammad kwa sababu ya umashuhuri wake na kuwe- po itifaki juu yake.

3. Ad-Dhahabiy aliyefariki mwaka 747 A.H. Amekiri ndani ya vitabu vyake vitatu kuwa Mahdi (a.s.) ameshazaliwa, na hatujafuatilia vitabu vyake vingine. Amesema ndani ya kitabu chake Al-Ibaru: “Na ndani ya mwaka huo (yaani ndani ya mwaka 256 A.H.) alizaliwa Muhammad bin Hasan bin Ali Al-Had bin Muhammad Al-Jawwad bin Ali Ar-Ridha bin Musa Al-Kadhim bin Jafar As-Sadiq Al-Alawi Al-Husayniy, Abu Qasim ambaye Shia walimpa lakabu ya Al-Khalafu Al-Hujjah, wakampa pia lak- abu ya Al-Mahdi na Al-Mantadhar, na wakampa lakabu ya Sahibuz-Zaman na yeye ndiye hitimisho la Maimamu kumi na wawili.”6

Na amesema kwenye kitabu Tarikh Duwalil-Islam katika wasifu wa Hasan Al-Askari kuwa: “Hasan bin Ali bin Muhammad bin Ali Ar-Ridha bin Musa bin Jafar As-Sadiq, Abu Muhammad Al-Hashimiy Al-Husayniy ni mmoja wa Maimamu ambao Shia wanadai utakaso wao, na huitwa Hasani Al-Askari kwa kuwa aliishi Samrau, kwani eneo hilo huitwa Al-Askari, na yeye ndiye mzazi wa yule anayengojewa na Shia. Alifariki huko Samrau mwezi nane mfunguo sita mwaka mia mbili na sitini na akazikwa ubavuni mwa mzazi wake.

Ama mwanaye Muhammad bin Hasan ambaye Shia wanamwita Al-Qaim Al-Khalafu Al-Hujjah yeye alizaliwa mwaka wa hamsini na nane, na inase- mekana ni mwaka hamsini na sita.”7

Na amesema ndani ya kitabu Siru Aalamin-Nubalai: “Sharifu Al- Muntadhar Abu Qasim Muhammad bin Hasan Al-Askari bin Ali Al-Hadiy bin Muhammad Al-Jawwad bin Ali Ar-Ridha bin Musa Al-Kadhim bin Jafar As-Sadiq bin Muhammad Al-Baqir Ibnu Zaynul-Abidina Ali bin Husein As-Shahidu Ibnu Imam Ali bin Abi Talib Al-Alawi Al-Husayni ni hitimisho la mabwana kumi na wawili.”8

Nasema: Kinachotuhusu sisi katika rai ya Ad-Dhahabiy kuhusu kuzaliwa kwa Mahdi tayari tumeshakifafanua. Ama kuhusu imani yake juu ya Mahdi ni kuwa yeye ni kama katika kauli zake zote nyingine bado alikuwa anan- gojea sirabi, kama tulivyoweka wazi hilo kuhusu mtu anayeamini kuwa Mahdi ni Muhammad bin Abdullah.

4. Ibnu Al-Wardiy aliyefariki mwaka 749 A.H. mwishoni mwa muhtasari ujulikanao kwa jina la Tarikh Ibnul-Wardiy: “Muhammad bin Hasan Al- Khalisu alizaliwa mwaka mia mbili hamsini na tano.”9

5. Ahmad bin Hajar Al-Haythamiy Ash-Shafiy aliyefariki mwaka 974 A.H. amesema kwa maelezo haya ndani ya kitabu chake As-Sawaiqul-Muhriqah mwishoni mwa sura ya tatu ya mlango wa kumi na moja: “Abu Muhammad Hasan Al-Khalisu, na Ibnu Khallakani amemfanya huyu kuwa ndio Al-Askari, alizaliwa mwaka mia mbili thelathini na mbili…..alifia huko Samrau na alizikwa karibu na baba yake na ami yake akiwa na umri wa miaka ishirini na minane, na inasemekana kuwa alipewa sumu, na wala hakumwacha ila mwanae wa kiume Abu Qasim Al-Hujah, na alikuwa na umri wa miaka mitano baba yake alipofariki. Lakini Mwenyezi Mungu alimpa hekima na anaitwa Al-Qaim Al-Muntadhar. Imesemekena ni kwa kuwa alifichwa huko Madina na akatoweka na haikujulikana amekwenda wapi.”10

6- As-Shabrawiy Ash-Shafiy aliyefariki mwaka 1171 A.H. ametamka wazi ndani ya kitabu chake Al-Ittihafu kuwa: “Imam Mahdi Muhammad bin Hasan Al-Askari (a.s.) amezaliwa usiku wa nusu ya Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano hijiriya.11

7. Muumin bin Hasan As-Shablanjiy aliyefariki mwaka 1308 A.H. Ndani ya kitabu chake Nurul-Absar amekiri ndani ya maneno mengi kuwepo jina Imam Mahdi na nasaba yake tukufu toharifu, na kuniya yake na lakabu zake, mpaka akasema: “Na yeye ndiye Imam wa mwisho katika maimamu kumi na wawili kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyya.”12

8’. Khayrud-Dini Az-Zarkiliy aliyefariki mwaka 1396 A.H. Amesema ndani ya kitabu chake Al-Aalam katika wasifu wa Imam Mahdi Al- Muntadhar: “Muhammad bin Hasan Al-Askari Al-Khalisu bin Ali Al- Hadiy Abu Qasim, Imam wa mwisho kati ya maimamu kumi na mbili wa Shia Imamiyya….alizaliwa Samrau na baba yake alifariki yeye akiwa na umri wa miaka mitano….Na katika tarehe ya kuzaliwa kwake inasemekana kuwa ni nusu ya Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano, na katika tare- he ya kwenda ghaibu ni mwaka mia mbili sitini hijiriya.”13

Nasema: Tarehe ya kuanza ghaibu ndogo ni mia mbili na sitini hijiriya, hiyo ni kwa itifaki ya Shia wote pamoja na wengine walioandika kuhusu ghaibu ndogo katika vitabu tulivyoviona, na huenda tarehe iliyomo ndani ya kitabu Al-Aalam inatokana na makosa ya chapa, kwa sababu Az- Zarkiliy hajaandika tarehe ya ghaibu kwa herufi bali kaandika kwa tarakimu, na hivyo uwezekano wa kuwepo makosa katika kuchapa tarakimu ni jambo rahisi mno. Na kuna matamko mengine mengi ya kukiri ambayo uchambuzi hauturuhusu kuyanukuu.14
________________________
1. Rejea kitabu Al-Iman As-Sahih cha As-Sayyid Al-Qazwiniy. Kitabu Al-Imam Al-Mahdi fi Nahjul-Balagha cha Sheikh Mahdi Faqih Imaniy. Kitabu Man huwa Imamul-Mahdi cha At-Tabriziy. Kitabu Ilzamun-Naswib cha Sheikh Ali Al-Yazdiy Al-Hairiy. Kitabu Al-Imam Al-Mahdi cha ustadhi Ali Muhammad Dakhil. Kitabu Difau Anil-Kafiy cha As-Sayyid Thamir Al-Umaydiy. Ndani ya hiki cha mwisho wametajwa watu mia moja na ishirini na nane kutoka Sunni ambao wamekiri kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshazaliwa huku akiwapanga kulingana na karne zao, hivyo wa kwanza wao alikuwa ni Abubakri Muhammad bin Harun Ar-Riwayaniy ndani ya kitabu chake Al-Musnad aliyefariki mwaka 307 A.H. Na wa mwisho wao alikuwa ni ustadhi wa zama zetu Yunus Ahmad As-Samirai ndani ya kitabu chake Samirau fi Adabul-Qurni At-Thalithu Al-Hijiriy, kilichochapwa kwa msaada wa chuo kikuu cha Baghdadi mwaka 1968 A.D. Tazama Difau Anil-Kafiy 1: 568 – 592 chini ya anwani: Dalili ya sita: Matamko ya kukiri kwa Sunni.

