Rafed English

Hukumu za Kusisimua Zilizotolewa na Imam Ali [a]

Hukumu za Kusisimua Zilizotolewa na Imam Ali [a] by : al-islam.org

 

Al-Kulaini na Sheikh Muhiyud-Din ibn 'Arabi wameelezea kwa mamlaka ya Aasim bin Hamza Al-Saluli,ambaye anasema kuwa yeye alimwona kijana mmoja akilia katika mtaa mmoja mjini Madina:"Ewe Allah swt! Amua kesi baina yangu na mama yangu." Umar al-Khattab,ambaye alikuwa akipita hapo,alimkanya kijana huyo:"Usilitaje jina la mama yako!"

Kijana huyo alisema:"Ewe Amiral-muminiin! Mama yangu alinizaa na kuninyonyesha maziwa kwa miaka miwili, lakini sasa nilipokua,ananikataa kata kata kuwa mimi si mtoto wake.Yeye pia anakana kuolewa na baba yangu,ambaye alishafariki,na anataka kujichukulia milki yote huku akidai kuwa alikuwa ni ndugu yake tu,na hivyo kuninyima sehemu yangu ya urithi."

Kwa kuyasikia hayo, Umar alimwita yule mwanamke ambaye alikuja na mashahidi arobaini wa upande wake. Hao wote walitoa ushahidi kumpendelea yeye. Kwa hayo, Umar alitoa hukumu ya kijana yule kufungwa kwa kosa la 'iftara (kusingizia)

Wakati yule kijana alipokuwa akichukuliwa kifungoni, alikutana njiani na Imam ‘Ali a.s. Kijana yule alimlilia Imam ‘Ali a.s. kumsaidia na akamwelezea kisa chote. Hapo Imam ‘Ali a.s. aliwaamrisha wasindikizaji wake kumpeleka tena kwa Umar. Walipofika Umar aliwauliza sababu ya kumrudisha, nao walijibu kuwa Imam ‘Ali a.s. ndiye aliyewaambia hivyo kuwa wamrudishe. Na wakati huo Imam ‘Ali a.s. alifika hapo na kumwambia Umar kutaka kwake kutoa uamuzi. Kwa hiyo, Umar alisema: "Vyovyote iwe vile, je ni kipi kitakachokuwa afadhali kuliko haya? Mimi nimemsikia Mtume s.a.w.w. akisema kuwa ilimu yako ni bora kuliko sisi sote."

Imam ‘Ali a.s. alimwita yule mwanamke pamoja na mashahidi wake wote. Wao wote mmoja baada ya mwingine walisema vile vile walivyokuwa wamesema mbele ya Umar. Baada ya kuyasikiliza hayo, Imam ‘Ali a.s. aliwaambia jamaa zake mwanamke iwapo wataridhika kuolewa kwa mwanamke huyo, nao wote walikubali.

Hapo ndipo Imam ‘Ali a.s. alipomwambia mtumwa wake Qambar alete Dirham 400, na alimwambia yule mwanamke: "Mimi nakuoza wewe kwa huyu kijana kwa mahari ya Dirham 400." Wakati Dirham zilipoletwa alimkabidhi kijana huyo na alimwambia aende na mwanamke huyo na ampatie mahari yake.

Wakati yule kijana alipotaka kuondoka, Imam ‘Ali a.s. alisema: "Njoo kwangu tena, kwa sharti la kupitisha usiku mmoja kama bibi na bwana!"

Kwa kuyasikia hayo, yule mwanamke akapiga kelele: "Loh! Ewe nduguye Mtume s.a.w.w. wewe unanioza mtoto wangu?"

Mwanamke akaomba msamaha na kwa kushika mkono wa mtoto wake, wote waliondoka kwa furaha.

Baada ya hao wote kuondoka Bwana Umar alisema: "Lau asingalikuwapo Ali, Umar angalikuwa ameangamia.

Tukio hilo pia limeelezwa na Sahab Fazail ibn Shaazan kutokea Waqadi, kutokea Jabir na kutokea Salman kwa wakati, pamoja na tofauti kidogo.
Imeelezwa na Kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. kuwa katika kipindi cha Ukhalifa wa Imam ‘Ali a.s. watu wawili, mtumwa na bwana, walikuwa wakielekea kufa baada ya Hijja.

Mtumwa alifanya kosa na bwana wake alimpiga kwa kosa hilo. Hapo kwa maajabu, yule mtumwa alimwambia bwana wake. "Loh! Wewe u mtumwa wangu na wanipigia bure tu!" Ama kwa kusikia hayo, watu waliokuwa katika msafara huo walistaajabishwa na hawakuweza kuamua baina yao, na huyo mtumwa alirudia kila mara, hadi wakaingia mjini kufa.

Bwana alimwambia mtumwa: "Twende kwa Amir ul Muminiin ili tuamuliwe, "Kwa hayo Mtumwa alikubali na hivyo walitokea mbele ya Imam ‘Ali a.s., na wakati walipokuwa wakitoa maelezo na hoja zao, wote walidai kuwa bwana. Yule mtu aliyekuwa bwana wa kweli alielezea akililia: "Baba yangu alinipeleka Hijja na wakati tulipokuwa tukirudi mtumwa huyu alifanya makosa ambayo nilimpiga. Hivyo hizi ndizo, mbinu zake za kutaka kunidhulumu mali yangu yote."

Na mtumwa pia alielezea vivyo hivyo huku akila kila aina ya viapo. Baada ya kuwasikiliza wote wawili, aliwaambia: "Nendeni na mrudi kwangu hapo kesho."

Imam ‘Ali a.s. aliamrisha kutobolewa matundu mawili katika ukuta kiasi cha kupitisha kichwa cha mtu mmoja hadi mabega. Siku ya pili, wote wawili walifika mbele ya Imam ‘Ali a.s., na waliamrishwa kuweka vichwa vyao katika yale matundu, kila mmoja. Baada ya hapo, Imam ‘Ali a.s. alimwamwa ni wake, hadi kuchukuliwa kwa Umar ambaye pia aliona ugumu kufikia hukumu. Hivyo nae pia aliielekeza kesi hiyo kwa Imam ‘Ali a.s.s. ili ipatiwe ufumbuzi ipasavyo.

Imam ‘Ali a.s. aliwaita wanawake wote wawili na kujaribu kuwatishia. Lakini wote wawili hawakuogopa wala kushtushwa kwa hayo na walibakia katika mabishano yao- ukaidi wao!.

Imam ‘Ali a.s. alitamka "Nileteeni msumeno mkali!"

"Je wataka kuufanyia nini?" Wote wawili waliuliza.

"Nitamkata mtoto katika sehemu mbili zilizo sawa, na nitawapatieni kipande kimoja kimoja kila mtu."

Mmoja wao alibakia kimya wakati mwingine alisema: "E Mungu wangu! Abul Hasan, iwapo hapana ufumbuzi mwingine, basi mwachie huyo mwenzangu amchukue huyo mtoto, ninamwachia." huku machozi yakimtiririka.

Imam ‘Ali a.s. alisema: "Allah akbar! Huyu ndiye mtoto wako na wala si wa mwenzako. Iwapo angalikuwa mtoto wake, basi naye pia angalihangaika na kutapatapa."

Kwa hayo huyo mwanamke mwenye madai ya uongo alikiri kuwa yu mwongo.

Hivyo Bwana Umar alisaidiwa na alimshukuru Amir al Muminiin a.s. kwa kumwokoa katika maamuzi yake.
Imeripotiwa na kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Zazaan kuwa wanaume wawili waliweka amana yao kwa mwanamke mmoja kwa masharti kuwa asiwarudishie amana hiyo hadi wao wote wawili waje kwa pamoja.

Baada ya muda kupita, mmoja wao alimwendea yule mwanamke na kumwambia: "Nipe ile amana yetu tuliyokuachia kwani mwenzangu amefariki. "Yule mwanamke alimpa amana hiyo kwa kuyaamini ayasemayo. Baada ya muda kupita, akaja yule mtu wa pili akielezea vile alivyokuwa ameelezea mtu wa kwanza.

Mtu huyo alipoelezwa yaliyotokea, alimshtaki mwanamke kwa Bwana Umar, ambaye alishindwa kutoa hukumu, hiyo alielekeza mbele ya Imam ‘Ali a.s. kwa kupatiwa hukumu.

