Rafed English

Hukumu za Kifikihi Zinazowahusu Wanawake

Hukumu za Kifikihi Zinazowahusu Wanawake by : Mustafa Ranjbar Shirazi

 
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Fiqhu ‘l-Fatayaat kilichoandikwa na Mustafa Ranjbar wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kitabu hiki chenye manufaa sana kinahudumia mahitaji ya wajibu wa dini ya Kiislamu ya mwanamke kuhusiana na vipindi vyake vya kila mwezi. Baadhi ya mas’ala na hukumu za kuhudumia maiti ni makala muhimu zilizoongezwa kwenye kitabu hiki.

Sharia na kanuni zilizowekwa na Uislamu kwa ajili ya namna ya maisha ya usafi iliyodhibitiwa ni wajibu kwa kila Mwislamu kujifunza na kuzipandikiza ndani ya nafsi yake. Hili ni dhahiri kabisa kwamba litamwezesha yeye kudumu ndani ya mipaka ya mahitaji ya kisharia yaliyowekwa.

Shukrani zetu nyingi zimwendee ndugu yetu Ukhti Maysara Ali kwa kazi yake ya kutarjumi kitabu hiki. Vilevile shukrani zetu kwa wale wote waliochangia kwa njia moja au nyingine kwenye kufanikisha kukamilika kwa kazi hii tukufu.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es- Salaam
Tanzania
Ni jambo la wajibu juu ya (kila) mtu kujifunza mas’ala ambayo yanamtokea mara kwa mara. (Hii ni kauli ya Wanavyuoni Ndani ya Vitabu vinavyohusu Matendo ya Kisharia.)

Hakika kipindi cha ujana kinahesabika kuwa ndiyo fursa yenye thamani katika kujipatia maarifa na kuyavuta kutoka kwenye vyanzo vya elimu ambavyo mtu atafaidika navyo muda wote wa uhai wake.

Kila umri wa mwanadamu unavyosonga mbele, ndivyo majukumu yake yanavyozidi na maisha yake kuwa na msongamano. Kwa hali hiyo basi hukosa fursa ya faragha itakayomruhusu kujifunza yale yanayomlazimu miongoni mwa kanuni za sharia, na maoni ya wanachuoni wa sharia, ambazo nyingi miongoni mwa hizo huenda atazihitajia katika maisha yake hapo baadaye.

Bila shaka mwanadamu anahitaji kuwa na wigo katika kufanya mabadiliko ya kibinadamu ndani ya safari yake ya maisha. Na wigo huu ni mambo matatu yafuatayo:-

Kwanza: Utashi. Pili: Maarifa, na tatu: Ni Uwezo wa kusubiri na kuyavumilia matatizo mpaka afikie kwenye lengo. Kwa hali hiyo basi, mtu mwenye (tabia ya kuwa na) matarajio (bila kujituma) hawezi kuyafikia baadhi ya matarajio yake au yote, isipokuwa tu kama atakuwa amebeba ndani ya moyo wake utashi na mapenzi ya dhati katika kuiendea njia hiyo. Inampasa (mtu huyu) ajiandae kwa silaha ya maarifa na ujuzi utakaomnufaisha katika hilo, na awe na uwezo wa kusimama kidete kukabiliana na vikwazo na matatizo.

Na zaidi ya hayo yote ni kuwa; mwenye kupita njia ya haki na mwenye kutafuta wema wa dunia na akhera, anahitaji huruma na msaada wa Mwenyezi Mungu. Kadhalika (anahitaji kupata) uangalizi na usaidizi kutoka kwa Imamu wa zama hizi (Imamul-Mahdi a.s.) ili aweze kuendelea, na kuimarika juu ya njia ya uongofu wa Mwenyezi Mungu mpaka mwisho wa njia.

Tumeandika mafunzo haya ambayo yanahusu kanuni za wanawake, ili nasi tupate kutoa mchango (wetu) miongoni mwa wale wenye mapenzi ya kuchukua maarifa (ya dini) kutoka kwenye chem chem asilia ya mafunzo ya sharia kutoka kwa kizazi cha watu wa nyumba ya Mtume s.a.w. Kisha juu ya hayo yameongezwa mas’ala na uchambuzi mwingine, ambapo yamefikia hapo yalipo sasa.

Wakati tunapo kiwasilisha kitabu hiki mbele ya dada zetu waumini (wa kawaida) na wale wahubiri wa kike wenye kufuata nyayo za Bibi Fatmah Zahraa (a.s) na bibi Zainab, tunataraji mtatupa maoni na rai zitakazo tun- ufaisha ili tuweze kuzitumia kwenye chapa zitakazofuatia.

Kipindi hiki tulicho nacho, ni kipindi cha kumbukumbu ya miaka kumi na minane tangu kuondoka kwa mmoja miongoni mwa waalimu wakubwa wa sharia ya ki-Islamu na muasisi wa jamuhuri ya ki-Isilamu ya Iran iliyobarikiwa, naye ni Imam Khomein (Mwenyeezi Mungu amrehemu).

Tunamwomba Mwenyeezi Mungu Mtukufu Atuongoze katika yale Ayapendayo. Na (tunamuomba) ayakubali na kuyaridhia matendo yetu (mema). Na (tunamuomba pia) aturuzuku maombezi ya Mtume Muhammad (s.a.w.), na kizazi chake kilichotakasika. Na mwisho wa maombi yetu tunasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyeezi Mungu Mola Mlezi wa Viumbe.”

Mustafa Ranjbar Shirazi.
Mwanzoni mwa kipindi cha ujana hutokea mabadiliko makubwa na ya kina ambapo nguvu za kimwili na kiroho hufunguka.

Si hivyo tu, bali katka kipindi hichi ndani ya akili ya mwanadamu huchomoza matarajio na fikra mpya na kumwonesha kuwa anayo hadhi inayowavutia wengine kushirikiana naye.

Bila shaka kuanzia hapo mtu huyu hukataa kuwa (mwenye) kufuata tu, ambapo sasa hutafuta uhuru katika mambo yake binafsi na katika maamuzi yake anayoyachukua. Hali hiyo humaanisha kuwa amefikia kipindi cha Baleghe na kuwa anataka kuchagua njia moja baina ya njia nyingi mbali mbali.

Na njia hii (anayoitafuta) ni ile itakayo mfikisha kwenye wema wake binafsi, kama ambavyo ni wajibu wake binafsi kuichagua njia hiyo, kwani katika bahari hii yenye wingi wa fikra zinazo gongana huenda akajikuta anamhitajia (mwanachuoni) atakayemsaidia kumuongoza na kumvusha Swalama na kumfikisha ufukweni kwa amani.

Basi ndani ya kipindi hiki, huruma ya Mwenyeezi Mungu humfunika na rehema humteremkia kwa msaada wa ujumbe unaokunjukiwa na muono unaotokana na aina (mbali mbali) za fikra, kwa lengo la kuzingatiwa misingi yake na kusomwa maandiko yake.

Kwa hali hii basi, mara atajikuta anahisi furaha na kuingia katika mazingira mazuri hali ya kuwa uso wake ni wenye nuru na huku ulimi wake ukimhimidi na kumshukuru (Mola) juu ya yale aliyoelezwa na kule kufikia kipindi cha kuwajibika kisharia.

Hakika Baleghe ni kitabu cha habari na matendo ambacho ni lazima kukihifadhi ili nuru yake idumu na usafi wa kurasa zake uendelee mpaka mwisho wa uhai.