2. Al-Kamil fit-Tarikh 7: 274 mwishoni mwa matukio ya mwaka 260 A.H.

3. Wafayatul-Aayan 4: 176, 562.

4. Usulul-Kafiy 1: 514, mlango wa 125.

5. Kamalud-Dini 2: 430, mlango wa 42.

6. Al-Ibaru fi Khabari Man Ghabara 3: 31.

7. Tarikhul-Islam: Juzuu ya kumi na tisa, kwenye matukio na vifo (251 – 260 A.H.): 113.

8. Siru Aalamin-Nubalai 13: 119, wasifu namba 60.

9. Nurul-Absar: 186. Hatujapata ndani ya Tarikh Ibnu Al-Wardiy ndani ya mwaka uliyotajwa, hatujui je, maelezo yaliondolewa?!!!

10. As-Sawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar Al-Haythamiy, chapa ya kwanza: 207 na chapa ya pili: 124 na chapa ya tatu: 313 – 314.

11. Al-Ittihafu Bihubil-Ashrafi: 68.

12. Nurul-Absar: 186.

13. Al-A’alam 6: 80.

14. Rejea Al-Mahdi Al-Muntadhar fil-Fikri Al-Islamiy, kilichotolewa na Markazur-Risalah: 123 – 127.
Mwenye kufuatilia Hadithi sahihi zilizopatikana kuhusu jina na nasaba ya Mahdi ndani ya vitabu vya Sunni atazikuta nyingi mno zikisisitiza uhalisia mmoja nao ni: Nasaba ya Mahdi inarejea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kuwa yeye ni miongoni mwa Ahlul-Bait na miongoni mwa maimamu kumi na wawili walio watakasifu, na yeye ndiye wa mwisho wao. Naye ni Muhammad bin Hasan Al-Askari (a.s.) Ibnu Ali Al- Hadi bin Muhammad Al-Jawad bin Ali Ar-Ridha bin Musa Al-Kadhim bin Jafar As-Sadiq bin Muhammad Al-Baqir bin Ali As-Sajjad bin Husein As- Shahid wa Karbala bin Ali bin Abi Talib (a.s.).

Na ndiyo mwenye lakabu ya Al-Mahdi Al-Muntadhar anayeoana na ile imani ya Shia Imamiyya. Zifuatazo ni riwaya zinazozungumzia jina lake na nasaba yake:
Mahdi ni: Mkinana, Mkurayshi na Hashimia
Imepokewa kutoka kwa Qatadah amesema: “Nilimwambia Said bin Al- Musayyab: Mahdi ni haki? Akasema: ‘Ndio ni haki.’ Nikamwambia: Anatokana na nani yeye? Akasema: ‘Anatokana na Kinana.’ Nikasema: Kisha kutoka kwa nani? Akasema: ‘Kutoka kwa Kurayshi.’ Nikasema: Kisha kutoka kwa nani? Akasema: ‘Kutoka kwa wana wa Hashim.”1

Hivyo kwa mujibu wa riwaya hii Mahdi ni mkinana, mkurayshi na muhashimia, na wala hakuna mgongano katika lakabu hizi, kwa sababu kila muhashimia anatokana na mkurayshi na kila mkurayshi anatokana na mkinana, kwa sababu Kurayshi ni An-Nadhar bin Kinanah, kwa itifaki ya wasomi wote wa nasaba za watu.
Mahdi ni kutoka kwa watoto wa Abdul-Muttalib
Ibnu Majah amepokea kutoka kwa Anas bin Malik amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Sisi ni kizazi cha Abdul-Mutwalib mabwana wa watu wa Peponi, mimi, Hamza, Ali, Jafar, Hasan, Husein na Mahdi.”2 Kwa mujibu wa riwaya hii Mahdi anakuwa miongoni mwa watoto wa Abdul-Mutwalib.
Mahdi ni kutoka kizazi cha Abu Talib
Imepokewa kutoka kwa Saif bin Umayrah amesema: Nilikuwa kwa Abu Jafar Al-Mansur akaanza kuniambia: “Ewe Saif bin Umayrah! Ni lazima atapatikana mwenye kunadi tokea mbinguni kwa jina la mtu kutoka kizazi cha Abu Talib.”

Nikamwambia: Ewe kiongozi wa waumini! Mimi ni fidia kwako; hii ni riwaya? Akasema: “Ndiyo, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika nimeisikia kwa masikio yangu mawili.”

Nikamwambia: Ewe kiongozi wa waumini! Hakika Hadithi hii sijaisikia kabla ya muda huu. Akasema: “Ewe Saif! Hakika yenyewe ni kweli, na iki- tokea basi mimi nitakuwa wa kwanza kumkubali, kwani hakika wito ni kuelekea kwa mtu kutoka wana wa ami yetu.”

Nikamwambia: Ni mtu kutoka kizazi cha Fatima? Akasema: “Ndiyo ewe Saif, laiti nisingeisikia kutoka kwa Abu Jafar Muhammad bin Ali akiniha- dithia basi nisingeikubali kutoka kwa mtu yeyote hata kama wangenisimu- lia watu wote wa aridhini, lakini aliyenisimulia ni Muhammad bin Ali.”3

Na Hadithi hii inasisitiza kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha Abu Talib.
Mahdi ni kutoka Ahlul-Bayt (a.s.)
Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Kiyama hakitosimama mpaka ardhi ijae dhuluma na uadui.” Akasema: “Kisha atokee mtu kutoka ndani ya kizazi changu au watu wa nyumba yangu atakayeijaza usawa na uadilifu kama ilivyojaa dhuluma na uadui.”4

Na mfano wake ni ile iliyotoka kwa Abdullah kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kiyama hakitosimama mpaka aje mtu miongoni mwa watu wa nyumba yangu, jina lake linalingana na jina langu.”5

Imepokewa kutoka kwa Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amese- ma: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mahdi ni kutoka kwetu sisi Ahlul-Bayt, Mwenyezi Mungu atamleta ndani ya usiku mmoja.”6
Mahdi ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)
Kutoka kwa Ibnu Umar amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Zama za mwisho atatokea mtu kutoka kwenye kizazi changu, jina lake ni jina langu, kuniya yake ni kuniya yangu, ataijaza ardhi uadili- fu kama itakavyokuwa imejaa ujeuri, na huyo ndiye Mahdi.”7
Mahdi ni kutoka kizazi cha Fatima (a.s.)
1- Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mahdi ni kweli na yeye ni kutoka kizazi cha Fatima.”8

2- Kutoka kwa Ummu Salamah amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Mahdi ni kutoka ndani ya kizazi changu kutoka kwenye kizazi cha Fatima.”9
Mahdi ni kutoka kizazi cha Husein (a.s.)
Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamani (r.a.) amesema: “Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alituhutubia, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akatutajia yatakayotokea, kisha akasema: “Hata kama dunia itabakiwa na siku moja, basi Mwenyezi Mungu ataire- fusha siku hiyo mpaka amlete mtu kutoka ndani ya kizazi changu, jina lake ni jina langu.”