Imam ‘Ali a.s. aliwaita wote na akamwambia yule mwanamme: "Hiyo amana ipo kwangu, na mimi sitaweza kuitoa kwa yeyote yule hadi muje wote wawili kwa pamoja,kwa mujibu wa masharti yenu wenyewe!"

Kwa hivyo,aliendelea Imam a.s.: "Nenda ukamlete mwenzako ili niwarudishie amana yenu."

Mtu huyo aliaibika na akaondoka zake.(Inaonekana kuwa hao walikula njama ya kutaka kumtapeli mwanamke huyo)
Imeelezwa na kulaini na Sheikh Sadduq vile vile katika sahihi Bukhari, kwa mamlaka ya Imam Jaafar as-Sadiq a.s. kuwa kijakazi aliletwa mbele ya Bwana Umar kwa mashtaka ya kwenda kinyume na bwana wake.

Kisa chenyewe kilikuwa hivi:-

Mtu mmoja alimtunza binti mmoja yatima. Kwa kuwa alikuwa akienda safari za kikazi kila mara, hivyo alimkabidhi mke wake ili amlee.

Hali hii iliendelea kwa miaka kadhaa na binti yule alikua na kupendeza. Yule mwanamke, akitafuta mbinu za kumzuia mume wake asimwoe kijakazi huyo, alimlewesha, kwa mbinu zake na kwa msaada wa wanawake wenzake na vile vile alithubutu hata kuuharibu ubikira wake.

Bwana yule aliporudi kutoka safari, alimkuta yule kijakazi hayupo na hivyo alimwuliza mke wake kuhusu huyo.

Mwanamke huyo alijibu: "Huyu ametoroka pamoja na kijana wa majirani."

Bwana huyo kwa hasira, alitoka kumtafuta huyo kijakazi, na alipompata, alimburuta hadi mbele ya Umar, allipokuwa Khalifa.

Bwana Umar alipoisikiliza kesi hiyo, aliiona ngumu kuihukumu na hivyo aliielekeza kwa Imam ‘Ali a.s. kwani alikwisha shughulikia kesi kama hizo.

Imam ‘Ali a.s. aliwaagiza Bwana, Bibi, kijakazi na mashahidi wote kuhudhuria mbele yake katika kesi hiyo. Bwana na Bibi walisimulia kisa vile vile walivyofanya mbele ya bwana Umar, na waliwaleta wanawake wanne kwa upande wao wa ushahidi kama vile alivyotaja yule mke wake, dhidi ya mshitakiwa.

Imam ‘Ali a.s. allimwita mwanamke wa kwanza wa upande wa mashtaka na aliuweka upanga baina yake na ya yule, na akasema: "Je wajua, kuwa mimi ni Ali ibn Abi Talib? Na hivyo nakutaka uniambie ukweli na ukweli mtupu na kwamba si chochote kile ila ukweli mtupu."

Kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa mjanja, hivyo alielezea uongo vile vile kama alivyokuwa ameelezea mbele ya Umar, na alisisitizia pia.

Imam ‘Ali a.s. alipoyaona hayo, alisema kuwa huyo atengwe na mashahidi wengine. Baada ya hapo, Ali a.s. alimwita shahidi mwingine, kumwambia: "Je unauona upanga huu? Iwapo hautaniambia ukweli basi nitakukata kichwa chako kwa upanga huu huu . Vile vile kumbuka kuwa huyo mwanamke aliyekutangulia katika kutoa ushahidi, amenielezea yote kwa ukweli na wazi wazi, kwa sababu hiyo, nimemsamehe. "Kwa kusikia hayo na kwa kuhofia maisha yake, alielezea yote kwa ukweli, bila ubishi au uzushi wowote.

Baada ya kusikiliza hayo yaliyo ya ukweli, Imam ‘Ali a.s. alisema: "Baada ya Mtume Daniel, mimi ni mtu wa kwanza katika kulazimisha mshahidi wa tofauti katika mashahidi wawili."

Alitoa hukumu ya adhabu kwa mke wa yule. Na alimwamrisha yule mtu kumpa talaqa mkewe na kumwoa yule kijakazi. Baada ya kutekelezwa kwa hukumu zake, alilipa mahari kutoka mfukoni mwake. Vile vile aliwatoza adhabu ya Dirham mia moja kila mmoja wa mashahidi katika kesi hiyo, na alimpa yule kijakazi Dirham zote hizo.

Baada ya kumalizika kwa maamuzi yaliyo sahihi, Bwana Umar alimshukuru mno Imam ‘Ali a.s. kwa yote hayo na vile vile alimwomba amsimulie masimulizi ya Mtume Daniel a.s.

Imam ‘Ali a.s. kwa ombi hilo, alianza:

"Mtume Daniel alikuwa ni yatima, ambaye alifiwa na wazazi wake wote wawili. Wakati huo kulikuwa na mtawala kutoka Bani Israili, ambaye alikuwa na Qadhi wawili katika Baraza lake. Qadhi wote wawili, walikuwa wakimtembelea mtawala huyo wakiwa pamoja na mcha Mungu mno mmoja katika siku zao.

Siku moja mtawala ikamtokea kazi ya dharura na muhimu kabisa nje ya dola yake, hivyo aliwaomba wale Qadhi wamtafutie mtu mwaminifu mno katika raia wake.

Qadhi wale walimshauri amtume yule yule mcha Mungu ambaye huwa wanakwenda wote kila leo.

Mtawala alimkabidhi kazi hiyo yule mcha mcha Mungu pamoja na maelekezo yote.

Yule mcha Mungu alikuwa na mke mrembo mno na mwenye kupendeza pia, vile vile alikuwa mcha Mungu kama bwana wake. Sasa yule bwana alipokuwa akienda safari hiyo aliyotumwa, aliwaomba Qadhi wale wawili wamtunze mke wake kwa uwema na vyema na kumsaidia iwapo angalihitaji msaada wao. Ndipo alipoondoka.

Siku moja Qadhi hao walifikia nyumbani mwa huyo mcha Mungu, na waliweza kumwona mke wake na vile alivyo. Kwa kumwona huyo mwanamke, wote wawili walighadhalibiwa na shaitani na hivyo walimwashiki.

Wao walimwelezea mwanamke huyo tamaa yao na mwanamke yule mwema, alikataa kata kata. Kwa hayo wao walimtishia kwa kumstaki kwa Mfalme kwa kuzini hivyo angaliuawa kwa kupigwa na mawe.

Katika majibu yake, aliwaambia: ,"semeni chochote kile mukitakacho, lakini mimi kamwe sitakubali uovu huo."

Baada ya hapo, wale Qadhi walimwambia mfalme kuwa mke wa yule mcha Mungu amezini. Kwa hayo, Mfalme alishangaa mno kwa taarifa hiyo kwani alijua luwa mwanamke yule alikuwa mcha Mungu. Alikiinamisha kichwa chake chini, na alipokiinua, aliwaambia:

"Mimi naamini ushahidi wenu lakini nawaombeni munipatie siku tatu kabla sijatoa amri yoyote katika swala hili."

Hapo Mfalme alishauriana na Waziri wake, akimwambia "Mimi sidhani kuwa yeye amezini, je wasemaje?"

Kwa kuyasikia hayo, Waziri pia alistajaabishwa na alimwambia Mfalme: "Mimi pia nimestaajabishwa kwa hayo!"

Siku ya tatu, Waziri huyo alipita mahala ambapo walikuwa wakicheza watoto wadogo, na Mtume Daniel a.s. alikuwa mmoja wa watoto hao.

Kwa kumwona Waziri huyo akipita, Mtume Daniel a.s. alimwambia mmoja wa watoto wenzake: "Njooni sisi tucheze mchezo wa kuigiza - Mchezo wa Qadhi wawili na mke wa mcha Mungu. Wewe utakuwa mke wa mcha Mungu na nyie mutakuwa Qadhi.

Wakati huo Mfalme alikuwa ameshapiga mbiu ya mgambo, kwa kuwaita watu wote kuja kushuhudia kutolewa hukumu ya mwanamke wa Mcha Mungu kunyongwa kwa kuzini kwa mujibu na desturi zao kwani Qadhi wawili waliripoti hivyo.