Hakika siku ya kubaleghe ndiyo siku ambayo Malaika wana haki ya kukaa kushotoni na kuliani: “Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.” Na hali ya kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu inamjumuisha inasema: “Enyi Mlioamini…..”
Alama Za Baleghe
Kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kupitiwa na miezi kadhaa tangu kubaleghe, hali ya kuwa hawalijuwi suala hili muhimu. Na kwa wakati huo utekelezaji wa wajibu wa mambo ya kisharia utakuwa umempita katika kipindi hicho.

Hakika utambuzi wa jambo hili unahitaji kuwa makini kwa namna Fulani, japokuwa ni jambo jepesi kwa upande wa wasichana kwani lina uhusiano na alama tatu ambazo moja miongoni mwa hizo inatosha kuwa dalili ya kubaleghe. Alama hizo ni hizi zifuatazo:-
1. Umri
Nao ni kutimiza miaka tisa ya mwaka unaofuta kalenda ya mwezi mwandamo.1 Na mwaka wa kalenda ya mwezi mwandamo ni pungufu kwa siku kumi na saa kumi na nane ukilinganisha na mwaka unaofuata kalenda ya Jua wa mawiyo.2
2. Nywele ngumu za Sehemu ya Siri:
Hizi ni nywele zinazodhihiri chini ya tumbo.
3. Damu ya Mwezi:
Miongoni mwa alama za kubaleghe, ni kupata damu ya mwezi (yaani hedhi). Na mara nyingine hupatikana alama nyingine kama vile kuongezeka kimo, kuota matiti na kupanuka kwa uke.
________________________
1. Mwaka Mwandamo ni Mwaka upatikanao kutokana na mzunguko wa Mwezi Mwandamo. (Mfasiri)

2. Mwaka Mawiyo ni Mwaka wa kawaida uliozoeleka ujulikanao kama Mwaka wa Kizungu. (Mfasiri)
Mara nyingi upatikanaji wa damu ya mwezi kwa wasichana hutokea kati ya umri wa miaka kumi na mbili hadi miaka kumi na nne.

Tofauti hii inatokana na sababu za kimazingira, kijografia na kinasaba. Hivyo katika nchi zenye baridi damu ya mwezi huchelewa kuonekana mpaka kwenye umri wa kati ya miaka kumi na sita hadi kumi na nane. Na katika nchi zenye joto huonekana mapema kwenye umri wa kati ya miaka kumi hadi kumi na mbili.

Msichana anapotimiza miaka tisa ya mwandamo analazimika kumrejea mwanachuoni mwenye daraja ya ijtihad aliyetimiza masharti.

Atamrejea mwanachuoni huyo ili amfuate katika nadharia zake na rai zake zinazohusu sharia katika namna ya utekelezaji wa wajibu wa kisharia, kuanzia Swala, swaumu na sharia nyinginezo.

Bila shaka vigawanyo vya damu ambayo huiona mwanamke ni vigawanyo saba, na kila kimoja kati ya hivyo kina kanuni zake mbalimbali za kisharia. Sisi tutavitaja vigawanyo hivi na kisha baada ya hapo tutazifafanua kanuni za wajibu.
1. Aina za Damu:
A- Damu ya majeraha itokayo toka ndani ya kizazi.

B- Damu ya vidonda vinavyo patikana kwenye ngozi.

C- Damu ya puani ambayo hutoka puani.

D- Damu ya bikira. (Damu inayosabishwa na kufanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza).

E- Damu ya hedhi. (Damu inayotoka kwenye kizazi).

Damu ya istihadha. (Hii ni damu ambayo hutoka kabla au baada ya hedhi au nifasi)

Damu ya nifasi (Hii ni damu ambayo hutoka baada au wakati wa kujifungua).
Mas’ala Mawili:
Damu inayosamehewa ni ile yenye kiwango cha upana wa dirhamu inapokuwa kwenye vazi au mwili, na Swala inasihi hata ukiwa nayo.

Damu hiyo ni damu ya jeraha la kawaida peke yake (ndiyo inayo sameheka) na wala si damu nyingine zinazo wahusu wanawake.

Damu ya kawaida ya mwili inapochanganyika na najsi au na kitu kingine, basi hapo haihusiki na msamaha huu wala ruhusa hii.
2: Majosho Ya Wajibu, Nayo Ni Saba:
Josho la janaba
Josho la istihadha
Josho lanifasi Josho la janaba
Josho la maiti1
Josho la kumgusa maiti
Josho la sunna ambalo huwajibika kwa nadhiri au kiapo.
Kwanza: Kanuni Za Hedhi:
Mwenyeezi Mungu anasema: “Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Waambie: Huo ni uchafu, basi jitengeni na wanawake katika hedhi….”2
Maana Ya Hedhi:
Hedhi ni Damu anayoiona mwanamke katika baadhi ya siku, aghlabu huwa ndani ya kila mwezi.

Na ndani ya siku za kutoka kwa damu hiyo, mwanamke huitwa Mwenye Hedhi.
Alama Za Damu Ya Hedhi:
Damu ya Hedhi ni nyekunde yenye kuelekea kwenye weusi, au nyekundu nzito, yenye msukumo, joto na harara3
Sharti:
Balehe ya kisharia, nayo ni kutimiza miaka kumi ya mwandamo. Uchache wa Hedhi ni siku tatu.

Wingi wake ni siku kumi, hivyo kila damu aionayo mwanamke chini ya siku tatu au iliyozidi baada ya siku kumi, siyo hedhi.

Kauli yenye nguvu ni kuwa, kipimo ni siku tatu zenye kufuatana, na hilo haliharibiwi na ukatikaji wa muda mchache.

Mpaka unaotenganisha kati ya hedhi na hedhi nyingine (ambao ndio uchache wa siku za tohara) ni siku kumi, na hapo ni lazima damu mpya ipimwe kwa alama za hedhi.

Mfano: Iwapo mwanamke ataona damu baada ya vipindi viwili vya tohara ya mzunguko wa mwezi na baada ya kuwa zimepita siku kumi basi (ili ihesabike ni damu ya mwezi) ni lazima damu hii iwe na sifa zilizotajwa.

Na kama mpaka unaotenganisha utakuwa chini ya siku kumi basi damu hii haitahesabika kuwa ni hedhi hata kama itakuwa na alama za hedhi bali itakuwa ni damu ya Istihadha.4

Damu ya hedhi kama tulivyosema, hupatikana baada ya kutimiza miaka tisa ya mwandamo na kabla ya ukomo wa hedhi, na damu itokayo baada ya miaka ya ukomo wa hedhi huwa ni damu ya Istihadha.

Umri wa kukoma kutokwa na hedhi (Maana yake, Alama zake na Hukumu zake):
Maana Yake:
Mwenye kukoma kutokwa na hedhi ni mwanamke aliyetimiza umri wa miaka sitini ya mwandamo ikiwa ni mwanamke wa ki-Qurayshi, na miaka hamsini kama si mwanamke wa ki-Qurayshi.

Kutimia umri wa miaka sitini ya mwandamo kwa mwana mke wa ki-Qurayshi, taqriban ni sawa na miaka hamsini na nane na miezi miwili ya mwaka wa mawiyo5

Aidha kwa mwana mke asiyekuwa Mquraishi kutimiza umri wa miaka hamsini, taqriban ni sawa na umri wa miaka arobaini na nane na miezi mitano ya mwaka wa mawiyo.

Mwanamke mwenye kukoma kutokwa na hedhi huwa haoni damu ya hedhi, na iwapo ataona damu kwa namna ya kuendelea au ya kukata huhesabiwa kuwa ni damu ya Istihadha.
Mas’ala:
Ni upi wajibu alionao mwanamke anapokuwa ndani ya siku za kujichunguza?

Ni lazima kwa mwanamke ambaye ametimiza alama na masharti ya hedhi ajichunguze mwenyewe kwa muda wa siku tatu kuanzia pale linapotoka tone la kwanza la damu.