Salman Al-Farsi (r.a.) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni kutoka kwa mwanao yupi? Akasema: “Ni kutoka kwa huyu.” Akawa amempiga Husein (a.s.) kwa mkono wake.10

Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliugua ugonjwa ambao ulimdhoofisha, basi Fatima (a.s.) akaingia kumtembelea na mimi nikiwa nimeketi kuliani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.w.), basi alipoona udhaifu alio nao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza kulia mpaka machozi yakafika mashavuni. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: “Ewe Fatima! Kitu gani chakuliza? Hivi hujui kuwa Mwenyezi Mungu aliitazama ardhi yote mara moja akamchagua baba yako kutoka humo na kumfanya nabii, kisha akaitazama mara ya pili akamchagua mume wako, ndipo akanifunulia na nikakuoza kwake na nikamfanya wasii. Hivi hujui kuwa wewe uko katika heshima ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa baba yako alikuoza kwa mtu mwenye elimu mno zaidi yao, mvumilivu mno kuliko wao na wa kwanza wao kuukubali Uislamu.”

Ndipo Fatima akacheka na kufurahi. Mtume wa Mwenyezi Mungu akata- ka kumuongezea nyongeza ya kheri ambayo Mwenyezi Mungu aliigawa kwa Muhammad na kizazi cha Muhammad, akamwambia: “Ewe Fatima! Ali ana fadhila nane: Kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hekima yake, mke wake, watoto wake Hasan na Husein, kuamrisha kwake mema na kukataza kwake maovu.

“Ewe Fatima! Sisi Ahlul-Bayt tumepewa vitu sita, ambavyo hajapewa yeyote vitu hivyo kati ya watu waliotangulia kabla yetu na wala hatovipa- ta yeyote atakayekuja baada yetu asiyekuwa Ahlul-Bayt: nabii wetu ndiye mbora wa manabii, naye ni baba yako. Wasii wetu ndiye mbora wa mawasii, naye ni mume wako. Shahidi wetu ndiye mbora wa mashahidi, naye ni Hamza ami ya baba yako. Na wajukuu wawili wa umma huu wana- toka kwetu, nao ni wanao wawili.

“Na Mahdi wa umma huu ambaye Isa ataswali nyuma yake anatoka kwetu.” Kisha akapiga mkono wake juu ya bega la Husein (a.s.) na kuse- ma: “Mahdi wa umma huu atatoka kwa huyu.”11
Jina la mzazi wa kike wa Mahdi na kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha As-Sadiq (a.s.)
Imepokewa kutoka kwa mfafanuzi wa lugha ajulikanaye kwa jina la Ibnul-Khashabu, amesema: Alinisimulia Abu Qasim At-Tahir bin Harun bin Musa Al-Kadhim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, amesema: Bwana wangu Jafar bin Muhammad alisema: “Mrithi mwema ni kutoka kizazi changu naye ni Mahdi, jina lake ni Muhammad na kuniya yake ni Abu Qasim, atatokea zama za mwisho, mama yake ataitwa Nargis na juu ya kichwa chake (a.s.) kutakuwa na wingu likimkinga na jua, litazunguka pamoja naye popote atakapokwenda huku likinadi kwa sauti fasaha huyu ndiye Mahdi mfuateni.”12
Mahdi ni kutoka kizazi cha Ar-Ridha (a.s.)
Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Khalid, amesema: Ali bin Musa Ar- Ridhaa alisema: “Hana dini asiyekuwa na ujidhibiti, na hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mcha Mungu kuliko nyinyi.” Kisha akase- ma: “Hakika mtu wa nne kutoka katika kizazi changu ni mwana wa bibi wa watumwa, kupitia yeye Mwenyezi Mungu atatoharisha ardhi dhidi ya kila ujeuri na dhuluma….”13
Jina la mzazi wa kiume wa Imam Mahdi (a.s.)
Ar-Riwayyaniy na At-Tabaraniy na wengineo wametoa: “Mahdi ni kutoka kizazi changu, uso wake ni kama nyota ing’aayo, rangi yake ni rangi ya kiarabu, na kiwiliwili cha kiisraeli – yaani mrefu – ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhulma. Watu wa mbinguni na ardhini watarid- hia ukhalifa wake.”

Pia katika kitabu chake Al-Hilyatu imepatikana: “Yeye ni kijana mwenye macho yenye wanja, mwenye nyusi laini zilizolala kwa urefu, mwenye pua nyembamba yenye mwinuko, mwenye ndevu fupi zilizosokotana, na juu ya shavu lake la kulia kuna weusi.”

Sheikh Al-Qutub Al-Ghawthiy Sayyidiy Muhyid-Din Ibnul-Arabiy amese- ma ndani ya kitabu Al-Futuhati: “Fahamuni kuwa ni lazima atatokeza Mahdi, lakini hatoki mpaka ardhi ijae ukatili na dhuluma na ndipo aje kui- jaza uadilifu na usawa, na yeye ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kutoka kizazi cha Fatima Mola awe radhi naye, babu yake ni Husein bin Ali bin Abu Talib na mzazi wake wa kiume ni Hasan Al-Askari mwana wa Imam Ali An-Naqiy mwana wa Imam Muhammad At-Taqiy mwana wa Imam Ali Ar-Ridhaa mwana wa Imam Musa Al- Kadhim mwana wa Imam Ja’far As-Sadiq mwana wa Imam Muhammad Al-Baqir mwana wa Imam Zaynul-Abidina mwana wa Imam Husein mwana wa Imam Ali bin Abu Talib, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.

“Jina lake linaoana na jina la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), waislamu watampa kiapo cha utii eneo la kati ya Ruknu na Maqam. Anafanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu katika maumbile na anakarib- iana naye katika maadili, watu wema kupitia yeye ni watu wa Kufa, ata- gawa mali kwa usawa, atafanya uadilifu kwa raia na maisha bora yatakuwa mikononi mwake.”14
________________________
1. Uqadud-Durari: 42 – 44, mlango wa kwanza. Mustadrak Al-Hakim 4: 553. Maj’mauz

2. Sunanu Ibnu Majah 2: 1368, Hadithi ya 4087, mlango wa kutokeza kwa Mahdi.

Mustadrak Al-Hakim 3: 211. Maj’maul-Jawamiu cha As-Suyuti 1: 851.

3. Uqadu Ad-Durar cha Al-Muqaddasiy As-Shafiiy: 149 – 150, mlango wa nne.

4. Musnad Ahmad 3: 424, Hadithi ya 10920. Musnad Abu Yaala 2: 274, Hadithi ya 987. Al- Mustadrak 4: 577. Uqadu Ad-Durar: 36, mlango wa 1. Mawaridu Ad-Dham’ani: 464, Hadithi ya 1879 na 1880. Muqadimah cha Ibnu Khalduni: 250, sura ya 53. Jam’ul-Jawamiu
1: 902. Kanzul-ummal 14: 271, Hadithi 38691. Yanabiul-Mawaddah 433, mlango wa 73.