Mtume Daniel alimwita kijana mmoja ambaye alikuwa akiigiza kama Qadhi, na kumwuliza:- "Je wewe unasemaje kuhusu swala hili?" Yeye pia aliuelekeza upanga wa ubao ulioviringwa katika nguo, "iwapo utasema uongo basi nitakukata kichwa chako kwa upanga huu."

Kijana huyo, kama Qadhi, alimjibu: "Ewe Mfalme! mke wa mcha Mungu huyo amezini, na mimi ninatoa ushahidi wangu kwa hayo."

Hapo Mtume Daniel a.s. alimwuliza: "Wapi na lini na siku gani na wakati gani?"

Kijana huyo aliyejibu maswali yote aliyokuwa ameulizwa na Mtume Daniel a.s. Baadaye, Mtume Daniel a.s. alimwita kijana wa pili, kama Qadhi wa pili, na alimwuliza maswali hayo hayo, lakini majibu yake yalikuwa ni tofauti kabisa.

Baada ya kuyasikia yote hayo, Mtume Daniel a.s. alisema: "Allah Akbar! Nyie mmetoa ushahidi wa uongo na kumsingizia mwanamke mcha Mungu katika kesi hii."

Baada ya hapo alimwachilia yule mwanamke kwa heshima zote na kuwahukumu kifo wale vijana waliocheza kama Qadhi wawili.

Yule Waziri aliutazama kwa makini mno ule mchezo wa watoto wale na uamuzi ulivyotolewa na Mtume Daniel a.s. katika mchezo huo, na aliripoti vyote kwa Mfalme ambaye pia alifuata vile vile ile kesi na akatoa hukumu yake vivyo hivyo."
Mnigro mmoja alimwijia Bwana Umar. Mke wake alikuwa mweusi. Yeye alimwambia Umar kuwa yeye pamoja na mke wake ni mweusi, lakini amezaa mtoto mwenye rangi ya kunde kinyume na rangi yao. Yeye pia alisema kuwa haina shaka kuwa mke wake amezini na mtu mwingine ambaye ana rangi ya mtoto huyo.

Bwana Umar hakuwa na majibu ya swala hilo hivyo alielekeza kesi hiyo kwa Imam ‘Ali a.s. ili kupatiwa ufumbuzi wake.

Imam ‘Ali a.s. alimwuliza Mnigro huyo: "Je iwapo nitakuuliza swali, utanijibu kwa usahihi?

Mnigro huyo alimjibu: "Ndiyo Bwana! Kwa uwezo wangu wote na kwa usahihi."

Imam ‘Ali a.s alimwuliza huyo Mnigro: "Je ulimwendea mke wako yaani ulimwingilia yeye akiwa katika vipindi vyake vya mwezini?"

Mnigro alijibu: "Ndiyo Bwana, nafikiri nilifanya hivyo."

Kwa majibu hayo, Imam ‘Ali a.s. alimwambia: "Rangi ya mtoto ni matokeo ya tendo lako hilo. Kwa hivyo, wewe ndiwe mwenye hatia na wala si mke wako." Mnigro aliaibika na akajiondokea.
Kesi hii ya kwanza kutolewa hukumu baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. na ni ya aina yake.

Bwana Kulaini ameripoti kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. kuwa: "Katika zama za Abubakar mlevi mmoja aliletwa ili ahukumiwe kisharia.

Hata hivyo, mtu alisema: "Mimi ingawaje ni Mwislamu, lakini naishi miongoni mwa watu ambao hawajui kuwa pombe ni haramu katika Islam na wala mimi sikuwahi kusikia hivyo."

Kwa hayo, Abubakar alishangazwa na hali hiyo na akaona vigumu kutoa hukumu. Wengine waliokuwa pamoja nae walimwambia, mwulizie Imam ‘Ali a.s. kwani ni yeye pekee atakayeweza kujibu swala hili.

Imam ‘Ali a.s. aliwatuma Waislamu wawili waaminifu katika makazi ya Muhajirin na Ansar na kuwaambia "Wawaulize iwapo yeyote miongoni mwao amemsomea (huyu mtu) Aya ya Quran zinazoharamisha pombe au iwapo alishawahi kuwambia Hadith za Mtume s.a.w.w. Iwapo yeyote miongoni mwao atatoa ushahidi basi atatolewa huku na iwapo hatapatikana mtu basi ataambiwa aombe msamaha na kutubu, hivyo ataachiwa huru."

Hao watu wawili walirejea kwa majibu ya kutoambiwa kwa mtu huyo chochote kile kihusianacho na kuharamishwa kwa pombe.

Kwa matokeo hayo, Imam ‘Ali a.s. alimkanya vikali mtu kulewa kwake tena na alitubu huyo mtu. Aliachwa huru.
Imeripotiwa kuwa Siku moja Imam ‘Ali a.s. aliingia msikitini kufa, akamwona kijana mmoja akilia mno huku akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wakimhurumia. Imam ‘Ali a.s. aliwauliza hoja ya kilio hicho.

Kijana huyo alisema: "ya Amir Ul-Muminiin, Shurayh, Qadhi wetu amenihukumu kesi dhidi yangu na kuninyima haki yangu."

Imam ‘Ali a.s. alimwuliza: "Je kesi yako inahusiana na jambo gani?"

"Watu hawa" alisema kwa kuwaelekeza watu waliokuwapo, "walimchukua baba yangu katika safari pamoja nao. Wao wamerejea lakini yeye hakurejea. Mimi niliwauliza kuhusu baba yangu, nao walinijibu kuwa amefariki safarini. Nami niliwauliza kuhusu mali aliyokuwanayo, nao waliniambia: 'Sisi hatujui lolote lile kuhusu mali yake hiyo! Hapo ndipo Qadhi Shurayh alipowaambia wale viapo kwa maelezo yao, nao walikula viapo, hapo ndipo aliponiambia kuwa nisiwabughudhi hao watu au kuwaingilia katika mambo yao.

Imam ‘Ali a.s. alimwambia Qambar: "Waite na wakusanye watu na shurtat al-Khamis1

Aliketi na kuwaita wale watu (waje mbele yake) pamoja na yule kijana. Alimwambia yule kijana aelezee, naye alielezea vile vile kama awali huku akilia, kwa kusema: "Kwa kiapo cha Mwenyezi mungu, mimi ninawashtaki hawa watu kwa kumwua baba yangu. Ewe Amiral-Muminiin. Wao walimdanganya na kumchukua pamoja nao ili wao waweze kunyang'anya mali yake."

Imam ‘Ali aliwageukia hao watu kwa kuwauliza nao walimjibu vile vile kama vile walivyokuwa wamemjibu Qadhi Shurayh: "Huyo bwana alikufa tu na wala hatujui kuhusu mali yake."

Baada ya hapo, aliwatazama usoni mwao na kuwaambia: "Je mnafikiriaje? Je mnadhani kuwa mimi sijui lolote lile mulilomfanyia huyo baba wa kijana huyu? Basi itamaanisha kuwa mimi nitakuwa na ilimu kidogo kabisa."

Alitoa amri ya kutenganishwa, nao walitenanishwa humo msikitini. Kila mmoja alisimamishwa kwenye kizingiti. Alimwamrisha Ubayd Allah b. Abi Rafi, mwandishi wake wakati huo, aketi karibu hapo. Na hapo alimwita mmoja wao, na alimwambia: "Niambie ni siku gani mulipotoka nyumbani kwa ajili ya safari pamoja na babake huyu kijana? Na uyaseme hayo bila ya kuipaza sauti yako."

"Siku fulani na fulani "yeye alijibu.

"Yaandike hayo," alimwambia Ubayd Allah.

"Ulikuwa mwezi gani" aliuliza Imam ‘Ali a.s.

"Ulikuwa mwezi fulani fulani " alijibiwa.

"Yaandike hayo pia," alisema.

"Ulikuwa mwaka gani?" "Ulikuwa mwaka fulani."

"Yaandike,

Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo.

"Kwa magonjwa gani alifariki? aliuliza

"Kwa ugonjwa fulani fulani" alijibiwa.

"Mahala gani alifariki?"