Nini maana ya mwanamke kujichunguza kwa muda wa siku tatu?
Jibu:
Maana yake ni kuwa: Baada tu ya mwanamke kuona tone la kwanza la damu anatakiwa kuyaacha matendo yake ya kiibada kwa muda wa siku tatu mpaka itakapobainika hali yake upande wa wajibu wa kisharia na kujua je, atatumia kanuni za hedhi au atatumia kanuni za damu ya Istihadha?

Kwa hiyo ndani ya siku hizi tatu, ni lazima kwake kuyaacha mambo yote yaliyoharamishwa kwa mwanamke mwenye hedhi.

Na iwapo damu itaendelea kwa muda wa siku tatu bila kukatika atachukulia kuwa ni hedhi, na hapo atalazimika kutumia kanuni za hedhi.

(Mfano, ikiwa siku hizi zimo ndani ya mfungo mtukufu wa Ramadhan ni lazima kwake kulipa swaumu na wala si lazima kulipa Swala.)

Na iwapo ni kinyume na hivyo basi atachukulia kuwa ni damu ya Istihadha na atawajibika kutumia kanuni zake, hivyo atalazimika kulipa saumu pia Swala iliyompita ndani ya siku hizo.
Mas’ala:
Ndani ya siku za kujichunguza ambazo bado wajibu wake kisharia haujabainika, haifai (kwake) kuswali au (kufunga) swaumu au kuingia msikitini na kila jambo linalohitaji tohara.
Mwanzo Wa Hedhi:
Kwa wasichana wengi hedhi hudhihirika kama ilivyo kwa mama zao, na kwa ujumla inakuwa kati ya umri wa miaka tisa hadi kumi na sita ya miaka ya mwandamo. Wakati huo huo suala hili lina athiriwa na sababu za kimazingira (kutegemeana) na kiwango cha joto.

Ama katika nchi za mashariki ya kati, inakuwa ni kati ya miaka kumi na moja hadi kumi na mbili. Asilimia tano ya wasichana huchelewa hadi umri wa miaka kumi na sita mpaka kumi na nane.

Hatuna budi kugusia kuwa, miezi ya mwanzo ya kudhihiri damu ya mwezi huwa haina mpangilio maalumu kwa wasichana wengi, kwani msichana anaweza kuiona damu kuanzia siku tatu mpaka tano, lakini baada ya kupita miezi miwili au mitatu damu hiyo (kwa kawaida) hutulia kwenye siku zenye mpangilio maalum.
Vigawanyo vya Hedhi:
Mwenye kuanza: Naye ni mwanamke ambaye anaishuhudia damu kwa mara ya kwanza.

Mwenye Kukoma kutokwa na Hedhi: Kama tulivyosema tangu mwanzo kuwa mwanamke wa ki-Quraysh anaingia miaka ya ukomo wa kutokwa na hedhi baada ya kutimiza miaka sitini ya mwandamo, na yule asiye Mquraysh huwa (anakoma) baada ya kutimiza miaka hamsini ya mwandamo, na mwanamke wa namna hii kwa mujibu wa wanachuoni wa sharia ya ki-Islamu, huitwa Mwenye kukoma kutokwa na hedhi.

Mwenye Ada ya Wakati na Idadi: Huyu ni mwanamke ambaye anaiona damu kwa utaratibu wa namna moja ndani ya miezi miwili yenye kufuatana. Damu inaanza kumtoka ndani ya siku maalumu na kukomea ndani ya siku maalum.

Hivyo Siku za hedhi yake zikilingana huitwa Mwenye Ada ya Wakati na Idadi. Na kwa maana nyingine ni mwanamke ambaye hedhi yake inalingana, kwa uchache (kanuni hii inapimwa) ndani ya miezi miwili yenye kufuatana.

Mwenye Ada ya Idadi: Naye ni mwanamke ambaye anaona damu kwa idadi ya siku maalum ndani ya miezi miwili yenye kufuatana, isipokuwa muda wa kuanza unapishana. Kwa mfano mwezi wa kwanza, ada yake ya mwezi inaanza siku ya tano mpaka siku ya kumi, na katika mwezi wa pili inaanza siku ya saba mpaka siku ya kumi na mbili. (Hapo idadi ya siku inalingana lakini unapishana wakati wa kuanza).

Mwenye Ada ya Wakati: Huyu ni mwanamke ambaye anaona damu ndani ya wakati maalumu ndani ya miezi miwili yenye kufuatana, isipokuwa ndani ya kila mara idadi ya siku inapishana. Kwa mfano katika mwezi wa kwanza damu inaanza siku ya kwanza mpaka siku ya tano, na katika mwezi wa pili inaanza siku ya kwanza mpaka siku ya saba. (Hapo wakati wa kuanza umelingana, na tofauti iko kwenye idadi ya siku).

Asiye na Ada Maalumu: Naye ni mwanamke ambaye tangu alipoanza kupata damu ya mwezi kwa miezi kadhaa, damu yake haina muda maalum wa kuanza wala idadi maalum ya siku. Aliyesahau: Huyu ni mwanamke aliye sahau aina ya Ada yake.
Nukta Muhimu:
Ni vizuri kwa mwanamke kuzitambua siku za hedhi yake kulingana na kalenda maalumu katika miezi iliyopita na miezi itakayofuata ili aweze kupanga utaratibu wa matendo yake na ibada zake kulingana na kalenda hiyo. Lifuatalo ni swali ambalo tutalijibu kulingana na vigawanyo hivyo tofauti.

Swali: Iwapo mwanamke ataona damu kwa muda wa siku kumi na mbili, basi ni ipi kanuni yake?

Mwenye kuanza: Iwapo atashuhudia damu zaidi ya siku kumi zenye kufuatana, basi muda wa chini (kwa mujibu wa sharia) ni siku tatu, na wingi wa muda wa (kutoka damu) itambidi kuwarejea ndugu zake. Kwa hali hiyo atatumia kanuni ya hedhi kwa idadi ya siku za hedhi yao, na siku zitaka-zozidi atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha.

Mfano ikiwa idadi ya siku za hedhi kwa mzazi wake ni siku saba, basi na yeye atafanya siku saba kuwa ndio hedhi yake (kwa sharti kwamba damu ile iwe na sifa na masharti yanayohusu hedhi), na siku zilizobaki atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha. Aidha ndugu ambao mwanamke huyu atawatumia katika kanuni hii, ni wafuatao kwa kufuata utaratibu huu: Mama, dada, mama mdogo (au mkubwa), shangazi, binti wa dada na binti wa shangazi.

Mwenye Ada ya Wakati na Idadi: Iwapo mwenye ada ya wakati na idadi ataona damu zaidi ya idadi ya siku za ada yake basi zilizozidi atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha.

Mwenye Ada ya Idadi: Aidha mwanamke huyu naye pia atafanya idadi ya siku za hedhi ya miezi iliyotangulia kuwa ndio hedhi, na zilizozidi atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha. Mfano: Iwapo katika miezi iliyotangulia hedhi yake ilikuwa ni siku tano basi na ndani ya mwezi huu ni siku tano na siku zilizobaki ni damu ya Istihadha.

Mwenye Ada ya Wakati: Iwapo Mwenye Ada ya Wakati ataiona damu zaidi ya siku kumi, basi jambo hilo lina sura nyingi:

a. Ikiwa kutokana na sifa za damu anaweza kugundua ni ipi damu ya hedhi, na ni ipi damu ya Istihadha, basi analazimika kutenda kulingana na hali hiyo.

b. Na ikiwa hawezi kutenganisha sifa za damu basi atarejea kwa jamaa zake ambao ni (Mama, dada na mama mdogo). Kwa hiyo atatambua siku za ada yake kwa kufuata ada zao.

c. Ikiwa siku za hedhi kwa ndugu zake hazina ada maalumu, basi siku saba za mwanzo atazifanya kuwa ni hedhi, na siku zilizobaki atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha.