5. Musnadul-Bazzaz 1: 281. Musnad Ahmad: 3761. Sunan At-Tirmidhiy 4: 505, mlango wa
52, Hadithi ya 2230. Al-Muujam Al-Kabir 10: 135, Hadithi ya 10221 ikiwa na tofauti kido- go. Tarikh Baghdad 4: 388. Uqad Ad-Durar: 38, mlango wa 3. Matwalibu As-Suul 2: 81. Al-Bayan fi Akhbari Swahibuz-Zaman cha Muhammad An-Nawfaliy Al-Qurayshiy Al- Kunjiy As-Shafiiy: 91. Faraidu As-Samtwayn 2: 327, Hadithi ya 576. Ad-Durul-Manthur 6:58. Jam’ul-Jawamiu 1:903. Kanzul-ummal 14: 271, Hadithi ya 38692. Burhanul-Muttaqiy: 90, mlango wa 2, Hadithi ya 4.

6. Ibnu Abu Shayba 8: 678, Hadithi 190. Futunu Ibnu Hammad. Musnad Ahmad 1: 84. Tarikh Al-Bukhari 1: 371, Hadithi ya 994. Sunan Ibnu Majah 2: 1367, mlango wa 34, Hadithi ya 4085. Musnad Abu Yaala 1: 359, Hadithi ya 465. Hilyatul-Awliyai 3: 177. Al- Kamil cha Ibnu Adiy 7: 2643. Al-Firdawsu 4: 222, Hadithi ya 6619. Al-Bayani fi Akhbari Swahibuz-Zaman cha Al-Kunjiy As-Shafiiy: 100. Uqadu Ad-Durar: 183, mlango wa 6. Al- Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 2856, Hadithi ya 1432. Faraidu As-Samtwayni 2: 331, Hadithi ya 583. Mizanul-Iitidal 4: 359, Hadithi ya 9444. Muqadimah Ibnu Khalduni 1: 396, mlango 53. Tahdhibu At-Tahdhibu 11: 152, Hadithi ya 294. Urufus-Suyutiy Al-Hawiy 2: 213. Ad- Durul-Manthur 6: 58. Jam’ul-Jawamiu 1: 449. Al-Jamiu As-Saghir 2: 672, Hadithi ya 9243. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 163, mlango wa 511, sura ya 1. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38664. Burhanul-Muttaqiy: 87, mlango wa 1, Hadithi ya 43, na ukurasa wa 89, mlango wa 2, Hadithi ya 1. Mirqatul-Mafatihi 9: 349 humo mna tofauti kidogo. Faydhul-Qadir 6: 278, Hadithi ya 9243.

7. Tadhkiratul-Khawwas: 363, Uqadu Ad-Durar: 43, mlango wa 1. Minihajus- Sunnah cha Ibnu Taymiyah 4: 86 – 87.

8. Tarikh Bukhari 3: 364. Al-Muujam Al-Kabir 23: 267, Hadithi ya 566. Mustadak Al-Hakim 4: 557.

9. Sunan Abu Dawdi 4: 104, Hadithi ya 4284. Sunan Ibnu Majah 2: 1368, mlan- go wa 34, Hadithi ya 4086. Al-Firdawsu 4: 497, Hadithi ya 6943. Maswabihul- Baghawi 3: 492, mlango wa 3, Hadithi ya 4211. Jamiul-Usul 5: 343. Matwalibu As-Suul: 8. Uqadu Ad-Durar: 36, mlango wa 1. Mizanul-Iiitidal 2: 87. Mishkatul- Maswabihi 3: 24, sura ya 2, Hadithi ya 5453. Tuhfatul-Ashraf 13: 7, Hadithi ya 18153. Al-Jamiu As-Saghir 2: 672, Hadithi ya 9241. Ad-Durul-Manthur 6: 57.

Jam’ul-Jawamiu 1: 449. As-Swawaiq cha Ibnu Hajar: 141, mlango wa 11, sura ya 1. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38662. Mirqatul-Mafatihi 9: 350. Is’afur- Raghibina: 145. Faydhul-Qadir 6: 277, Hadithi ya 9241. At-Taju Al-Jamiu Lil- Usul 5: 343.

10. Al-Manaru Al-Munifu cha Ibnul-Qayyim: 148, 329, sura ya 50, kutoka kwa At- Tabaraniy ndani ya kitabu Al-Awsatu. Uqadu Ad-Durar: 45, mlango wa kwanza, humo mna: “Ameitoa Al-Hafidhu Abu Nua’im katika sifa ya Mahdi.”. Dhakhairul-Uqba cha Al-Muhibu At-Tabari: 136, humo mna: “Maelezo yasiyoainishi yanatafsiriwa na haya yaliyoainishi.” Faraidu As-Samtwayni 2: 325, 575, mlango wa 61. Al-Qawlu Al-Mukhtasar cha Ibnu Hajar 7: 37, mlango wa 1. Faraidu Fawaidul-Fikri: 2, mlango wa 1. As-Siratul-Halbiyah 1: 193. Yanabiul- Mawaddah 3: 63, mlango wa 94. Na kuna Hadithi nyingine zenye kuelezea sifa hizi mahususi ndani ya kitabu Maqtalul-Imam Al-Husayn cha Al-Khawarazamiy Al-Hanafiy 1: 196. Faraidu As-Samtwayn 2: 310 – 315, Hadithi za 561 – 569. Yanabiul-Mawadah 3: 170: 212, mlango wa 93 na mlango wa 94.

11. Al-Bayanu: 120, mlango 9. Al-Fusulul-Muhimmah: 286, chapa ya Darul- Adh’wai, sura ya 12. Yanabiul-Mawadah: 490 na 493, mlango wa 94, japokuwa kuna tofauti kidogo.

12. Yanabiul-Mawaddah: 491 kutoka kwenye kitabu Al-Arbauni cha Al-Hafidhu Abu Naim Al-Isbihaniy.

13. Yanabiul-Mawaddah: 448 na 489, imenukuliwa kutoka kitabu Faraidu As- Samtwayni.

14. Mashariqul-An’wari Fifawzi Ahlil-Iitibar cha Sheikh Hasan Al-Adawi Al- Hamzawiy Al-Misriy: 476 – 477, sura inayohusu Mahdi. Yawaqitul-Jawahir 562, mlango unaohusu alama zote za Kiyama, imenukuliwa kutoka kwenye kitabu Al-
Baada ya kubainika jina la Imam Mahdi na nasaba yake, basi katika jambo hili tutazungumzia riwaya zilizopatikana ndani ya vitabu vya Sunni zina- zohusu sifa za kimaumbile za Imam (a.s), kuanzia sifa ya uso, rangi yake, nywele na mfano wa hayo. Tutabainisha hayo ndani ya riwaya mbalimbali.

1- Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Mahdi wa kutoka kwangu ni mwenye paji bapa na pua nyembamba yenye mwinuko, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa ukatili na dhuluma…”1

2 - Imepokewa kutoka kwa Hudhayfa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mahdi ni mtu kutoka ndani ya kizazi changu, uso wake ni kama mwezi ung’aao, rangi yake ni rangi ya kiarabu, kiwili- wili chake ni kiwiliwili cha kiisraeli, ataijaza ardhi uadilifu, kama itakavyokuwa imejaa dhulma. Wataridhia ukhalifa wake watu wa mbingu- ni na aridhini na ndege wa angani….” 2

3- Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Mahdi ni kutoka kwetu Ahlul-Bayt, ni mwenye pua nyembamba yenye mwinuko ulionyooka, mwenye paji bapa, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa ukatili na dhuluma. Ataishi hivi.” Akawa amefungua mkono wake wa kushoto na vidole viwili – kidolegumba na kidoleshahada – vya mkono wa kulia na akawa amefumba vitatu vilivyobaki.3

4- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Al-Harthu amesema: “Mahdi ata- jitokeza akiwa na miaka arubaini kama mtu kutoka kizazi cha Israil.”4

5- Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Jubayri amesema: “Mahdi ni mwenye nyusi laini zilizolala kwa urefu, paji bapa na macho meusi mno, atakuja kutokea Hijazi na kutulia juu ya mimbari ya Damascus akiwa kijana wa miaka kumi na minane.”5

6- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Bashir kutoka kwa Kaab amese- ma: “Mahdi ni mnyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama unyenyekevu wa mbawa za furukombe.”6

7- Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Mahdi ni kijana kutoka kwetu Ahlul-Bait.”7

8- Imepokewa kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Awfi kutoka kwa baba yake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu atamleta mtu kutoka ndani ya kizazi changu, ana mwanya na paji bapa, ataijaza ardhi usawa na uadilifu na ataimwagia mali nyingi.”8

9- Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Ja’far kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Hakika mwana wa huyu ni bwana kama alivy- omwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Mwenyezi Mungu ata- toa kwenye mgongo wake mtu mwenye jina la nabii wenu, anafanana naye kwa maumbile na tabia, atatoka wakati ambao watu watakuwa katika mghafala, wakiifisha haki na kudhihirisha dhulma. Wallahi laiti angekuwa hatokei basi ningemkata shingo yake. Kwa kutokeza kwake watafurahia watu wa mbinguni na wakazi wake, na yeye ni mtu mwenye paji bapa, pua nyembemba yenye mwinuko, tumbo pana, mwenye matege huku paja lake la kulia likiwa na weusi na ni mwenye mwanya, ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ukatili.”9

10- Imepokewa kutoka kwa Sulayman bin Habib amesema: “Nilimsikia Abu Umamah Al-Bahiliy akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Kati yenu na Rum kutakuwa na vituo vinne vya kupumzika kwa siku, cha nne atakifungua mikononi mwa mtu kutoka jamaa wa mteule na atadumu miaka saba.” Basi mtu mmoja kutoka ukoo wa Abdul-Qaysi aliyekuwa akiitwa Al-Mustawradu bin Ghaylan aka- muuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani atakuwa Imam wa watu zama hizo? Akasema: “Mahdi kutoka ndani ya kizazi changu, mwenye miaka arubaini, uso wake kama nyota ing’aayo huku kwenye shavu lake la kulia kukiwa na weusi….”10

11- Imepokewa kutoka kwa Al-Haytham bin Abdur-Rahman kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Mahdi sehemu ya kuzaliwa kwake ni Madina, ni kutoka Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), jina lake ni jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), eneo atakalohamia ni Baytul-Maqdas, ana ndevu za msokotano, mwenye macho ya wanja, meno yake ya mbele ni yenye kung’aa, usoni mwake ana weusi, mwenye pua nyembamba yenye mwinuko, mwenye paji bapa, begani kwake kuna alama ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). bendera yake inatokana na kitambaa kisichoshonwa yenye utande wa nyuzinyuzi, ni nyeusi ya pembe nne na imekunjwakun- jwa, haijapepea tangu afariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na haitopeperush- wa mpaka atokeze Mahdi (a.s.). Mwenyezi Mungu atampa msaada kwa Malaika elfu tatu watakaowapiga mbele na nyuma wale waliowakhalifu.”11
________________________
1. Sunan Abi Dawdi 4: 107, Hadithi ya 428. Mustadrak Al-Hakim 4: 557, japo ina tofauti kidogo. Maalimus-Sunan 4: 344. Maswabihul-Bahgawi 3: 492, Hadithi ya 4212. Al-Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 859, Hadithi ya 1443. Jamiul-Usul 5: 343, mlango 7. Matalibus-Su’ul 2: 80, mlango wa 12. Al-Bayan: 117. Uqadu Ad-Durar: 59, mlango wa 3. Mishkatul-Maswabihi 3: 171, mlango wa 2, sura ya 2, Hadithi ya 5454. Al-Jamiu As-Swaghir 2: 672, Hadithi ya 9244. Jam’ul-Jawamiu 1: 449. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38665. Mirqatul-Mafatihu 9: 351, Hadithi ya 5454. Faydhul-Qadir 6: 278, Hadithi ya 9244. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 34, mlango wa 7.

2. Al-Firdawsu 4: 496, Hadithi ya 6940. Al-Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 858, Hadithi ya 1439. Al-Bayan: 118, mlango wa 8. Dhakhairul-Uqba: 136. Uqadu Ad-Durar: 60, mlango wa 3, humo mna “Kama nyota ing’aayo.”. Mizanul-Iitidal 3: 449. Lisanul-Mizan 5: 24. Al-Fussul Al-Muhimmah: 284. Al-Jamiu As-Swaghir 2: 672, Hadithi ya 9245. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura ya 1. Kanzul- ummal 14: 264, Hadithi ya 38666. Mirqatul-Mafatihi 9: 350. Lawaihus-Safawiniy 2: 4. Is’afur-Raghibina: 146. Nurul-Absar: 187. Faydhul-Qadir 6: 279, Hadithi ya 9245.

3. Mustadrak Al-Hakim 4: 558. Uqad Ad-Durar: 60, mlango wa 3, japo mna tofauti kidogo. Faraidu As-Samtwayni 2: 330, Hadithi ya 580. Burhanul-Muttaqiy: 98, mlango wa 2, Hadithi ya 28 na 99, mlango wa 3, Hadithi ya 3. Yanabiul- Mawaddah: 488, mlango wa 94.

4. Futunu Ibnu Hammad: 258, Hadithi ya 1008. Urufu As-Suyuti Al-Hawiy 2:232. Burhanul-Muttaqiy: 99, mlango wa 3, Hadithi ya 2. Kanzul-ummal 14: 586, Hadithi ya 39660.

5. Burhanul-Muttaqiy: 100, mlango wa 3, Hadithi ya 5. Uqadu Ad-Durar: 64, mlango wa 3. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Faraidu Fawaidul-Fikri: 4, mlango 2.

6. Ibnu Hammad: 258. Uqad Ad-Durar: 65, mlango wa 3. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 98, mlango wa 3, Hadithi ya 29. Burhanul- Muttaqiy 101, mlango wa 3, Hadithi ya 10.

7. Ibnu Hammad: 102. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Burhanul-Muttaqiy 98, mlango wa 2, Hadithi ya 26 na 27. Kanzul-ummal 14: 585, Hadithi ya 39658, japo kuna tofauti kidogo. Faraidu Fawaidul-Fikri: 2, mlango 1.

