Rafed English

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume by : al-islam.org

 
Mitala na ndoa za Mtume imekuwa ni maneno ya kawaida katika mashambulizi yao dhidi ya Uislamu yaliyo tumiwa nje ya muktadha wa Uislamu na vyombo vya habari visivyo amini (Uislamu) vya mlengo wa kulia, wanasiasa na pia wanahistoria. Sayyid Muhammad Rizvi ameelezea tu hapa kwa ufupi kuhusu mitala na ndoa za Mtume katika muktadha wake wa kweli.
Dhana Ya Ndoa Ya Mitala Na Ndoa Za Mtukufu Mtume
“Nasi hatukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu.” 21 : 107

“Nimeumchunguza yeye (Mohammad). Ni umtu anayevutia ajabu; na kwa maoni yangu, mbali na kuwa mpinga Kristo, ni lazima aitwe mwokozi wa wanadamu.”

“Nina amini kwamba endapo umtu kama huyo angeshika udikteta wa ulimwengu wa kisasa, ange fanikiwa katika kutatua matatizo yake katika namna ambayo ingeuletea ile amani na furaha inayohitajika hasa”

“Kama dini yoyote ingekuwa na fursa ya kutawala uingireza, hasha, bali Ulaya nzima katika kipindi cha miaka 100 ijayo, itakuwa ni Uislamu.”

“Siku zote nimeichukulia dini ya Mohammad katika hadhi ya hali ya juu kwa sababu ya changamoto zake za ajabu. Ndiyo dini pekee ambayo kwangu mimi ninaiona kuwa na uwezo wakuwiana mabadiliko ya kila zama za maisha ambayo inaweza kuvutia katika kila zama.”

George Barnard Shaw katika “The Genuine Islam” Juz. 11 na. 8 (1936)

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

Al-Itrah Foundation
Kijitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahihi kutoka Kiingereza.

Ni tafsiri pana ya khutba iliyotolewa na mmoja wa wanachuoni wetu mashuhuri wa Kiislamu Sayyid Muhammad Rizvi, katika programu ya TV juu ya .Islam in Focus. ya tarehe 5 Januari, 2002 katika lugha ya Kiingereza.

Mitala na ndoa za Mtume imekuwa ni maneno ya kawaida katika mashambulizi yao dhidi ya Uislamu yaliyo tumiwa nje ya muktadha wa Uislamu na vyombo vya habari visivyo amini (Uislamu) vya mlengo wa kulia, wanasiasa na pia wanahistoria.

Sayyid Muhammad Rizvi ameelezea tu hapa kwa ufupi kuhusu mitala na ndoa za Mtume katika muktadha wake wa kweli.

Tarjuma yake inatolewa hapa kwa faida ya ndugu zetu wazungamzaji wa Kiswhili wa Afrika ya Mashariki na pengine popote.

Kwa hakika wasomaji wasio na upendeleo watafaidika kutokana na toleo hili.

Tunawashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia katika utoaji wa tarjuma hii ya Kiswahili ambayo inawasilishwa hapa.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es- Salaam , Tanzania.
Utangulizi
Tangu lile tukio la (9/11) Septemba kumi na moja, tunaona kwamba vikundi fulani vimejaribu kuutumia mkasa ule kwa faida yao kwa kuushambulia Uislam kutoka kila upande. Kwa bahati mbaya sana, hata baadhi ya idhaa za televisheni za Kikristo zimejiunga katika upondaji Uislam huu na zinajaribu kufifisha na kuipotezea nuru picha ya Uislam na ya Mtume Muhammad (s.a.w.).

Moja ya dhamira au mada ya kawaida waliyotumia katika mashambulizi yao dhidi ya Uislam ni juu ya wake wengi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.).

Tunapenda kwanza kuelezea hii dhana ya ndoa za Mitala katika Uislam, ikifuatiwa baadaye na hizo ndoa za Mtukufu Mtume.
Ndoa katika Uislam ni ishara ya mamlaka na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Qur.ani Tukufu inasema:

.Na katika dalili zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika
jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na
huruma baina yenu. Bila shaka katika hiyo mna mazingatio
kwa watu wanaofikiri.. (30:21)
Kuzungumzia kawaida, kuna aina mbili za ndoa katika Uislam:

• Ndoa ya Mke Mmoja: Mwanaume kwa Mke mmoja
• Mitala iliyokadiriwa (aina ya ndoa ya mitala): Mume mmoja aliyeoa wake wawili, au watatu au kwa kuzidi sana wake wanne.