Asiye na Ada Maalum: Iwapo ndani ya mwezi huu itatokea kuona damu zaidi ya siku kumi, basi atafuatilia sifa za damu. Endapo zinafanana na sifa ya hedhi, basi siku kumi za mwanzo atazifanya kuwa ni hedhi na zilizobakia atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha. Na kama hazifanani na sifa ya hedhi, basi ni wajibu juu yake atende kulingana na vipengele viwili vya A na B vinavyohusu kanuni ya Mwenye Ada ya Wakati.

Aliyesahau: Iwapo ataona damu zaidi ya siku kumi, basi anawajibika kutenda kulingana na hukumu za kifungu cha tano, yaani cha yule Asiye na Ada Maalum.
Yaliyoharamishwa Kwa Mtu Mwenye Hedhi:
Ibada: Kwa mfano; Swala, swaumu, kutufu Al-Kaaba, kukaa itikafu na kila lile ambalo utekelezaji wake unahitajia josho au udhu au kutayammam.

Kila lililo haramishwa kwa mtu mwenye janaba; kwa mfano: kugusa andiko la Qur’an, kuingia Msikiti Mtukufu wa Makkah6 na Msikiti wa Mtume (s.a.w.). Hairuhusiwi hata kama itakuwa ni kwa namna ya kupita, kukaa ndani ya Msikiti wowote ule usiyokuwa hiyo miwili. Si ruhusa pia (kuingia na) kuweka kitu Msikitini, kusoma moja ya Sura zenye Aya ya Sijida ya Wajibu, hata ikiwa baadhi yake kama vile Bismillahi au herufi yoyote ya Sura hizo (kwa nia ya kuwa ni sehemu yake). Kujamiana kati ya Wanandoa. (Na uharamu wake unahusu pande zote mbili, yaani mume na mke).
Mas’ala:
Kafara ya kujamiana ndani ya theluthi ya kwanza ya siku za hedhi ni dinari moja,7 na ndani ya theluthi ya pili ni nusu dinari, na ndani ya theluthi ya mwisho ni robo dinari. Na inawezekana kutoa thamani hiyo kwa fukara mmoja au kwa mafukara watatu.
Mas’ala Muhimu Kuhusu Hedhi:
Ndani ya siku za hedhi haisihi kutekeleza Swala za wajibu za kila siku, na wala mwanamke hawajibiki kuzilipa. Ama swaumu nayo pia haisihi, lakini ni lazima kuilipa. Iwapo mwanamke atapatwa na hedhi akiwa ndani ya Swala, basi Swala yake inabatilika.

Iwapo mwanamke ataichelewesha Swala na muda wa kuweza kuitekeleza Swala nzima ukampita, (mfano baada ya adhana ya adhuhuri akawa ameichelewesha Swala kwa muda wa kuweza kutimiza rakaa nne), kisha ndipo hedhi ikaanza kumtoka, basi katika hali kama hiyo ni lazima kulipa Swala hiyo iliyompita.

Iwapo Mwanamke atatoharika na akawa ana muda wa kutosha kuoga na kufanya vitangulizi, kuanzia kuandaa mavazi na mengineyo na kutekeleza rakaa moja ya Swala au zaidi ya moja, basi katika hali kama hiyo atalazimika kuoga na kutekeleza Swala, na kama hatofanya hivyo basi atalazimika kulipa Swala hiyo.

Mwanamke mwenye hedhi baada ya kutoharika analazimika kuoga na kisha kutia udhu pindi anapotaka kusali au kufanya ibada nyingine, na bora ni kutia udhu kabla ya kuoga iwapo anataka kusali. Talaka inayotolewa kwa mwanamke akiwa katika hedhi ni batili, (isipokuwa katika baadhi ya hali, lakini inasihi kuolewa).

Ni sunna kwa mwanamke mwenye hedhi kubadili pamba (na kujiweka katika hali ya unadhifu) kisha kutia udhu ndani ya kila wakati wa Swala (unapoingia) halafu akae chini (kwa kiasi cha) muda wa kuweza kutekeleza Swala nzima huku akiwa ameelekea Qibla hali ya kuwa akimtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Pili: Damu Ya Istihadha: Maana Yake:
Hii ni moja ya damu ambazo humtoka mwanamke. Na pindi inapomtoka, basi mwanamke huyo huitwa Mwenye Istihadha.
Alama Zake:
Kwa kawaida damu ya Istihadha huwa ya njano, yenye baridi, tena nyepesi, wala haitoki kwa nguvu na wala haichomi, japokuwa inaweza ikawa na sifa za hedhi.
Vigawanyo Vya Damu Ya Istihadha:
Istihadha Nyingi
Istihadha ya Wastani
Istihadha Chache.
Jinsi Mwanamke Atakavyo Tambua Kanuni Za Damu Ya Istihadha
Iwapo mwanamke hajui damu yake ni ya kifungu kipi, basi anaweza kulala chali kisha ainue nyayo zake na kuingiza kipande cha pamba ndani ya utupu wake, kisha asubiri kidogo na ndipo akitoe.

Iwapo pamba itachafuka (italowana) kwa damu bila damu kupenya ndani ya pamba ile, na bila kuonekana upande wa pili, basi hiyo ni Istihadha chache.

Iwapo Damu itapenya ndani ya pamba na kuonekana upande wa pili lakini bila kutiririka kutoka kwenye pamba, basi hiyo ni Istihadha ya wastani.

Na iwapo itatiririka toka kwenye pamba mpaka nje ya pamba basi hiyo ni Istihadha nyingi.
Hukmu Zinazo Shirikiana Kati Ya Vigawanyo Vitatu:
Kutia udhu kwa ajili ya kila Swala. Kwa hiyo Swala ya Adhuhuri inahitaji udhu wake, na Swala ya alasiri itahitaji udhu mwingine.

Kubadili pamba, na kuyatoharisha mavazi ambayo yamepatwa na najisi hata kama ni chache.

Kuutoharisha mwili kutokana na najisi iliyompata mwilini.
Hukmu Makhsusi Kwa Kila Kifungu:
Hukmu ya Istihadha Chache: Ni kutenda mambo matatu yenye kushirikiana ambayo yametajwa hapo nyuma kwa ajili ya kila Swala. (Inakusudiwa kutia udhu, kubadili pamba au pedi, na kuyatoharisha mavazi yaliyo najisika, na sehemu ya mwili iliyopatwa na najisi).

Hukmu ya Istihadha ya Wastani: Hukmu ya mwenye istihadha hii pamoja na kutenda mambo matatu yenye kushirikiana kwa ajili ya kila Swala; pia ni lazima kila siku kuoga kwa ajili ya Swala ya kwanza baada ya kupatwa na istihadha. Kwa mfano iwapo ataoga josho la istihadha ya wastani kwa ajili ya Swala ya asubuhi, basi siku ya pili ataoga kwa ajili ya Swala hiyo hiyo ya asubuhi. Na iwapo ataoga kwa ajili ya Swala ya adhuhuri, basi pia siku ya pili ataoga kwa ajili ya Swala ya adhuhuri, na hali itakuwa hivyo hivyo iwapo (ataanza kuoga kwa ajili ya) Swala nyingine. Ama katika Swala zitakazobaki ataendelea kutenda mambo matatu yenye kushirikiana.