"Mahala fulani fulani"

"Nani aliyemwosha na kumvisha sanda?"

"Fulani fulani,"

"Mulimvisha sanda ya nini?"

"Kwa kitu fulani fulani,"

"Nani aliyesalisha sala ya maiti?"

"Fulani fulani."

"Ni nani, aliyemteremsha kaburini?"

"Fulani fulani.

Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo yaliyokuwa yakiulizwa na kujibiwa. Walipofikia swali la kaburi, Imam ‘Ali a.s. alitoa Takbiri kwa nguvu kiasi kwamba kila mtu aliyekuwapo hapo Msikitini alisikia. Hapo akaamrisha yule mtu arejeshwe mahala pake.

Baada ya huyo, alimwita mtu wa pili akae karibu naye. Imam ‘Ali a.s. alimwuliza maswali hayo hayo aliyomwuliza mtu wa kwanza, majibu yake yote kwa pamoja yalikuwa kinyume kabisa na ya yule wa kwanza. Hayo yote pia yalikuwa yakiandikwa na ubayad Allah. Alipomaliza mtu huyo kutoa majibu yake, Imam ‘Ali a.s. alitoa Takbir kwa sauti kiasi kwamba wote walisikia. Aliamrisha wote wawili wafungwe kifungo lakini wasubiri kwenye mlango wa Msikiti.

Imam ‘Ali a.s. alimwita mtu wa tatu na kumwuliza vile vile alivyowauliza waliotangulia. Naye pia alijibu kinyume na wenzake wawili. Imam ‘Ali a.s. aliamrisha achukuliwe kwa wenzake wawili.

Hapo alimwita mtu wa nne. Maneno yake yalitatanisha na kubabaisha. Imam ‘Ali a.s. alimwonya na kumtishia. Mtu huyo alikiri kwa wenzake walimwua yule bwana na kuchukua mali na kwamba alizikwa mahala fulani fulani karibu na mji wa Kufa. Imam ‘Ali a.s. alitoa Takbir, na kuamrisha achukuliwe mahabusu.

Kwa mara nyingine tena, Imam ‘Ali a.s. alimwita mmoja wa wale waliokwisha kuulizwa, na kumwambia: "Wewe ulidai kuwa mtu huyo alikufa akiwa kitandani. Ambapo nyie mumemwua. Niambie ukweli kabisa kuhusu hali halisi, ama sivyo nitakuadhibu vikali kiasi kwamba utakuwa ni fundisho kwa wengine kwamba niwe nikiambiwa ukweli mtupu." Mtu yule alikiri kumwua yule bwana kama vile alivyokuwa ameelezea mwenzake.

Hapo aliwaita wote waje mbele yake, nao wote walikiri kumwua yule bwana. Imam ‘Ali a.s. aliwaamrisha baadhi ya watu wake waondoke na hao hadi pale walipokuwa wameizika mali ya bwana, hivyo kumpa mtoto wake marehemu.

Imam ‘Ali a.s. alimwuliza yule kijana: "Je umetaka kufanyiwa nini hawa watu kwani umekwishajua kile walichomtendea baba yako."

"Mimi nataka Mungu atuamue siku ya Qiyama na hivyo ninawaachilia humu duniani." alijibu kijana.

Kwa hivyo, Imam ‘Ali a.s. hakuwaadhibu kwa mujibu wa adhabu za kuuwa bali aliwaadhibu vikali kwa madhambi yao.

Qadhi Shuryh alistaajabishwa kwa uamuzi huo wa Imam ‘Ali a.s. na hakuweza kujizuia kwa kumwuliza Imam ‘Ali a.s. "Ewe Amir ul-Muuminiin! Je umewezaje kufikia uamuzi huu?"

Imam ‘Ali a.s. alimjibu: "Mtume Daudi a.s. aliwapita baadhi ya watoto waliokuwa wakicheza na aliitwa mmoja wao, 'Dini imekufa'. Hapo alikuwa akiwajibu. Mtume Daudi a.s. aliwaendea, na kumwuliza mmoja, "Ewe, kijana, je unaitwa nani?"

'Jina langu ni Dini imekufa,' alijibu.

'Je ni nani aliyekupatia jina hilo?" aliuliza Mtume Daud a.s.

Alijibu, "Mama yangu, aliye nyumbani. 'Ndipo Mtume Daud a.s. alipomwambia, twende utupeleke nyumbani kwenu. "Hivyo walikwenda hadi nyumbani kwao na kumwita nje mama yake, 'Ewe mama je, mtoto wako anaitwa nani?' Jina lake ni Dini imekufa.' alijibu huyo mama. Mtume Daudi a.s. aliendelea kumwulizia,'Je ni nani aliyempatia, jina hilo? Huyo mama alijibu, "Baba yake mzazi."

Imam ‘Ali a.s. alimwuliza, "Je ni kwa sababu zipi alimpatia jina hilo?" Huyo mwanamke alijibu: nilipokuwa mja mzito, baba yake alikwenda safari pamoja na baadhi ya watu. Wale watu wote walirejea salama lakini yeye hakurejea. Mimi nilijaribu sana kuwauliza kuhusu bwana wangu lakini wao walijibu kuwa alifariki safarini. Vile vile niliwaulizia kuhusu mali aliyokuwa nayo, lakini wao walisema kuwa hakuwa na chochote na hivyo wao hawakujua chochote kile! Vile vile niliwauliza iwapo alisema chochote katika usia wake. Nao walisema kuwa aliwaambia mtoto atakayezaliwa aitwe Dini imekufa, na hivyo ndivyo nilivyomwita hivyo kwani sikutaka kwenda kinyume na usia wake.'

Hapo Mtume Daudi alipomwuliza yule mwanamke, "Je unawajua watu hao?" Mwanamke alijibu 'Naam!' Wale wote waliochukuliwa nesi hiyo ilipokuja mbele ya Imam ‘Ali a.s. alitoa hukumu ya mtu wa kwanza mwenye amana ya Dinar mbili alipwe Dinar moja na wagawane sawasawa na mtu wa pili ile Dinar ya pili.22
Mwanajeshi mmoja aliporejea nyumbani kwake alikuta mke wake amezaa mtoto wa kiume ambapo yeye anadai kuwa aliishi nao kwa miezi sita tu. Mwanajeshi huyo alimkatalia huyo mtoto,na kupeleka kesi yake mbele ya Umar,ambaye alitoa hukumu ya kupigwa mawe huyo mwanamke (mama mtoto)

Kwa bahati Imam ‘Ali a.s. pia alikuwapo hapo, alisema: "Iwapo utapingana na kitabu cha Allah s.w.t. basi tutaikhatalafiana. Allah s.w.t. amesema katika Quran tukufu: "Nabeba mimba yake hata kumwachisha ziwa (uchache wake) ni miezi thelathini. -(46:5) Vile vile Allah s.w.t. amesema katika Quran Tukufu: "Wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili.......'(2:233) Wakati mwanamke alipotimiza kunyonyesha kwa miezi thelathini.... Kwa sasa (yeye ametimiza tu) wajibu (wa kumnyonyesha) kwa miezi sita (na hivyo hawezikuuawa)"

Umar alimwachilia huru yule mwanamke na alikubaliana na uamuzi huo. Ma-Sahaba walifuata hilo na vile vile al-tabi'un pia wameitumia hadi leo.
Kisa kama kile cha Na. 10 kilitokea katika zama za Bwana Uthman ambapo aliamrisha yule mwanamke auawe kwa kupigwa mawe.

Imam ‘Ali a.s. alipoingilia kati, Uthmani alimpeleka mtu kwenda kuzuia utekelezaji wa adhabu aliyoitoa, mwanamke akawa ameshauwa.
Al-Hassan b. Mahbub ameripoti: Abd al-Rahman b. al-Hajjaaj aliniambia: Nimemsikia Ibn Abi Layla akisema:

Amir ul-Muminiin a.s. ameamua kesi ambayo haikuweza kuamuliwa na mtu mwingine kabla yake.

Watu wawili waliondoka kwenda safari, wakakaa kula chakula kwa pamoja. Mmoja wao alitoa vipande vitano vya mkate na mwenzake vitatu. Alitokezea mtu mmoja akapita aliwasalimia. Nao walimkaribisha ale nao. Naye alipomaliza kula nao, aliwapa Dirham nane akisema: "Hii ni malipo ya chakula nilichokula."