Katika Uislam ndoa iliyobora ni ile ya mke mmoja. Ndoa ya Mitala iliyokadiriwa (kiwango cha wake) ni fursa iliyotolewa na Uislam na kuidhinishwa kwa ajili ya mazingira ya kipekee tu, na hivyo pia kwa masharti makali mengi ya kutiwa.

Idadi kubwa sana ya Waislam wanaume wana mke mmoja katika uhusiano wa ndoa zao; wale ambao wana mke zaidi ya mmoja hao ni wachache sana, labda kama asilimia chini ya moja ya wote katika dunia ya Kiislam.
Uislam haukubuni huo mfumo au mtindo wa ndoa ya mitala. Ulikuwepo siku nyingi sana kabla ya Uislam kuingia katika mandhari ya matukio ya dunia. Bilblia inasema kwamba Lameki; mjukuu wa Nabii Adam .alijitwalia wake wawili: jina la mmoja wa kwanza lilikuwa ni Adah, na jina la huyo mwingine ni Zillah.. Hivyo mitala imekuwepo tangu siku za mwanzo kabisa za historia ya mwanadamu.

Watu watakatifu wengi wa ndani ya Biblia walikuwa na wake wengi au vimada kwa wakati huo huo. Abraham alikuwa na Sarah na Hajar. Abraham mwanzoni alijaaliwa na kupata motto wa kiume kupitia kwa Hajar, ambaye huyu alimwita Ishmael, na halafu akajaaliwa kupata mtoto wa kiume mwingine kupitia kwa Sarah, ambaye huyu alimwita Isaaka.

Hebu angalia mfano wa Yakobo (Yaquub); yeye alikuwa na wake wanne na vimada: Leah na Rachel (wote walikuwa binamu zake Yakobo), na yeye pia alikuwa na Bilhah na Zilpah (wote walikuwa ni wajakazi waliotolewa zawadi kwa Yakobo kutoka kwa wake zake). Ni kutoka kwa mabibi hawa ambapo Yakobo alipata watoto wa kiume kumi na mbili ambao walikuja kuwa wahenga wa yale makabila kumi na mbili ya Israeli.

David, anayejulikana kwa kuarabu kama Nabii Dawud, alikuwa na takriban wake wanane ambao majina yao yanajulikana, alikuwa na wengine wengi ambao majina yao hakuwahi kujulikana na kuwekwa kwenye kumbukumbu. Kile kitabu cha Pili cha Samuel (katika Biblia) kinazungumzia kuhusu .wale wake zake. Dawud huko Hebron na vile vile huko Jerusalem.

Lamech, mjukuu wa Adam, alikuwa na wake wawili.
Abraham alikuwa na wake wawili: Sarah na Hajar
Yakub alikuwa na wake wawili na vimada wawili:
Yale makabila kumi na mbili ya Waisrail yanatokana na
mabibi hawa wane.
Dawud alikuwa na wake wengi
Na hivyo ifahamike kwamba Uislam haukuanzisha huo mfumo wa mitala; ulikuwepo tangu mwanzo wa kuchomoza historia ya mwanadamu. Wakati Uislam ulipoingia kwenye mandhari ya dunia katika karne ya saba ya zama za kawaida, ulirithi mfumo wa ndoa uliokuwepo. Kuruhusu mitala kusije kukaonekana kama ni sehemu ya ujinsia halisi wa kinaume. Kwa maneno ya Karen Cermstrong; .Mitala hayakukusudiwa kuboresha yale maisha ya kijinsia ya wavulana . yalikuwa ni sehemu ye sheria ya kijamii.

Sifa ni kwa Uislam ambao ulibadili na kuurekebisha ule mfumo uliokuwepo wakati ule.

Kwanza kabisa, Uislam uliweka kikomo kwenye idadi ya wake ambayo mtu anaweza kuwa nayo kwa wakati mmoja . mwisho kabisa ukiwa wa wake wane kwa wakati mmoja.