Hukumu ya Istihadha Nyingi: Hukmu ya istihadha nyingi ni pamoja na kutenda mambo matatu yenye kushirikiana kwa ajili ya kila Swala, piaataoga kwa ajili ya kila Swala.

Kwa hiyo basi, ataoga kwa ajili ya Swala ya asubuhi, na kama anakusanya Swala, basi ataoga kwa ajili ya Swala za adhuhuri na alasiri na ataoga tena kwa ajili ya Swala za magharibi na isha iwapo atazikusanya.

Kusihi kwa josho moja katika kukusanya Swala ya adhuhuri na alasiri na magharibi na isha ni kwa sharti asitenganishe baina ya Swala mbili.

Kinyume na hivyo atalazimika kuoga kwa ajili ya kila Swala huku akitenda yale mambo matatu ya wajibu yanayo shirikiana.
Nukta Muhimu:
Kwa ajili ya kufafanua hukumu zinazohusu vigawanyo vya damu ya istihadha tumeweka jedwali la vigawanyo kama ifatavyo:
________________________
1. Majosho haya mawili (Josho la Maiti na Josho la Kugusa Maiti) yanamuhusu Maiti. Katika uchambuzi ujao tutatoa baadhi ya ufafanuzi kuhusu hilo.

2. Al-Baqara: 222

3. Tahriril-Wasilah: 44.

4. Somo la Damu ya Istihadha litakufikia muda mfupi ujao.

5. Mwaka wa mawiyo ni mwaka uliozoeleka na unaojulikana kama mwaka wa kizungu. (Mtarjuma)

6. Huu ni Msikiti uliyoko Makkah. Ama Msikiti wa Mtume ni ule uliyoko Madina.
7. Dinari moja ni sawa na gramu kumi na tisa za Dhahabu Safi.
AinayaDamu
Chache
Wastani
Nyingi
Alama
 
Damu ilowanishe ichafue pamba bila kupenya ndani
Damu ilowanishe ichafue panda zote mbili za pamba bila kutoka nje
Damu itembee kutoka kwenye pamba mpaka nje(kiasi cha kutapakaa kwenye pendi au kitambaa
Hukumu ya Swala
 
Kila Swala:
1. Kubadili pamba au pendi
2. Kutia Udhu
3. Kutoharisha mavazi na mwili sehemu iliyona jisija moja
Pamoja na kutenda mambo matatu yenye kushirikiana, pia anawajibija kuoga kila siku mara
Pamoja na wajibu wa kutenda mambo matatu yenye kushirikiana pia:
1. Kuoaga kabla ya Swala ya asubuhi
2. Kuoaga kabla ya Swala ya adhuhuri na alasiri(kwa sharti iwapo atazikusa nya pamoja
3. Kuoga kabla ya magharibi na isha (kwa sharti iwapo atazikusanya pamoja)
Hukumu ya Swaumu
Sahihi wala haihi taji udhu
Sahihi kwa sharti ya kuoga josho la wajibu la kila siku
Sahihi kwa sharti ya kuoga majosho ya wajibu ya kila siku
 
Mas’ala Muhimu:
a. Iwapo baada ya Swala ya asubuhi istihadha chache itaongezeka na kuwa ya wastani, basi atawajibika kuoga kwa ajili ya Swala za adhuhuri na alasiri. Na iwapo itaongezeka baada ya Swala za adhuhuri na alasiri, basi atawajibika kuoga kwa ajili ya Swala za magharibi na isha.

b. Iwapo istihadha ya wastani itabadilika na kuwa nyingi, basi ni lazima kuoga kwa ajili ya kila Swala (yaani atende matendo ya mwenye istihadha nyingi).

c. Istihadha itakapokatika, ni wajibu kutekeleza mambo ya wajibu ambayo yanahusu istihadha husika kwa ajili ya Swala ya kwanza tu, na wala si kwa Swala zitakazofuata. Kwa hiyo iwapo damu ya mwenye istihadha ya wastani au nyingi itakatika ni lazima aoge.

Lakini ikiwa ametenda mambo ya wajibu wakati wa kuoga kwa ajili ya Swala iliyotangulia; hatowajibika kuoga mara nyingine iwapo damu yoyote haijadhihiri.

Na iwapo Mwenye istihadha chache atatoharika kutokana na Damu basi atatumia Kanuni zake kwa ajili ya Swala ya kwanza atakayoitekeleza baada ya kusafika, na atatumia utaratibu wa kawaida kwenye Swala zitakazofuatia.
Nukta Muhimu:
Hukumu zilizotajwa hapo juu kuhusu damu ya istihadha ndizo fat’wa za Wanachuoni wengi Wakuu wa Madhehebu ya Shia Imamiya, na wala hakuna tofauti kubwa kati yao kuhusu mas’ala hayo.
Tatu: Nifasi:

Maana Yake:
Nifasi au damu ya uzazi ni damu inayoonekana wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua. Inapoonekana na isikatike mpaka siku kumi tokea alipojifungua, basi huitwa damu ya nifasi. Na ndani ya istilahi ya sharia ya ki-Islamu mwanamke huyo anayeona damu ya uzazi nifasi huitwa Mwenye Nifasi.
Alama Zake:
1. Damu ya nifasi huenda ikaonekana kwa kiasi cha muda mchache tu baada ya kujifungua au (kuharibu mimba). Ama damu inayoonekana baada ya siku kumi tangu kujifungua haihesabiki kuwa ni nifasi.

2. Iwapo atakuwa anaona damu leo, kisha kesho haoni, mpaka muda wa siku kumi; basi yote ataifanya kuwa ni nifasi.

3. Iwapo ataona damu zaidi ya siku kumi, na kuendelea kwa muda wa mwezi mzima, hali hiyo ina sura mbili:

a. Ikiwa mzunguko wa damu yake ya mwezi una ada maalumu, basi kati- ka hali kama hii atachukua idadi ya siku zake za damu ya mwezi afanye ndiyo nifasi, na zitakazobakia afanye kuwa ni istihadha.

b. Ikiwa mzunguko wa Damu yake ya Mwezi hauna Ada Maalumu basi katika hali kama hii Siku kumi za mwanzo atazifanya Nifasi na zilizozidi atazifanya Istihadha.
Nukta Muhimu:
Iwapo baada ya kujifungua damu itaendelea zaidi ya siku kumi, na ikawa siku ya kwanza baada ya siku ya kumi imegongana na siku ya kwanza ya damu yake ya mwezi, na akawa ni mwenye ada maalumu, na hali ya kuwa damu ina sifa za hedhi; basi siku kumi za mwanzo atazifanya kuwa ni nifasi na siku nyingine atazifanya kuwa ni siku za damu yake ya mwezi.
Kanuni:
1. Kanuni za mwenye nifasi ni sawa na za mwenye hedhi. Hairuhusiwi kumwingilia, haisihi kumpa talaka, na ni haramu kwake kusali, kufunga, kugusa andiko la Qur’ani na kusoma sura zenye Aya ya sijida ya wajibu.

2. Kila lililo wajibu au sunna au karaha kwa mwenye hedhi pia ndivyo lilivyo kwa mwenye nifasi.

3. Ni lazima kwa mwanamke baada ya kutoharika kutokana na nifasi, aoge kisha atekeleze ibada zake.
Nne: Josho La Janaba:
Mwenyezi Mungu amesema: “Na mkiwa na janaba, basi ogeni…”1
Janaba Ni Nini?
1. Janaba hupatikana kwa mwanadamu kwa moja kati ya mambo mawili:

2. Kujamiana.

Manii kutoka kwenye mwili wa mwanadamu usingizini au hali ya kuwa macho. Na ni lazima kuoga janaba kutokana na moja ya sababu hizo mbili.
Utambulisho:
Manii: Hayo ni maji yanayotoka ndani ya mwili wa mwanadamu pindi yanapopatikana matamanio, na kwa wanaume hali ya kutoka kwa manii huambatana na msukumo na (hatimaye) uchovu wa mwili.