Hao watu wawili walianza kuzozana juu ya Dirham hizo nane. Yule aliyekuwa na vipande vitatu alidai kuwa "Tugawane sote sawa sawa yaani Dirham nne wewe na Dirham nne mimi."

Mwenzake alisema: "Mimi lazima nipate tano na wewe tatu."

Kwa kuwa hawakuweza kuafikiana hivyo, walifikia kwa Imam ‘Ali a.s. kuweza kupatiwa ufumbuzi. Hivyo, walimwelezea mambo yote. Imam a.s. aliwajibu."

Hili ni jambo dogo, halihitaji mzozo wala ngumi kwani suluhisho ndilo jambo bora.

"Mimi nitaridhishwa tu pale utakapotoa uamuzi wako Ewe Amir ul-Muminiin! alisema mwenye vipande vitatu vya mkate.

"Kwa kuwa wewe utaridhishwa na hukumu yangu" alisema Imam ‘Ali a.s. "wewe utapata Dirham moja tu ambapo rafiki yako atapata Dirham saba. " alimalizia Imam a.s.

"Mungu asifiwe, " alinena, "Je itawezekanaje swala hili kuwa hivi?"

"Nilikuambia siyo?" alisema "Si ulikuwa na vipande vitatu tu vya mkate?"

"Naam! alijibu

"Yaani ni ishirini na nne (inapozidishwa) kwa tatu, alisema Imam a.s. "Kwa hiyo wewe ulikula nane, mwenzako nane,na mgeni wenu nane (kwani alitoa saba ya nane ya chakula cha mgeni wenu) na moja kwako wewe (kwani wewe ulitoa moja ya nane ya chakula cha mgeni)" Wote wawili waliondoka kwa furaha.
Imam ‘Ali a.s. alipokuwa Yemen aliweza kutatua kesi nyingi mno, na mojawapo ilikuwa kama ifuatavyo:

Kulichimbwa shimo la kumnasa simba. Ikaja Simba ikatumbukia humo, na watu walizunguka lile shimo kumtazama yule simba. Mtu mmoja alikuwa amesimama ukingoni mwake, na mara ghafla akateleza, alipokuwa anaanguka shimoni, alimshika mtu aliyekuwa karibu nae. Mtu huyo alimshika mtu wa tatu, nae pia alishika wa nne. Lakini kwa bahati mbaya, wote wanne walianguka shimoni na waliuawa na simba.

Sasa je ni nani mwenye hatia? Na nani alipe fidia kati ya hao wanne?

Imam ‘Ali a.s. alitoa uamuzi kuwa mtu wa kwanza (na familia yake) wanawajibika kulipa fidia ya theluthi ya thamani ya damu ya mtu wa pili, na hivyo, mtu wa poli na (familia yake) alipe hiyo kwa mtu wa pili, na hivyo, mtu wa pili na (familia yake) alipe hiyo kwa ajili ya mtu wa tatu na mtu wa tatu alipe hiyo kwa mtu wa nne.
Vile vile Imam ‘Ali a.s. aliletewa kesi wakati akiwa Yemen.

Msichana mmoja alimbeba msichana mwingine mabegani mwake wakati wakiwa wanacheza. Akatokezea msichana mwingine ambaye alimfinya yule msichana aliyekuwa amebebwa alianguka na shingo likavunjika, na akafa.

Hivyo, Imam ‘Ali a.s. alitoa uamuzi kuwa msichana aliyefinya ndiye anayehusika na ulipaji wa theluthi ya thamani ya damu, na msichana aliyegutuka na kuruka anawajibika theluthi yake na sehemu ya tatu haina mtu kwani ajali hiyo ilitokea wakati wao wakiwa katika michezo.
Kesi ifuatayo ililetwa mbele ya Imam ‘Ali a.s. wakati akiwa bado hapo Yemen.

Watu waliangukiwa na ukuta na wote walikufa. Miongoni mwao alikuwa kijakazi na mwanamke huru. Yule mwanamke huru alikuwa na mtoto mchanga aliyezaliwa kwa bwana aliye huru, na yule kijakazi alikuwa na mtoto mchanga aliyezaliwa na mtumwa. Sasa ikatokea kuwa mtoto huru hakuweza kutambuliwa na mtoto wa kijakazi.

Alipiga kura baina yao; yeye alihukumu uhuru kwa yule aliyepata kura za uhuru na mtumwa kwa yule aliyepata kura za utumwa. Hapo alimfanya huru yule mtumwa na kumfanya bwana wa yule aliyekuwa huru. Vile vile alitoa uamuzi juu ya urithi wao kwa mujibu wa bwana na mtumwa wake.

Hukumu zote hizo alizozitoa Imam ‘Ali a.s. akiwa Yemen, zilisifiwa mno na Mtume s.a.w.w. Kwani zilitolewa katika uhai wake.
Watu wawili walifika mbele ya Mtume s.a.w.w. wakiwa wanazozana juu ya ng'ombe kumwua punda.

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!" alisema mmoja wao, "Ng'ombe wake huyu amemwua punda wangu."

Mwendee Abu Bakr, Mwulize kuhusu hayo."

Alisema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

Wao walimwijia Abu Bakr na kumwelezea yote.

"Je kwa nini hamkumwendea Mtume s.a.w.w. kabla ya kuja kwangu?" Aliuliza Abu Bakr.

"Sisi tumeelekezwa na Mtume s.a.w.w. mwenyewe." Wao walimjibu.

"Iwapo mnyama amemwua mnyama mwingine, basi hakuna shitaka dhidi ya mwenye mnyama (kwa ajili ya mnyama aliyeuawa)" alijibu.

Baada ya hapo, walirejea kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na walimwelezea hivyo. Aliwajibu: "Mwendeeni Umar al-Khattab na kumwelezea kisa hicho, mwulizeni hukumu yake kuhusiana na swala hili."

Hao walimwendea na kumwelezea kisa chote. Yeye aliwauliza, "Je kwa nini mumemwacha Mtume s.a.w.w. na kunijia mimi?"

"Yeye ndiye aliyetuambia hivyo." Walimwambia.

"Je kwa nini hakuwaambia kumwendea Abu Bakr? aliuliza.

"Sisi tuliambiwa hivyo, "wao walisema, "nasi tulikwenda kwake."

"Je, aliwaambia nini kuhusu kesi hii?" aliuliza.

"Alisema kuwa mnyama anapomwua mnyama basi hapana shitaka dhidi ya mnyama mwingine. "walijibu.

"Omar alijibu: "Kwa hakika, majibu yangu pia yanakubaliana na Abu Bakr."

Wao walirejea kwa Mtume s.a.w.w. na kumpatia ripoti hiyo. Hapo Mtume s.a.w.w. "Nendeni kwa Ali ibn Abi Talib ili awatoleeni hukumu yenu."

Basi wao walimwendea Imam ‘Ali a.s. na kumwelezea kisa chote. Imam ‘Ali a.s. aliwauliza maswali mengi kuhusu kisa hicho.

Swali la kwanza: "Je wanyama hao wawili walikuwa pamoja wakati wa tukio hilo?"

"La, hawakuwa pamoja. "walijibu.

"Je wote wawili walikuwa wamefungwa kwa kamba?"

"La, hawakufungwa kamba," walijibu.

"Je punda alikuwa amefungwa na ng'ombe wazi?"

"Naam!" wao walijibu.

"Hivyo, Imam ‘Ali a.s. alisema: Mwenye ng'ombe inambidi amfidie mwenye punda aliyeuawa."

Yaani kwa kifupi, Imam ‘Ali a.s. aliwaambia: "Iwapo ng'ombe aliingia katika zizi la punda, hivyo mwenye ng'ombe lazima alipe thamani ya punda kwa mwenye punda lakini, iwapo punda aliingia katika zizi la ng'ombe, na ng'ombe akamwua punda huyo, basi mwenye punda hana haki ya kudai fidia kutoka kwa mwenye ng'ombe."