Pili, Uislam uliweka masharti magumu na makali juu ya mtu ambaye alitaka kuoa mke wa pili. Ni lazima awe na uwezo wa kuihudumia na kuitunza hiyo familia, na vile vile aweze kushughulika nao wote katika misingi ya uadilifu na haki. Katika Sura ya nne, aya ya 3, baada ya kutoa ruhusa kwa Muislam mwanaume kuoa wake wawili, watatu, au wanne, Qur.ani mara tu inasema .Lakini mkihofia kuwa hamtaweza kuwa waadilifu baina yao, basi bakieni na mmoja....

Ukiangalia kwenye saikolojia ya mwanadamu, ni watu wachache tu walio na sifa au tabia ya uadilifu na haki. Qur.ani yenyewe, katika Sura hiyo hiyo ya 4 aya ya 129 inasema: .Na hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, japokuwa mtajitahidi...

Kutegemea kwenye aya kama hizo, Serikali kadhaa za Kiislam (kama Irani na Misri) zinaidhibiti hii ruksa ya mitala; Yule mtu anayetaka kuoa mke wa pili anapaswa kupata idhini kutoka kweye baraza la familia na kuthibitisha hiyo haja ya mke wa pili na uwezo wa kuwahudumia wote kwa namna ya kutosheleza.

Uislam ni dini ya kivitendo; sheria zake zinaendana na tabia ya utu wa kibinadamu. Uislam haukatai zile nguvu za asili ndani ya binadamu, bali nakabiliana nazo na kutoa mwongozo wa kuzidhibiti bila kuvuruga amani iliyopo katika jamii.

Takriban serikali zote za magharibi zimekataza ndoa za mitala; lakini uzinifu umetapakaa sana katika nchi hizi hizi hasa. Mbali na majaribio yote katika kuinua mahusiano ya ndoa moja, wanaume wengi waliooa wana mabibi au wanahusika masuala ya ndoa za ziada ambazo zinapelekea kwenye kiwango cha hali ya juu cha talaka; familia zilizosambaratika na watoto wanaokua bila ya kuwa na mababa zao. Na tabia kama hiyo imezigusa ofisi kubwa kubwa . za kidini na za kiserikali vile vile za nchi ya Marekani.

Kama mtu anataka kufanya mchezo mchezo, Uislam utamfanya awajibike na kumfunga kwenye majukumu kwa upande wa yule .mke wa pili. na watoto wake. Ira Lurvey wa sehemu ya sheria za Familia za Muungano wa Baa za Marekani amesema: .Tunaondoka kutoka kwenye ndoa ya mke mmoja na kuelekea kwenye kitu kinachoitwa mfululizo wa ndoa za mke mmoja na hatuna sheria na miongozo, tunapapasa kwenye giza ni jinsi gani sisi tutaendesha maisha yetu..6Vema, ndani ya Uislam, wewe huhitaji kupapasa katika giza; Uislam umetoa miongozo ya wazi wazi kabisa juu ya mahusiano ya aina zote: Ndoa za mke mmoja hadi ndoa za mitala.
Moja ya mifano ya kudhalilisha Uislam ambayo tunaiona kwenye T.V na mitandao ya Intaneti siku hizi ni kauli ya msitari mmoja kama: .Muhammad alikuwa mfuata wanawake; alikuwa na wake tisa.. Kwa Waislam ambao wamevichunguza vitabu vya hao mustashirki na wale wamisionari wenye mawazo ya Krusedi, kauli na sentensi kama hizo sio jambo jipya kwao. Ni muinyo ule ule wa zamani uliowekwa kwenye chupa mpya na jina jipya!

Soma na uyachunguze maisha ya Mtume Muhammad (Rehema na amani juu yake na juu ya kizazi chake) na utaona kwamba Mtume alikuwa ni mtu wa tabia njema za hali ya juu hata siku nyingi sana kabla hajaanza kutangaza Uislam.

Akiwa na umri wa miaka ishirini na tano, Mtume Muhammad alimua Bibi maarufu na aliyeheshimika sana wa hapo Makkah kwa jina akijulikana kama Khadija bint Khuwaylid, ambaye aliuwa mkubwa kuliko yeye kwa umri (kwa mujibu wa maoni yaliyoenea sana, yeye Khadija alikuwa na miaka 15 zaidi yake Mtume, lakini kwa kutegemea utafiti zaidi juu ya suala hili, tunaweza tukasema kwamba yeye alikuwa mkubwa kwa tofauti ya miaka miwili tu).