8. Al-Bayanu: 139, mlango wa 19. Uqadu Ad-Durar: 37, mlango wa 1. Faraidu As-Samtwayni 2: 331, Hadithi ya 582, japo mna tofauti kidogo. Urufus-Suyuti Al- Hawi 2: 220. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura ya 1. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 43, mlango wa 1, Hadithi ya 33. Burhanul-Muttaqiy: 84, mlango wa 1, Hadithi ya 32. Is’afur-Raghibina: 146. Yanabiul-Mawaddah: 433, na 436, mlango wa73, sura ya 2. Faraidu Fawaidul-Fikri: 4, mlango 2.

9. Sunan Ibnu Dawdi 6: 162, Hadithi ya 4121. Uqadu Ad-Durar: 45, mlango wa 1. Futunu Ibnu Kathir 1: 38. Muqaddimatu Ibnu Khaliduni: 391, sura ya 53. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 214. Ad-Durrul-Manthur 6: 39, mwishoni mwa Aya ya 8. Jam’ul-Jawamiu 2:35. Kanzul-ummal 13: 647, Hadithi ya 37636. Mirqatul- Mafatihu 9: 363, Hadithi ya 5462. Yanabiul-Mawaddah: 432, mlango wa72. At- Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 343, Hadithi ya 10.

10. Al-Bayan: 137–138, mlango wa 18, kutoka kwenye Al-Muujam Al-Kabir na Manaqib Al-Mahdawi cha Abu Nua’im.

11. Al-Bayan: 140, kutoka kwenye Al-Muujam Al-Kabir cha At-Tabaraniy na Manaqib Al-Mahdawi cha Abu Nua’im.
Baada ya kuwa tumejua jina la Imam Mahdi na sifa zake, basi ndani ya kifungu hiki tutazungumzia hadhi ya kiroho aliyonayo Imam Mahdi na nafasi yake mbele ya Mola ambayo humsukuma kutekeleza jukumu lake, na kuwa yeye ni khalifa wa Mwenyezi Mungu tuliyeahidiwa, ambaye ni wajibu kumtii kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Tutazungumzia hilo ndani ya riwaya mbalimbali.

1- Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Sisi kizazi cha Abdul-Muttalib ni mabwana wa watu wa Peponi, mimi Hamza, Ali, Ja’far, Hasan, Husein na Mahdi.”1

2- Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mahdi ni tausi wa watu wa Peponi.”2

3- Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Umma huu utakuwa na khalifa, Abubakri na Umar si bora kuliko yeye.”3

4- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mahdi atatokeza huku juu ya kichwa chake kukiwa na wingu. Na kuna mnadi atakayenadi: Huyu ndiye Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu mfuateni.”4

5- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Amru kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Atatokeza Mahdi huku juu ya kichwa chake kukiwa na Malaika akinadi: Hakika huyu ndiye Mahdi mfuateni.”5
________________________
1. Sunan Ibnu Majah 2: 1368, mlango wa 34, Hadithi ya 4087. Mustadrak Al- Hakim 3: 211. Tarikh Baghdad 9: 434, Hadithi ya 5050. Matwalibus-Suul 2: 81, mlango wa 12. Al-Bayan: 101, mlango 3. Dhakhairul-Uqba: 15 na 89. Ar-Riyadh An-Nadhirah 3: 4 na 182, sura ya 8. Uqad Ad-Durar: 194, mlango wa 7. Faraidu As-Samtwayn 2: 32, mlango 7, Hadithi ya 380. Muqaddimati Ibnu Khalduni: 398, mlango wa 53. Al-Fusulu Al-Muhimmah: 284, chapa ya Darul-Adh’wai, sura ya 12. Jam’ul-Jawamiu 1: 851. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 160, mlango wa 11, sura ya 1 na ukurasa wa 187, mlango wa 11, sura ya 2, Hadithi ya 19. Burhanul- Muttaqiy: 89, mlango wa 2, Hadithi ya 3. Is’afur-Raghibina: 124. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 214.

2. Al-Firdawsu 4: 222, Hadithi ya 6668. Al-Bayanu: 118, mlango wa 8. Uqad Ad- Durar: 199, mlango wa 7. Al-Fusul Al-Muhimmah: 284, sura ya 12. Burhanul- Muttaqiy: 171, mlango wa 12, Hadithi 2. Kunuzud-Daqaiq: 152. Nurul-Absar: 187. Yanabiul-Mawaddah: 181, mlango wa 56.

3. Ibnu Abi Shaybah 15: 198, Hadithi ya 19496. Al-Kamil cha Ibnu Adiy 6: 2433. Uqad Ad-Durar: 199, malngo wa 7. Burhanul-Muttaqiy: 172, mlango wa 12, Hadithi ya 6.

4. Al-Bayan: 132, mlango wa 15. Uqad Ad-Durar: 183, mlango wa 6. Faraidu As- Samtwayni 2: 316, mlango 61, Hadithi ya 566 – 569. Al-Fusul Al-Muhimmah: 298, sura ya 12. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Tarikhul-Khamis 2: 288. Nurul-Absar:

5. Takhlisul-Mutashabihi 1: 417. Al-Bayan: 133, mlango wa 16. Faraidu As- Samtwayni 2: 316, mlango 61, Hadithi ya 569. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Al- Qawlu Al-Mukhtasar: 39, mlango wa 1, Hadithi ya 24. Burhanul-Muttaqiy: 72, mlango wa 1, Hadithi ya 2. Yanabiul-Mawaddah: 447, mlango wa 78.
Ikiwa Imam Mahdi tuliyeahidiwa ndiye Muhammad bin Hasan Al-Askari (a.s.), na nafasi yake kwa Mwenyezi Mungu ni khalifa wa haki ambaye ni lazima kumtii. Basi tunajiuliza: Je, kuna Imam mwingine atakuja baada yake? Au yeye ndiye khalifa wa mwisho kutoka Ahlul-Bayt (a.s.) na hitimisho lao, kama wanavyoamini Shia Imamiyya na kumngojea?

Riwaya zifuatazo ambazo ni kutoka kwenye vitabu vya Sunni zinazungumza kuwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye Imam wa mwisho na hitimisho la makhalifa (a.s.).

1- Kutoka kwa Thawbani amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Watatu watagombana kwenye hazina yenu wote wakigombania ukhalifa, kisha hakuna hata mmoja miongoni mwao atakayeupata, kisha zitatokeza bendera nyeusi upande wa Mashariki na kuwauwa mauaji yasiyowahi kufanywa na kaumu yoyote.” – kisha akase- ma jambo ambalo silikumbuki – Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Mkimuona basi mpeni kiapo cha utii angalau kwa kutambaa juu ya thelu- ji, kwani hakika yeye ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu.”1

2- Imepokewa kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Nilimwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mahdi ni kutoka kwetu sisi maimamu wa uongofu au ni kutoka kwa asiye sisi? Akasema: “Bali ni kutoka kwetu, dini inahitimishwa kupitia kwetu kama ilivyofun- guliwa kupitia kwetu, na kupitia kwetu wataokolewa dhidi ya upotovu wa fitina kama walivyookolewa dhidi ya upotovu wa shirki. Kupitia kwetu Mwenyezi Mungu ataunganisha kati ya nyoyo zao ndani ya dini baada ya uadui wa fitina kama alivyounganisha nyoyo zao na dini Yake baada ya uadui wa shirki.”2