Wakati walipomwendea Mtume s.a.w.w. kumjulisha juu ya swala hilo la hapo juu na vile Imam ‘Ali a.s. alivyoliamua, Mtume s.a.w.w. alisema: " Ali ibn Abi Talib amewaamua kama vile uamuzi wa Allah ulivyo."
Katika zama za Imam ‘Ali a.s. wanaume wanne walilewa pombe. Pombe ilipowakolea, walianza kupigana kwa visu. Kila mmoja wao alijeruhiwa vibaya sana. Mashtaka yao yalifikishwa mbele ya Imam ‘Ali a.s. ambaye aliwaaamrisha wafungwe hadi watakapopata fahamu zao timamu. Wawili kati ya hao wanne walikufa bado wakiwa mahabusu. Familia zao (waliokufa) walimwijia Imam ‘Ali a.s. na kudai: "Turuhusu sisi kulipiza kisasi dhidi ya watu hawa wawili, ewe Amir al-Muminiin! Kwani hao ndio waliowaua watu wetu."

"Je mmejuaje hivyo?" Imam ‘Ali a.s. aliwauliza "labda inawezekana hawa wawili waliuawa."

"Sisi hatujui hayo," wao walijibu, "Kwa hivyo waamue kama vile Mwenyezi Mungu alivyokufundisha.

Yeye alisema: "Ubishi wa damu ya watu wawili ambao waliuawa ni wajibu wa makabila ya watu wanne baada ya kusawazishwa kwa mahesabu ya malipo ya watu wawili walio hai kwa ubishi wa damu kwa ajili ya jeraha zao."
Watu sita walikwenda kuogelea mtoni Furati. Mmoja wao alizama - akafa maji.

Watu watatu walidai kuwa wenzao wawili walimzamisha yule mtu.

Na vile vile wale watu wawili walidai kuwa wale watu watatu walimzamisha yule mtu.

Imam ‘Ali a.s. aligawa fidia ya damu kwa sehemu tano yao. Wawili walitakiwa walipe sehemu tatu za tano kwa mujibu wa madai yao na wale watatu walitakiwa walipe sehemu mbili za tano kwa mujibu wa mashitaka dhidi yao.
Mtu mmoja alimwijia Imam ‘Ali a.s. na kumwambia: "Ewe Amir al-Muminiin! Mimi nilikuwa na tende mke wangu alitoa kokwa moja aliweka mdomoni. Nilikula kiapo cha yeye asimeze wala kutema."

Imam ‘Ali a.s. alimwambia: "Mwambie ale nusu na ateme nusu, kwani ndivyo utakuwa huru kwa kiapo chako."
Mjamzito mmoja alizini, na kesi yake ililtwa mbele ya Umar, naye aliamuru kupigwa mawe.

Imam ‘Ali a.s. alimwambia: "Lazima uwe mwangalifu mno kwa kuwa na haki ya kumwadhibu huyo, kwani itamaanisha kumwadhibu hata yule aliye tumboni mwake. Ambapo Allah s.w.t. anasema katika Quran: "Wala mbebaji hatabeba mizigo ya mwingine' (6:164)"

Kwa kusikia hayo Umar alisema: "Kwa hakika katika maisha yangu sijawahi kuona swala lolote lile ambalo Abul Hasan a.s. ameshindwa kulijibu kwa ufasaha." Hapo ndipo alipouliza: "Je sasa nimfanyeje?"

"Mwangalie hadi atakapojifungua, "alijibu Imam ‘Ali a.s. "Wakati atakapojifungua na wewe kumpata mtu wa kumtunza mtoto wake, hapo ndipo utakapoweza kumwadhibu."

Kwa hayo, Umar alisaidiwa na Imam ‘Ali a.s. na alishukuru kwa hayo.
Mzee mmoja aliona mwanamke, ambaye alishika mimba huku mzee yule aliikataa kuwa si yake, kwani alisema: "Mimi sijawahi mumwingilia huyu mwanamke tangu nimwoe," sasa mimba hiyo inatokea wapi?"

Kwa kusikia hayo, Uthman bin Affan alishangaa kwa hoja hiyo, "Je mzee huyu ameumaliza ubikira wako ulipokuwa bikira?" Aliuliza Uthman.

"La!" alijibu yule mwanamke.

"Mtoleeni hukumu kwa mujibu wa Sharia," alitoa amri Uthman.

"Mwanamke huwa na matundu mawili," alinena Imam ‘Ali bin Abi Talib a.s." tundu la kupitia damu za mwezini na tundu la mkojo. Inawezekana kwa huyu mzee alikuwa karibu na tundu la damu ambapo alitokwa na shahawa ambazo zimemfanya huyu ashike mimba hiyo."

Yule mzee alipoulizwa kuhusu hayo, alijibu: "Naam, mimi nimekuwa na mazoea ya kumwaga shahawa zangu wakati tulipokuwa tukifanya mapenzi naye lakini sijawahi kuvunja ubikira wake."

"Basi mimba hiyo imetokana nayo!" alibainisha Imam ‘Ali a.s., "na mtoto huyo ni wake tu. Mimi nadhani kuwa huyu mzee aadhibiwe kwa tuhuma zake."

Uthman bin Affan alistaajabishwa mno kwa hukumu iliyofikiwa na akaitekeleza hivyo hivyo.
Mtu mmoja alikuwa na suria (kijakazi) na alimpatia mtoto. Baadaye alitengana naye na kumwoza kwa mtumwa wake. Mmiliki wake, yule mtu, alikufa. Huyo mwanamke alikuwa huru kwa sababu ya kuwa na mtoto wa yule mtu, na vile vile yule mtoto alimrithi baba yake. Yule mtoto pia alifariki, hivyo alimrithi bwana wake kutokea mtoto wake.

Wakati hayo yanatokea, kulizuka mzozo baina yake na mwanamke (yule mtumwa) Hivyo wao walimwijia Uthman bin Affan, yeye alidai: "Huyu mwanamme ni mtumwa wangu." Na yule mwanamme alikuwa akidai: "Huyu mwanamke ni mke wangu nami sitamwachia (kutoka katika ndoa yangu)"

"Ama kwa kweli, hili ndilo swala gumu mno. "Alisema Uthman.

Katika kikao hicho, alikuwapo pia Imam ‘Ali a.s. Yeye alisema: "Hebu mwulize huyo mwanamke kama alikuwa ameingiliana kimwili na huyo bwana baada ya kupata urithi."

"La!, hatukufuata hivyo." alijibu yule mwanamke.

"Lau ningalikuwa nimefahamu kuwa huyo bwana amefanya hivyo, basi ningelimwadhibu. "Alisema Imam a.s. " Nenda. huyo ni mtumwa wako bila ya kuwa na haki zozote juu yako. Iwapo utapenda kumweka, au kumpatia uhuru, au kumwuza, yote hayo ni haki yako."
Mwanamke mmoja alizaa kitandani mwa bwana wake, mtoto mwenye vichwa viwili na miili ikiwa imeungana kiuno kimoja tu.

Kwa hayo, wanafamilia wote walistaajabishwa na hawakuelewa iwapo ni watoto wawili au ni mmoja.

Hivyo wao walimwendea Imam ‘Ali a.s. kuhusu kujua iwapo ni mmoja au wawili na hukumu za sharia kuhusiana na swala hilo.

Imam ‘Ali a.s. alimwambia. "Mtazameni pale aendapo kulala. Jaribuni kuuamsha mwili mmoja na kichwa chake. Iwapo miili na vichwa vyote viwili vitaamka kwa pamoja, basi wao ni binadamu mmoja tu. Na iwapo mmoja ataamka na mwingine atabakia amelala, basi mutambue kuwa wao ni binaadamu wawili tofauti na watakuwa na haki za watu wawili katika urithi."
Al-Hasan bin Ali al-Abdi ameripoti kwa mamlaka ya Sa'ad bin Tarif kwa mamlaka ya al-Asbagh bin Nubata ambaye alisema:

Wakati Shurayh, alipokuwa katika kikao cha kutoa hukumu, mtu mmoja alimwijia akisema: "Abu Umayya, naomba kuongea nawe katika faragha, kwani nahitaji hivyo mno."

Aliwaamrisha wote waondoke, isipokuwa wale waliokuwa washiriki (Khassa) wake tu ndio waliobakia. Ndipo alipomwambia:"Haya sema, unahitaji nini?"