Jambo la muhimu ni kwamba yeye alibaki akiwa kwenye ndoa naye kwa mda wa miaka ishirini na tano mpaka alipofariki (Khadija) hapo Makkah. Miaka miwili baada ya kifo chake Khadija, Mtume akahamia Madina kutoka Makkah ambako alianzisha jamii ya kwanza ya Kiislam hapo.

Kwa hiyo, kwa miaka yake hamsini ya mwanzo ya maisha yake, Mtukufu Mtume alikuwa na mke mmoja tu, Bibi Khadija, ambaye yeye alimpenda sana na ambaye alikuwa ndiye nguzo imara kabisa ya kufadhili katika kuendeleza kazi yake. Katika ule muda wa miaka kumi na tatu ya maisha yake yeye alioa wake wengine.

Mtume Muhammad

· Tangu kuzaliwa hadi umri wa miaka 25: bila mke
· Umri wa miaka 25 hadi 50: ameoa mke mmoja, Khadija
· Tangu umri wa miaka 50 hadi 63: ameoa wake kumi
Katika miaka kumi na tatu ya mwisho ya maisha yake, Mtume alioa wake kumi. Hii imekuwa shabaha rahisi sana kwa waandishi na wasemaji wasiokuwa waislam ambao wangependa kufifisha nuru ya picha ya Mtukufu Mtume Muhammad (amani juu yake na kizazi chake) na kumwelezea kama mtu ambaye alitawaliwa na kusukumwa na tama na mapenzi.

Wale ambao wanapendelea kuchunguza zaidi juu ya swali la endapo Ruqayya na Zainab na Umm Kulthum walikuwa ni watoto hasa au mabinti wa kupanga wa Mtume waangalie makala ya Sayyid Ja.far Murtadha al- Amili kiitwacho .Banatun-Nabi am Raba.ibuhu? Katika gazeti la kila robo mwaka Turathuna (Qum Mu.assasatu Ahli Bayt, 1413) namba 30-31.

Kama Mtukufu Mtume Muhammad angekuwa ni mtu wa tama, basi kwa nini yeye hakuoa mke mwingine wakati alipokuwa bado ni kijana na tajiri na aliishi katika jamii ambayo ilikubaliana na ndoa ya mitala isiyokuwa na mipaka? Kwa nini hakuoa mwanamke mwingine yoyote pindi Khadija alipokuwa yuko hai ingawa ilikuwa ni wakati wa upeo kamilifu wa ujana wake?

Na kwa hiyo swali linakuja, ni nini ilikuwa sababu ya msingi au mantiki nyuma ya hizi ndoa nyingine za Mtume katika kipindi cha miaka kumi na tatu ya mwisho ya maisha yake.

Ndoa zote za Mtume, mbali na ile ya Bi. Khadija, zilikuwa na busara na maana nzuri ya kisiasa au kidini. Tunaweza tukazigawanya ndoa hizi katika makundi manne, na baadhi ya ndoa zilikuwa na malengo au sababu mara mbili.
1. Bibi Sawdah bint Zam.ah: Bibi wa Kiislam ambaye Mume wake alikuwa amekufa huko Abyssinia. Wakati aliporejea Makkah alikuwa ni mjane: baba yake na kaka yake hawakuwa ni makafiri tu, bali pia walikuwa ni maadui wa Uislam. Yeye hakuweza kutafuta hifadhi kwao hao; wao walikuwa ni wapinzani wakubwa wa Uislam kiasi kwamba angeweza kumtesa mpaka kumuua.

Mtume, na yeye naye wakati huo alikuwa mjane alimuoa Sawdah ili kumpatia ulinzi yeye na vile vile kuunda kiungo muhimu cha undugu na wale maadui zake.

2. Bibi Zaynab bint Khuzaymah: mjane kwa mara ya pili baada ya mume wake wa pili, Abdullah bin Jahsh alipouawa kishahidi katika vita vya Uhud. Alijulikana kwa ukarimu wake bibi huyu, na alikuwa maarufu kwa jina la .Ummul-Masakin, - mama wa masikini.. Sasa yeye mwenyewe binafsi alikabiliwa na wakati mgumu. Mtume alitaka kudumisha hadhi yake, na kwa hiyo akamuoa katika mwaka wa 3 hijiria. Alifariki chini ya mwaka mmoja baada ya ndoa hii.