Kwa matokeo hayo, janaba huthibiti kwa masharti yafuatayo:

a. Kutoka manii hali ya kuhisi matamanio.

b. Kutoka manii pamoja na kuwepo msukumo.

c. Kutoka manii pamoja na kupatikana uchovu wa mwili.

Kutokana na maelezo hayo ni kuwa; unyevunyevu unaotoka mwilini ambao hauna moja ya sifa hizo hauchukuliwi kuwa ni manii.

Lakini kwa mgonjwa na mwanamke halizingatiwi sharti la msukumo na uchovu wa mwili, hivyo ikiwa unyevunyevu utatoka huku akiwa na hali ya matamanio ni lazima aoge.

Hatuna budi kusema kuwa wanachuoni wetu watukufu, wengi hawazingatii nukta mbili: Ya pili na ya tatu kuwa ni sharti kwa mwanamke.
Mambo Mawili Muhimu:
i. Iwapo mtu atapatwa na hali ya matamanio na uchovu wa mwili kwa sababu ya kutazama filamu za ngono au picha za uchi (Mungu apishie mbali) na akawa na yakini kuwa manii yamemtoka, basi kanuni za janaba zitamuhusu na hivyo atawajibika kuoga.

ii. Iwapo mtu anajua kuwa, lau akitazama filamu za ngono au kusoma baadhi ya majarida au vitabu vyenye kuamsha hisia za matamanio na hatoweza kujizuia na hivyo atapata janaba, basi ni lazima kwake kujiepusha na mambo hayo.
Yaliyoharamishwa Kwa Mwenye Janaba
a. Mwili wake kugusa Qur’an au jina la Mwenyezi Mungu, aidha ni wajibu kujiepusha kugusa majina ya manabii na maimamu (a.s.) na pia jina la bibi Fatimat Zahraa (a.s.).

b. Kuingia msikiti mtukufu (wa Makkah) na msikiti wa Mtume (s.a.w.) hata kama itakuwa ni kwa kuvuka, aidha ni wajibu kujiepusha kuingia ndani ya maeneo yalimo makaburi matukufu ya Maimamu walio takasika (a.s.) hata kama ni kwa kuvuka.

c. Kuketi na kusimama ndani ya misikiti mingine. Si vibaya kuvuka kwa kuingilia mlango mmoja na kutokea mlango wa pili.

d. Kuweka kitu msikitini hata kama ataweka akiwa nje au wakati wa kuvuka.

e. Kusoma sura nne zenye sijida ya wajibu, hata kama itakuwa herufi moja ya sura hiyo. Nazo ni:-

• As-Sajda-Sura ya 32,

• Al- Fuswilatu-Sura ya 41,

• An-Najmu-Sura ya 53,

• Al-Alaqi-Sura ya 96
Mambo Yaliyo Karaha Kwa Mwenye Janaba
a. Kula na kunywa, na karaha yake huondoka kwa kutia udhu.

b. Kusoma zaidi ya Aya saba za sura nyingine zisizokuwa na Aya ya sijida ya wajibu.

c. Kugusa sehemu nyingine ya msahafu isiyokuwa na andiko, kuanzia jalada, karatasi, maelezo ya ziada na eneo lililopo kati ya mistari. Hapa tunapenda kuhimiza kuwa, uharamu wa kugusa andiko la Qur’an kwa mwenye janaba, haukomei kwenye Mashafu Tukufu tu, bali unahusu kila ilipoandikwa Aya Tukufu, sawa iwe kwenye karatasi, gazeti, kitabu (au kitu chochote).

d. Kubeba Mashafu Tukufu. e. Kubadili nywele rangi.

e. Kupaka mafuta kichwani na mwilini.

f. Kulala. Na karaha yake huondoka kwa kutia udhu au kutayamamu.
Nukta Muhimu:
Iwapo mtu atapatwa na janaba kisha akaoga, basi kuanzia hapo si karaha kwake kutenda mambo yaliyotajwa hapo juu.
Tano: Josho La Maiti

Sita: Josho La Kugusa Maiti

Utangulizi:
Kwa kuwa haya mambo mawili yanahusu kanuni za maiti na mas’ala haya yana umuhimu mkubwa, basi ni vizuri dada zetu waumini wakajua angalau muhtasari wa mas’ala haya na yale yanayowahusu wao, na ili waweze kuwafunza wenzao pindi yanapohitajika au wakati wa dharura.
Kanuni Za Maiti:
1. Wakati wa kutoka roho.

2. Hukumu za baada ya kifo.

3. Josho la maiti

4. Kumpaka karafuu maiti

5. Kumvisha sanda

6. Swala ya jeneza

7. Mazishi

8. Josho la kugusa maiti
Wakati Wa Kutoka Roho
Dakika za mwisho za uhai wa mwanadamu ambazo ndani yake alama za kifo huonekana, ni pale ambapo mwislamu anakuwa katika hali ya kutokwa na roho. Na hali hii huitwa Al-Ihtidhaar. Ndani ya dakika hizo kuna mambo ya wajibu yafuatayo:

1. Mtu ambaye yumo katika hali ya kutoka roho, alazwe chali na nyayo zake kwa ndani zielekezwe kibla, kiasi kwamba lau ataketi uso wake utakuwa umeelekea Qibla. Ni sawa sawa akiwa mwanamke au mwana mume, mtoto au mkubwa.

2. Kumwelekeza Qibla mtu anayekaribia kutokwa na roho, ni wajibu wa kutoshelezana kwa waislamu, wala jambo hili halihitajii idhini ya walii wake.
Mambo Yaliyo Sunna Kumfanyia Mtu anaye kata roho
1. Kumtamkisha shahada mbili na kukiri Maimamu kumi na mbili (a.s.) na itikadi nyingine za haki na maneno ya faraja.

2. Kumtamkisha dua hii: “Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mengi miongoni mwa (maasi) niliyokuasi, na pokea kichache kutoka kwangu miongoni mwa yale niliyokutii. Ewe (Mola) ambaye anapokea kichache na anasamehe mengi, pokea kichache kutoka kwangu na unisamehe mengi, hakika wewe ni Msamehevu na Mwingi wa Msamaha. Ewe Mwenyezi Mungu! Nirehemu kwani hakika wewe ni Mrehemevu.”

3. Ili kumrahisishia utokaji wa roho, ni sunna kumsomea sura tuku- fu Yasini, As-Swafati, Al-Ahzabu na Aya ya Al-Kursiyu, Aya ya hamsini na nne ya Sura Al-Aarafu na Aya tatu za mwishoni mwa Sura Al-Baqara.

4. Mwenya kukata roho ahamishiwe kwenye mSwala wake.
Mambo Yaliyo Karaha:
1. Kumwacha huyu mwenye kukata roho peke yake.

2. Kuweka uzito juu ya tumbo lake.

3. Kukithirisha mazungumzo na kilio mbele yake.

4. Mwenye hedhi na mwenye janaba kuhudhuria mbele yake.

5. Kumgusa awapo katika hali ya kutokwa roho.
Hukumu za Baada ya Kifo:
1. Ni Sunna kumfumba macho, kumfumba kinywa na kufunga taya

2. Kuinyoosha mikono yake kwenye mbavu zake, kunyoosha miguu yake na kumfunika kwa nguo.

3. Kumuwashia taa usiku.

4. Kuwaarifu waumini ili wahudhurie mazishi yake.

5. Kuharakisha kumuandaa (isipokuwa kama kuna utata wa hali yake, hivyo atasubiriwa mpaka upatikane uhakika wa kifo chake).