3- Ibnu Hajar Al-Haythamiy aliyefariki mwaka 974 A.H. Amesema: “Abu Hasan Al-Abiriy amesema: Zimekuwa nyingi mno habari na zikazidi kwa uwingi wa wapokezi wake kutoka kwa Al-Mustafa (s.a.w.w.) kuhusu kutokeza kwake – Mahdi – na kuwa yeye ni kutoka ndani ya Ahlul-Bayt wake, na kuwa ataijaza ardhi uadilifu, na kuwa yeye atatoka pamoja na Isa (a.s.) na hivyo atamsaidia katika kumuuwa Dajjal huko kwenye mlango wa Ludi kwenye ardhi ya Palestina, na kuwa yeye atasalisha umma huu akiwa Imam na Isa ataswali nyuma yake.”3

4- Sheikh As-Swabbani aliyefariki mwaka 1206 A.H. Amesema: “Zimekuwa nyingi mno habari kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu kutokeza kwake – Mahdi – na kuwa yeye ni kutoka ndani ya Ahlul- Bayt wake, na kuwa ataijaza ardhi uadilifu, na kuwa yeye atamsaidia Isa (a.s.) katika kumuuwa Dajjal huko kwenye mlango wa Ludi kwenye ardhi ya Palestina, na kuwa yeye atasalisha umma huu akiwa Imam na Isa atasali nyuma yake.”4

5- Hadithi ya Abu Saidi Al-Khudri: “Ardhi itajaa ukatili na dhuluma, ndipo atatokeza mtu kutoka ndani ya kizazi changu…”5
________________________
1. Al-Bayan: 104, mlango wa 3. Sunan Ibnu Majah: 2 / 1367, Hadithi ya 4084. Al- Mustadrak: 4 / 463. Talkhisul-Mustadrak: 4 / 463 na 464. Musnad Ahmad bin Hanbal: 5 / 277, japo kuna tofauti kidogo.

2. Al-Muujamu Al-Awsatu 1: 136, Hadithi ya 157. Al-Bayan: 125, mlango wa 11. Uqadu Ad-Durar: 192, mlango wa 7. Majmauz-Zawaidi 7: 316 – 317. Muqaddimati Ibnu Khalduni: 396 na 397, mlango wa 53. Al-Fusul Al-Muhimmah: 288, japo kuna tofauti kidogo, sura ya 12. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Jam’ul- Jawamiu 2: 67. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 163, mlango wa 11, sura 1. Kanzul- ummal 14: 598, Hadithi ya 39682. Burhanul-Muttaqiy: 91, mlango wa 2, Hadithi ya 7 na 8. Faraidu Fawaidul-Fikri: 3, mlango 1. Nurul-Absar: 188.

3. As-Sawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 165, chapa ya Misri.

4. Is’afur-Raghibina cha As-Swaban: 140.

5. Mustadrak Al-Hakim 4: 558.
Ikiwa dalili za nukuu zilizomo ndani ya Sahih Sita na vitabu vingine zina- sisitiza ukweli wa Imam Mahdi, kuanzia utu wake, jina lake, nasaba yake hadi sifa zake nyingine, hivi je, muislamu wa zama atakazodhihiri ame- ongezewa alama nyingine zitakazoimarisha imani yake kwake na utiifu kwa huyu mtu aliye Imam mwenyewe, na kumwepusha na mafuriko nyuma ya madai na mkondo wa upotovu?

Hakika riwaya zifuatazo zinasisitiza ukweli huu wa kihistoria nao ni kuwa, Nabii Isa (a.s.) atateremka kutoka mbinguni na kusali nyuma ya Imam Mahdi mwana wa Hasan Al-Askari (a.s.).

1- Ile aliyoitoa Ibnu Shaybah ndani ya kitabu Al-Muswannaf, kutoka kwa Ibnu Sirini amesema: “Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu, na yeye ndiye atakayemsalisha Isa bin Maryam.”1

2- Ile aliyoitoa Abu Nua’im kutoka kwa Abdullah bin Amru amesema: “Mahdi atateremkiwa na Isa bin Maryam, na Isa atasali nyuma yake.”2

3- Ile aliyoisema Al-Munawi katika kufafanua Hadithi: “Ni kutoka kwetu yule ambaye Isa bin Maryam atasali nyuma yake.” Akasema: “Kutoka kwetu” yaani sisi Ahlul-Bayt. “Ambaye” yaani mtu ambaye. “Isa bin Maryam atasali” yaani Ruhullah pindi atakapoteremka kutoka mbinguni zama za mwisho pindi Dajjal atakapodhihiri. “Nyuma yake” yaani atateremka wakati wa swala ya Asubuhi juu ya mnara mweupe Mashariki mwa Damascus, na kumkuta Imam Mahdi akitaka kusali, hivyo atamuhisi na hapo atarudi nyuma ili (Isa) atangulie, lakini Isa atamtanguliza na kusali nyuma yake. Na hapo umma huu utapata fadhila na sharafu kubwa kupitia kwake.”3

4- Aliyoisema Ibnu Burhani As-Shafiy kuhusu kuteremka kwa Isa (a.s.): “Kuteremka kwake kutakuwa wakati wa swala ya Alfajiri, atasali nyuma ya Mahdi baada ya Mahdi kumwambia: “Tangulia ewe Ruhullah” naye ata- jibu: Tangulia imekimiwa kwa ajili yako.”

Akaendelea mpaka akasema: “Hakika Mahdi atatokeza pamoja na Isa na hivyo kumsaidia kumuua Dajjal. Na imepokewa kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kupitia kizazi cha Fatima.”4

5- Ile iliyokuja ndani ya kitabu Fat’hul-Bari: “Abu Hasani Al-Khasaiy Al-Abadiy5 ndani ya kitabu Manaqib Ash-Shafiiy amesema: Zimekuwa nyin- gi mno habari kuwa Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu na kuwa Isa ataswali nyuma yake. Amelitaja hilo ikiwa ni kujibu Hadithi ambayo ime- tolewa na Ibnu Majah kutoka kwa Anas isemayo: “Hakuna Mahdi ila ndiye Isa mwenyewe.” Kisha akajibu kauli ya At-Twibiy isemayo kuwa maana yake ni: “Isa atawasalisha akiwa ndani ya dini yenu.” Akajibu kwa kuse- ma: “Inabatilishwa na kauli yake iliyomo kwenye Hadithi nyingine ya Muslim: “Ataambiwa tusalishe. Atasema hapana, hakika wao kwa wao ni viongozi kwa ajili ya kuupa heshima umma huu.”

Kisha akanukuu kutoka kwa Ibnu Al-Jawziy kauli yake: “Laiti Isa ange- tangulia kama Imam basi nafsi ingeingiwa na utata, na ingesemwa: Unaona ametangulia kama naibu au nabii mpya kisheria? Hivyo ataswali kama maamuma ili asichafuliwe na vumbi za utata kutokana na kauli ya (s.a.w.w.): “Hakuna nabii yeyote baada yangu.”