"Abu Umayya," aliyasema huyo mtu, "mimi ninacho kile walichonacho wanaume na kile walichonacho wanawake. Hivyo nataka uamuzi wako iwapo mimi ni mwanamme au mwanamke."

Shurayh alijibu: "Mimi nimewahi kuyasikia hayo kutoka kwa Amirul Muminiin Ali bin Abi Talib a.s. na ninayakumbuka vyema. Hebu uniambie ni kutokea tundu lipi ambalo mkojo wako unatikea?"

"Kutoka katika matundu yote mawili," alijibu yule mtu.

"Huishia tundu lipi?" aliuliza Shurayh.

"Katika matundu yote mawili kwa pamoja." alijibiwa.

Shuray alistaajabishwa. Yule mtu aliongezea kusema:

"Mimi ninakuambia kuhusu tabia zangu za ajabu ambazo zitakustaajabisha kabisa."

"Ehee! Ati tabia zipi hizo?" aliuliza Shurayh.

"Baba yangu alinioza kwa kunichukulia kuwa mimi ni mwanamke. Nami nilishika mimba kwa bwana wangu na nilimnunua kijakazi ili anitunze. Siku moja nilimwingilia huyo kijakazi wangu, naye akashika mimba yangu."

Loh! Shurayh alipiga makofi kwa mshangao mkubwa na alisema: "Swala hili ni lazima lichukuliwe mbele ya Imam ‘Ali a.s. ili alitatue kwani mimi sina Ilimu ya kutoa hukumu yake."

Yeye aliinuka na yule mtu pamoja na wengineo wafuata. Walipomfikia Amirul Muminiin Ali Abi Talib a.s. alimwelezea mambo yote. Imam ‘Ali a.s. alimwita huyo mtu na akamwuliza habari zote alizoelezwa na Shurayh, naye alikiri yote yote hayo.

"Je, mume wako ni nani?" aliuliza:

"Fulani bin fulani," alijibu, "Naye pia yupo hapa mjini."

Huyo mume wake pia aliitea, na baada ya kuelezwa yote hayo, naye pia aliyasadikisha hivyo. "Naam yote ni kweli," alijibu.

"Kwa hakika inakubidi uwe mshupavu kuliko simba unapokutana na hali kama hii." alisema Imam ‘Ali a.s. Hapo alimwita Qambar na kumwambia: "Mchukue mtu huyo katika chumba pamoja na wanawake wanne walio waadilifu na uwaambie wamvue nguo na wazihesabu mifupa ya mbavu zake baada ya kuhakikisha kuwa sehemu zake zimefunikwa. Qambar alisema: "Ewe Amirul Muminiin! Si wanaume au wanawake watakaosalimika naye."

Kwa hiyo, Imam ‘Ali a.s. aliamrisha kuwa afunikwe kwa majani makavu na kuachwa pekee katika chumba. Hapo ndipo alipokwenda chumbani na kuzihesabu mbavu zake. Zilikuwa saba upande wa kushoto na upande wa kulia kulikuwa na nane. Hapo alipobainisha wazi wazi kuwa "Huyu ni mwanamme."

Hapo ndipo Imam ‘Ali a.s. alipoamrisha akatwe nywele zake na amvalishe pamoja na kofia, viatu na joho (rida) Yeye pia alimtenganisha na mume wake.
Mwanamke mmoja alimwashiki kijana mmoja na alifanya kila jitihada ya kumvutia kwake, lakini yule kijana alimkatalia kabisa kabisa. Basi kwa hasira zote aliondoka na akachukua yai la kuku. Huyo mwanamke alijipaka uweupe wa yai juu ya nguo zake, huku akifanya madai ya kunajisiwa na yule kijana wa kiume, hadi akaletwa mbele ya Imam ‘Ali a.s.

Huyo mwanamke alidai: "Huyu ndiye kijana aliyeninajisi."

"Hii hapa shahawa (manii) yake juu ya nguo zangu." Aliendelea kusema yule mwanamke.

Kwa hayo, yule kijana alilia huku akila viapo vya kutotenda uovu huo.

"Nileteeni maji yaliyo na moto kabisa," Imam ‘Ali a.s. alimwambia Qambar.

Maji moto kabisa yalipoletwa mbele yake, aliamrisha ya mwagiwe juu ya nguo za yule mwanamke. Yalipomwagiwa juu ya nguo za yule mwanamke, kulianza kubadilika rangi kuwa nyeupe ya mayai.

Ili kuthibitisha hayo, watu wawili walionja iwapo ni kweli, nao walisadikisha kuwa yalikuwa ni uweupe wa mayai.

Papo hapo Imam ‘Ali a.s. aliamrisha yule kijana aachiliwe huru na yule mwanamke alipewa adhabu ya kuchapwa sana kwa kosa la kusingizia.
Ushahidi kamili ulitolewa mbele ya Umar dhidi ya mwanamke mmoja aliyekuwa ameona akizini pamoja na mtu mwingine mbali na mume wake hapo jangwani.

Umar papo hapo alitoa amri ya kuuawa kwake kwa kupigwa mawe kwani alikuwa na mume wake halali. Kwa hayo alisema yule mwanamke: "Ewe Milipoishiwa na maji niliomba anisaidie maziwa, lakini yeye alitaka nijitolee kwake badala ya maji. Nilimkatalia kata kata. Ulifika wakati ambapo maisha yangu yalikuwa yanataka kukatika, ndipo hapo nilipojisalimisha mbele yake bila ya ridhaa yangu."

"Allahu akbar!" alisema Imam ‘Ali a.s. kwani aliye lazimishwa au kuzidiwa hana kosa wala hana dhambi kea mujibu wa Aya ya 123 katika Sura al-Baqarah."

Umar aliyasikia hayo kwa makini na alimwachilia huru yule mwanamke.
Mtu mmoja alimwijia Imam ‘Ali bin Husayn a.s. na kusema: "Mimi nimezoea mno zinaa na kuingiliana na wanawake kila usiku na hufunga saumu asubuhi."

Imam ‘Ali a.s. alimjibu: "Utiifu wa Allah s.w.t. ni bora ya kila kitu, usizini wala kufunga saumu."

Hapo Imam Mohammed Baquir a.s. aliwambia: "Ewe bwana! Matendo yako ni ya kisheitani na huku ukitarajia kupata Pepo?"
Imam ‘Ali a.s. alikuwa akiwaadhibu watu wasiooa, walipozini kwa kuchapwa viboko mia moja na kuwapeleka uhamishoni.
Iwapo mwanaume au mwanamke aliyeolewa alipozini, Imam ‘Ali a.s. aliwaadhibu kuwa kupigwa mawe hadi kufa kwao.
Imam ‘Ali a.s. alisema: "Mtu aliyembaka mwanamke hatalipa mahari yoyote kwa mwanamke yule bali ataadhibiwa kwa kupigwa mawe hadi kufa kwake. Hata hivyo, yule mwanamke hataadhibiwa kwani amelazimishwa pasi na hiari yake.
Mwanamke mmoja alishitakiwa kuzini wakati ambapo bwana wake alikuwa amefungwa jela. Imam ‘Ali a.s. alitoa hukumu ya kuchapwa viboko badala ya kupigwa mawe hadi kufa.
Imam ‘Ali a.s. alipokuwa Yemen, aliletewa kesi moja kuwa nyumba moja imeporomoka na katika mabaki ya ile nyumba walipatikana watoto wawili. Mmoja wao alikuwa mtumwa wakati mwingine alikuwa huru.

Imam ‘Ali a.s. alimpatia mtumwa kile kilichopatikana chini ya mabaki ya nyumba iliyoporomoka na alimpatia umilikaji wa nyumba ambamo kiwanja chake yule aliyekuwa huru. Vile vile alimfanya huru yule aliyekuwa mtumwa.
Asbagh bin Nabata ameripori kuwa watu watano waliotuhumiwa kwa kuzini, waliletwa mbele yake Umar, ambaye alitoa amri ya papo hapo ya kupigwa mawe hadi kufa kwao.

Imam ‘Ali a.s. alipoyasikia hayo, alisema kuwa hukumu hiyo haikuwasahihi.