6. Atakapofariki mjamzito, basi ni wajibu kumtoa mtoto tumboni (akiwa yuko hai) na ndipo azikwe.
Josho La Maiti:
Nalo ni josho la tano katika orodha ya majosho saba ya wajibu. Ni lazima kuuosha mwili wa maiti kwa maji ya aina tatu kwa kufuata utaratibu ufuatao:

1. Kwa maji yaliyochangwa na mkunazi, (maji yatawekwa mkunazi kidogo ili maji yaendelee kubakia katika hali yake halisi).

2. Kwa maji yaliyochangwa karafuu maiti, (maji yatawekwa karafuu maiti kidogo ili maji yaendelee kubakia katika hali yake halisi.

3. Kwa maji halisi.
Mambo Yanayohusu Josho La Maiti:
a. Iwapo mwanaume atamwosha mwanamke, au kinyume chake basi josho hilo ni batili. Naam; Mwanamke anaweza kumwosha mumewe kama ambavyo mwana mume anaweza kumwosha mkewe.

b. Iwapo itashindikana kupatikana mwana mke wa kuweza kumwosha maiti wa kike, basi inawezekana wanaume maharimu kufanya hivyo, angalau nyuma ya mavazi.

c. Ni lazima kutoharisha mwili wa maiti kutokana na najisi kabla ya kuanza kumwosha.

d. Mwanamke aliyefariki akiwa katika hali ya damu ya mwezi au janaba hahitajii majosho haya mawili, bali josho la maiti pekee linamtosha.

e. Iwapo itashindikana kupatikana mkunazi au karafuu maiti basi maiti ataoshwa katika josho mbili za mwanzo kwa maji khalisi, badala ya yale majosho mawili. (Lakini kwa niya ya badala.)

f. Iwapo itashindikana kupatikana maji basi atatayamamu badala ya kila josho.

g. Mtoto wa ki-Islamu wa mamba iliyotoka ni lazima kumwosha iwapo ametimiza mwezi wa nne.
Kumpaka Karafuu Maiti:
Nalo ni jambo la wajibu, na ni sharti iwe baada ya kumwosha na iwe kwa kumpaka hiyo karafuu maiti juu ya viungo saba vya kusujudia, navyo ni paji, matumbo ya viganja viwili. Na kwa upande wa miguu, ni magoti mawili na ncha za vidole gumba. Kitendo hiki cha kumpaka karafuu maiti huitwa Al-Hanuut. (Na ni lazima karafuu maiti hiyo iwe imesagwa na kuwa unga, na iwe mpya. Kwa hiyo kama itakuwa kuukuu ambayo haina harufu haitofaa). Na wala haisihi kutumia manukato mengine badala ya karafuu maiti.

Katika suala la kumpaka karafuu maiti, tunaweza kuashiria mambo yafuatayo:

1. Ni sunna kuchanganya karafuu maiti na kiasi kidogo cha udongo wa Imamu Huseini a.s, (kutoka ardhi ya Karbala).

2. Ni bora kumpaka karafuu maiti kabla ya kumvisha sanda.

3. Ni karaha kutumia manukato na udi kwa ajili ya maiti.
Kumvisha Sanda:
Baada ya kumwosha na kumpaka karafuu maiti, ni lazima kuuvisha sanda mwili wa maiti wa Ki-Islamu. Na kuvisha sanda hiyo kunakuwa kwa kutumia nguo tatu ambazo ni kikoi, kanzu na shuka. Na hiyo ndiyo huitwa sanda. Nukta zifuatazo zinahusiana na suala hili:

1. Kikoi chenye kusitiri eneo la kati ya kitovu na magoti, na kanzu itakayofika kwenye nusu ya muundi, na shuka itakayofunika mwili mzima.

2. Gharama za maziko na sanda ya mke ni juu ya mume, hata kama mke ni tajiri.

3. Haisihi kumvisha sanda kwa kutumia kitambaa chepesi ambacho kinaonyesha mwili.

4. Ni lazima sanda iwe safi yenye tohara, na iwe ni ya halali (isiyo ya kunyang’anya).
Swala Ya Maiti:
Nayo ni takbira tano, na katika kila baada ya takbira moja kupatikane dhikri (kisomo maalum) isipokuwa katika takbira ya mwisho. Na uchache wa kisomo cha wajibu katika swala hiyo ni kama ifuatavyo:

1. Allah Akbar. Ash-haduallah ilaha illa llah Wa ash-had anna Muhammadarrasulullah (Allah ni Mkubwa. Nakiri kwamba hakuna Mungu ila Allah, na ninakiri kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah.)

2. Allah Akbar. Allhumma swalli ala Muhammadin wali Muhammad (Allah ni Mkubwa. Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka juu ya Muhammad na juu ya familia ya Muhammad).

3. Allah Akbar. Allhummaghfir lilimuminina wal-mu’minat (Allah ni Mkubwa. Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe waumini wa kiume na waumini wa kike).

4. Allah Akbar. (Allah ni Mkubwa) Kama maiti ni mwanaume itasemwa: Allhummghfir lihadhalmayyit (Ewe Mwenyezi Mungu msamehe maiti huyu). Kwa mwanamke: Allhummghfir lihadhi-hilmayyit Ewe Mwenyezi Mungu msamehe maiti huyu).

5. Allah Akbar. Allah ni Mkubwa.
الله أكبر: اشهد أن الا الله واشهد أنّ محمدا رّسول الله
 
الله أكبر: اللهم قلّ على محمّد وآل محمّد
 
الله أكبر: اللهم اغفر للمؤمنين والمؤمنات
 
الله أكبر: اللهم اغفر لهذا الميّت/ لهذه الميَت 
 
الله أكبر
 
Mambo Yanayo Husiana Na Suala Hili:
A. Kisomo cha sunna katika swala hii kimetajwa kwa ukamilifu ndani ya vitabu vya dua na vitabu vya matendo ya kisharia vya waheshimiwa wanachuoni wetu.

B. Kwenye Swala ya maiti, mwenye kusali atasimama huku ameelekea Qibla hali ya kuwa jeneza likiwa juu ya ardhi, huku kichwa cha maiti kikiwa kuliani mwa mwenye kuswali na miguu ikiwa kushotoni mwake.

C. Ni wajibu kumsalia maiti mwislamu aliyetimiza miaka sita. d. Udhu si sharti katika Swala ya maiti.
Mazishi:
Baada ya kumwosha ni lazima kumpaka karafuu maiti kisha kumvisha sanda, halafu kumswalia na hatimaye mwili kuzikwa ardhini kwa namna ambayo itazuia harufu kutoka nje, au kufukuliwa na wanyama.
Katika Mazishi Kuna Mas’ala Kadhaa, Miongoni Mwa Hayo Ni:
1. Hairuhusiwi kumzika mwislamu kwenye makaburi ya makafiri, wala kumzika kafiri kwenye makaburi ya waislamu.

2. Mwili wa mwana mke utawekwa kaburini kupitia mmoja wa maharimu wake au mwana mke mwenzake.

3. Maiti hulalia ubavu wake wa kulia awekwapo kaburini kiasi kwamba uso wake na mwili wake utaelekea Qibla, na nyuma ya mgongo wake huwekwa mto wa udongo ili asilale chali, huku mikono yake ikiwekwa juu ya udongo.