3. Bibi Umm Salamah: Alikuwa ameolewa mara ya kwanza na Abdullah Abu Salamah. Alihamia Abyssinia pamoja na mume. Alijulikana kwa uchamungu wake na hekima. Alipokuja kuwa mjane na alikuwa na watoto yatima, Mtume akamuoa katika mwaka wa 4 hijiria. Yeye alikuwa pia ni dada wa mkuu wa kabila moja lenye nguvu sana la mjini Makkah la Makhzum. Ndoa hii ilikuwa ishara ya msingi wa kuanzisha kiungo cha undugu pamoja na wapinzani na maadui zake huko Makkah.
4. Bibi Juwayriyyah binti al-Harith. Baada ya vita vya Banu Mustaliq mnamo mwaka wa 5 Hijiria, Waislamu walizichukua familia mia mbili za kabila hilo kwenye utumwa. Juwayriyyah, binti yake mkuu wa kabila hilo, alikwishakuwa mjane. Mtume alimuacha huru kisha akamuoa.

Kwa nini? Waislam, ambao walikuwa wamezichukua familia zile mia mbili za Banu Mustaliq kama watumwa wao, walitambua kwamba kwa ndoa ya Juwayriyyah na Mtume, familia zote mia mbili hizi sasa zilikuwa kwenye uhusiano na Mtume kwa kuoleana. Kutokana na adabu kwa Mtume, Waislam waliziachia familia zote hizi huru. Kwa kuvutiwa na uhamasishwaji huu, lile kabila lote la Banu Mustaliq likawa kabila la Waislam. Kwa ndoa hii, Mtume aliweza kuligeuza kabila lenye uhasama kuwa lenye urafiki na fungamano.
5. Bibi Aisha bint Abi Bakr. Ingawa kufunga uchumba kulifanyika huko Makkah, yeye aliingia kwenye nyumba ya Mtume baada ya yeye Mtume kuhamia kwake Madina. Yeye alikuwa ndiye mke mdogo kabisa wa Mtukufu Mtume. Ndoa hii ilikamilisha ushirikiano na Abu Bakr ili kwamba atakujakuwa upande wa Waislam wakati wa makabiliano dhidi ya waabudu masanamu wa Makkah.

6. Bibi Hafsah bint Umar ibn Umar ibn al-Khattab: Alikuja kuwa mjane baada ya mumewe kuuawa katika vita vya Badr. Mtume alimuoa katika mwaka wa 4 Hijiria. Ndoa hii pia ilifungwa ili kukamilisha ushirikiano wa Mtume na Umar.

7. Bibi Umm Habibah, binti ya Abu Sufyan. Alikuwa ameolewa na Ubaydullah Ibn Jahsh na alikuwa amehamia Abyssinia. Ubaydullah aliingia kwenye Ukristo; wakati yeye alibakia kuendelea na imani yake ya dini ya Kiislam na akatengana naye Ubaydullah. Baba yake, Abu Sufyan, alikuwa adui mbaya kabisa wa Uislam na alipanga mapambano na mapigano dhidi ya Waislam. Wakati Umm Habeba aliporejea Madina, Mtume akamuoa ili yeye ampatie ulinzi bibi huyu na pia aweze japo kulegeza moyo wa Abu Sufyan. Hata hivyo, ndoa hiyo haikuwa na athari au matokeo yaliyotarajiwa kwa Abu Sufyan.

Zile habari maarufu za umri wa ujana wa Aisha zimekuwa zikitumiwa vibaya na vikundi pinzani vya Uislam kumshambulia Mtume kwa .kuowa mtoto mdogo.. Ukweli wa jambo hili ni kwamba Bibi Aisha hakuwa motto mdogo wakati alipoolewa na Mtume katika mwaka wa 2 Hijiria. Al-Tabari, yule mwanahistoria wa kiislam mashuhuri sana anaandika kwamba Abu Bakr wake zake wawili wa kwanza na watoto wao, wote walizaliwa katika zama za kabla ya Uislam (Tarikh Tabari, Jz. 2 . Beirut al-Alam n.d.) uk. 616) Kwa kutegemeana na hili, hata kama angezaliwa mwaka mmoja kabla ya kuanza kwa Uislam, Aisha angeweza kuwa na umri wa miaka 15 au 16 wakati wa ndoa yake na Mtume . umri ambao kwamba ndoa ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi. Ibn Kathir katika kitabu chake al-Bidayah wa an-Nihayah (Jz. 8, uk. 381) anaeleza kwamba Asma bint Abu Bakr, dada yake Aisha, alikuwa na umri wa miaka kumi zaidi ya Aisha. Anaelezea pia kwamba Asma alifariki mnamo mwaka wa 73 Hijiria akiwa a umri wa miaka 100. Kutegemea juu ya hesabu hii, Aisha alikuwa na umri wa miaka 18 au 19 wakati wa ndoa yake.