Hapo ndipo alipokutanana kuwahoji kila mmoja wao pekee na akatoa hukumu kama ifuatavyo:

Mtu wa kwanza akatwe kichwa, wa pili apigwe mawe hadi kufa kwake, watatu achapwe viboko na nusu ya adhabu kamili kwa mtu wa nne. Ama mtu wa tano aliachiliwa huru baada ya kuadhibiwa kikawaida tu.

Umar alimwomba Imam ‘Ali a.s. amwelezee juu ya uamuzi huo wa kiajabu.

"Mtu wa kwanza ni Zimmi3 ambaye amezini pamoja na mwanamke Muislamu; mtu wa pili ni yule aliyeoa ambaye kwa mujibu wa sharia za Di ni kurajimiwa4; mtu wa tatu ni yule asiyeoa achapwe viboko; mtu wa nne ni mtumwa ambaye ataadhibiwa nusu ya adhabu kamili kwa mujibu wa sharia za Sin, na wa tano ni nusu-mwendawazimu hivyo anastahili adhabu ya kawaida kwa kosa kama la wenzake."

Umar alisema: "Nisije kuishi katika nchi ambapo Abul Hasan hayupo kuyatatua matatizo kama hayo."
Imam ‘Ali a.s. alipokuwa akienda Makka kuhiji, aliletewa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuzini.

Umar alitoa hukumu ya kupigwa mawe hadi kufa.

Kwa kuyasikia hayo yaliyotokana na Umar, alimwambia: "Adhabu kamili iliyowekwa na Sharia za Din ni kuchapwa viboko na wala si kurajimiwa kwani ana mke, ambaye wakati huo yupo mbali nae."
Bwana Muhammad bin Abu Bakr alimwandikia Imam ‘Ali a.s. akimwulizia adhabu kwa mwanaume Muislamu kuzini pamoja na mwanamke mkristo au Myahudi.

Imam ‘Ali a.s. alimjibu: "Iwapo mwanamme wa Kiislamu ameoa, basi arajimiwe, na iwapo bado hajaoa, achapwe viboko mia moja. Ama mwanamke wa kikristo au Kiyahudi, apelekwe uhamishoni.
Kesi ya zinaa ya mwanamke mzima pamoja na mtoto mdogo iliamriwa na Umar kuwa mwanamke huyo arajimiwe.

Imam ‘Ali a.s. aliposikia hivyo, alisema: "mwanamke huyo asirajimiwe bali achapwe viboko kwani mtoto katika swala hili bado yu mdogo hivyo hawezi kutofautisha lipi si sahihi."
Imam ‘Ali a.s. alitoa uamuzi wa kesi moja ambapo mtu alizini zaidi ya mara moja kwa siku hiyo hiyo pamoja na mwanamke mmoja, alisema kuwa adhabu itakuwa ni mara moja tu, ama iwapo mtu atazini pamoja na wanawake tofauti tofauti kwa siku moja hiyo hiyo, basi adhabu zitatolewa kwa mujibu wa idadi ya zinaa kwa siku hiyo.
Mtu mmoja alimtuhumu mke wake kwa zinaa, walifika kwa Uthman bin Affan kwa kumwita mke wake 'mzinifu.'

Mwanamke yule alijibu: "Wewe ni mzinifu zaidi yangu mimi!"

Kwa kusikia hayo, Umar aliamrisha wote wawili wachapwe viboko.

Imam ‘Ali a.s. alipoyasikia hayo, alimwambia Umar asiwe akifanya haraka katika kufikia uamuzi wake kwani si sahihi hivyo.

Imam ‘Ali a.s. alisema: "Kwa maneno ya mwanamke mwenyewe, amekiri kwa yeye ni mzinifu ambapo amestahili adhabu mara dufu. Adhabu moja ni kule kukiri kwake kwa zinaa na pili ni kule kumsingizia mume wake. Lakini adhabu yake ya uzinifu itakuwa nusu kwa sababu hajakiri mara nne ambavyo inavyotakiwa katika sharia za Din.

"Ama mume wake" aliendelea Imam a.s. kusema: "Ataachiliwa huru kwani yeye hajakiri wala hakuna ushahidi dhidi yake."

Uthman alikiri hayo, na kuhukumu vile Imam ‘Ali a.s. alivyoelezea.
Mwanamke mmoja alimpenda na kumwashiki mwanamme mmoja, hivyo alitafuta mbinu za kuweza kutimiza hamu yake pamoja nae. Alilala kitandani mwa yule mwanamme akijigeuza kama kijakazi wake.

Wakati yule meanamme alifika kitandani, akamuona mwanamke amelala, na hivyo hakutaka kupoteza fursa hiyo, akazini nae.

Kesi hiyo ilipofikishwa mbele ya Imam ‘Ali a.s., alimwamrisha kuwa mwanamke yule aadhibiwe hadharani wakati mwanaume arajimiwe katika faragha kwa sababu kosa lake lilikuwa dogo kuliko la mwanamke yule, kwani yeye ndiye chanzo cha kosa hilo. Na huyo mwanamme ameadhibiwa kwa sababu alikwisha fahamu na kutambua yule mwanamke ama sivyo, angaliachiwa huru bila ya kuadhibiwa.
Mzee mmoja wa kiume alizini pamoja na mzee mmoja wa kike, Imam ‘Ali a.s. aliwaadhibu kwa kuchapwa viboko mia moja kila mmoja wao na kurajimiwa.
Mtu mmoja aliyekuwa na majeraha mwilini alishitakiwa mbele ya Imam ‘Ali a.s. ambaye alitoa hukumu ya kusubiri hadi atakapopona kabisa.

Baada ya kipindi, alipopona, aliadhibiwa kikamilifu.

Kesi moja ililetwa mbele ya Mtume s.a.w.w. ya mgonjwa istiska (tumbo la maji) kazini kwa nguvu pamoja na mwanamke yule, ambapo yeye alikuwa hajaoa.

Hapo Mtume s.a.w.w. aliagiza makuti mia moja na akachapwa kwa mara moja.5
Imam ‘Ali a.s. asema: "Iwapo mtu atazini pamoja na mama yake, basi achapwe viboko mia akiwa mwili uchi na baadaye akatwe kichwa."
Mtu mmoja alimleta mtu mwingine mbele ya Abu Bakr akidai kuwa: "Huyu mtu amesema kuwa ametokwa na manii kwa kuota kuwa amezini pamoja na mama yangu."

Khalifa alishangaa kwani hakuwa na lakujibu.

Imam ‘Ali a.s. wakati huo alikuwa msikitini, alisema "Mtu aliyeilezea ndoto yake, asimame juani na adhabu zake zipatwe kivuli chake kwani alizini akiota tu, na vile vile achapwe kiboko kimoja au viwili ili akome kuwasumbua watu kwa maneno ya kipuuzi."
________________________
1. Kwa mujibu wa Ahmad b.Abi Abd Allah al-Barqi, shurtat al-Khamis walikuwa ni wafuasi elfu sita wa Imam ‘Ali a.s. ambao wamekula viapo vya kumtumikia hadi kufa kwao, Al-Rijal (Teheran 1342 A.H.),wao vile vile wanasemekana kuchanganyikana na wanamgambo,polisi na wapiganaji wa mstari wa mbele.

2. Mtu aliyewekesha Dinar mbili anayo Dinar moja ililsalimika hata kama tutachukulia kuwa Dinar yake moja imeibiwa,ambapo mtu wa pili,iwapo itakuwa Dinar yake moja ndiyo iliyoibiwa,basi hatabakia na chochote. Kwa kuwa uwizi uliathiri Dinar ya pili,hivyo wote waligawana faida na hasara yake.

3. Zimmi ni mtu alupaye kiasi fulani cha fedha kwa Dola ya Kiislamu kwa ajili ya kupatiwa usalama wa maisha yake.

4. Rajm yaani kupigwa mawe hadi kufa.

5. Hakimu kabla ya kutoa hukumu inambidi atambue hali na wakati wa tukio hilo.Iwapo mgonjwa anayo matumaini ya kupona,basi asubiriwe hadi atakapo pona ndipo adhabu itolewe na iwapo hatapona,basi inaweza kutekelezwa kama vile Mtume s.a.w.w. alivyofanya.

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