4. Hairuhusiwi kufukua kaburi la maiti ya ki-Isilamu kwa lengo la kumzika mwislamu mwingine.

5. Ni sunna kusali swala ya (rakaa mbili ambayo ni) zawadi kwa ajili ya maiti usiku ule wa mazishi. Ndani ya rakaa ya kwanza atasoma Al-Hamdu na Ayatul-Kurusiyy mara moja, na katika rakaa ya pili atasoma Al-Hamdu na Suratul-Qadri mara kumi,

kisha baada ya swala aatasema: “Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na familia ya Muhammad na peleka thawabu zake kwenye kaburi la fulani.” Atataja jina la marehemu huyo.
Nukta Muhimu:
Ndani ya vitabu vya dua na vitabu vya matendo ya kisharia vya waheshimiwa wanachuoni wetu wakuu, kumepatikana mafunzo na sunna nyingi zinazohusiana na mazishi. Miongoni mwa vitabu hivyo, ni kitabu kiitwacho Mafatihul-Jinani cha Sheikh Abasi Al-Qummi. Kwa mwenye kutaka ziyada arejee humo.
Josho La Kumgusa Maiti:
Nalo ni josho la sita katika orodha ya majosho saba ya wajibu:

1. Iwapo sehemu ya mwili wa mwanadamu itagusa mwili wa maiti baada ya mwili wake wote kupoa na kabla hajaoshwa, basi ni wajibu kuoga josho la kumgusa maiti.

2. Josho hili si wajibu iwapo umegusa maiti ya mimba iliyotoka ambayo haijatimiza miezi minne.

3. Josho hili ni wajibu kwa mama aliyetoa mimba ambayo imetimiza miezi minne.

4. Josho hili pia ni wajibu iwapo mwanadamu atagusa kipande kilichokatika kutoka kwenye mwili wa maiti kabla maiti hajaoshwa.

5. Namna ya kuoga josho la kumgusa maiti, ni kama namna ya kuoga janaba.
Majosho Ya Sunna Ambayo Huwa Wajibu Kwa Sababu Ya

Nadhiri Au Kiapo:
Sehemu ya saba ya majosho ya wajibu ni pindi mwenye kulazimikiwa na sharia atakapoweka nadhiri ya kisharia (kama ilivyo fafanuliwa ndani ya vitabu vya Fiqihi. Au akaapa kiapo cha kisharia kuwa ni lazima aoge moja kati ya majosho ya sunna, basi hapo josho hilo la sunna linakuwa wajibu juu yake.
________________________
1. Al-Maida: 6.
i. Majosho ya Sunna ya wakati maalum.

ii. Majosho ya Sunna ya sehemu maalum.

iii. iii.Majosho ya Sunna kwa ajili ya vitendo maalum
Jedwali La Majosho Ya Sunna Ya Nyakati Maalum
 
NO
JINALAJOSHO
WAKATIWAKE
1
Ijumaa (ni Sunna iliyohimizwa)
Kuanzia adhana ya asubuhi mpaka adhana ya adhuhuri
2
Siku zote za usiku tasa unaopati kana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan
Usiku wote, na bora akutanishe na kuzama kwa jua
3
Usiku wa 15, 17,19,21,23,25,27, na 29 katika mwezi mtukufu wa Ramadhan (ni Sunna iliyohimi zwa)
Kati ya Magharibi na Isha
4
Usiku wa ishirini na tatu ya mwezi wa Ramadhan (josho la pili)
Mwisho wa usiku
5
Siku ya siku kuu ya Idi ya kufunga
(ni Sunna iliyohimizwa)
Kuanzia kuchomoza kwa alfajiri mpaka adhuhuri, na hienda ikawa ni mpaka kuzama kwa jua.
6
Siku kuu ya Idi ya Kuchinja (ni Sunna iliyohimizwa)
Kuanzia kuchomoza kwa alfajiri mpaka adhuhuri, na inaweze kana mpaka kuzama kwa jua.
7
Siku ya nane ya Mfungo tatu (Siku ya Tar’wiya)
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
8
Siku ya tisa ya Mfungo tatu (Siku ya Arafa)
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
9
(Mwezi wa Rajaba) Siku ya kwanza ya Mfungo kumi, ya mwisho na nusu yake
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
10
Siku ya Maapizano Mubahala (Mwezi ishirini na nne ya Mfungo tatu)
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
11
Siku ya ishirini na tano ya Mfungo pili
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
12
Siku ya Mtume kukabidhiwa Utume (Mwezi ishirini na saba ya Mfungo kumi) (Rajabu)
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
13
Siku ya nysy ta Mfungo kumi na moja (Shaban)
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
14
Siku aliyozaliwa Mtume, Mwezi kumi na Mfungo sita
Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
Jedwali La Majosho Ya Sunna Ya Sehemu Maalum
NO
MAHALI
WAKATI
1
Josho kwa ajili ya kuingia Eneo Tukufu la Makkah
Kabla ya kwenda (bila kuwepo umbali mkubwa)
2
Josho kwa ajili ya kuingia Makkah
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoaga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
3
Josho kwa ajili ya kuingia Miskiti Mtukufu
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
4
Josho kwa ajili ya kuingia Kaabah
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
5
Josho kwa ajili ya kuingia Eneo Tukufu la Madina
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
6
Josho kwa ajili ya kuingia Madina Yenye Nuru
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
7
Josho kwa ajili ya kuzuru Misikiti wa Mtume
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
8
Josho kwa ajili ya kuzuru maneneo ya makaburi matukufu ya Maimamu Waliyo takaswa
Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleze kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
Jedwali Ya Majosho Ya Sunna Ya Vitendo Maalum
NO
SABABU
WAKATI
1
Josho kwa ajili ya kuhirimia
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
2
Josho kwa ajili ya kutufu
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
3
Josho kwa ajili ya ziara
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
4
Josho kwa ajili ya kusimama Arafa
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
5
Josho kwa ajili ya kusimama Mash’ari
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
6
Josho kwa ajili ya kuchinja
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
7
Josho kwa ajili ya kunyoa nywele (Hija)
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
8
Josho kwa ajili ya kumwona Ma’suum (a.s) usingizini
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
9
Josho kwa ajili ya Swala ya Haja
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
10
Josho kwa ajili ya Istikhara
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
11
Josho kwa ajili ya Amali za siku ya Ummu Daudi
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake.
Na hivyo kwa upande wa usiku
12
Josho kwa ajili ya safari
Kabla ya kitendo
13
Josho la kumzuru Imamu Hussein (as.)
Kabla ya kitendo
14
Josho la Swala ya Kuomba mvua
Kabla ya kitendo
Majosho yaliyotangulia kutajwa hapo kabla, unaweza kuyatimiza kwa namna moja kati ya namna mbili:
Utaratibu Maalum:
Niya: Kisha kuosha kichwa na shingo. Kuosha upande wa kulia wa mwili pamoja na tupu mbili. Kuosha upande wa kushoto wa mwili pamoja na tupu mbili.
Nukta Muhimu
Ili kuwa na yakini (ya ukamilifu) wa kuoshwa kwa maeneo yote ya mwili, basi anapo osha upande mmoja aingie kidogo hadi upande wa pili ili kuhakikisha kuwa ameosha sehemu zote wakati wa kuoga.
Kupiga Mbizi
Niya: Kisha aingize mwili wote ndani ya maji kwa mara moja. Aingie ndani ya maji hatua kwa hatua mpaka maji yafunike mwili wake wote.

Aingize mwili wake ndani ya maji kwa namna yoyote kisha anuwiye na hatimaye atikise mwili wake huku akiwa ndani ya maji.
Nukta Muhimu
i. Inawezekana kwa mtu akanuwiya niya mbali mbali kwenye josho moja.

ii. Majosho yote namna ya kuyaoga ni moja, to

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