8. Bibi Safiyyah Bint Huyaiy Ibn Akhtab. Yeye huyu alikuwa bint ya Mkuu wa Kabila la Banu Nadhir, kabila la Kiyahudi la Khaybar. Alikuwa mjane wakati mume wake alipouawa kishahidi katika vita vya Khaybar.Alichukuliwa kama mateka na majeshi ya Waislam. Mtume alimuoa mnamo mwaka wa 7 hijiria ili kudumisha hali yake ya utukufu na uungwana na vile vile kuanzisha uhusiano wa kuoleana na kabila lake la Kiyahudi.
Nne: Hamu na hajaya kuhusiana na mtume
9. Bibi Maymunah Bint al-Harith al-Hilaliyyah. Mume wake wa pili alifariki mnamo mwaka \ wa 7 Hijiria. Alikuja kwa Mtume na akajitoa zawadi mwenyewe kwake Mtume kama yeye angemkubali kumuoa. Yeye alitamani tu ile heshima ya kuitwa .mke wa Mtume.. Mtume naye (kwa kutegemeana na aya 33:50 ya Qur.ani) alikubali yeye kuwa mke wake.
10. Bibi Zaynab bint Jahsh. Yeye alikuwa ni binamu yake Mtume; na alikuwa mjane na mtalaka. Mazingira ya ndoa yake na Mtume yalikuwa sio ya kawaida kabisa.

Uislam ulikuja kumaliza vigezo vyote vya tofauti za kimali na kijamii. Kila Muislam alikuwa sawa na mwingine. Wakati wa kulingania usawa huu, Mtume, kama mtoa mfano aliwatoa ndugu zake wa kike watatu kwenye ndoa kwa watu ambao wanaitwa ni wa kizazi cha hali ya chini kijamii. Miongoni mwa hao ndugu watatu alikuwa ni Zaynab bint Jahsh. Yeye alitolewa kwenye ndoa na Zayd ibn Haritha, mtumwa wa Kiarabu ambaye Mtume alimuacha huru na kisha akamtwaa kama mwana wakumlea. Baada ya kumtwaa huko; Zayd alikuwa akiitwa, Zayd bin Muhammad . Zayd mwana wa Muhammad.

Ile ndoa ya Zaynab kwa Zayd mara tu ikatumbukia nyongo . ikawa chungu. Zaynab hakuweza kustahimili ukweli wa kwamba yeye ni wa uzawa mtukufu kuliko wa mumewe. Haidhuru ni kiasi gani Mtume alivyojaribu kutoa ushauri kwao, tabia ya Zaynab haikubadilika. Hivyo hatimaye Zayd alimtaliki.

Kwa wakati huo huo, aya ya 4 na 5 na Sura ya 33 zilishuka ambazo zilitangaza kwamba kutwaa watoto kulikuwa hakutambuliwi katika Uislam.9 Baada ya aya hizi, watu wakaanza kumwita Zayd kwa jina la baba yake halisi, Zayd bin Haritha.

Lakini ili kukomesha kabisa ule mtindo wa kutwaa watoto, Mwenyezi Mungu alimuagiza Mtume kumuoa Zaynab, yule mtalaka wa Zayd. Katika jamii ya Kiarabu kabla ya Uislam, mtoto wa kiume wa kupanga alichukuliwa kama mtoto halisi: pamoja na haki sawa na wajibu: Kwa mfano, mke wa mtoto wa kupanga alichukuliwa kama mke wa mwana halisi ambaye kuoana naye kulikatazwa kabisa kudumu. Na hivyo ili kuuvunja mwiko huo, Mtume akamuoa Zaynab, mtalaka wa aliyekuwa mwanawe wa kupanga.