Kisha akasema: “Isa kusali nyuma ya mtu wa kutoka ndani ya umma huu ilihali ikiwa ni zama za mwisho, na ile kukaribia Kiyama ni dalili zithibitishazo usahihi wa kauli zisemazo: Hakika ardhi haikosi khalifa wa Mwenyezi Mungu aliye hoja.” Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.6

6- Aliyoitoa Ibnu Abu Shaybah kutoka kwa Ibnu Sirin: “Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu na yeye ndiye atakayemswalisha Isa mwana wa Maryam.”7
________________________
1. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 15: 198: 19495

2. Al-Hawi Lil-Fatawa cha As-Suyutiy 2: 78.

3. Faydhul-Qadir cha Al-Munawi 6: 17

4. As-Siratu Al-Halbiyah cha Ibnu Burhani As-Shafiy 1: 226 – 227.

5. Hivyo ndivyo ilivyo, na sahihi ni Al-Abariy. Baadhi wamemwita kwa kuniya ya Abu Husein, na sahihi ni Abu Hasani. Alifariki mwaka 363 A.H. Kama ilivyo ndani ya wasifu wake.

6. Fat’hul-Bari Bisharhi Sahih Bukhar cha Ibnu Hajar Al-Asqalaniy 6: 383 – 385.

7. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 15: 198, 19495.
Na miongoni mwa alama alizoongezewa mwislamu wa zama za kudhihiri kwake (a.s.) ili ajikinge na asiweze kuingia ndani ya mikondo ya upotovu ni wasifu wa bendera ya Imam Mahdi na wito wake unaosubiriwa. Kwani bendera yake (a.s.) ina alama itakayowaongoza wenye kungojea kudhihiri kwake, basi hebu tuzitazame riwaya hizi mbili zifuatazo:

1- Kutoka kwa Abdullah bin Sharik, amesema: “Mahdi atakuwa na ben- dera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) iliyohukumiwa kushinda. Natamani ningekutana naye ilhali nikiwa ni mwenye nguvu mno.”1

2- Kutoka kwa Abu Is’haqa kutoka kwa Nufu Al-Bukaiy: “Bendera ya Mahdi imeandikwa: Kiapo cha utii ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”2
________________________
1. Ibnu Hammad: 249, Hadithi ya 972. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 100, mlango wa 3, Hadithi ya 35. Burhanul-Muttaqiy: 152, mlango wa 7, Hadithi ya 24.

2. Ibnu Hammad: 249, Hadithi ya 973. Uqad Ad-Durar: 274, mlango wa 9. Al- Qawlu Al-Mukhtasar: 101, mlango wa 3, Hadithi ya 36. Burhanul-Muttaqiy: 152, mlango wa 7, Hadithi ya 25. Faraidu Fawaidul-Fikri: 8, mlango wa 4. Yanabiul- Mawaddah: 435, mlango wa 73.
Miongoni mwa mambo yasiyo na shaka kabisa ni kuwa uadilifu kwa maana yake yote utatimia chini ya utawala wa Mahdi (a.s.), ardhi na mbin- gu zitamwaga kheri zake na dola yake itakuwa ni dola ya mfano bora tuliyoahidiwa na Mola, dola ambayo ndani yake mwanadamu atakuwa mwema kwani hakutokuwa na dhuluma, unyang’anyi, ufakiri wala ufisadi. Hakika maelezo ya riwaya zifuatazo yanaashiria ukweli huu halisi:

1- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Umma wangu utaneemeka zama za Mahdi kwa neema ambayo katu hawajawahi kuneemeka kwa mfano wake, watatumi- wa mvua nyingi na ardhi haitoacha mmea wowote ila itauotesha, na mali yenye kulundikana, itakuwa mtu anasimama na kusema: Ewe Mahdi nipe, naye anamjibu chukua.”1

2- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ndani ya umma wangu atakuwemo Mahdi, ikipungua ni miaka saba na kama si hivyo ni miaka tisa, ndani ya muda huo umma wangu utaneemeshwa kwa neema ambazo katu haujaneemeshwa kwa mfano wake. Ardhi itapatwa na mazao yake na wala hawatowekeza chochote. Kipindi hicho mali itakuwa imelundikana na hivyo mtu anasi- mama na kusema: Ewe Mahdi nipe, naye anamwambia chukua.”2

3- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika ndani ya umma wangu yumo Mahdi, atatokeza na kuishi mitano au saba au tisa.” Amesema: Tukasema ni nini hiyo? Akasema: “Miaka.” Akasema: “Atakuwa anajiwa na mtu na kusema: Nipe, nipe.” Akasema: “Ndipo anapomjazia nguo yake kwa kadiri atakavy- oweza kubeba.”3

4- Kutoka kwa Jabir bin Abdullah Al-Ansariy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Zama za mwisho atakuwepo khal- ifa anawajazia mali nyingi bila kuzihesabu mara kwa mara.”4

5- Muslim ametoa ndani ya Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Abdullah Al- Ansariy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alise- ma: “Zama za mwisho atakuwepo khalifa anayegawa mali bila kuzihesabu.”5
________________________
1. Ibnu Hammad: 253, Hadithi ya 992. Al-Bayan: 145, mlango wa 23. Uqad Ad- Durar: 225, mlango wa 8. Al-Fusul Al-Muhimmah: 288 na 289, sura ya 12. Nurul- Absar: 189, mlango wa 2.

2. Sunan Ibnu Majah 2: 1366 – 1367, Hadithi ya 4083. Mustadrak Al-Hakim 4:558. Burhanul-Muttaqiy: 81, mlango wa 1, Hadithi ya 25 na 82 mlango wa 1, Hadithi ya 26.

3. Sunan At-Tirmidhi 4: 439, mlango wa 53, Hadithi ya 2232. Al-Bayan: 107, mlango wa 6. Al-Ilal Al-Mutanahiyah 2: 858, Hadithi ya 1440. Mishkatul- Maswabihi 3: 24, sura ya 2, Hadithi ya 5455. Muqaddimatu Ibnu Khalduni: 393, sura 53. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 215. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura 1. Kanzul-ummal 14: 262, Hadithi ya 38654. Mirqatul-Mafatihu 9:352. Mashariqul-An’war: 114, sura ya 2. Tuhfatul-Ahwadhiy 6: 404, Hadithi ya 2333. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 342 – 343.

4. Maswabihus-Sunnah 3: 488, Hadithi ya 4199. Pia kuna Hadithi nyingine muhimu ndani ya kitabu Muswannaf cha Abdur-Ridhaq 11: 371, Hadithi ya 20770, mlango wa Mahdi, ameitoa mwandishi wa kitabu Difau Anil-Kafiy 1: 266.

5. Sahih Muslim ufafanuzi wa An-Nawawiy 18: 39.
Ikiwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye mmoja kati ya maimamu watakasifu, kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyya ni lazima Imam huyu atakuwa na vipaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama vile elimu pana na uwezo wake wa kufanya miujiza ambayo ataitoa kwa watu ili kuhimiza uimamu wake na ukhalifa wake wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kama vitendo vya nguvu ya ghaibu vilivyokuwa vikitoka kwa baba zake, kwani baba zake kumi na moja watakasifu walikuwa na miujiza na karama mbalimbali iliyosisitiza hadhi yao mbele ya Mola. Maelezo ya riwaya zifuatazo yanaashiria ukweli huu halisi:

1- Kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Twalib (a.s.) amesema: “Mahdi atakuwa anamwashiria ndege na kuanguka mikononi mwake, na atakuwa anapanda mti sehemu ndogo ya ardhi basi unastawi na kutoa majani.”1

2- Kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Twalib (a.s.) amesema: “Bendera tatu zitatofautiana: B

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