Ndoa zote za Zaynab bint Jahsh zilitumika katika kutilia nguvu utekelezaji wa kanuni mbili muhimu za Uislam; kwanza, usawa miongoni mwa Waislam bila kujali tofauti zao za kimbari, utamaduni au kijamii; na pili ilionyesha ule ukweli kwamba uhusiano wa kunyonya au kupanga haukuwa kuunganisha damu hivyo hauwezi kuwa kizuizi katika ndoa.
Wakati Mtume alipokuwa ni kijana na mwenye mali, alikuwa na mke mmoja tu. Lakini katika ile miaka kumi na tatu ya mwisho ya maisha yake, alipokuwa ana umri wa zaidi ya miaka hamsini, yeye alioa wanawake tofauti tofauti . ukiacha mmoja tu, wote walikuwa wajane na wazee.

Ni ukweli usiopingika kwamba hata pale Mtume alipokuwa na hawa wakeze wengine, mapenzi yake kwa mkewe wa kwanza, Bibi Khadija, kamwe hayakumwisha. Al-Bukhari anamnukuu Yule mdogo kabisa katika wake zake, Bibi Aisha kama ifuatavyo:

Sikuona wivu kwa mke yoyote kati ya wake za Mtume Muhammad kwa kiasi kama nilivyokuwa kwa Khadija. Kwa sababu Mtume alikuwa (akimkumbuka na) kumtaja kila mara. Na kila wakati yeye alipochinja kondoo, angepeleka (zile sehemu nzuri za nyama hiyo) kwa marafiki zake Khadija. Wakati mwingine nilipomwambia .Inaonekana kwamba Khadija alikuw ndio mwanamke pekee katika dunia hii,. Mtume angesema .Khadija alikuwa hivi na vile, na kutokana na yeye mimi nilipata watoto

Katika riwaya nyingine, kwa mujibu wa al-Bukhari, Bibi Aisha anasema. .Wakati mmoja Halah, dada yake Khadija aliomba ruksa ya kuingia ndani.. Katika kule kusikia sauti ya Halah, ambayo ilikuwa ikisikika sawa kabisa na ile ya Khadija, Mtume akamkumbuka mke wake kipenzi. Aisha anasema, .Nilishikwa na wivu na nikasema, .Ni nini kinachokufanya umkumbuke mwanamke mzee miongoni mwa wanawake wazee wa Quraishi, mwanamke mzee asiye na meno aliyekufa zamani, ambapo Mwenyezi Mungu amekupatia mtu mwingine bora kuliko yeye?.

Mtume alivurugikiwa waziwazi, naye akasema, .Wallahi sina mtu yeyote bora kuliko Khadija. Yeye aliniamini mimi wakati wengine walibobea kwenye ukafiri. Alishuhudia kwenye ukweli wangu ambapo wengine waliyakataa madai yangu. Yeye alinisaidia

kwa utajiri wake wakati wengine walininyima na Mwenyezi Mungu akanipa watoto kupitia kwake

Hisia hizi za Mtume alizoonyesha kwa wake zake wadogo zinaonyesha wazi kwamba kwake yeye Khadija alikuwa bado ndiye Bibi wa kwanza . mke mashuhuri . bibi mkuu wa Uislam. Ndoa nyingine zote zilikuwa na baadhi ya sababu za kijamii, kisiasa au kidini nyuma yake. Ndoa hizi hazikuegemea kwenye tama au mapenzi, kama maadui wengi wa Uislam ambavyo wangependa kusema.

Natumaini mazungumzo haya yamekusaidia katika kuelewa maoni ya Uislam juu ya ndoa za wake wengi . (mitala) na vilevile sababu za ndoa za Mtume. Uislam ni dini inayoendana na desturi za asili za mwanadamu na una sheria na miongozo kwa ajili ya matatizo makali ya kijamii ya wakati wetu huu.
Kumbukumbu juu ya Mungu ni Rafiki yangu
Hekima ndiyo mzizi wa Imani yangu
Upendo ndio Msingi wangu
Shauku ndiyo Farasi wangu
Kumjua Mungu ndio Mtaji wangu
Uimara ndiyo Hazina yangu
Huzuni ndiyo Mwenza wangu
Elimu ndiyo Silaha yangu
Subira ndiyo Joho langu
Kinaa ndiyo Ngawira yangu
Ufukara ndiyo Fahari yangu
Upendo ndio Sanaa yangu
Uhakika ndiyo Nguvu yangu
Ukweli ndiyo Mkombozi wangu
Utii ndiyo Kitoshelezo changu
Jitihada ndiyo Tabia yangu
Na furaha yangu iko ndani ya swala

Share this article

Comments 0

Your comment

Comment description

Latest Post

Most Reviews

MOST READ